Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Spika anaujua ukweli hata kama anakula na CCM lakini hawezi kuwaeleza wasomi wa Kikristo kwamba Waraka haufai maana huko kwao atakuwa kajimaliza na Ubunge hatauona tena
 
Assume our next president (2010-2015) is a Muslim, person of high integrity and capable leader. He/She could play a healing role in the country divided by, inter alia, religious beliefs.
 
Date: 7/20/2009

Pentekoste yawawakia wanaopinga waraka

Na Elizabeth Suleyman

UMOJA wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (FPCT), umewajia juu viongozi wanaoupinga mwongozo uliotolewa na Kanisa Katoliki unaohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ukiwafananisha na mafisadi ambao wanahofia maovu yao kuwekwa bayana.

Pia, umoja huo umeitaka serikali kutambua kuwa mpango huo wa kutoa mwongozo si wa Wakatoliki peke yao, bali ni mpango wa makanisa yote ya Kikristo nchini.

Waraka huo wa Kanisa Katoliki unazungumzia sifa za viongozi ambao wanafaa kuchaguliwa kwenye uchaguzi ujao na kanisa hilo limejitetea kuwa mwongozo huo si kwa ajili ya waumini wake pekee, bali Watanzania wote. Lakini umepokewa kwa hisia tofauti na wanasiasa ambao wanadai unaweza kuligawa taifa, akiwemo mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru.

Jana Askofu Msaidizi wa Kanisa la Pentekoste Tanzania, David Mwasota alisema kwamba, wanaunga mkono waraka huo wa Katoliki na kuwataka viongozi kutouhofia.

"Viongozi wanaosema kwamba waraka huu unaweza kuligawa taifa si wakweli, bali hao viongozi ndio wanataka kulifanya taifa ligawanyike kutokana na kuhofia maovu yao kujulikana," alisema Mwasota.

"Kama Kanisa la Pentekoste Tanzania, hilo tumeliona na tumeamua kuunga mkono waraka huo; na kuitaka serikali itambue kuwa kitabu hicho kilichoandaliwa na Wakatoliki ni mkakati ambao na sisi tulikuwa nao," alisema.

"Wakatoliki wametutangulia tu.. lakini nasi kama FPCT tulikuwa ni miongoni mwao kwa kuwa tuna mpango wa kutoa waraka kwa waumini na wananchi wote kuwataka wawe macho na wajue ni kiongozi yupi anayefaa kuwa madarakani na si kuchagua tu watu ambao wamekaa kwa lengo la kutaka kuingamiza nchi," alisema.

Mwasota alisema siasa za zamani zilizotokana na watu kusikiliza taarifa kwenye redio tu, zimepita na kwamba jamii ya sasa imeelimika kutokana na kuongezeka kwa utandawazi na hivyo ni vigumu kuwadanganya Watanzania.

Alisema kutokana na kipindi hiki kuwa cha zama za uwazi na ukweli, viongozi wadini zote wanao wajibu wa kuwaelimisha wananchi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ili wajitokeza kupiga kura na pia kuchagua kiongozi anayefaa na mwenye maadili mema.

"Jukumu letu viongozi wa dini ni kutoa elimu kwa maumini wetu, waweze kujua mwongozo mzima wa uchanguzi kwani nchi haina dini, bali wananchi ndio wenye dini, hivyo ni vema kufuata misingi na taratibu hizo," alisema.

Hata hivyo, Mwasota alifafanua kwamba msimamo si tu kuangalia kiongozi bora ni yupi, bali pia kuangalia sheria na maadili ya dini inasemaje ili kuweza kupata kiongozi atakayetuongoza katika msingi imara.

"Tatizo lenyewe ni kuhusu mafisadi... hili si suala la kuficha kwani linajulikana wazi... kwamba waziri fulani amepatikana na hujuma fulani na kuondolewa madarakani, sasa haya siyo mambo ya kuyafumbia macho katika uchaguzi unaokuja," alisema.

Alisema mwongozo utasaidia kuweza kuziba hata mianya ya rushwa kwa kuwa wananchi watakuwa wamejua ni yupi kiongozi bora anayefaa kuchaguliwa.

Mwasota alitoa changamoto kwa serikali kuweka mipango madhubuti ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa dini ili kuweza kusikiliza maoni yao na kuondokana na kushutumiana bila ya sababu za msingi.

Alisema serikali isiishie tu kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari bali iweke pia mkakati wa kusikiliza hoja za viongozi wa dini, kwani itasaidia kuweka mfumo nzuri katika uchaguzi
 
Haya kayaanzisha Kikwete, naona anafanikiwa sana kuigawa hii nchi kwa misingi ya kidini.
 
Baada ya kuusoma waraka huu, sijasadiki madai ya kina Kingunge na wengine wenye mtazamo wa kuupinga.

Kifupi ni kwamba waraka unatuelekeza kuchagua viongozi waadilifu. Kama na dini nyingine na asasi nyingine zingetoa nyaraka zenye mwelekeo huo, hiyo ingekuwa habari njema sana, kwani ningetegemea watu wengi zaidi wangeelimika na kuchagua viongozi wazuri, watumishi wa wananchi.
 
Haya kayaanzisha Kikwete, naona anafanikiwa sana kuigawa hii nchi kwa misingi ya kidini.

Ametekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm. Na kiujanja ujanja ameahirisha bomu la OIC mpaka baada ya uchaguzi na miaka 3 kabla hajamaliza kipindi chake cha pili (KAMA ATACHAGULIWA 2010) ili ikifika muda huo a-dictate kuwepo kwa mahakama ya kadhi kwa sababu hatakugombea urais tena kwa mjibu wa katika hivyo kumuachia mzigo mgombea wa 2015.
 
Kutaka kupambana na mafisadi ni kutaka kuigawa nchi? Kingunge na waongo wenzake waache uwongo wa kitoto.
 
safi sana FCPT....

ni wakati wa makundi yote ya kijamii kuamka na kukomboa nchi kuondokana na tabia ya wizi, uzembe, unafiki, ubabaishaji (huu ni wa kiwangoo cha juu mnooo), uwongo, ukosefu wa maadili ya umma, rushwa, ulafi nk nk..

kwa pamoja; wanasiasa, viongozi wa dini, sekta binafsi, vyama vya kiraia (we need strong civil society), na jamii kwa ujumla TUAMKE kwa ajili ya maendeleo..

ahadi kila siku hakuna kinachoonekanaa..ISIPEWE NAFASI..
 
Wana jf habari zenu,
jana nilipata wakati mzuri kuupitia waraka wa kanisa katoliki,kwa ufupi waraka ni makini na hauna tatizo,umejaa points mwanzo hadi wisho,vipaombele vyote ni sahihi.
Ninawashauri viongozi wa madhehebu mengine,ngo's,na wananchi kwa ujumla kuinga mfano na kuelimisha wananchi kujua nini cha kufanya ili 2010 tuwaadhibu wote waliozoea kufanya watanzania ni chekechea
 


Mpendwa Msomaji,



Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania inayo furaha kukuletea Ilani hii.
Madhumuni ya matini hii ni kukualika tutafakari pamoja juu ya masuala muhimu yanayotukabili kama Taifa.
Tunawashukuru Wanataaluma Wakristo wa Tanzania walioandaa hati hii.
Kwasababu chaguzi za mwaka 2010 haziko mbali mnaona ni muhimu kupendekeza vipaumbele vyetu kama jamii tukiwaambia viongozi wetu wajao yale ambayo tungependa yafanyike kwa ajili ya jamii yetu. Katika uchaguzi hatupigi kura tu, tunapaswa kueleza makusudio yetu kwa yale tunayofikiri kuwa muhimu sana kwa Taifa.

Kwa kuchapisha Ilani hii tunataka kutekeleza haki yetu ya uzalendo ili kujenga maisha yaliyo mema zaidi kwetu sote katika siku zijazo.


Askofu Mkuu P. Ruzoka
Askofu Mkuu wa Tabora
MWENYEKITI
Tume ya Haki na Amani - TEC




WANATAALUMA WAKRISTO TANZANIA (CPT)
ILANI
MAPENDEKEZO YETU YA VIPAUMBELE VYA KITAIFA
A: Fikra Msingi

Maswali ya msingi

Uchumi na Siasa vipo kwa madhumuni gani?
Chimbuko la uwepo wa mfumo wa kisiasa ni nini?

Dira yetu

Maadili ndio dira yetu msingi ambapo kiini chake ni wanadamu walioumbwa katika sura na mfano wa Mungu, wakiwa na hadhi katika utu wao, haki yao na wajibu zao. Watu ndio kusudio na sababu ya shughuli zote za kiuchumi na kisiasa. Tunu za Ujamaa ambazo ndizo zilizojenga utamaduni wa nchi yetu zinakubaliana kabisa na maoni haya ya kimaadili. Tunu hizo ambazo ni umoja mshikamano, maelewano, mtazamo wa kifamilia (familyhood) zinabeba maana pana zaidi ya itikadi ya kisiasa. Uamuzi wetu wa kuchagua kufuata uchumi wa ujamaa wa kisoshalisti kulituletea matokeo mazuri na mabaya (chanya na hasi), kwa hiyo basi sio vema kudharau na kutupilia mbali kila kitu.

Marekebisho ya sera yanayofanyika sasa ni mengi, na baadhi ni ya lazima na ni mazuri. Lakini sio yote ambayo ni ya kujenga jamii yetu. Tunaweza kuona kuna ukuaji mzuri wa uchumi, lakini panakosekana usawa kwa kiwango kikubwa katika kunufaika na ukuaji huo wa uchumi. Kimsingi kanuni za uchumi wa soko huria sio tu kwamba zina kasoro za kiuchumi na kijamii tu, bali pia kasoro zake zinajionyesha katika maisha ya watu kiutamaduni na kimaadili. Watu wanaona mabadiliko haya kuwa yameingizwa kwa nguvu kutoka nje na hivyo yananufaisha matajiri na wenye uwezo.

Kumekuwa na ongezeko kubwa mno la tofauti/pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho, wanaosonga mbele kimaendeleo na wanaoachwa nyuma. Sera zetu nyingi za sasa zinajiridhisha kuwa msukumo wa maendeleo ni katika ukuaji wa uchumi kwa kutazama fedha taslimu (monetary terms). Kwa hiyo tunatilia mkazo shughuli na mambo yanayoonekana kusaidia ukuaji uchumi. Mtazamo huu ni wa kibepari kabisa.

Matokeo ya kubaki katika mtazamo wetu finyu, kutengeneza sera zetu kwa kuzingatia sekta chache zenye kulenga ukuaji uchumi tu, kumewaacha nje watu wetu wengi. Kuweza kuwachukulia watanzania wote kuwa ndio msingi wa sera zetu za kiuchumi na maendeleo yetu, sio suala la kimaadili tu bali pia inaleta maana kamili kiuchumi. Ni pale tu taifa zima litakaposhiriki katika uzalishaji na katika matumizi ya bidhaa na huduma (faida ya ukuaji uchumi) ndipo tu soko litakapopanuka.

Nchi za Magharibi zimeweza kupiga hatua mbele katika maendeleo ya kiuchumi pale tu walipoweza kupanua na kuimarisha soko lao la ndani, katika maana ya uzalishaji na matumizi. Vile vile kwa uzingatiifu huo huo nchi za Mashariki zimefanikiwa (kama vila Japani, Korea, Vietinam) na hali hiyo hiyo inaonekana wakati huu katika nchi za China, India, Brazil.

Katika Tanzania sisi tunaonekana kufanya kinyume chake. Kuweza kufanya maboresho yenye manufaa, ni lazima tubadili mtazamo wetu kutoka ule wa kukazania ukuaji uchumi tu na badala yake lengo liwe kuinua maisha ya watu wa kawaida: wake kwa waume. Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua tatizo la umaskini kwa kufikia ukuaji katika sekta chache tu kama ya utalii na madini. Mtindo tunaotumia sasa hauwezi kutusaidia kupunguza kiwango kikubwa cha umaskini uliopo ambao pia umeenea nchi nzima.

Kuzungumzia sekta rasmi na isiyo rasmi ni mfano mmoja wa fikra finyu tuliyo nayo ya kugawa katika matabaka mfumo wetu wa kiuchumi. Kwa kuwa wengi miongoni mwa watanzania wamo katika sekta isiyo rasmi, kwa sababu hiyo wamegeuzwa kuwa watu wasio na umuhimu, ambao kiuchumi thamani yao ni ndogo.


Kitendawili msingi cha Tanzania

Tanzania ni tajiri katika rasilimali na bado watanzania wengi ni maskini. Kwa nini? Hiki ni kitendawili kikubwa ambacho tunapaswa kukijibu.

Umaskini katika Tanzania sio ugonjwa ambao tiba yake haipatikani kwa urahisi. Kwa kweli umaskini tulionao huku tukiwa tumejaliwa rasilimali nyingi na utajiri mwingi unaotokana na mchakato wa mambo mengi yanayokuwepo kwa wakati mmoja.

Hali tuliyo nayo imeletwa na mchanganyiko wa mambo mengi. Tunapaswa kuchunguza na kuchanganua mambo hayo na hasa tukijiangalia sisi wenyewe, mienendo yetu, na kisha tuelewe ukweli wetu, mazuri na kasoro zetu. Kuondokana na umaskini, ni lazima kufuata mchakato wa kubadilika. Mwenye wajibu katika kuongoza mchakato huo ni sisi wenyewe. Ni lazima tuwe viongozi wa mchakato huo. Haifai kuwaachia watu wa nje, wafadhili, ama fedha kutoka kwingine popote. Hatuwezi kufaulu kwa kujifunza na kupokea njia zilizosaidia nchi nyingine. Kikwazo cha maendeleo yetu ni utegemezi na kukosa uwajibikaji miongoni mwa mawakala katika jitihada za kuleta maendeleo. Kukosa uwajibikaji ndio sababu kuu na jambo kuu linalosababisha umaskini wetu. Ni lazima, kwa hiyo, tujiwajibishe wenyewe katika kujinasua na mtego huu. Lazima tujisumbue na tuhangaikie kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu tukitumia ubunifu wetu wenyewe na rasilimali zetu wenyewe.


Madhumuni/Lengo la Ilani

Mipango tunayo, sera, taratibu na kanuni tunazo na pia mikakati mingi imewekwa. Licha ya hayo, ujuzi wa kinadharia juu ya ufumbuzi wa matatizo yetu tunao. Na bado hatufanyi vizuri katika kupambana na matatizo yetu. Kimsingi kinachokosekana ni uwajibikaji wetu katika utekelezaji wake. Tunakosa ujasiri na utashi katika utendaji, kujitoa kweli na kufanya kazi kwa bidii: kutimiza majukumu na kujitoa katika kutoa huduma yetu kwa ajili ya manufaa kwa wote; kuwa mawakala na wafanyakazi wazalendo waaminifu kwa jamii yetu. Tukubali kuukabili ukweli kuhusu sisi wenyewe. Alisema Mtume Yohane “Ukweli utawaweka huru” (Yh. 8: 32).

Kwa ilani hii, tunatoa mwaliko kwa wote na kuwasihi watanzania wote kufikiri kwa makini changamoto kuu zinazokabili nchi yetu na wananchi wake wengi ambao ni maskini wa mali, waliotengwa na wasio na uwezo. Kuzishughulikia changamoto hizi kunahitaji kuweka vipaumbele sahihi na njia sahihi za ufumbuzi ambazo zinashughulikia kikamilifu matatizo ya umaskini, utenganisho wa kijamii na hali ya kukosa uwezo kwa watanzania wengi. Ilani hii itakuwa mwongozo kwa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010.


























B: Vidokezi vya vipaumbele katika sera

Katika kuzingatia maoni yetu ya msingi juu ya jamii yetu, na uchunguzi wetu wa jumla juu ya utendaji na mfanikio, hapa sasa tunawasilisha mawazo yetu juu ya vipaumbele kwa taifa letu. Huu ni mchango wetu kwa ajili ya watu kutafakari na kuchangia katika mijadala kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

1) Hadhi ya Utu wa Mwanadamu

Lengo na sababu ya mahusiano yote katika jamii ni kumpa kila mtu hadhi ya kiutu ambayo ni stahili yake. Maana yake ni kwamba, kila mtu apatiwe mahitaji msingi kumwezesha kuishi maisha yanayostahili mwanadamu. Hicho ni kipaumbele namba moja. Watu wote wameumbwa na Mungu katika usawa. Kwa hiyo kila mtu ni sawa na mwingine.
Hapa tunapendekeza:

- Lazima tunu za kimaadili ziwe ndio msingi wa taifa letu, haya yakiwa yamehifadhiwa katika Katiba na kuongoza kanuni na taratibu zote za uendeshaji na utendaji.
- Kutengeneza na kutekeleza programu ya elimu ya uraia kwa watu wazima wengi juu ya haki msingi za binadamu na wajibu kwa kila raia.
- Kuwafundisha watu umuhimu na njia za uchunguzi wa malalamiko ya watu ili kusukuma huduma ambazo ni stahili ya watu zitolewe kikamilifu. Huduma hizo ni pamoja na zile za utawala wa umma. Hapo ni pamoja na kuwapa watu nafasi na kuweka njia fanisi za kupeleka malalamiko yao ngazi za juu.
- Ni haki ya msingi kwa kila raia kupatiwa fursa ya kutoa malalamiko yake na kusikilizwa. Haki hii lazima iweze kutendeka kwa kuiwekea mifumo ya kisheria na kiutawala.
- Kanuni na taratibu za kimaadili na weledi (meritocracy) viwe ndio vigezo au sifa za kuwapa watu kazi na kupandishwa cheo.


2) Marekebisho ya Katiba

Katiba inaeleza Mkataba Msingi wa Kijamii wa watu kuhusiana na namna ya kujipanga katika maisha yao ya pamoja. Katiba ni zaidi ya hati ya kisheria. Ni dira ya kimaadili na maelezo ya kifalsafa ya tunu na kanuni watu wanazotaka kuzizingatia katika maisha yao ili kuwahakikishia amani, haki na vile vile kuheshimiana na kuvumiliana katika kuwa na maoni tofauti. Hakuna chama cha kisiasa wala serikali ya wakati huu wanaoweza kihalali kutumia Katiba kwa faida zao za kisiasa.

Katiba inamilikiwa na watu na ni ya watu katika anuwai (diversity) na katika upokeaji wa watu wenye tofauti mbalimbali (plurality). Kwa kuwa taifa ni kitu kinachoishi ni jambo la kiasili na la muhimu hivyo ni sharti kuruhusu mapitio ya vipindi kwa vipindi yafanyike ili kuwapa watu fursa kueleza maoni yao. Haifai kuachia kundi moja kushinikiza au pande/kundi/chama chenye maslahi (kijamii, kiuchumi au kidini) kuchochea mabadiliko. Tangu Tume ya Nyalali imetoa ripoti yake (1991), ombi la marekebisho ya Katiba halijapokelewa kwa namna na kiwango cha kuridhisha. Kuhusiana na suala hili tungependa masuala haya yapewe kipaumbele:
- Tamko dhahiri juu ya tunu msingi za maadili ya kitaifa ambayo yapasa yazingatiwe katika mchakato wa kurekebisha Katiba.
- Pana haja ya kuunda Baraza la Mapitio ya Katiba. Katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kuna njia kadhaa za kuwezesha suala kutekelezwa: Mahakama ya Kikatiba, Chamba ya pili katika Bunge, Mkutano wa Katiba.
Tunapendekeza paundwe baraza la wazee, wanaoteuliwa na sekta za kijami, ama wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo hiki kingechaguliwa na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake kulingana na Katiba yenyewe. Kiwe huru, na kisibanwe na serikali.
- Kanuni za marekebisho na udhibiti (regulations) na kuwezesha uwazi kisheria kuhusiana na upatikanaji wa fedha za chama ama mgombea.
- Kanuni za udhibiti na marekebisho ya kuchagua wagombea kutoka ndani ya chama kwa lengo la kusaidia mchakato mzima. Kufanyika kwa uwazi na kwa kidemokrasia zaidi.
- Kuanzisha mfumo wa kiuwiano katika uwakilishi badala ya huu wa sasa wa mwenye kupata kura nyingi kuwa ndiye mshindi.
- Kuruhusu wagombea binafsi (isipokuwa katika nafasi ya Urais).
- Kuheshimu kanuni ya kuwa Serikali haina dini na kutoruhusu taasisi za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi (mfano. Mahakama ya Kadhi na uanachama wa OIC).
- Kulinda haki ya watoto ambao hawajazaliwa.




3) Uongozi wa Umma

Kwa kiongozi, huduma kwa umma ni dhima muhimu sana kwa jamii yoyote ile ya wanadamu. Ndio maana lazima pawepo uangalifu mkubwa kwa jamii yoyote katika njia na namna (means) inavyochagua viongozi wake na namna inavyoweka taratibu za kusimamia na kudhibiti mienendo ya viongozi wao. Mamlaka mikononi mwa wanadamu kwahitaji uangalifu mkubwa ikiwa tunataka madaraka hayo yasiegemee upande mmoja yawe na uwiano, yasitumike vibaya na hata kuwa ya rushwa.

Kwa wakati huu, tumesikia matukio mengi ya ufisadi, maamuzi yanayopendelea upande fulani kwa sababu ya maslahi ya kiuchumi (kwa watu wa nje na wa ndani). Hapa tunaweka kipaumbele katika yafuatayo:

- Uwazi zaidi katika michakato yote ya uteuzi katika huduma na ofisi za umma, Tume za umma na bodi za utawala.
- Kufanya mapitio ya mamlaka ya Rais katika kuwateua mawaziri, idadi ya wizara, na pia uwezo na uhuru zaidi wa bodi za usimamizi wa mashirika ya huduma za umma.
- Kanuni na taratibu za uongozi ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kuondoa wale wanaothibitika kutumia vibaya nafasi zao.
- Kuhimiza na kuunga mkono kazi halali ya uandaaji wa ripoti zilizofanyiwa uchunguzi na kutafuta taarifa juu ya utendaji fanisi katika huduma za umma kama huduma msingi kwa raia wote.
- Kuhimiza utamaduni wa kufanya tathmini makini juu ya utendaji fanisi wa viongozi, kwa kuweka njia ya kuwezesha wasomi, vyombo vya habari, jumuiya za kiraia na vikundi vya kiraia kushiriki katika tathmini hiyo ya umma.


4) Mfumo wa Kisheria

Kutenda haki ni zaidi ya kufuata sheria na taratibu. Sifa ya uadilifu kwa wale wanaosimamia uendeshaji wa taasisi za sheria na taratibu, na msingi wa mawakala hao wa kuheshimu utu wa kila mtu na kwa ajili ya manufaa kwa wote na kutunza amani na utulivu na maelewano, ni mahitaji ambayo kamwe hayapaswi kupuuzwa, na yafaa liwe ni somo la kila mara katika malezi yao endelevu.

Polisi, maafisa wa mahakama, mawakili, maofisa magereza, watunga sheria, na watawala sio “mabosi” mbele ya watu. Wao ni walinzi wa taratibu nzuri za jamii yetu.

Lazima hawa wajali sana wigo mpana wa mahitaji ya jamii yetu, na sio wawe na ufinyu wa kujiona kuwa wasimamia sheria tu. Kwa ulingo huu tunaleta vipaumbele hivi:

- Lazima kuweka na kudumisha uwiano mzuri zaidi katika mgawanyo wa madaraka katika mihimili mikuu mitatu ya Dola, Serikali, Bunge na Mahakamu. Ilivyo sasa uwiano hakuna na kuna uegemeo upande wa mkono wa Utawala/Utendaji (Executive). Sio kweli kudhani kwamba kudhibiti uwezo wa maamuzi ya madaraka kutaleta ucheleweshaji na kukosa ufanisi, bali kinyume chake ndio kweli. Maamuzi mengi mabaya na ubishani wenye mvutano yangeweza kuzuilika. Ni muhimu pia kuachia madaraka ya maamuzi katika masuala ya kiutawala kwa ngazi za kati na chini yakiandamana na haki ya kukata rufaa kwa ngazi za juu.
- Dhima ya Bunge ya kudhibiti Serikali Kuu inapaswa kuiimarishwa. Pamoja na hatua njema iliyopigwa hapa karibuni, udhibiti makini unatakiwa kwasababu Bunge likiwa ndilo mwakilishi wa majimbo yote linatarajiwa kutoa tathmini yakinifu ya maamuzi yanayofanywa na Serikali.
Wabunge nao wawe na mawasiliano ya karibu na wapiga kura wao wakiwa na ziara zilizopangiliwa majimboni mwao ambako watu wataweza kukutana nao. Wabunge wajizuie kujipendelea kwa kujipangia marupurupu na mapato maalumu pamoja na bonasi nyingi.
- Kupunguza usiri katika mchakato wa maamuzi yanayofanya katika ngazi za juu. Uwazi huboresha maamuzi yanayofanyika.
- Maamuzi yanayofanywa na utekelezaji unaohitajika vinazuiwa na kukosekana matumizi ya kanuni ya auni, badala yake mfumo unategemea maamuzi ya viongozi wa juu wanaohusika. Watu wa chini yake wanaweza kukatishwa tamaa katika uwajibikaji. Kwa hiyo wakubwa lazima wajifunze kugawa madaraka yao kwa walio chini yao. Kwa kufanya hivi, mfumo wa kisiasa unaweza kufikia maboresho makubwa.
- Kupunguza kiwango cha wanasiasa kuingilia mambo ya utawala na huduma.
- Hasira ya kijamii yapasa ishughulikiwe na taasisi za kisiasa na wakala wa sheria na taratibu. Tunaunga mkono sera ya ulinzi shirikishi na kupendekeza kuongeza idadi ya njia mbadala ya adhabu kwa watenda makosa madogo madogo (mfano; huduma kwa jamii, kulipa fidia, kemeo/karipio/onyo rasmi la umma). Pia kuanzisha vituo zaidi kwa ajili ya majaribio kwa wakosaji vijana kuishi bila kufanya kosa.
- Magereza yetu yanapaswa kuendesha programu za mafunzo kwa ajili ya marekebisho ya wafungwa kimaadili, kutoa fursa kwa wafungwa kuwa na mawasiliano na upande wa pili (mshtaki/mhanga) kwa lengo la kufikia usuluhishi.
- Mfumo wetu wa kisheria uchunguzi na kutafiti, na kutekeleza nyenzo na taratibu zinazoongeza ufanisi na utendaji wenye kuleta mafanikio yanayotakiwa kufikia matarajio ya watu. Ucheleweshaji na uzembe/uchovu (lethargy), kukosa uwajibikaji na kukosekana utendaji mzuri wa mahakama kunawafanya wananchi wakose matumaini na kukatishwa tamaa (frustrating) na kuwakosesha imani katika mahakama kama chombo cha kuwasaidia kupata haki kwa njia ya mfumo wa kisheria. Watu hawaoni uwezekano wa kushughulikiwa kesi zao kwa wakati na hivyo kujenga mazoea ya kujichukulia sheria mkononi.
Lazima mfumo wenyewe wa sheria uanzishe njia za kujinidhamisha na kujitathimini utendaji wake na kutumia kanuni za kisasa zaidi za kusimamia utendaji.
- Mahakama inapaswa kutumia sehemu kubwa ya fedha na mali zake zilizopo kwa ajili ya Mahakama za Mwanzo na za Wilaya na za Hakimu Mkazi (kwa mishahara, majengo, kutengeneza ofisi ziwe za kisasa na vifaa na huduma nyinginezo, kuongeza idadi na ujuzi wa mahakimu na makarani). Ni kweli kwamba ni katika ngazi hizi za mahakama ndipo watanzania wengi wanapoijua (wanapofika) mahakama.

5) Viwanda, Biashara na Fedha.

Ni vivutio vingi mno vinatolewa kwa wawekezaji wakubwa na hakuna jitihada na kujali vya kutosha wawekezaji katika uzalishaji mdogo. Wawekezaji wa nje pamoja na makampuni makubwa sio ufumbuzi katika kupunguza umaskini wa watanzania wengi. Upande mwingine wanataaluma wengi wanavutiwa na “mambo makubwa na ya kisasa na ya ughaibuni.” Wanakimbilia mitaji ya nje na njia za nje ya nchi wakati fedha ya ndani inabaki tu pasipo kutumika vizuri katika taasisi zetu za fedha.
Hatua hizi tunazipendekeza ziwekewe kipaumbele:
- Kabla ya yote kabisa, lazima tuangalie suala la utu katika kazi na wajibu wa kimaadili wa kila mmoja kuchangia katika jamii na sio kuwa mnyonyaji wa jamii. Kukaa bure bila kufanya kazi na uvivu ni dhambi mbele ya Muumba na pia ni kosa mbele ya macho ya jamii. Uzururaji ni kosa kisheria. Kutofanya chochote ni tabia isiyoridhisha, malipo sio kitu pekee kinachosukuma mtu kufanya kazi. Utu wa mtu wenyewe unamtaka mtu afanye kazi.
- Kuhusisha taasisi zinazosaidia uwekezaji (huduma za mikopo, miundo mbinu na huduma za ushauri, utafiti wa masoko) kwa ajili ya sekta ya uzalishaji mdogo.
- Kuweka kipaumbele katika kutengeneza soko la ndani na kuongeza uwezo wa watumiaji wa ndani na hapo tutawezesha uzalishaji wa ndani kuwa ndio nguvu ya kukuza uchumi wetu. Viwanda na biashara zetu lazima zikue kutoka ndani ya nchi yetu.
- Kuingilia kati uzalishaji katika sekta ya kilimo ili kuwahakikishia mapato wakulima wadogo wadogo kwa kuweka sera za bei ambazo zinawapa wazalishaji wadogo kipato cha uhakika kutokana na mazao yao. Njia za kuwalinda wakulima dhidi ya anguko la bei ya soko la dunia lazima ziwekwe.
- Maslahi ya wafugaji, haki zao na wajibu wao yanahitaji kufikiriwa kwa makini zaidi na kuwekewa njia nzuri zaidi za kisheria na kiutawala ambazo zitawahakikishia haki zao msingi na uhuru kwa mujibu wa Katiba.
- Kuweka njia imara za marekebisho ya kifedha kwa ajili ya faida ya wawekezaji na kunufaika na upendeleo zaidi kwa watu wetu badala ya kuwajali zaidi wawekezaji wa nje.
- Kufanya mapitio makini ya kuongoza vigezo vya vivutio kwa wawekezaji wa nje. Ni lazima tusiwachukulie kama wahisani wetu.
- Serikali iingilie katika kudhibiti soko la fedha ili kuwajali wakopaji wadogo. Kuna haja ya kuchukua hatua za kusaidia huduma za mikopo na akiba kuwafikia watu vijijini.
- Waendesha maduka madogo yasiyo rasmi sio kero kwa jamii. Tunakubaliana kuwa sekta hii inahitaji mabadiliko, lakini sio kwa njia ya polisi, bali kwa njia ya kuweka jitihada za kiuchumi zinazowawezesha watu wawe mawakala wenye thamani na faida. Hivyo lazima kuwaingiza katika sekta nzima ya biashara ikiwa ni pamoja na mambo ya huduma za mikopo, kuchangia kodi, huduma zilizo katika kiwango, utoaji leseni na mahala pa kuendeshea biashara ndogo ndogo na sio tu katika bustani za majumba makubwa.
- Kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi. Kuanzisha sera ya dhamana au rehani kwa kuwalinda na kutoa upendeleo kwa wenye kipato cha kawaida. Ujenzi wa majengo na barabara ni kichochea muhimu katika kukuza uchumi wan chi.


6) Uchumi

Kwa kuangalia changamoto za sasa kufuatana na ukubwa wa tatizo la umaskini, kuangalia mahitaji ya kiuchumi katika upeo mpana zaidi ya ukuaji uchumi. Tunahitaji kuweka mkazo katika watu wengi zaidi kuzifikia fursa, hasa kwa watu maskini na wasio na uwezo. Ukuaji uchumi lazima unufaishe watu kwa kuangalia walio maskini zaidi, kunufaisha wengi badala ya kuangalia wachache tu wenye kupewa upendeleo.

Kwa hiyo watu yapasa wapewe fursa ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji na katika mchakato wa ukuaji ili wanufaike kwa njia ya ushiriki wao wenye kuleta tija na kuweza kufikia maendeleo ya jumla ya nchi yetu. Watu wanahitaji kuwezeshwa ili ushiriki wao uwe wa tija. Uwezeshaji huu unaweza kufanyika kwa njia ya kuwekeza katika elimu, afya, miundo mbinu n.k.

Panahitajika mfumo sahihi uandaliwe kuhakikisha matumizi mazuri na ya kisheria juu ya urithi wa pamoja wa rasilimali zetu. Hapa panahitajika kuimarisha uwezo wa utawala na taasisi zenye wajibu huo. Pawepo uwiano kuhusiana na dhima ya Dola na soko.

Lingine muhimu ni juu ya namna tunavyojenga mahusiano yetu na jumuiya ya kimataifa. Ushirikiano wenye tija lazima uwekwe na kulindwa kwa misingi ya kuheshimiana, na maslahi ya taifa lazima yawe ndio yanaongoza ushirikiano huo. Hivyo umiliki wa nchi yetu na uongozi katika kutengeneza sera, mikakati, programu na menejimenti ya mchakato wa bajeti yapasa ziwe ndio kanuni zinazoongoza.

Sasa tunaelewa kwamba kinachotupatia lengo la uchumi na sera za kiuchumi sio tu uzalishaji na upatikanaji wa bidhaa na huduma. Uchumi lazima uwe chombo cha kutuhakikishia ubora wa maisha ya raia wote, ukiwa unahudumia manufaa kwa wote na uhalali na usawa wa kupata mali na huduma zilizopo. Sera yetu ya kiuchumi inaangalia mno upande mmoja, upendeleo ukiwa ni kwa wale ambao wana uwezo tayari. Masuala ya kijamii yanahitaji kutiliwa mkazo upya. Hapa maoni yetu ni haya:

- Tunapendekeza kwamba huduma ya afya na elimu ziwe ndio kipaumbele namba moja katika kupanga uchumi wetu.
Rasilimali kubwa ya taifa letu ni watu wake. Kushughulikia afya na elimu ya watu, kwanza kabisa ni wajibu wa kimaadili, kutunza maisha na kuongeza ustawi wa watu. Lengo hili hili yapasa liwe ndilo la kwanza katika mipango yote ya kisiasa na kiuchumi. Kuacha kujali afya na elimu kwa watu wetu ni kosa kimaadili.

Kwa maoni ya kiuchumi kuzungumzia gharama za huduma hizo ni kupotoka. Ni bora kuzungumzia kuwezesha ubora wa rasilimali watu ili uwezo wao uongezeke. Gawio linalotokana na uwekezaji huu tu linatokea haraka mara tu na ni la muda mrefu na huongeza kiwango cha jumla cha tija katika nchi.
- Watu wanaofanya kazi katika huduma ya afya na elimu wako katika taaluma za kiwito. Ubora wa elimu na afya unatokana kwanza kabisa na kujitoa kimapendo na uwajibikaji wa kitaaluma.
Tunatoa changamoto kwa dhana msingi ya mtazamo wa uchumi wetu wa sasa ambao mkazo wake ni kwamba lazima nia iwe ukuaji uchumi, kisha tutaweza kuongeza matumizi katika huduma za jamii. Maoni yetu ni kwamba tunahitaji kuwekeza zaidi katika afya na elimu ili tija ya kiuchumi na ukuaji wake vitokane na uwekezaji/matumizi hayo.
- Tunapendekeza mapitio katika sera ya kuchangia huduma za jamii. Sera hii ya ushirikiano wa Umma-Binafsi (UBIA) inaleta mambo mengi yasiyoridhisha na inachangia moja kwa moja katika kuyumbisha na kuzidi kuongeza mgawanyo wa matabaka katika jamii yetu, kwa kuwa baadhi wanazimudu gharama za huduma hizo na wengine wanashindwa kwa hiyo hawawezi kupata huduma hizo msingi.

· Sera ya Elimu

Mkazo lazima uwe katika kiwango cha juu katika elimu cha shule zote na kuondoka na kiwango cha chini kwa watu maskini na kwa shule za vijijini.
Ubora huu wa kiwango kizuri na sawa kwa wote, lazima kikubalike katika ufundishaji na kujifunza na vile vile katika usimamizi na utawala wa shule katika ngazi zote za elimu: msingi, sekondari na vyuoni.

Ø Katika ngazi ya shule ya msingi elimu iwe bure na gharama zibebwe na kodi inayolipwa Serikali kuu na Serikali za Mitaa.
Ø Kwa ngazi ya Sekondari na vyuo sera nzima ya elimu inahitaji kufanyiwa mapitio na mpango lazima uongozwe na Serikali na hivyo hapatakuwa na mwingiliano wa programu kama ilivyo sasa. Pia hali ya mazingira ya kazi kwa waalimu yafanyiwe mapitio. Tuisheni/mafundisho ya ziada yafanyiwe mapitio pia, ulipaji ada na viwango vyake lazima udhibitiwe, mfumo wa mikopo uwe wazi zaidi na iwe ni juu ya mfumo mzima wa kodi na sio mzigo umwangukie mzazi pekee yake.
Ø Mapitio katika mfumo wa mitihani na kupima wanafunzi kwa kutumia maendeleo yake, na sio tukio moja la kufanya mtihani.

· Sera ya Afya

Ø Tunapendekeza kurudi katika huduma bure ya tiba kwa mahitaji msingi ya kiafya katika zahanati na hospitali ngazi zote na kuanza mtindo wa kuzipiga faini hospitali za Serikali ngazi za chini ikiwa huduma hizi za msingi hazipatikani katika eneo lao.
Ø Kushirikisha kikamilifu hospitali na zahanati zinazotoa huduma bila kujitafutia faida, nazo ni zile zinazoendeshwa kwa kujitolea ama zile za mashirika ya kidini. Hizi ziingizwe katika mfumo wa uendeshaji wa zahanati na hospitali za umma na zipate misaada sawa.
Ø Kuifanya huduma ya bima ya afya kuwa ni hitaji msingi na la lazima kwa kila Mtanzania.

· Sera ya Kazi na Ajira

Ø Sera hii inahitaji kufikiriwa upya haraka. Jambo hili limekuwa kitendawili cha hali za kihistoria na maoni na upendeleo na imeathiri sekta mbalimbali na makundi ya watu wa namna mbalimbali. Msingi ungekuwa pato la mshahara ambao unamwezesha mtu kuishi na sio mshahara wa kima cha chini. Malipo ya ziada kama zawadi kwa mafanikio mazuri (bonus), marupurupu (allowances) ya kila namna, gharama maalum sasa yamekuwa sambamba na kipato na wala hayatozwi kodi wala kudhibitiwa. Wale walio katika nafasi za kujipangia upendeleo huu wanafanya hivyo kwa makusudi na hawako radhi kujipunguzia au kujiondolea upendeleo huo. Na hii ni kuanzia na ngazi za juu za nafasi za umma.

Sio tu kwamba sera ya ajira sio ya haki, bali pia sio nzuri na inaleta mtikisiko na hali ya kutoridhika katika jamii kama ambavyo migomo ya waalimu na watumishi wa afya ilivyodhihirisha hivi karibuni. Na njia ya kutumia nguvu iliyotumika kukabili migomo hiyo ni jambo la aibu.

· Mtazamo wa jumla wa sera ya kiuchumi – kijamii

Ø Lazima tuwe na ujasiri na tuthubutu kutambua mahitaji yetu na kuweka vipaumbele na kujua namna ya utekelezaji wenye kuleta kilichokusudiwa. Wafadhili, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), nchi wahisani wanaweza kuwa na la kusema. Lakini wasiwe ndio wanatuamulia namna ya kupanga mahitaji na vipaumbele vyetu na kuwa ndio wasimamizi (take charge) katika mchakato wa maboresho ya kimaendeleo kama ambavyo imeonekana kuwa.

Kwa haya lawama zinatuangukia sisi wenyewe. Kila mara tunavutwa na pesa na hivyo tunakuwa tayari mno kukubali masharti yoyote bila kufikiria matokeo yake na bila kujali sura kamili; bila hata kujifunza mahusiano yaliyomo baina ya hali mbalimbali ya nchi yetu kiuchumi na kimuundo. Mara nyingi mno tunakuwa na mtazamo katika mradi tu (project – focused) na tunashindwa kuwa na mtazamo kamili katika kupanga maendeleo yetu.

Ø Kilimo na ufugaji yapasa vipewe uzito na kipaumbele kadiri inavyostahili, kwa kuwa bado ni muhimili/uti wa mgongo wa uchumi wetu. Mazao ya kilimo na biashara yanayostawi katika kila sehemu (mkoa au wilaya) yapasa yatambuliwe kisayansi na watu wasaidiwe kushughulikia kilimo kwa njia ya kuwezeshwa kuwekeza katika viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na ufugaji, huduma za ugavi wa pembejeo, mashine za kilimo (agri-machinery), masoko na huduma za ugani kwa kulenga kupata mazao mengi na yenye ubora.





7) Hifadhi ya Jamii

Njia ya moja kwa moja inayoweza kuisaidia Tanzania kupunguza umaskini ni kuhakikisha huduma ya hifadhi ya jamii kwa walengwa na makundi ya wasio na uwezo. Sera hii inaweza kupunguza umaskini uliokithiri kwa nusu ndani ya muda mfupi na kwa kutumia gharama tunayoimudu.

· Tunapendekeza:

- Mpango wa mafao ya uzeeni kwa watanzania wote walio na umri wa zaidi ya miaka 60.
- Kuwapatia watoto wote wa shule za msingi chakula cha mchana bure/bila malipo.
- Malipo ya kila mwezi kwa kila mtoto mlemavu.
- Zaidi ya hayo tunapendekeza kuimarisha mfumo wa kijamii wa ustawi (welfare): hifadhi ya jamii inahitaji mambo mengine zaidi ya pesa. Hali ya kukosa uwezo na ulemavu vinahitaji raia wote kumjali mtu huyo. Jamii haiwezi kuwa imestaaribika na kuwa na msimamo wa kimaadili ikiwa inawadharau wale wasio na uwezo ama walio na ulemavu. Kuheshimu hadhi ya utu wao ni sehemu ya kuonyesha mwenendo na tabia ya kiutu. Kuwatendea kwa kiwango kilicho chini ya utu wa mwanadamu ni tabia ya kiuhalifu (criminal) na vile vile ni dhambi kimaadili.

Tunapotoa wito wa kuimarisha mfumo wa ustawi wa kijamii (social welfare) tunapendekeza kupanua ushirikiano baina ya jitihada za vikundi vya kujitolea kama vile vya Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo na vya Mfumo wa zakat kwa waislamu na vile vya Serikali kuu na Serikali ngazi za chini. Hii inaleta hitaji la kuongeza wafanyakazi (social workers) ambao wataunganisha jitihada za vikundi vya kujitolea na zile za taasisi za Serikali. Kushughulikia na kutunza watu wasio na uwezo na walemavu sio kazi rahisi, na hivyo ili kuweza kufaulu tunahitaji kushirikiana wote miongoni mwetu.

Ni lazima tushawishike kwamba hii ni kazi yenye thamani na maana kubwa. na kwa kweli matokeo mazuri ya jitihada kama hizo za jamii ni kwamba jamii yetu itakuwa ya kiutu zaidi, yenye msimamo wa kimaadili na itaonyesha sifa nzuri ya ubora wa kujali, ambayo itameza au kuondoa tabia na mienendo mibaya kama uchoyo, ubinafsi na rushwa/ufisadi. Kutunza kwa kujali watu wasio na uwezo yapasa, na hatimaye kunaifanya jamii yetu kuwa nzuri zaidi kimaadili na ya kiutu zaidi.



HITIMISHO

Mwisho kabisa tunapendekeza tafakari ya kina juu ya nini na nani wanaongoza uchumi wetu na maslahi ya taifa letu. Na kwa hiyo kwa uwezo mkubwa tuhimize mijadala juu ya kama uchumi wetu unavutiwa na ongezeko la mahitaji ama na kuwezesha ongezeko la upatikanaji vitu? Nini kinasukuma/kuongoza uchumi wetu? Je, ni uwekezaji, au ni ongezeko la fedha, kuongeza ajira na bidhaa na miundombinu? Tuna nia ya kuongeza mahitaji na matumizi ya ndani ili kuchochea uzalishaji wa ndani kukamilisha mahitaji ya ndani na hapo tuweze kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha bidhaa zenye thamani zaidi badala ya kuwa na bidhaa za malighafi.

Kwa kusikiliza mjadala huu kuwa mahitaji yetu hasa sio pesa, bali tunachohitaji ni utashi, mawazo na kufanya kazi kwa bidii. Kuna tabia imejijenga katika jamii yetu, nayo ni ile ya kutojishughulisha, na watu wana kiu ya kutaka fedha bila kufanya kazi. Mwenendo huu hautatuletea maendeleo ya kweli.

Naam, nchi ina utajiri mkubwa wa rasilimali na utaalam, na pia kuna fursa nyingi ambazo hazijatumika. Na bado nchi ina vikwazo vingi vya kiurasimu ambavyo huruhusu wachache kunyonya kwa faida yao binafsi. Tunahitaji kuweka mfumo wa kuweka mikakati na kuanzisha chombo cha kujitoa kweli katika kuhamasisha na kulinda manufaa kwa wote na mafanikio mazuri kabisa kwa ajili ya urithi wa kitaifa.

Tunahitaji kufufua maadili, kurudi katika tunu msingi za kimaadili na matashi ya kujenga maelewano, mshikamano, kujali manufaa kwa wote na kumpatia kila mmoja mahali, nafasi, fursa na wajibu.



KAMATI YA TAIFA
CPT


 
gonga hapa
[ame=http://www.youtube.com/watch?v=G0dqLxJ1TzI&feature=related]YouTube - MCHUNGAJI MUNISHI AIKEMEA SERIKALI YA KIKWETE GTV[/ame]
 
Wana jamvi
Siku nyingi nimekuwa porini lakini nikikodolea macho mjadala huu. Jambo moja ni wazi, nalo ni kuwa serikali inaogopa kivuli chake. Sasa kuna uvumi unaoelekea kuwa ni kweli, usemao kuwa, waraka wa kanisa Katoliki umelenga kumtengenezea JK njia ya kuendelea na awamu yake ya pili. Hii ni kwa sababu, ni hao hao waliosema yeye ni chaguo la Mungu. Kwa hiyo Mzee Kingunge amekosea kuwapinga wanaomuunga mkono kijana wake.
Narudi msituni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom