Si Tanzania tu ambako Mabaraza ya Maaskofu huhimiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora. Uchaguzi wa mara ya kwanza wa Tonny Blair ulisaidiwa sana na jarida la "The Common Good" ambalo lilitolewa na maaskofu katoliki wa huko.
Kaka mazingira tofauti,
Uingereza malkia ni kiongozi wa dini hata kama sio mfuasi wa kanisa la katoliki. Lakini pia Uwiano wa kidini ni tofauti sana na sisi hapa. Na vilevile wenzetu wamekomaa kidemokrasia na asasi zenye jukumu za kupunguza athari za mambo haya zipo na zimekomaa....
Sio kwenye demokrasia hovyohovyo kama tulionayo sisi...sio kwenye jamii inayofundisha waumini ubaya wa imani za wengine zaidi kuliko uzuri wa imani zao....
Kuna mtu anasema CHANGE IS COMING...
Ni kweli inakuja lakini ni change ya aina gani? Ni kwa manufaa ya nani?
Kila wakati nimekuwa nikionya kuhusu kushabikia hii inayodaiwa vita ya Ufisadi na zaidi hatari ya UMASIHA FEKI....tusipokuwa makini, uchungu na chuki zetu kuhusiana na hali mbaya tuliyonayo (UFISADI NA MAOVU MENGINE), tutajikuta tunashabikia kina HITLER wa enzi hizi...Wanaweza wasiwe wabaya kama tunavyoambiwa HITLER alivyokuwa, lakini wakawa wenye kutupeleka kama kule HITLER alipowapeleka WAJERUMANI....
Katika nyakati kama hizi ambazo serikali na wanasiasa walio wengi wamepoteza UHALALI (LEGITIMACY) ni wazi akili na busara za wananchi ndio zaweza kutulinda. Busara za viongozi wa kijamii nazo zina umuhimu wake mkubwa sasa.
Hata kama ni kweli serikali za CCM zimetuharibia nchi, hata kama mfumo wa siasa tulionao unalinda na kuneemesha ufisadi, hata kama ni kweli dini na siasa haziwezi kutenganishwa, lakini ukweli unabaki palepale....
Kwa Tanzania ni hatari sana kuchanganya mambo haya mawili haswa waziwazi kama inavyoendelea sasa....
Haihitaji kuwa genious kujua kuwa zaidi ya wakati wowote ule, huu sio wakati wa viongozi ama asasi za kikristo kuonekana wanamobilize wafuasi wao dhidi ya serikali inayoongozwa na MUISLAM.....Its wrong moraly but also strategically.
Ni wazi kuwa kanisa la Katoliki wakati wote limekuwa mstari wa mbele katika kufanya haya lakini kulikuwa na umakini mkubwa na sio kama sasa. Naamini hii ni dalili ya kuwa hali sio nzuri kimaadili, kiasasi na kiuongozi katika kanisa hili.
Na unapoingiza na makanisa ya kilokole ambayo ukweli ni kuwa katika enzi hizi yako more established, well networked and well financed kuliko THE MIGHTY CATHOLIC CHURCH, na ambayo upatikanaje wake wa viongozi hauko thorughly kama wenzao (CATHOLIC CHURCH) ndio kabisa tunawasha sigara katikati ya bwawa la petroli.....
Ndugu zangu tujihadhari kushabikia hizi njia za mkato katika kutafuta suluhu ya majanga yanayotukumba.....pale tu tutakapokuwa tayari kufuata njia iliyonyooka ndio tutakapojihakikishia tunapata mafanikio yaliyonyooka...
omarilyas