Elections 2010 Waraka wa Lowassa kwa vyombo vya habari

kampeni zimekwisha, rais amepatikana, chadema mmepata mlichokitaka cha kuwa serikali kivuli hivyo matusi na kupakaziana uishe tujenge nchi yetu!!!
 
Lowassa aachane na hadaa zake kwa watanzania kwa sababu mwizi na jangiri mkubwa nani kamwambia kuwa watanzania wamechoka na amani hivi ni kwa nini CCM hufanay madhambi wakinyooshewa kidole wanaanza kuimba amani?

Lowassa na wenzake wanatakiwa kujua kuwa Duniani kote watu wote ni wapenda amani ila utawala uliipo husababisha kuondoka kwa amani baada ya kutumia mabavu na watu kuamua kutokubali tawala za kidhalimu hapa wapinzani hawahusiki kabisa ni watawala wenyewe ndo husababisha mambo haya

Kitendo kilichofanya machafuko yakatokea nchini Kenya ulikuwa utawala uliopo baada ya kuwanyang'anya wapinzani ushindi vivyo hivyo Museveni alikwenda msituni baada ya kudhulumiwa haki kwa hiyo CCM waache kudhulumu haki wakitegemea kutumia neno amani kwa sababu kuna wakati watu wanachoka na dhuluma wanaamua kuwaondoa watawala kwa nguvu (mapinduzi) baadaya kuona njia ya kawaida imeshindikana tokana na wizi wa kura na kubli matokeo kama uchaguzi wa mwaka huu Tanzania
 
sema lowasa wehu wa chadema wanatuzingua tu na maneno ya kuumba, sema maji hayajafika kijijini kwenu diwani akusaidia na wananchi wenzako mlete maendeleo na sio kuzusha na kuongea uongo, kidumu chama tawala
Uchaguzi mmemaliza kwa kuiba kura rudini mlikomkua mtuachie JF yetu!
 
kampeni zimekwisha, rais amepatikana, chadema mmepata mlichokitaka cha kuwa serikali kivuli hivyo matusi na kupakaziana uishe tujenge nchi yetu!!!
wote mliotumwa sasa mrudi mkawaambie maboss wenu mlichovuna huku jf!
 
Inachekesha sana maana kutoka monduli kwenda mwanza ni masaa7 kwa gari V8 landcruiser sasa je kama amepanda ndege za coast chater atatumia mda gani?hivyo siswala lakujadili tena kwani tayari rais,mbunge wameishatangazwa!
 
Jana Mheshimiwa Lowassa alitoa mada yake kwenye vyombo vya habari ambayo pamoja na mambo mengine ilibeza jitihada za Dr. Slaa katika kupanua demokrasia hapa nchini....

Lowassa alidai Dr. Slaa yafaa sasa akajifunza siasa za nchi hii ya kuwa mahudhurio makubwa kwenye mikutano ya kampeni zake siyo kigezo cha kukubalika na hivyo kushinda Uraisi.........Ikumbukwe Dr. Slaa amekuwa mbunge wa jimbo la Karatu kwa miaka 15 na hivyo si mgeni kwenye ulingo wa siasa za nchi hii....................

Bw. Lowassa kwa kauli yake anataka tuiamini NEC kuwa ilifanya kazi kwa usahihi na bila upendeleo wowote ule jambo ambalo wengi wetu tunalipinga kwa nguvu zote......

Kabla hatujaanza kusikiliza porojo za Lowassa inabidi kwanza atuthibitishie NEC ni chombo huru na siyo zao la serikali ya CCM na ya kuwa waangalizi wa kimataifa wanaodai NEC ni bomu kuanzia mwaka 1995 basi ni punguani..................kama atashindwa kufanya hivyo basi itabidi tumpuuze Bw. Lowassa ambaye yeye mwenyewe ni matunda ya mfumo wa chama kimoja na kamwe hatumtegemei kuwa mwalimu au hata mwanafunzi wa demokrasia ya mfumo wa kiushindani wa vyama vingi...............
 
kwa mtazamo wangu binafsi lowasa anajiandalia mandalizi ya uraisi mwaka 2015.

Muheshimiwa lowasa anapaswa afahamu haya yafuatayo

1. Tunafahamu wanamakubaliano na kikwete atakapo maliza muda wake wa uraisi jmk,itabidi ampe tafu EL kwani yeye pia alimpa tafu.lakini kwa hali halisi EL ajihakikishie maumivu tu kwani mkwere lazima atamtosa.hivyo EL aache kujipendekeza hatopata lolote.

2. EL hakubaliki najamii ya tz kwa sasa,ht ikatakea akapitishwa na ccm 2015 kupeperusha bendera ya uraisi ya ccm,hatopata kitu chochote kwani jina lake ni tukano kwa sasa tz,labda waibe kama walivyofanya sasa,ila nachojua anguko lake litakuwa kubwa kuliko la kikwete.na hata km mkoa wake wa arusha ungekuwa ndio nchi na hakika asingepita.

Ninamuasa EL aache kujilinganisha na dr wa ukweli.nani asiyejua kama wameiba kura za watanzania.ushaihidi upo wazi ht mtoto wa miaka5 anajua hilo km ccm wameiba kura.angalia kigoma mjini shy mjini,karagwe,ngara,kibaha,segerea,ukonga,kilombero. N.k
 
kwa mliokuwa arusha El alionekana wazi akiingia manispaa?au mlijuaje kaja kumnusuri batilda? hapo napo patahitaji ushahidi km kweli alionekana km ilivyosemwa!
 
Inachekesha sana maana kutoka monduli kwenda mwanza ni masaa7 kwa gari V8 landcruiser sasa je kama amepanda ndege za coast chater atatumia mda gani?hivyo siswala lakujadili tena kwani tayari rais,mbunge wameishatangazwa!

Utuambie vizuri unamaanisha nini? kutokuwepo uwezekano wa kwenda Mwanza? kwanza kabisa, Lowasa anasema tarehe 19/10/2010 hakwenda Mwanza, lakini waraka unasema kikao kilikaa tarehe 16/10/2010.

Kama anakana tarehe 19 Oktoba hakwenda Mwanza, ni nani aliyesema alienda Mwanza tarehe 19 Oktoba? Tarehe inayozungumzwa kama tarehe ya kikao ni tarehe 16 Oktoba. wewe Kakakiiza unatetea nini? Mbona unazungumza kama mlevi mlevi hivi?
 
Katika hili Lowassa kajisafisha nadhani waraka wa Dr Slaa ulikuwa wa bandia labda kama tutapata maelezo yake baada ya watuhumiwa kadhaa kukanusha na kueleza umma jinsi wasivyohusika na kikao cha siri kule mwanza.

kwa maneno mengine ni kwamba, tunahitaji maelezo ya ziada kutoka kwa Dr Slaa juu ya makanusho hayo
 
Hivi ni kweli kwamba Nyerere alimkataa Lowasa? Hivi kwa nini alimkataa?

Jamani muacheni Baba wa Taifa apumzike huko aliko. Hawa jamaa wameshaanza kumkana na kumbeza, alianaza Kikwete kwa kusema Nyerere alishindwa katika kutoa elimu bure wakati sisi wengine wengi (wakiwamo kina JK) tumesoma bure maana wazazi wetu hawakuwa na uwezo
 
Lowassa alifanya vyema kupumzika kwa amani na akwa kimya...sasa anafikiri watanzania wameshasahau mambo yake...huyu mwacheni tu aanze kuja, ni mwepesi mno kumalizika na kama wana huo mkataba na wenzake eti wamrithi JK, mwisho wa CCM utakuwa umefika rasmi.

Lakini kuhusu yeye na Slaa kuna haya mawali nayaona.
1.Kwanza Lowassa anaonekana anajua yaliyoko katika Tume ya Uchaguzi kuliko NEC yenyewe. NEC w3amekiri makosa kadhaa, Lowassa anasema walisimamia uchaguzi vyema, amejuaje na yeye alikuwa Monduli muda mwingi na kama anavyodau hata La Cairo hakuwepo.Hapa tunapa ushahidi kuwa alikuwa karibu na mambo ya NEC.

2.Pili kwa uelewa wa Dr. Slaa katika taaluma nyingi kama sheria, saikolojia, sosholojia, filosofia na lugha anuai vinavyobebwa na dhamira yake yab wazi katika siasa Lowassa msanii kitaaluma (an BA katika mambo ya fine and performing arts) ni nani hata asimame na kumkosoa?
 
Jamani nawaomba at least hapa JF tusimuite huyu fisadi kuwa mheshimiwa!!! hawezi kuheshimika katu. mwizi ni mwizi tu hata akishinda ubunge!!!!

Na kama tunavyosikia eti safari hii atapewa U-PM basi atarudia ile project ya wizi wa mchana kweupeee wa mvua ya kutengeneza kwa kutumia moshi wa ndege zitakazotoka Thailand...Lowassa hanaga aibu kabisa kabisa katika kuchota hifadhi yetu ya taifa halafu eti ...nchi yetu ya amani...mara nyerere katuachia nchii brabra brabraaaa...to hell Lowassa
 
Lowasa ni nani asiyejua kuwa wewe ni FISADI? Ni nani asiyejua kuwa unamr...............de mama Batilda Buriani?? ukianza kukanusha hapa kuwa haukuwa Arusha kusaidia huyo dada ashinde utafanya watu waanze kumwaga data nyingine nyeti zaidi, watu wamekuchoka watu hawakutaki ni vyema ukatuymia hizo fedha ulizokwishazipata kwenye maswala ya Siasa kuliko kuendelea kukera watu, alafu AMANI unayoizungumzia wewe ni ipi?? unajua maana ya amani wewe?? AMANI ni kuchukua pesa za watu kuwaletea mitambo feki ya kufua umeme? Amani ni wewe na familia yako kuishi maisha ya kifahari while wengine wanaishi bila kula?? Amani ni kuwa na mabiashara kila kona ya nchi hii while machinga wanakamatwa kila kukicha huko barabarani? AMANI ni kujiona upo juu ya watu wote nchi hii?? Lowasa we are tired with you bwana ni vyema ukakaa kimya maana ulivyo wa ajabu umeshindwa hata kwenda sambamba na tarehe zilizotajwa kwenye barua husika. WACHA KUKURUPUKA
 
wasifanye hii nchi ya mjomba wao hawa?
na wasitufanye sie mabwege

:tape::tape:
 
kampeni zimekwisha, rais amepatikana, chadema mmepata mlichokitaka cha kuwa serikali kivuli hivyo matusi na kupakaziana uishe tujenge nchi yetu!!!
Zubeda kampeni zimeisha na rais kapatikana. Haya ndiyo maneno watakayokuwa wanatumia mafisadi kutufanya tusahau udhalimu waliotufanyia wananchi. Wao wanafikiri wamemkomoa Dr Slaa kumbe wametuchokoza wananchi make wametunyima viongozi tuliowataka kwa kuchakachua kura.
Hatunyamazi mpaka itakapotambulika na mataifa yote na watanzania wote hata wale wanaowanunulia khanga na kofia kuwa wamewatendea watanzania uovu usiopimika.
Hatumpakazii mtu kila mtu anavuna alichokipanda.
 
Katika hili Lowassa kajisafisha nadhani waraka wa Dr Slaa ulikuwa wa bandia labda kama tutapata maelezo yake baada ya watuhumiwa kadhaa kukanusha na kueleza umma jinsi wasivyohusika na kikao cha siri kule mwanza.

kwa maneno mengine ni kwamba, tunahitaji maelezo ya ziada kutoka kwa Dr Slaa juu ya makanusho hayo

Maelezo yanatakiwa yatolewe na Wilson Kabwe aliyeandika barua na si Dr Slaa. Inaonekena shuleni kuelewa kwako ilikuwa ngumu.
 
Back
Top Bottom