Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Kuna mengi nakubaliana na waraka huu ila hili la kuangalia na kumlazimisha kuwa mtanzania huyu ni wa dini hii au ile hilo lina utata.

Kugawana keki ya taifa n.k kungetumia kikokotoo cha kanda maana kutumia imani bado imani fulani itazidiwa wingi na kuleta mgawanyiko ktk taifa, jamii na familia ila kuangazia kanda inafuta mgawanyiko kwa kufuata imani.
 
Asiwe Kibri, Dikteta Mkandamizaji na Mdhalilishaji wa watu anaowaongoza.
Asiwe mtu mwenye kujali maslahi yake na kundi lake sambamba na kufikiria sheria za kujilinda
dhidi ya mkondo wa sheria kwa tuhuma za ufisadi na uvunjaji wa Haki za Binadamu.
Ukisikia spirit kwenye kidonda kibichi ndio hii.
 
Kuna mengi nakubaliana na waraka huu ila hili la kuangalia na kumlazimisha kuwa mtanzania huyu ni wa dini hii au ile hilo lina utata.

Kugawana keki ya taifa n.k kungetumia kikokotoo cha kanda maana kutumia imani bado imani fulani itazidiwa wingi na kuleta mgawanyiko ktk taifa, jamii na familia ila kuangazia kanda inafuta mgawanyiko kwa kufuata imani.
Hakuna kigezo cha ukanda , ukabila wala udini.
Vigezo viwe kwenye sifa (merits) za muombaji kama elimu, uzoefu, uadilifu, uchapakazi, n.k.
 
Imeandikwa kitaalam sana.
Jamaa nimewakubali sana. Kesho kile kikosi kinamtafuta Katibu na Secretary aliyedrafti hii kitu. Ni wajanja sana hawawezi kuwakatamata wote waliohusika watakachofanya ni devide and rule. Hapa utakiskia aliyekuwa mjumbe na katibu wa shura ya maimamu tanzania akamatwa na Takukuru nyumbani kwake.😆😆😆
 
Hakuna kigezo cha ukanda , ukabila wala udini.
Vigezo viwe kwenye sifa (merits) za muombaji kama elimu, uzoefu, uadilifu, uchapakazi, n.k.
Titi...
Tutafanyaje inapokuwa waumini wa dini moja tu ndiyo wanakuwa na sifa za elimu, uxoefu, uadilifu, uchapakazi nk. kwa hiyo ndiyo wanaoongoza serikali na wengine wako nje?

Katika hali kama hii tunafanyaje?
 
Naona umeng"ang'ania kihoja hicho tu. Je huyaoni mengine muhimu waliyo analyze??
Mimi nimechagua kujadili na kuchagia hoja hiyo tu kwa sasa, nimetumia uhuru wangu wa maoni kama walivyotumia hawa Shura ya Maimamu.
Nawewe tumia uhuru wako kujadili hizo zingine unazotaka nijadili mimi.

Au nimekosea kuchangia maoni yangu? Ulitakiwa ujiulize kwanini sijalaani maoni yao kabla ya kunilazimisha nichangie kitu ambacho sijapenda kuchangia.

Tusilazimishane hoja za kujadili bali tuachiane uhuru wa maoni ilimradi tusivunje sheria au haki za wengine.
 
Titi...
Tutafanyaje inapokuwa waumini wa dini moja tu ndiyo wanakuwa na sifa za elimu, uxoefu, uadilifu, uchapakazi nk. kwa hiyo ndiyo wanaoongoza serikali na wengine wako nje?

Katika hali kama hii tunafanyaje?
Na wa dini za Buddhism, Hinduism, wapagani walistahili wawepo wote kwenye teuzi kwa uwiano sawa na wakrito na waislam.
Makundi hayo mengine ambayo maimamu hawakuyajumuisha kwenye takwimu zao nayo yamo humu nchini kwetu.
 
Na wa dini za Buddhism , Hinduism, wapagani walistahili wawepo wote kwenye teuzi kwa uwiano sawa na wakrito na waislam.
Makundi hayo mengine ambayo maimamu hawakuyajumuisha kwenye takwimu zao nayo yamo humu nchini kwetu.
Titi...
Huwezi kufananisha historia ya Waislam na kundi lolote labda ikiwa unataka kuchekesha watu.

Unaweza kuanza kujifunza kwa kusoma kitabu cha Abdul Sykes (1998).
 
Hao toka lini waliongoza nchi?
Wanachotaka hawa Maimamu ni usawa katika kugawana keki ya taifa. Usawa kwa kila kitu kwa raia wote.

Hoja yao siyo dini fulani tu washikie fursa zaidi ya waumini wa dini zingine au wasiokuwa na dini.
Sijui wewe umewaelewaje? labda unifafanulie walikuwa wanakusudia kusema nini hapo kwenye teuzi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom