Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

Pengine mimi ningesaidiwa ufafanuzi wa yafuatayo:
-DINI zimeshika kasi sana kwenye SIASA za NCHI yetu hivi sasa sio tu kwenye vyama vya SIASA bali hata kwenye TEUZI mbalimbali ndani ya serikali. Ni nini hatma ya suala hili?
-VIONGOZI wa DINI wamekuwa na ushawishi mkubwa mno kwa viongozi wetu wa kisiasa. Tunawaona wanaSIASA wetu wanavyotembelea MAKANISA na MISIKITI kwa hafla hizi na zile. Kiongozi wa namna hii akishika madaraka atajinasua vipi na ushawishi wa viongozi wa dini?
Kwangu mimi changamoto kubwa iliyopo ni namna ya kukabiliana na UDINI unaokua na kukomaa sana sasa. Sina tatizo na CHAMA chochote kushika madaraka nchi hii endapo tu tutaiandika vizuri na kwa makini KATIBA MPYA ijayo.
 
Kama mumenisoma vizuri utagundua kwamba nachozungumzia mimi ni Chadema kutokuwa na defensive strategy inayohusiana na maswala haya. Tuna silaha nyingi sana za kuishambulia CCM na Mchambuzi katupa hints ni ngao zipi CCM inajivunia leo. lakini hapo hapo hakutazama kama Chadema nayo ipo uchi sana haina ngao zake isipokuwa silaha tupu za mashambulizi. Tukishambuliwa ktk Ukanda, Udini au Ukabila mara zote huja na mifano ya Zitto.. Yaani kweli Zitto pekee ndio sababu ya kutulinda ktk Ukanda, Ukabila na Udini. Nini ngao zetu? sisi tunaweza vipi kujivunia kutoshiriki ktk hizi tuhuma za KUJUANA tofauti na CCM ambao hadi kesho tunaunga mkono baadhi ya ushirika wao wenyewe. Hatuna majibu mkuu wangu tunaulizwa kila siku hapa JF mara zote majibu hutolewa na kina Mkandara au Mohammed Mtoi.. Mimi na Mohammed Mtoi tunaweza vipi kuwa na majibu ya uongozi wa Chadema inapokabiriwa na tuhuma nzito kama hizi hata kama najua sii kweli.. sema kweli maana janvi hili ni mawazo ya mtu mmoja mmoja sio janvi la chama.

Uvumi siku zote ndio hujenga imani za watu, wanasema Chadema ni chama cha Ukanda au udini, wewe huzioni, mimi zisioni na vile vile kumbuka hata mtu wa CUF anaamini hivyo hivyo. Na sidhani kama tunaweza kuonyesha Udini wa CUF lakini Je ni watanzania wangapi wanaamini CUF sio chama cha Waislaam au Wazanibar?..wamepewa majibu gani?.. maana ukweli ni kwamba CUF wenyewe hawana ngao, hawana majibu wala defence mechanism inayo onekana isipokuwa wao wenyewe wanajiingiza zaidi ktk ukimya.. Je ktk hali hiyo unafuu na credit zinakwenda wapi - CCM, uongo! I have done my study mkuu wangu na nakuhakikishia najua nilichokiandika..

Mkuu nimekupata vizuri. Naona hawataki kukubali changamoto unazowapa. Nadhani hawataki kukubali kuwa, popotte pale walipo, Wachagga wote ni pro CDM na hawajifichi kwa hilo na wako mstari wa mbele kuwashawishi non chagga kuwasupport. Mtu akijiuliza why chaggas atakuwa amekosea? Na kwa kuwa
most of all chaggas ni wakristo tena wa kweli , hoja ya anti muslim hata kama si yao, lakini shombo lake lazima liwapate. Hii ni kama ilivyokuwa kwa CUF. Ilikuwa ni rahisi kuwabrand udini kutokana na uhusiano wao wa karibu na Wapemba. Kwa hiyo ni vizuri wakaelewa kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo wanapaswa kukabiliana nazo.
 
Mhe.Mkandara;
Nimesoma andiko lako lote kwa utulivu mkubwa,Nimefuatilia michango yote ya wadau wengine na majibu yako kwao. Naomba kuikubali kwa namna ya kipekee michango ya Mr.Nicholas. Naelewa na kukubali kuwa umetumia muda mrefu sana kuandika uliyoandika. Kama kawaida ni lazima kuna kilichokusukuma hadi kuandika 'Waraka' huu. Nilichogundua ni kwamba ungependa ushauri wako uchukuliwe wote bila kuhojiwa au kuonyeshwa kuwa pengine ulichoandika kilishatekelezwa na chama kipo Imara kuelekea kuchukua dola 2015. Ukiwa na mawazo ya aina hiyo ni dhahiri kuwa unaweza ukakwazika kuishauri CHADEMA kama 'Alivyokwazika' Mr.Pasco. Chama chochote cha Siasa kina mikakati mipya kila siku. CHADEMA imekuwa na mikakati ya kila siku yenye mafanikio makubwa. Ukitaka kwenda kukabiliana na adui yako unapaswa kubeba silaha zako na si kusubiri yeye arushe mshale uudake na kuutumia kama silaha yako. Kauli za udini na ukabila kwangu mimi ni nyimbo za zamani zisizosikilizika tena! Ni nyimbo za Nape ambazo aliziimba zikakosa nafasi kwenye masikio ya wananchi. CHADEMA kama chama kukubali kuzibeba kauli hizo na kuhangaika kuzijibu ni kupoteza muda badala ya kuendelea na harakati za kujikita kujenga imani kwa wananchi waishio vijijini. Nitakuwa na hamu ya kuona majibu official kutoka kwa uliowalenga kwenye waraka huu (Kama wataona inafaa kujibu).
DF Mallya,
UDINI na UKABILA vipo. Kujifanya kwamba hatuvioni ni ujinga uliopitiliza. Jiulize maswali machache haya:
-Kwa nini KIONGOZI wa chama fulani cha SIASA anapokuwa dini au kabila fulani wafuasi wengi wa chama hicho wanakuwa wa dini au kabila la kiongozi wao?
-Moja ya vigezo vilivyotumika kumteua Pinda kuwa WAZIRI MKUU wetu ni DINI yake.
 
Unaweza kutupa asilimia ngapi? kutoka kanda tofauti kwenye uongozi na ubunge wa chadema.

Kwanza na wasiwasi na uelewa wako katika hesabu kwa ufupi CDM ina wabunge 3 wa kuchaguliwa kutoka mkoa wa K'manjaro Mbowe, Selasini na Ndesamburo waliobaki wamechaguliwa na kupitishwa na wananchi wa maeneo mengine. So compute 3 out 22 upate percentage. Ukiongelea akina Mdee utakuwa hauna akili kwani ni mbunge wa kawe ambapo wachaga hawafiki hata 10% kwa hiyo wanakawe walimpenda na kumpitisha na magamba wenu wakaachwa. Ningeeleza kwa kireft tatizo natumia simu. Ila cha muhimu Hao wabunge wote wamepata uhalali wa kisheria na kisiasa kuwapo walipo. Kuhusu viongozi angalia Mbowe, Arfi na composition ya makatibu wa chama. Wengine wataongezea.
 
Mkuu nimekupata vizuri. Naona hawataki kukubali changamoto unazowapa. Nadhani hawataki kukubali kuwa, popotte pale walipo, Wachagga wote ni pro CDM na hawajifichi kwa hilo na wako mstari wa mbele kuwashawishi non chagga kuwasupport. Mtu akijiuliza why chaggas atakuwa amekosea? Na kwa kuwa
most of all chaggas ni wakristo tena wa kweli , hoja ya anti muslim hata kama si yao, lakini shombo lake lazima liwapate. Hii ni kama ilivyokuwa kwa CUF. Ilikuwa ni rahisi kuwabrand udini kutokana na uhusiano wao wa karibu na Wapemba. Kwa hiyo ni vizuri wakaelewa kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo wanapaswa kukabiliana nazo.

Tatizo hata ukiwapa ushauri hawakubali. Kama nilivyosema, jana niliweka nyuzi humu, inayouliza maswala yanayofanana na haya, lakini kwa bahati mbaya kabisa wakaifuta ile nyuzi.

Unajuwa tolerance ya hizi dini haipatikani kama haijazungumzwa hususan kwenye hizi forums za kijamii, Utasikia mtu chadema hakuna udini lakini Waislaam tunasikia wakisema wanata wafikie "nchi ya ahadi", Tumeanza na Mungu tutamaliza na Mungu", tukiuliza, kama si wadini kwanini wasianze na Allah na Buddha na Mizimu na Krishna na Science. Wanashambulia hao, kila pembe. Tolerance lazima ioneshwe waziwazi kwa wa imani zote.

Bila hivyo nawaambia wazi, chadema kuchukuwa madaraka, ni ndoto za alinacha, watapata wabunge wachache na madiwani lakini uchaguzi mkuu, itakuwa kama CUF tu.
 
Mkuu siyo lazma ukopi uzi wote, wengine tunatumia vimeo vya mobile mnatuchosha bana

Umeniambia jambo zuri kwa kutumia maneno mabaya, kwani hukuwa na sababu ya kunilaumu, hunitendei haki unapotaka nizitumie mali zangu kama vile kwa ushirika na wengine.
mwisho kabisa umejaza dodoso refu kipengele cha maisha bora kwa kila mtanzania umesema "hakuna maisha bora kwa kila mtanzania" Andika bango liweke ndani kikinuka tu, unatoka nalo li-reflect ukata hadi kukulazimu kununua handset made by "gedanzuku"
 
Mkandara

Nimesoma na nimejaribu kukuelewa lakini nilivyoelewa mimi tatizo ni Image appeal ya CDM, na nitaandika bila kumumunya maneno.

Mwanzo ilikuwa rahisi kukiita CDM chama cha kikanda kwa ajili klilikuwa kina wabunge kutoka upande wa kaskazini, na hii ni kutokana na ukweli kwamba kiliapata wabunge wengi kutoka kaskazini kuliko upande wowote. Sasa hivi huwezi tena kukiita chama cha kaskazini kwa ajili kimejipambanua kwenye maeneo mbali mbali, kwa maana nyingine kinayo kinga (ngao) dhini ya hii shutuma.

Kwenye swala la udini CDM bado haina ngao, bado CDM kiitwa chama cha kiikristu kujitetea ni shida sana. Sana sana watakutajia ZZK kama CUF watakavyokutajia Mtatiro. Swali je viongozi wa CDM wanafanya juhudi gani kuhakikisha wanapenya mikoa yenye waislamu wengi?

kuna mchangiaji mmoja amemwambia Bob Mkandara kuwa anataka waislamu wapewe vyeo vya bure ndani ya CDM na amepinga kitu hicho, mimi nasema hivi kama kuna muislamu ambaye unadhani ana influence kubwa na anaweza kubring in many votes, na CDM wanaweza kumsajili basi wasisiste kumsajili na kumpa cheo. CDM needs support of the muslims more now than ever before.

CDM wasirudie kosa walilolifanya CUF, lakuitwa chama cha waislamu na kutofanya juhudi zozote za kuhakikisha wanapata wakristu wengi.

Kuna wakristu wengi humu JF wanapinga hichi kitu, lakini huu ni ukweli, muslim block ni kubwa na ina control votes nyingi TZ kama wakristu wanavo control. Ni wakati wa wote (christians & muslims) na sio sisi.

Jana CUF walijaza jangwani na ukiangalia waudhuriaji wengi kutokana na mavazi yao ni waislamu, what is CDM doing kuvutia hawa watu??

CDM needs to do more to appeal to muslim voters.
Nawakilisha
 
Last edited by a moderator:
DF Mallya,
UDINI na UKABILA vipo. Kujifanya kwamba hatuvioni ni ujinga uliopitiliza. Jiulize maswali machache haya:
-Kwa nini KIONGOZI wa chama fulani cha SIASA anapokuwa dini au kabila fulani wafuasi wengi wa chama hicho wanakuwa wa dini au kabila la kiongozi wao?
-Moja ya vigezo vilivyotumika kumteua Pinda kuwa WAZIRI MKUU wetu ni DINI yake.
Mkuu WildCard, hakuna kitu kizuri kama ukweli "truth", na kuukataa ukweli ambao upo ni "denial" lengo lake ni kujifariji kwa kujipa false hopes, realty ikikuumbua, unaishia kuwa frustrated!.

Kwa wale mliomsoma Hutaki Unaacha, alitumia kuhusu two sets of silent rule ya CCM kwa marais kupokezana kati ya bara na bara na visiwani, na kati ya Mkisto na Muislam!. Akimaanisha japo haikuandikwa popote, ilikuwa rais akitoka bara, anafuatia ni visiwani, then bara, then visiwani, akitoka Mkiristo, anafuatia Mwislamu etc. Hivyo, baada ya Nyerere -Mkisto(Bara), alikuja Mwinyi-Muislam (Visiwani), then Mkapa-Mkisto (Bara) na aliyemfuatia Mkapa ilitakiwa lazima awe Muislamu na atoke Visiwani!.

Kwa vile tayari mle mtandao wa hatari chini ya "the King Maker" ulishaundwa, hilo walilitambua na the next in line kumpokea Mkapa, alikuwa ni Dr. Omar, amini usiamini, he had to be eliminated silently ili ku create loop hole kuwa japo 2005 ni zamu ya Zanzibar, then ikajengwa hoja kuwa Zanzibar had no one, wengi mnakijua kilichompata Dr. Salim na shukrani za waliomshughulikia mnazijua!, hivyo JK akateuliwa as the only option kwa sababu ni Muslamu!. Hakuna ubishi mpaka leo, mpaka kesho, Dr. Salim would have made a beter president 100 times more than JK!. Hakuna ubishi Prof. Mwandosya would have made a better president 100 times more than JK!. Hakupigiwa kura kwa sababu ya ile silent code, "hawezi kutoka Mkapa Mkristu, akaingia Mwandosya Mkristu!, Na baada ya JK Muislamu, na bara tumefululiza, 2015 kwa CCM ilitakiwa iwe ni zamu Mkristo na ni zamu ya Zanzibar. Zilifanyika juhudi za Kumuelevate Brig. General Adam Mwakanjuki (RIP), watazama mbali hilo walisha liona na zamani walikwisha mshughulikia!.

Kihalali, kwa mujibu wa hiyo silent code ya CCM, zamu ya Zanzibar ndio imeshapita kwa kushikwa na JK na zamu ya Muislamu imeshapita, hivyo rule out Shein, rule out Dr. Asha Rose or Muislamu yoyote, game la 2015 ndani ya CCM lazima awe ni Mkristo!.

Ndani ya ukiristo nako kuna kiji secret silent code, kuwa zamu ya rais wa nchi hii kuwa Mkiristo, sio tuu kuwa ni Mkisto ili mradi ni Mkristo, bali Mkristo Mkatoliki!. Hivyo tangu JK anaingia, the 2nd most poweful na probale ni EL, tatizo yeye sii Mkatoliki!, akaundiwa zengwe akapigwa paranja!. 3 rd most powerful na probable ni Samwel Sitta tatizo yeye ni Muangalicana, kilichomkuta mnakijua hivyo the only one left kuteuliwa na CCM 2015 ni Membe, yeye ni Mkatiliki!.

Wa kwanza kuipinga hii secret silent code ni EL, haiwezekani kila rais Mkistu lazima awe Mkatoliki, akaambia huo ndio ukweli wa mambo, lakini kwa vile mkewe ni Mkatoliki, EL akashauriwa ili aweze kuteuliwa kugombea na kuchaguliwa kuwa ni rais wa nchi hii, lazima awe endorsed na Wakatoliki, ndio maana mmemshuhudia EL akijitoa kweli kweli kuchangia harambee za Makanisa ya Katoliki ili kupata hiyo endorsement!. Sitta is finished, just count him out!.

Wale wenye kumbukumbu, nawaombeni sana mlikumbuke bandiko hili, ingawa mimi namsuport EL ndie ateuliwe na CCM kwa sababu ni kupitia kwake, yeye ndiye mwenye uwezo wa kutupatia ukombozi wa pili na wa kweli wa Mtanzania, yale makosa mengine yote ya ufisadi ni mizigo tuu ya watu, ataitua kabla ya 2015, ila atakayeteuliwa ni Membe, sio kwa sababu ya kingine chochote, bali Ukatoliki wake na ndio maana huwezi kuwasikia Katoliki wengine wowote, Pinda, Magufuli etc wakiunusia urais!.

Udini upo, mkubali mkatae!, ila pia ukanda upo, na ukabila pia upo!.

Pasco.
 
Mkandara

Nimesoma na nimejaribu kukuelewa lakini nilivyoelewa mimi tatizo ni Image appeal ya CDM, na nitaandika bila kumumunya maneno.

Mwanzo ilikuwa rahisi kukiita CDM chama cha kikanda kwa ajili klilikuwa kina wabunge kutoka upande wa kaskazini, na hii ni kutokana na ukweli kwamba kiliapata wabunge wengi kutoka kaskazini kuliko upande wowote. Sasa hivi huwezi tena kukiita chama cha kaskazini kwa ajili kimejipambanua kwenye maeneo mbali mbali, kwa maana nyingine kinayo kinga (ngao) dhini ya hii shutuma.

Kwenye swala la udini CDM bado haina ngao, bado CDM kiitwa chama cha kiikristu kujitetea ni shida sana. Sana sana watakutajia ZZK kama CUF watakavyokutajia Mtatiro. Swali je viongozi wa CDM wanafanya juhudi gani kuhakikisha wanapenya mikoa yenye waislamu wengi?

kuna mchangiaji mmoja amemwambia Bob Mkandara kuwa anataka waislamu wapewe vyeo vya bure ndani ya CDM na amepinga kitu hicho, mimi nasema hivi kama kuna muislamu ambaye unadhani ana influence kubwa na anaweza kubring in many votes, na CDM wanaweza kumsajili basi wasisiste kumsajili na kumpa cheo. CDM needs support of the muslims more now than ever before.

CDM wasirudie kosa walilolifanya CUF, lakuitwa chama cha waislamu na kutofanya juhudi zozote za kuhakikisha wanapata wakristu wengi.

Kuna wakristu wengi humu JF wanapinga hichi kitu, lakini huu ni ukweli, muslim block ni kubwa na ina control votes nyingi TZ kama wakristu wanavo control. Ni wakati wa wote (christians & muslims) na sio sisi.

Jana CUF walijaza jangwani na ukiangalia waudhuriaji wengi kutokana na mavazi yao ni waislamu, what is CDM doing kuvutia hawa watu??

CDM needs to do more to appeal to muslim voters.
Nawakilisha
Mkuu Semilong, usemayo ni kweli tupu!.

Kwenye ile mada yangu ya CCM Imechokwa Chadema Haijajipanga, nimelizungumzia hili
Wanabodi,
Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu japo kipo juu, lakini bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa.
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.

Kwanza Freeman Mbowe, ajiuzulu uenyekiti, ampishe Dr. Slaa kwenye Usukani, Katibu Mkuu mpeni Zitto, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, ili Walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kuwapigia kura 2015.
Kiukweli, nilitukanwa sana, kuna wapenzi wa Chadema, wanawaabudu baadhi ya viongozi wao, hivyo ukiwaguza tuu, inaonekana kama ni kukufuru!. ZZK alipotaka kugombea uenyekiti kumpinga Mbowe, cha moto alikipata, kosa lake lilikuwa moja tuu, dini yake!. Profesa Safari alipojiunga Chadema, niliwaeleza huo ni mtaji!.

Hakuna ukombozi wa kweli pasipo kafara, lazima Chadema kikubali kutoa kafara baadhi ya nafasi zake za uongozi wa juu na kuwapa Waislamu. Nlishauri hata ikibidi kuwapa mahakama ya kadhi, wapeni, mbona Kenya na Uganda mahakama hizi zipo na hakuna any conflict of interest!.

Mkandara amefungua pandora box la udhaifu wa Chadema, naamini ni kupitia uzi huu Chadema lazima mkubali ukweli na kubadilika, vinginevyo 2015, ni CCM tena!, mimi na mgombea wangu EL tutapeta kiulaini na tutakutana tena humu kupeana pole!.

Pasco.
 
Pasco,
Shukrani sana kwa kulisasambua hilo. Tunatokaje kwenye UDINI ambalo sasa ndilo tatizo
na tishio kubwa kuliko yote. Hii SILENT CODE ya CCM walidhani ingewasaidia. Badala yake inageuka balaa kwao na NCHI yetu. Moja kati ya mambo ambayo Rais huyu wa sasa ameyasimamia kwa nguvu zake zote hasa kwenye TEUZI zake ni hii silent code. Karibu teuzi zake zote hata kwenye vyombo nyeti vya DOLA kaitumia code hii. Hivyo ndivyo ilivyo JWTZ, UwT, Police, Cabinet, maRC, maDC,..., imeshindikana tu BUNGENI ambako Spika na Naibu wake wote ni WAKRISTO.
TEUZI sasa hazizingatii kwanza UWEZO na WELEDI wa mteuliwa!
 
Mkuu Semilong, usemayo ni kweli tupu!.

Kwenye ile mada yangu ya CCM Imechokwa Chadema Haijajipanga, nimelizungumzia hili

Kiukweli, nilitukanwa sana, kuna wapenzi wa Chadema, wanawaabudu baadhi ya viongozi wao, hivyo ukiwaguza tuu, inaonekana kama ni kukufuru!. ZZK alipotaka kugombea uenyekiti kumpinga Mbowe, cha moto alikipata, kosa lake lilikuwa moja tuu, dini yake!. Profesa Safari alipojiunga Chadema, niliwaeleza huo ni mtaji!.

Hakuna ukombozi wa kweli pasipo kafara, lazima Chadema kikubali kutoa kafara baadhi ya nafasi zake za uongozi wa juu na kuwapa Waislamu. Nlishauri hata ikibidi kuwapa mahakama ya kadhi, wapeni, mbona Kenya na Uganda mahakama hizi zipo na hakuna any conflict of interest!.

Mkandara amefungua pandora box la udhaifu wa Chadema, naamini ni kupitia uzi huu Chadema lazima mkubali ukweli na kubadilika, vinginevyo 2015, ni CCM tena!, mimi na mgombea wangu EL tutapeta kiulaini na tutakutana tena humu kupeana pole!.

Pasco.
Pasco, hivi hawa CDM mbona mnawapa ushauri (consultancy) ya thamani kubwa bila kuwacharge chochote? Mnawapendea nini hawa? au mpaka watakapoteua IGP awapige virungu ndio mtajua kuwa hawa watu hawafai!!! Chondechonde huu ushauri mnaotoa usije kuwatokea puani siku moja. Hao waacheni na kiburi chao waendelee kuwa chama cha maandamano, dola hawaiwezi hao watatuharibia nchi...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Semilong, usemayo ni kweli tupu!.

Kwenye ile mada yangu ya CCM Imechokwa Chadema Haijajipanga, nimelizungumzia hili

Kiukweli, nilitukanwa sana, kuna wapenzi wa Chadema, wanawaabudu baadhi ya viongozi wao, hivyo ukiwaguza tuu, inaonekana kama ni kukufuru!. ZZK alipotaka kugombea uenyekiti kumpinga Mbowe, cha moto alikipata, kosa lake lilikuwa moja tuu, dini yake!. Profesa Safari alipojiunga Chadema, niliwaeleza huo ni mtaji!.

Hakuna ukombozi wa kweli pasipo kafara, lazima Chadema kikubali kutoa kafara baadhi ya nafasi zake za uongozi wa juu na kuwapa Waislamu. Nlishauri hata ikibidi kuwapa mahakama ya kadhi, wapeni, mbona Kenya na Uganda mahakama hizi zipo na hakuna any conflict of interest!.

Mkandara amefungua pandora box la udhaifu wa Chadema, naamini ni kupitia uzi huu Chadema lazima mkubali ukweli na kubadilika, vinginevyo 2015, ni CCM tena!, mimi na mgombea wangu EL tutapeta kiulaini na tutakutana tena humu kupeana pole!.

Pasco.
CHADEMA hata wamteue Ponda Issa Ponda kuwa Mwenyekiti na mgombea wao wa URAIS hakuna atakayewaondolea doa hili. Walichelewa kuing'amua ile SILENT CODE ya CCM nao waitumie au waipigie kelele waziwazi. Ni kama ambavyo CUF hawawezi kuuvua UISLAAM hata kama Askofu Kilaini angeteuliwa kuwa Mwenyekiti wao.
Tuanze mkakati wa kusema wazi kuhusu UDINI nchi hii. Tunakoelekea kugumu.
 
Mkuu WildCard, hakuna kitu kizuri kama ukweli "truth", na kuukataa ukweli ambao upo ni "denial" lengo lake ni kujifariji kwa kujipa false hopes, realty ikikuumbua, unaishia kuwa frustrated!.

Kwa wale mliomsoma Hutaki Unaacha, alitumia kuhusu two sets of silent rule ya CCM kwa marais kupokezana kati ya bara na bara na visiwani, na kati ya Mkisto na Muislam!. Akimaanisha japo haikuandikwa popote, ilikuwa rais akitoka bara, anafuatia ni visiwani, then bara, then visiwani, akitoka Mkiristo, anafuatia Mwislamu etc. Hivyo, baada ya Nyerere -Mkisto(Bara), alikuja Mwinyi-Muislam (Visiwani), then Mkapa-Mkisto (Bara) na aliyemfuatia Mkapa ilitakiwa lazima awe Muislamu na atoke Visiwani!.

Kwa vile tayari mle mtandao wa hatari chini ya "the King Maker" ulishaundwa, hilo walilitambua na the next in line kumpokea Mkapa, alikuwa ni Dr. Omar, amini usiamini, he had to be eliminated silently ili ku create loop hole kuwa japo 2005 ni zamu ya Zanzibar, then ikajengwa hoja kuwa Zanzibar had no one, wengi mnakijua kilichompata Dr. Salim na shukrani za waliomshughulikia mnazijua!, hivyo JK akateuliwa as the only option kwa sababu ni Muslamu!. Hakuna ubishi mpaka leo, mpaka kesho, Dr. Salim would have made a beter president 100 times more than JK!. Hakuna ubishi Prof. Mwandosya would have made a better president 100 times more than JK!. Hakupigiwa kura kwa sababu ya ile silent code, "hawezi kutoka Mkapa Mkristu, akaingia Mwandosya Mkristu!, Na baada ya JK Muislamu, na bara tumefululiza, 2015 kwa CCM ilitakiwa iwe ni zamu Mkristo na ni zamu ya Zanzibar. Zilifanyika juhudi za Kumuelevate Brig. General Adam Mwakanjuki (RIP), watazama mbali hilo walisha liona na zamani walikwisha mshughulikia!.

Kihalali, kwa mujibu wa hiyo silent code ya CCM, zamu ya Zanzibar ndio imeshapita kwa kushikwa na JK na zamu ya Muislamu imeshapita, hivyo rule out Shein, rule out Dr. Asha Rose or Muislamu yoyote, game la 2015 ndani ya CCM lazima awe ni Mkristo!.

Ndani ya ukiristo nako kuna kiji secret silent code, kuwa zamu ya rais wa nchi hii kuwa Mkiristo, sio tuu kuwa ni Mkisto ili mradi ni Mkristo, bali Mkristo Mkatoliki!. Hivyo tangu JK anaingia, the 2nd most poweful na probale ni EL, tatizo yeye sii Mkatoliki!, akaundiwa zengwe akapigwa paranja!. 3 rd most powerful na probable ni Samwel Sitta tatizo yeye ni Muangalicana, kilichomkuta mnakijua hivyo the only one left kuteuliwa na CCM 2015 ni Membe, yeye ni Mkatiliki!.

Wa kwanza kuipinga hii secret silent code ni EL, haiwezekani kila rais Mkistu lazima awe Mkatoliki, akaambia huo ndio ukweli wa mambo, lakini kwa vile mkewe ni Mkatoliki, EL akashauriwa ili aweze kuteuliwa kugombea na kuchaguliwa kuwa ni rais wa nchi hii, lazima awe endorsed na Wakatoliki, ndio maana mmemshuhudia EL akijitoa kweli kweli kuchangia harambee za Makanisa ya Katoliki ili kupata hiyo endorsement!. Sitta is finished, just count him out!.

Wale wenye kumbukumbu, nawaombeni sana mlikumbuke bandiko hili, ingawa mimi namsuport EL ndie ateuliwe na CCM kwa sababu ni kupitia kwake, yeye ndiye mwenye uwezo wa kutupatia ukombozi wa pili na wa kweli wa Mtanzania, yale makosa mengine yote ya ufisadi ni mizigo tuu ya watu, ataitua kabla ya 2015, ila atakayeteuliwa ni Membe, sio kwa sababu ya kingine chochote, bali Ukatoliki wake na ndio maana huwezi kuwasikia Katoliki wengine wowote, Pinda, Magufuli etc wakiunusia urais!.

Udini upo, mkubali mkatae!, ila pia ukanda upo, na ukabila pia upo!.

Pasco.

Paco, kwanini umeniwahi na kunukuu yale nilotaka kusema. Huo ndio ukweli nami nitakuwa shahidi wako Januari 2016 wakati wakatoliki watakapoiacha CDM kwenye mataa na kuinyanyua CCM mgombea akiwa Membe. Kaeni mikijua madhehebu mengine ya kikiristo hufuata upepo wa maamuzi ya wakatoliki kwa mfano waraka wa kanisa katoliki, madhehebu yote waliupigia upatu na hata CDM wamepata nguvu 2010 kwa sababu ya uungwaji mkono na kanisa katoliki(Slaa)"HUTAKI UNAACHA". Kumbukeni askofu Kilaini na maneno ya JK ni chaguo la Mungu.
 
Hongera sana kwakutoa ushauri mzuri kwa chma kuelekea 2015,nami niseme tu waraka huu kwa kiasi kikubwa ulilenga kutoa ujumbe kuhusu propaganda za udini,ukabila,ukanda dhidi ya chadema na tuseme ukweli tu viongozi wetu wamekuwa wakipambana na hizi propaganda kila leo na jukumu hili tusiiwaachie viongozi peke yao hata mimi nawewe wenye mapenzi na cdm tunapaswa kupambana na hili jambo tuwe chachu ya mabadiliko kimtazamo kuanzia humu jamvini na huko uraini.

Mimi nawewe tuwe chachu katika kuwaunganisha watanzania wote kuelekea 2015,tuwarahisishie kazi viongozi kwa kupambana na hizi propaganda kwa vitendo,tujenge umoja,mshikamano bila kujali tofauti zetu ili kuifanya safari ya ukombozi kuwa rahisi.

Kamwe tusikubali kumuunga mkono mtu kwa sababu ya dini au kabila lake,bali mtu mwenye dhamira ya dhati kuleta maendeleo na ukombozi kwa watanzania wote bila kujali tofauti zao tuungane nae kwenye ukombozi wa taifa letu.

UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU
 
Ndg Mkandara ulicho kieleza ni sahihi kabisa kuna watu wanajaribu kutaka kulikwepesha hilo,suala la Chadema kuhusishwa na Ukristo hilo lipo sana kwa wauimini wa dini ya Kiisilaam ,wengi wa washabiki wa Chadema (sio wote)wana kebehi sana Waislam na Uislam,inaweza kuwa ni utashi wa mtu binafsi wala sio msimamo wa chama lakini haijapta kutokea kiongozi yeyote wa chama hicho kuja kukemea au kukanusha ya kuwa hawa wanaojiita washabiki au wafuasi wa chadema hizo kejeli na dhihaka wana zao zitoa hapa JF ni misimamo ya watu binafsi wala sio za chama ,Lakini hakuna hata siku mmoja statement yeyote imewahi kutolewa na chadema.

Kingine Chadema nao wanalijua ya kuwa wengi wa waumini wa dini ya kiislam hawawaungi mkono chadema wanalijua sana wana viongozi wenye weledi na upeo mkubwa sana tu katika kuchambua hilo.lakini kuna wakati wanajaribu kulikuwepa ,kutoa mfano ya kuwa pia wao wana viongozi wa ngazi za juu waumini wa dini ya kiislam haitoshi kukifanya chama hicho kunasibishwa na Ukristo.

Hivi jamani tuwe wakweli kabisa kama kutakuwa na kuchambua wanachama na washabiki wa chadema kama wataulizwa imani zao hao wanachama na wafuasi wa chadema asilimia ngapi watakuwa waimuni dini ya Kikristo na asilimia ngapi watakuwa Waisilam?Tuanzie hapo,na kama watakuwa nusu kwa nusu then tunaweza tambua hiki sio chama chenye kufuatwa na waumini wa dini fulani,na kama chama kina wafuasi wengi wenye dini moja kwa nini imekuwa hivyo na nini kifanyike ku balance.
Kisiasa huwezi sema utafute wafuasi au wanachama makanisani na misikitini lakini tutambue hao wana swali makanisani ana misikitini pia ni hao hao amabo pia wanakuwepo mitaani na maeneo mengine,hivi leo hii uende miskitini au uwalize waumini karibu misikitini yote Tanzania ni wangapi wana support Chadema?Jibu utapata wachache sana !
Mie navyo itazama hali hii endapo chadema watacheza vibaya karata yao hii kwa waislaam sidhani kama wataweza fanikiwa kutwaa dola!
 
Paco, kwanini umeniwahi na kunukuu yale nilotaka kusema. Huo ndio ukweli nami nitakuwa shahidi wako Januari 2016 wakati wakatoliki watakapoiacha CDM kwenye mataa na kuinyanyua CCM mgombea akiwa Membe. Kaeni mikijua madhehebu mengine ya kikiristo hufuata upepo wa maamuzi ya wakatoliki kwa mfano waraka wa kanisa katoliki, madhehebu yote waliupigia upatu na hata CDM wamepata nguvu 2010 kwa sababu ya uungwaji mkono na kanisa katoliki(Slaa)"HUTAKI UNAACHA". Kumbukeni askofu Kilaini na maneno ya JK ni chaguo la Mungu.

Naomba nikusaidie tu for your information pamoja na hizo secreat code zenu safari hii game litagoma kucheza na kwataarifa yako kwasababu moja ama nyingine wakatoliki hawawezi ku-risk kumpa Membe kuwa Rais wa nchi hii pamoja na kuwa anajitahidi sana ku cover hiz true colours na hiki ndicho hasa ninawaambia CDM has a better future maana hizo secreat code zote zina mwangukia mtu mmoja tu ....Ukweli ni kuwa wazalendo watagundua hili na watajaribu ku-rescue na bado watakuwa wamechelewa na hivyo there is no way CCM itasimama this time na hatari ni kuwa haitakubali kirahisi rahisi so tujiandae tu maana mwisho wataamua kuvuruga kila kitu japo wazalendo pia wataingilia kati na kusaidia vurugu za hao walafi hazisababishi impact kubwa....Watch and see!
 
Kule marekani kwa wenzetu kuna Democrats na Republicans halafu kuna majority ambao hupiga kura wao kwa kusiliza sera tu na kuona rais ajae atafanya nini kwenye mambo ya kiuchumi kama vile swala la ajira . Naamini hata hapa kwetu Tanzania tunao wengi ambao sio wanachama wa chama chochote na hawa wa kwetu hawana hata mpango wa kupiga kura. Na hapa ndio kwenye siri ya ushindi.
 
Back
Top Bottom