Elections 2010 Waraka wa Lowassa kwa vyombo vya habari

Amani hii imetumika kututia hofu ya kutosema ukweli na kutodai haki zetu........ Tufikiri kwa undani nini maana ya amani na tujifunze kutoa haki kwa yule anayestahili kwa moyo mweupe
 
Ok,

Lowassa; huyu Slaa karopoka. Naomba uliambie taifa, ni kauli gani ulitoa siku ile ulipokatiwa matangazo na TBC1? Nakumbuka ulianza kupanda mori na ukaonekana ulikuwa unaanza kumlenga JK moja kwa moja, unaweza kutueleza siri nyuma ya pazia?

Inapendeza mnaanza kuja public hivi!
Kamanda.... CCM umekua mnara wa babeli, kila mmoja anazungumza kivyake na dhambi yao imefika dead end, we subiri before June 2011 utaona mengi

Nadhani umenielewa
 
very stupid.. eti anasema mwalimu alituachia amani ambayo ni tunu la taifa hili....! amani ipi anayoiongelea huyo morani mzee? amani nchi hii imechakachuliwa! hamna amani tena hii nchi, kama mnapanga matokeo na kukataa maamuzi ya wananchi kuna amani hapo?

naskia anajipanga kupokea kijiti 2015!
 
Hiyo ni mbinu ya kukwepa ukweli.

Ukweli ni kwamba CCM inajua kuwa kile inachokitaka ndicho itakachopata na ndiyo maana haigopeshwi na kura halali zinazopigwa na Watanzania kwani inajua itazichakachua.

Kauli kama hii ya kipuuzi ilisemwa na Mkapa siku chache kuwa hata mwaka 1995 Mrema alipata mahudhurio makubwa lakini kura kdiogo. Wanajua kuwa walimuibia na kwani wana uwezo huo. CCM kukataa demokrasia ya kweli ni kama mtu kuhairisha kwenda haja!

Na watafanya kila njia waendelee kuwa madarakani. Kama uchakachuaji ukishindikana nina wasiwasi watu hawa wanaweza hata kutumia nguvu ya jeshi kutawala!!!
 
Mie nadhani ndugu Lowasa angeuliza kwa nini Ndugu Kabwe,msimamizi wa uchaguzi Jiji la Mwanza, katika barua aliyoindika, kuisaini na kuisambaza, aliwataja watu ambao HAWAKUHUDHURIA kikao! Alimaamisha nini? Pili, maudhui ya barua yenyewe yanawahusu waliotajwa? Tatu, hawa wanaokanusha, mbona hawakatai/hawakanushi MAUDHUI ya barua inayotajwa na ndugu Slaa (tamka TLAA)? Asanteni.
 
Sasa si amlaumu mtoa taarifa...yule aliyesaini barua ile ya Mwanza City Council? Dr SI alireje tu hiyo barua?Kosa liko wapi
 
Kama Lowassa hakutaka kumsaidia mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini alieangukia pua,alifata nini kwenye ofisi za manispaa tar 1 Nov? Lowassa aache mambo ya kitoto
 
wote wanakana kutokuwepo,lakini hawakani kama mkutano ulifanyika ama la.basi mmoja wao ajitokeze aseme hata mkutano haukuwepo siku hiyo kwenye hiyo hotel.
 
Huyu jamaaa anafikiri watu tunampenda anakuja na utetezi. Yeye ni mwizi tuu na ukweli huo haupingiki /Andhani ss ni mis*****nge **nge tu .Arusha aliingia Manispaa wakati wananchi wanadai matokeo wakiimba ....hiyo miiiimba , ni ya Lowasa . Labda hakusikia. Nyoo
 
Ok,

Lowassa; huyu Slaa karopoka. Naomba uliambie taifa, ni kauli gani ulitoa siku ile ulipokatiwa matangazo na TBC1? Nakumbuka ulianza kupanda mori na ukaonekana ulikuwa unaanza kumlenga JK moja kwa moja, unaweza kutueleza siri nyuma ya pazia?

Inapendeza mnaanza kuja public hivi!
Invisible tell us pleeeaaasee, aliropoka nini??
 
Ok,

Lowassa; huyu Slaa karopoka. Naomba uliambie taifa, ni kauli gani ulitoa siku ile ulipokatiwa matangazo na TBC1? Nakumbuka ulianza kupanda mori na ukaonekana ulikuwa unaanza kumlenga JK moja kwa moja, unaweza kutueleza siri nyuma ya pazia?

Inapendeza mnaanza kuja public hivi!
dah. mkuu sikuwezi kwa kumbukumbu.
mie nimejiinamia pembeni naangalia mambo yanavyokwenda. wakishamuapisha jeikei tujue kuwa maisha bora ni kwaheri baibai
 
Mwisho, namsihi Dk. Slaa ajipe muda wa kuzifahamu vyema siasa za nchi hii. Asidanganywe na mahudhurio ya mikutano ya hadhara akadhani ndizo kura katika masanduku ya kupigia kura. Namsihi ajifunze` zaidi jinsi ya kufanya siasa za kistaarabu bila kueneza uvumi, uongo, chuki na uzushi vyenye kutetelesha amani ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.
Hapo Lowasa umenena kwa vile ccm mnajua kuwa kura zinapigiwa kwenye offisi za ccm na upanga cvu. Hongera kwa vile utakuwa waziri mkuu na chenge kuwa spika ili mdhibiti wanaotaka kuchakachua ufisadi weni. Kumbuka kilio cha watanzania wengi wanaoteseka kwa sababu ya hujma zenu na hao wahindi mnaowaibia wananchi huku nyie mkiendelea kujinafasi. Kwa sasa watoto wako watahamia UK kuangalia mpira wa arsenal huku watanzania wakifa kwa maradhi, ujinga na umaskini wa kutupwa. siku zenu zinahesabika.
 
TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI NOVEMBA 5, 2010
Novemba 3, 2010 mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa aliwatuhumu makada 30 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa walifanya kikao cha kupanga mipango ya kumwibia kura mjini Mwanza. Kati ya makada aliowatuhumu ni pamoja na mimi.

Napenda kuufahamisha umma kuwa habari hizi si za kweli kwa sababu mwezi wote wa Oktoba, nilikuwa jimboni kwangu nikifanya kampeni za kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Monduli. Sikupata kusafiri kwenda Mwanza hata siku moja, na siku aliyoitaja ya Oktoba 19, nilikuwa katika vijiji vya Mfereji na Enguiki nikifanya kampeni siku nzima.

Ukiacha tuhuma hizo, pia upo uvumi uliosambazwa kwamba nilishiriki kikao cha mikakati ya kuchakachua kura, mjini Arusha kumsaidia mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Batilda Burian aweze kushinda kiti hicho. Nasema uvumi huu ni uzushi na si wa kweli.

Kutokana na yote haya, ninakwazika kwamba inaonekana katika nchi yetu umeanza kuingia utamaduni mpya wa kufanya siasa za uongo, uvumi, uzushi na kila aina ya hila kwa nia ya kujipatia ushindi. Kwa uzoefu wa mataifa mengi yaliyotuzunguka, ndani ya Afrika na sehemu nyingine duniani, amani hupotea kutokana usambazaji wa taarifa za uongo.

Mwasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alituachia amani na utulivu ambavyo ni tunu ya taifa hili.

Dalili zinazoonekana, kuna watu wanaelekea kuchoshwa na amani iliyopo.

Wanajiandaa kufanya vurugu, kuliingiza taifa hili katika machafuko, na sijui wanafanya hivyo kwa faida ya nani.

Wito wangu kwa Watanzania, ni kwamba tusiichoke amani. Amani tuliyonayo ndiyo imetutofautisha na mataifa mengi yaliyotuzunguka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kupigiwa mfano. Tuelekeze nguvu zetu katika shughuli halali za kutuletea kipato zisizoharibu amani yetu.

Tukiiharibu amani tuliyonayo, mwisho wa siku nchi yetu itateketea na sote hatutakuwa salama. Tutakuwa tumekwisha.

Mwisho, namsihi Dk. Slaa ajipe muda wa kuzifahamu vyema siasa za nchi hii. Asidanganywe na mahudhurio ya mikutano ya hadhara akadhani ndizo kura katika masanduku ya kupigia kura. Namsihi ajifunze` zaidi jinsi ya kufanya siasa za kistaarabu bila kueneza uvumi, uongo, chuki na uzushi vyenye kutetelesha amani ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.
Edward Lowassa
Mbunge Mteule wa Monduli




MTAZAMO WANGU KAMA HAKUHUSIKA KWANINI ASEME LOLOTE SI BORA ANGEKAA KIMYA? WEZI WAKUBWA HAWA NA WANAFIKI
 
mwasisi wa taifa hili, baba wa taifa, mwalimu julius kambarage nyerere, alituachia amani na utulivu ambavyo ni tunu ya taifa hili.
amani na utulivu vilikuwepo kwa sababu gap kati ya viongozi na wananchi halikuwa kubwa sana kama kiongozi lowassa na wananchi, hakika hawakuwepo mafisadi papa kama lower hasa
 
Hivi kwa nini wanahangaika kukanusha aliyosema Slaa? Dr Slaa alisoma barua tu iliyosainiwa na Kabwe na Kabwe anakiri sahihi ni yake isipokuwa si yeye aliyeiandika!!! Wanatakiwa wamuulize vizuri Kabwe sio kukimbilia kwa wananchi. Wameshikwa pabaya na sasa wanahaha
 
Huyu Fisadi anafikiri watu wote ni wajinga?

Cha msingi LOWASSA muogope MUNGU na Tambua ,,,mwisho wako hautakuwa mzuri kihivyo hata kama unahizo pesa za wizi
 
HIVI KWA NINI KILA ANAEGUSWA KUHUSU UTENDAJI WAKE ANAKIMBILIA KUSEMA """MSINIGUSE MKIFANYA HIVYO MTAHATARISHA AMANI YA NNCHI?????"""".....SWALA LA AMANI SASA LIMEKUWA KAMA NDO FICHO LA KILA ANAEKURUPUSHWA KWA UOZO WAKE....INACHEFUA SANA!!!!:A S angry:
 
TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI NOVEMBA 5, 2010


Mwisho, namsihi Dk. Slaa ajipe muda wa kuzifahamu vyema siasa za nchi hii. Asidanganywe na mahudhurio ya mikutano ya hadhara akadhani ndizo kura katika masanduku ya kupigia kura. Namsihi ajifunze` zaidi jinsi ya kufanya siasa za kistaarabu bila kueneza uvumi, uongo, chuki na uzushi vyenye kutetelesha amani ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.

Edward Lowassa


Mbunge Mteule wa Monduli
Inaonekana haya maudhurio ya dr slaa yamewauma sana.

Mara ya kwanza walikuwa wanatuambia wao ndio wanapendwa vijijini na upinzani hauna watu, sasa hivi dr anapata watu vijijini wanatuambia kuwa maudhurio sio kura

Kila mtu anajua uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa na high turnout and yet kura bado ni kidogo eti 8m, kura nyingine ziko wapi????
 
Back
Top Bottom