Wananchi: Maridhiano ni Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,159
22,662
Salaam ,shalom!!

Ni Kweli homa ya Uchaguzi imepanda, wengine wameanza kuacha kuongoza vyama na kukimbilia kuanza maandalizi ya kugombea ubunge nk nk.

Wananchi hatufurahii urafiki kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, maslah ya Wananchi yapo katika kutofautiana Kwa HOJA kuongeza Kasi ya maendeleo.

Tunasikia habari ya nusu mkate, kugawana vyeo, hiyo nusu mkate kugawana vyeo itasaidia vp

1. Kuondoa tatizo la mgao wa umeme nchini?

2. Nusu mkate, Itaondoa vp mfumuko wa bidhaa nchini?,

3. Nusu mkate, Itaondoa vp RUSHWA?,

4. Nusu mkate, Itaondoa vp urasimu kupata huduma mahospitalini?

5. Nusu mkate itasaidia vipi kulinda raslimali za nchi yetu?

6. Nusu mkate itasaidia vp kupatikana Kwa pesa kulipa mikopo na riba?

7. Nusu mkate itapunguza vipi pengo kubwa kati ya maskini na matajiri nchini?

8. Nusu mkate itasaidia vipi kupunguza ukubwa wa Serikali Kwa kupunguza gharama za uendeshaji serikalini, kupunguza idadi ya wabunge na baraza la mawaziri?

9. Nusu mkate, itasaidia Kwa kiasi Gani kuondoa watoto wanaorandaranda mitaani bila uangalizi wowote?

10. Kugawana majimbo kati ya CCM na upinzani kutachangia vipi kupunguza lindi la Umaskini Kwa wananchi maskini?

Wanasiasa jitahidini kuongea lugha ya wananchi tutaelewana.

ANGALIZO: Maridhiano ni kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Kheri ya mwaka mpya 2024, yajayo yanafikirisha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.
 
Wengi huwa wanapigania vyeo, nusu mkate, tumbo ila sioni nia ya dhati kupigania katiba mpya, tume huru, maslahi ya taifa.
 
Wananchi hawataki makaratasi, wanataka maendeleo
Ndo tunataka ukubwa wa Serikali upungue, baraza la mawaziri liwe dogo,

RUSHWA na wizi wa Mali ya umma utokomezwe!!

Maendeleo yatapatikana vp ikiwa Kodi zote zitaenda kuhudumia Serikali na kununua WAPINZANI Uchwara?
 
Kimeongeza mzigo kwa walipa kodi, sawa na Makamu wa Rais.
Sasa kupeana vyeo wanaona ndiyo maendeleo,

Wananchi tunaogharimia viongozi Kwa Kodi zetu ndo tunaona solution ni Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote Ili kupunguza Mzigo.

Uroho wa madaraka wa wanasiasa unatukwamisha wananchi.
 
Tanzania ni Nchi yetu, wanasiasa jueni kuwa Mungu anatawala Serikali zote za Dunia.

Hajikisheni wananchi waliowapa ridhaa wanatendewa HAKI na sauti zao zinasikizwa.

Aaamen
 
Salaam ,shalom!!

Ni Kweli homa ya Uchaguzi imepanda, wengine wameanza kuacha kuongoza vyama na kukimbilia kuanza maandalizi ya kugombea ubunge nk nk.

Wananchi hatufurahii urafiki kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, maslah ya Wananchi yapo katika kutofautiana Kwa HOJA kuongeza Kasi ya maendeleo.

Tunasikia habari ya nusu mkate, kugawana vyeo, hiyo nusu mkate kugawana vyeo itasaidia vp

1. Kuondoa tatizo la mgao wa umeme nchini?

2. Nusu mkate, Itaondoa vp mfumuko wa bidhaa nchini?,

3. Nusu mkate, Itaondoa vp RUSHWA?,

4. Nusu mkate, Itaondoa vp urasimu kupata huduma mahospitalini?

5. Nusu mkate itasaidia vipi kulinda raslimali za nchi yetu?

6. Nusu mkate itasaidia vp kupatikana Kwa pesa kulipa mikopo na riba?

7. Nusu mkate itapunguza vipi pengo kubwa kati ya maskini na matajiri nchini?

8. Nusu mkate itasaidia vipi kupunguza ukubwa wa Serikali Kwa kupunguza gharama za uendeshaji serikalini, kupunguza idadi ya wabunge na baraza la mawaziri?

9. Nusu mkate, itasaidia Kwa kiasi Gani kuondoa watoto wanaorandaranda mitaani bila uangalizi wowote?

10. Kugawana majimbo kati ya CCM na upinzani kutachangia vipi kupunguza lindi la Umaskini Kwa wananchi maskini?

Wanasiasa jitahidini kuongea lugha ya wananchi tutaelewana.

ANGALIZO: Maridhiano ni kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Kheri ya mwaka mpya 2024, yajayo yanafikirisha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.
Naomba ufafanuzi kidogo kuhusu nusu mkate, umegusa mambo ya msingi sana.
Tuielewe hii hoja ya nusu mkate kwa mapana na marefu.
 
Nusu mkate ni kutwambia wananchi tusubiri kwanza uchaguzi upite ndipo tuendelee na mchakato wa KATIBA mpya!!

Yaani Kwa wanasiasa kugawana majimbo kwao ni muhimu kuliko Katiba mpya inayoangazia maoni ya wananchi katika makundi mbalimbali ya wavuvi, wakulima, wafanyabiashara nk nk.

Unakubali kundi dogo la wanasiasa kuteka mchakato wa KATIBA mpya?
 
Wakati wananchi tunadai Katiba mpya Ili kupunguza idadi ya majimbo yawe machache kupunguza Mzigo wa wananchi kugharamia Serikali,

Pale Mbeya na maeneo mengine wanapanga kugawanya majimbo Ili Kila Mmoja apate cake yake!!

Kugawanya majimbo, kunapunguza Umaskini wa Watanzania Kwa kiasi Gani zaidi ya kuiongeza?

Unakubaliana na mambo hayo?
 
Nusu mkate ni kutwambia wananchi tusubiri kwanza uchaguzi upite ndipo tuendelee na mchakato wa KATIBA mpya!!

Yaani Kwa wanasiasa kugawana majimbo kwao ni muhimu kuliko Katiba mpya inayoangazia maoni ya wananchi katika makundi mbalimbali ya wavuvi, wakulima, wafanyabiashara nk nk.

Unakubali kundi dogo la wanasiasa kuteka mchakato wa KATIBA mpya?
Katiba mpya ni muhimu kwa mustakabali mwema wa taifa.
Wapinzanzani kukosa katiba mpya siyo nusu mkate bali kuukosa kabisa.
Twende kwenye ufafanuzi wa kugawana majimbo (labda hapo ndipo nusu mkate yaweza kupata kueleweka).
Je kuna namna yoyote wanasiasa wamekubaliana kugawana majimbo? (haya ni matusi kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom