Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
mbona hata za kkkt nyingi tu zimerudishwa.Ukumbuki magamba huko lushotosasa ni chuo kikuu. Minaki nayo Angilikan wanataka Kuna kuna majengo ya walimu kodi unalipa angilikan na mengine ni ya shule, mazengo DODOMA na.
 
Waislam nao watarudishiwa Tambaza, Azania, Jangwani, Kibasila, Zanaki, Mnazi Mmoja kwa kuzitaja chache za mkoa wa Dar es Salaam. Serikali itabakiwa na shule chache kama kila dhehebu litarudishiwa shule zake.
 
Pamoja na serikali ya awamu ya kwanza kugundua changamoto hiyo kubwa ya kuwa na shule na hospitali nyingi za kanisa, iliamua kuzitaifisha ili watanzania wote wapate fursa sawa. Leo hii Mwalimu Nyerere wapo watu wanamtuhumu aliwapendelea wakristu. Huu upendo kwa watanzania wote hauonekani.
Nafikiri kuna watu hatuna kazi za kufanya ni kutafuta short falls za wenzetu tu kama sisi ni malaika. Vita za kidini ushindi huwa haupo hata siku moja.Ireland walipigana miaka mingapi? Sudani je? Kwanini sisi tunataka kwenda kwenye mashindano ya kidini yasiyo na tija kwa yeyote yule?
 
anza na Tabora boys and girls, Pugu, kigonsera,tosamaganga,kilakala na nyingine nyiiigiii. nyingi sana, pia na hao walutherani, shule zao wenyewe nyingi hawajaweka seminari, wana shule nyingi sana lakini wanaruhusu hata waislam kusoma. hizo pia wakichukua je? waislam wana shule ngapi, WENZETU WAISLAM WATAJENGA LINI seminari zao hadi watukute? hamuoni kama hapo tunagawanyika?

na vyuo je, wakianza kuchagua kwa upendeleo kama vile Tumaini universities, St.Augustine, Ruaha ya iringa, mwenge, vile vyingi vya moshi, vile vya arusha nk. tutafika? tutaelekea wapi?
 
Waislam nao watarudishiwa Tambaza, Azania, Jangwani, Kibasila, Zanaki, Mnazi Mmoja kwa kuzitaja chache za mkoa wa Dar es Salaam. Serikali itabakiwa na shule chache kama kila dhehebu litarudishiwa shule zake.
shule hizi tu zinawatosha aisee watu mnaozaliana haraka kama nini nyie? vyuo je, mtabakiwa na cha morogoro ambacho hata hakitambuliki?

angalieni jamanie, acheni tu tuishi hivihivi kama tunavyoishi, tukianza kusambaratika, hakina nakwambia patakuwa padogo. sadaka zetu tu makanisani zinaweza kujenga mashule kibao, angalia television, nyie msikitini hamtoi sadaka? mbona hata tv moja hamna? mnazo radio tu kama radio kheri na radio kuran ambazo kuna watz hapa hawajui kama zipo duniani hapa.
 
shule hizi tu zinawatosha aisee watu mnaozaliana haraka kama nini nyie? vyuo je, mtabakiwa na cha morogoro ambacho hata hakitambuliki?

angalieni jamanie, acheni tu tuishi hivihivi kama tunavyoishi, tukianza kusambaratika, hakina nakwambia patakuwa padogo. sadaka zetu tu makanisani zinaweza kujenga mashule kibao, angalia television, nyie msikitini hamtoi sadaka? mbona hata tv moja hamna? mnazo radio tu kama radio kheri na radio kuran ambazo kuna watz hapa hawajui kama zipo duniani hapa.

Hivi umetembea Tanzania ujue kuwa kuna Radio Kheri na Quran pekee, unafurahisha na chuki yako. Kukosa TV sio hoja, ila karibuni tutapata ni suala la muda tu. Nyinyi sio Sadaka, soma mkataba wa Serikali na Makanisa, Serikali inawakopea hela kufungua na kuhudumia mashule, hospitali nk, na Serikali ndio inalipa. Mbona Waislam wasipewe hilo. Shule za Waislam nilizotaja na zilizopo zimejengwa kwa hela zetu. Ila nyinyi nyingi zilipatikana wakati wa mkoloni, ni kodi iliyotolewa na raia wote, hivyo huwezi kujisifi, hawa toka wakati wa ukoloni walipata fedha toka kwa mkoloni, wakati Waislam hawakupata kitu zaidi ya kulipa kosi.

Unapozungumzia shule za Waislam nilizotaja unasema chache. Nimesema hiyo ni Dar tu. Lakini uchache usikutishe kwani unataka sema hakuna nyingine. Pia unaposema Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro hakitambuliki unatumia kigezo gani?.
 
Nadhani ukisema....mnyakyu...utakuwa umemaanisha kuwa wewe na Mch.Antony Lusekelo hamko tofauti kimawazo kwa yale aliyochefua ktk kipindi hicho ila wewe umeenda upande mwingine zaidi wa Kibaguzi pasipo kuweka mjadala wa kimawazo kwa kuweka ujumla mawazo ya Mch.Antony Lusekelo kuwa ni mawazo ya ...wanyakyu..hiyo tu inakuweka ktk fikra mfinyu isiyo tabainisha kilichozungumzwa katika kipindi cha Makwaia pale Channel Ten.

Kwa ujumla Mch.Antony Lusekelo hakufunuliwa Kiroho nini kilimaanisha katika kipindi kile na akajipeleka bila maandalizi! na kwa kufanya hivyo akaishia kuongea asichokipenda akimaanisha anakipenda kumbe sivyo.Dini inafundisha watu wawe waadilifu,waaminifu,wenye subira na wenye kutanguliza utu na hicho kiluchoelezwa katika Ilani ya wakatoliki,anaposema inachefua anamaanisha basi hata anachokihubiri basi hakina mantiki ya kuwapeleka watu kumiliki na kula matunda ya nchi.Ndo maana nikasema hakujua nini anatakiwa kufanya kwenye luninga.nadhani atakaporudia kukiangalia kipindi atajua wapi alikosea.

Joune,
Ndikupasya Buno Malafyale anganile kangi Ambokile.


Ewaa Malafyale, oupijile wakumyetu..!!
 
Kwa maoni yangu binafsi, napenda waraka huu, naufagilia sana, mimi sio mkatoliki, lakini kwa hili nawaheshimu sana, na ninawasapoti. wengi hapa pamoja na kikwete mwenyewe tumesoma shule zilizojengwa na wakatoliki, hospitali tumezaliwa etc. hawa jamaa wana mchango mkubwa sana. ninawapongeza kwanza kwasababu hakika wana network moja kali sana, kuanzia kwa pengo mwenyewe hadi kwenye familia kwenye vigango vyao, kuna vigango vingi tu hapa bongo vingine vimenunua hadi mabasi, yaani wanakusanyika nyumba kwa nyumba ktk wiki asubuhi kabla ya kwenda kazini, na ikitokea msiba au arusi, hakika huwezi kujua hela wametoa wapi, wanachangiana kiasi kwamba mhusika hagarimii kabisa. kitu hiki kimefanya wao kuwa na network kubwa sana sana. na waraka huu karibia kila mtu kwa sasa huku mijini, hadi kwenye vigango wanaufahamu na wanaujadili na wamefundishwa. jinsi unavyozidi kujadiliwa, they feel as if they are attacked, au kwamba watu wana attack dhehebu lao hivyo kuutafuta na kusoma kuona what is happening. kitu hiki ni kizuri kwasababu kinawafanya wausomi wakatoliki karibia wote.

mimi sio mkatoliki,ila nawaheshimu. kwa ufupi, wakristo wachache tu, nao ni wale ambao hawana uelewa mzuri, wameukataa na kuuponda huu waraka. kwanza sijaona hata mmoja isipokuwa mchungaji mmoja tu, naye hawakilishi waumini wake wote b'se nijuavyo kanisani huwa tunaenda kusali tu, si kila anachosema mchungaji tunafuata hata kama ameteleza, yeye nibinadamu pia.

Nimependa Waluthelani kupitia malasusa kuufagilia waraka. nimependa wapentecost kuufagilia, nimependa cct kuufagilia, nimependa angrican kuufagilia, madhehebu yoote ya kikristo yameufagilia, tofauti na kipindi cha nyuma. hapo nyuma tulizoea kutokuwa na umoja, wakatoliki wamekuwa wakiwa attacked sana hata pale wanapofanya mambo mema, lakini lilipotokea jambo linalohusu maslahi ya taifa, wakristo woote tumeungana bila kujali mlokole wala mwanauamusho au mwanakigango n.k. hii ni kitu kizuri. yoote hii imetokea kwasababu ya fikra za mahakama ya kadhi na oic. Mungu ibariki Tanzania. may God send mahakama ya kadhi na oic to hell. amin.



sio maslahi taifa kumbe ni kwa ajili ya fikra za mahakama ya kadhi na OIC, kazi ipo! bila kadhi na OIC msingeungana! no comments, naendelea kuisoma na kuijua zaidi JF
 
Naona tunamis use maana ya breaking news,habari hauna then unaiita breaking news au kutafuta umaarufu.Unless kama JF nowdays imegeuka sehemu ya udaku.
Lete taarifa zilizokamilika apa sio blaa blaa.
I can comment nothing kuhusu izo shule as to me huo bado ni udaku.
 
Niombe mtu yeyeyote anayeweza ku-link huo waraka basi atufanyie hivyo na sisi tuweze kuupitie.
Baada ya kusema hayo ni wazi kua mtu yoyote ambaye kuchanguliwa kwake au uwepo wake katika nafasi fulani anaposikia watu au jamii fulani inahoji ulalali wa kuchanguli basi anakuaa na wasiwasi.
 
Pengo hakikisha unapata feedback to kila Jimbo na uhakikishe kule kwenye kigango changu ujumbe unafika maana wana taabika wale watu na hawana pa kutokea .Kama umeamua sasa basi hii ndiyo kazi hasa ya kitume , usirudi nyuma.

KWELI LUNYUNGU TUKO NYUMA YAKO................LEO HIIIIIIIIII NIMESIKITISHWA SANA KUMUONA KWENYE TV NAPE NNAUYE BAADA YA KUHAIDIWA ULAJI KWA KILA UCHAGUZI LEO HIII ANATHUBUTU KUTAMKA VIONGOZI WA DINI ACHANENI NA SERIKLI...KAMA NI MAFISADI WAOOMBEENI WAMJUE MUNGU NA SI KUWASEMA KWENYE MADHABAHU.......LOH!!!!!!!!!! SHAME NNAPE KWA HIYO ANASEMA TUWAACHIE SERIKALI KAMA MAFISADI NI HIYO HIYO SERIKALI.............,,JAMANI TUPELEKE TENA KESI HUKO....LOH

Kama kweli haya maneno yamesemwa na Nape Mnauye basi sasa na yeye ameshapoteza mwelekeo kabla hata hajaanza safari ya uongozi wa kisiasa Tanzania.Ni huyu huyu Nape aliyekuwa akilalamika kuwa kunaharufu ya ufisadi kwenye tenda ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya umoja wa Vijana pale mtaa wa Lumumba.

Tamshi lake hilo lilimponza mpaka akapoteza nafasi ya ugombeaji wenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa.Ni mafisadi hao hao aliokuwa anawatuhumu ndio walioshughulika nae mpaka kuipeperusha ndoto yake hiyo ya kuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa kupitia ccm.

Sasa hivi hilo halioni anadhubutu kusema viongozi wa kanisa hawana haki ya kuwasema mafisadi madhabahuni,hivi kwani yeye ni nani hasa mpaka awape viongozi wa kanisa maelekezo?

Kwa kweli hakuna kingine ambacho chaweza kumbadilisha mwelekeo kiasi hiki bwana Nape Mnauye isipokuwa tuu ama ameamua kula na mafisadi au na yeye ameamua kuwa fisadi.Na kwa hili watoto wa mitaani wana usemi usemao kuwa Nape umeshafualia kisiasa.
 
hivi huu waraka inatakiwa kila mtu aufagilie? kutokufanya hivyo ni ufinyu wa elimu? inaonekana hawa waliotoa waraka huu ndio wasomi, 100% perfect, na hawastahili kupingwa wala kukosolewa!

nadhani kila mtu ana uhuru wa kukukubali au kukataa! kumuandama mtu kwa kutokukubaliana nawaraka huo sidahanikama nisahihi, huo waraka ni wa kanisa katoliki, hivyo ni wa wakatoliki , naona kama badhi ya watu mnataka kuufanya ndio ilani ya uchaguzi kila mtu aukubali, au ndio manataka kudhihirisha kuwa nchi ya wakatoliki, hivyo la wakatoliki lisijadiliwe kwa mtizamo hasi!!

nadhani kama ni udini upo zaidi humu JF kwa kukuza na kulazimisha mambo!
 
Hivi umetembea Tanzania ujue kuwa kuna Radio Kheri na Quran pekee, unafurahisha na chuki yako. Kukosa TV sio hoja, ila karibuni tutapata ni suala la muda tu. Nyinyi sio Sadaka, soma mkataba wa Serikali na Makanisa, Serikali inawakopea hela kufungua na kuhudumia mashule, hospitali nk, na Serikali ndio inalipa. Mbona Waislam wasipewe hilo. Shule za Waislam nilizotaja na zilizopo zimejengwa kwa hela zetu. Ila nyinyi nyingi zilipatikana wakati wa mkoloni, ni kodi iliyotolewa na raia wote, hivyo huwezi kujisifi, hawa toka wakati wa ukoloni walipata fedha toka kwa mkoloni, wakati Waislam hawakupata kitu zaidi ya kulipa kosi.

Unapozungumzia shule za Waislam nilizotaja unasema chache. Nimesema hiyo ni Dar tu. Lakini uchache usikutishe kwani unataka sema hakuna nyingine. Pia unaposema Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro hakitambuliki unatumia kigezo gani?.
hivi kumbe mnazo shule nyingi ehee, sasa kwanini mwalimu aliwanyang'anya hawa jamaaa? Pili, point of correction,mimi sina chuki ya kidini ya aina hiyo, what i was trying to show here, ni NAMNA HAYA MAMBO YANAVYOLISAMBARATISHA TAIFA. nina uhakika wakristo na waislam wakisambaratika, kuna kundi moja(silitaji) litaathirika sana.

Pia, sisi wakristo, tunatoa sadaka. television karibia zoote tatu tulizoanzisha tumechanga na kutoa sadaka. kama hauamini tembelea makanisani. kama unazungumzia radio, asee wakristo karibia kila mkoa kuna radio. na radio zetu sisi hatusambazi chuki kama zile za radio heri na kuran. jaribu kuangalia. hamuna shule nyinyi, mnapendelea biashara tena ya madawa ambayo siku hizi haifanyi kazi. shule za wakristo zimewasaidia sana. Hizo shule ulizo taja hapo zilianzishwa na misikiti? zilianzishwa na misikiti au na nani? tuache hili, JAMANI TUSHIRIKIANE TU, WALA TUSIFIKE MBALI HIVYO. MATENGANO HAYATATUFIKISHA POPOTE.

kwa wale wanaotembelea makanisani, na misikitini, wanajua namna wachungaji karibia wooote, ujumbe wa jumapili siku hizi ni kadhi na oic. sijui huko misikitini kwasababu sijawai kwenda. halitufikishi sehemu yoyote.
 
kwanini asimkaribishe hata mtu mmoja aliyehusika katika kuuandaa huo waraka akasikia walikuwa na malengo gani wakati walipokuwa wanautayarisha...kuliko kutuletea watu ambao wanamawazo ya aina moja..

Haya nayo maneno.
 
Mtaniwia radhi mara nyingi mtu akicoment juu ya kitu huwa naanza kuevaluate ata elimu yake kwanza bse mwaeza mlaumu mtu kumbe ndo upeo wake wa kufikilia ulipofikia hasa uyu ndugu yetu Lusekelo.
Kama kanisa limetoa waraka kwa waumini wake kwako lazima uwe kichefuchefu bse haukuhusu DIRECTLY labda indirectly.Sasa atoa wake kwa waumini wake kama hatasema achaguliwe yeye bse ameoneshwa kwenye maoni kuwa ndiye raisi mtarajiwa wa Tz.
Ni busara kukaa kimya juu ya kitu ambacho haukifahamu kiundani
 
Jamani Lipumba yupi? Huyu huyu ama mwingine?

Waraka wa Kanisa Katoliki: Kingunge alikoroga
• Viongozi Wakatoliki wampinga, watetea waraka wao

na Mwandishi Wetu



HOJA iliyotolewa bungeni juzi na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, ya kuupinga waraka wa Kanisa Katoliki unaowaelekeza waumini wake namna ya kuwachagua viongozi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwakani, imeibua maoni tofauti kutoka katika makundi ya kijamii.
Miongoni mwa watu walioonyesha kuguswa kwa namna ya kushtushwa na msimamo huo wa Kingunge, ni viongozi wa Kanisa Katoliki ambalo liliandaa waraka huo.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Tanzania Daima jana, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, alielezea kauli hiyo ya Kingunge kuwa ni matokeo ya malezi ya kisiasa na kiutawala ndani ya mfumo wa siasa wa chama kimoja, yaliyokuwa yakitawaliwa na utamaduni wa ‘zidumu fikra za mwenyekiti'.
"Kingunge ajue kwamba karne hii ni ya kwenda na hoja. Si karne ya zidumu fikra za Mwenyekiti alizozizoea. Huu ni wakati wa vyama vingi, tuna vyama vya siasa zaidi ya 15, na madhehebu ya dini ni mengi, huwezi kutegemea mawazo yawe ya mtu mmoja, zamani waliamini kuwa kila kitu kitafuata mawazo ya chama kimoja, sasa ni lazima viongozi wakubali mabadiliko na changamoto za hoja tofauti," alisema Askofu Kilaini.
Alisema binafsi anaamini kama Kingunge ambaye alipaswa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono waraka huo unaohimiza kuhusu umuhimu wa kuwachagua viongozi waadilifu, anakerwa kuona watu wengine hata wasiokuwa serikalini, wakitoa mawazo yao kutokana na malezi aliyoyapata kisiasa.
Akifafanua, Askofu Kilaini alisema waraka huo haubagui dini, chama wala tabaka la watu na badala yake, unaimarisha mshikamano na kutoa elimu juu ya uraia na demokrasia katika mchakato wa kupata viongozi safi kwa njia safi.
"Mzee Kingunge na mwingine yeyote anayeuona waraka huo una mapungufu, aseme ili tuurekebishe, atoe hoja kuonyesha kosa lililopo kuliko kusema bila kuonyesha wala kujua kosa liko wapi, aongeze hoja na auonyeshe umma kipengele chenye matatizo, watu wanataka kujenga taifa si hisia, maana hoja nzuri ndiyo njia pekee itakayouondoa waraka huo.
"Wengine nao wakitoa waraka wao kama huu, watasaidia kuunganisha watu; Waprotestanti wakitoa, Waislamu wakatoa, KKKT nao wakatoa na wengine kisha tukachangia hoja kwa pamoja, tutakuwa na umoja na msimamo wenye nguvu katika kuwapata viongozi na kuijenga nchi yetu, hilo ndilo tunalolitaka," alisema.
Hata hivyo, alisema hatua ya wanasiasa kama Kingunge kujitokeza kuupinga waraka huo ni ya kutia moyo kwani kwa kufanya hivyo, wanakuwa chachu ya wananchi wengi kuusoma na kujua kile kilichomo ndani.
"Ninafurahi sana wanapousema maana unasambazwa sana kila tukichapisha, unaisha haraka na hii ni nzuri maana watu wengi sasa wanausoma na kuuelewa kuliko nyaraka nyingine zote tulizowahi kutoa," alisema Askofu Kilaini.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde, alisema tatizo linalozusha maneno ni hatua ya baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa, kuusoma kwa hisia huku wakiwa tayari na mitazamo hasi.
"Mwenye nia njema anapousoma, anauelewa vizuri, lakini hata hivyo, huu si msahafu kwamba usipousoma unavunja maadili ya dini, asiyeupenda halazimishwi kuusoma… Wasomi, wanasiasa na wote wenye mapenzi mema toka dini zote, wausome kwa mwelekeo chanya, watauelewa vizuri," alisema Padri Makunde.
Aliongeza kuwa, kwa asili yake, waraka huo unasisitiza umoja na namna nzuri ya kupata viongozi bora bila kujali ni Mkristo, Mwislamu au Mpagani.
Kuhusu kama kuna uwezekano wa Kanisa Katoliki kubatilisha waraka huo, Padri Makunde alisema kamwe hawawezi kuubatilisha kwa kuwa unahimiza maadili katika jamii.
"Suala linalohimizwa humo ni maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na viongozi safi; tena wanaopatikana kwa njia safi; sasa anayetaka tuubatilishe maana yake anataka kutuambia tubariki ufisadi, rushwa, wizi, ujambazi na mengine kama hayo? Hatuwezi kufanya hivyo, hayo si malengo yetu, vinginevyo basi hakutakuwa na maana ya kuwa na dini," alisema Padri Makunde.
Kwa upande wake, Ofisa Habari wa TEC, Padri Modest Katonto, alisema tatizo analoliona ni baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kushindwa kujadili hoja na badala yake kujikita kumjadili aliyetoa hoja jambo alilosema kamwe halileti tija katika jamii.
Alionyesha wasiwasi wake kuwa, huenda wanasiasa wengi wanaoupinga waraka huo ni wale wanaohofia kupoteza nafasi zao katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2010.
"Nadhani wengi wa wanaoupinga, ni wale wanaohofu kupoteza nafasi zao kutokana na ama kutotenda vizuri wakati wa uongozi wao au namna walivyoingia madarakani.
"Kama utaingia kwa njia halali madarakani na ukatenda kazi ipasavyo, sielewi kwanini uogope waraka huo elimishi. Hii ni kama kuogopa kivuli chako," alisema.
Aidha, wasomi mbalimbali walioshiriki mkutano wa kujadili uandishi wa habari za uchaguzi, uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), jijini Dar es Salaam jana, walitoa maoni tofauti kuhusu waraka huo, huku baadhi yao wakiuunga mkono na wengine kuupinga.
Mhadhiri maarufu wa masuala ya siasa na uchaguzi, Profesa Amon Chaligha, na ambaye pia ni mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), alisema yeye alipata bahati ya kuzisoma mada zote za waraka huo na kujiridhisha kuwa hazina tatizo na wala hazikiuki sheria yoyote ya nchi.
"Hakuna mgongano wowote wa kidini unaosababishwa na waraka huo. Mgongano unaletwa kwa makusudi na watu kwa chuki zao au maslahi yao binafsi au kwa lengo la kutaka kuligombanisha kanisa na serikali. Nimepitia mada zote na hakuna sehemu inasema mchague fulani," alisisitiza Profesa Chaligha.
Kwa upande wake, Profesa Paramagamba Kabudi kutoka Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema anashangaa kuona suala hilo limekuwa zito hivi sasa, wakati waraka huo si kitu kipya kwani Kanisa Katoliki lilishawahi kufanya kitu hicho kwenye miaka ya 1990.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, aliupinga waraka huo wa Kanisa Katoliki, na kuuita kuwa ni sawa na ilani ya uchaguzi, ambayo alidai haipaswi kutolewa na kanisa au taasisi yoyote ya dini, isipokuwa wanasiasa tu.
Naye, Profesa Issa Shivji, alisema anaushangaa waraka huo, kwani kila kundi katika jamii likifanya hivyo, kutakuwa na mvurugano mkubwa nchini.
Wakati maoni tofauti yakitolewa, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavelli Lwaitama, yeye alieleza kushangazwa na hatua ya Kingunge kuushambulia waraka huo wa kanisa.
Akizungumza kwa simu na Tanzania Daima, Lwaitama ambaye alisema amekuwa akimuheshimu sana Kingunge, alimtaka mwanasiasa huyo mkongwe kujitokeza na kuliomba radhi kanisa hilo na Watanzania kwa kutoa kauli yenye mwelekeo wa wazi wa kibaguzi.
Lwaitama, mmoja wa wasomi wenye msimamo mkali, alisema kauli ya Kingunge kuushambulia waraka huo unaohimiza Watanzania kujiandaa kwa ajili ya kuwachagua viongozi waaadilifu na wasio mafisadi, ni ya kushangaza na kushtusha.
"Namheshimu sana Kingunge, lakini kwa heshima napenda niseme bayana kwamba msimamo wake wa kuushambulia waraka wa Kanisa Katoliki unaonyesha dhamira ya kichochezi ya kuligombanisha kanisa hilo na madhehebu mengine na watu wa imani tofauti, jambo ambalo ni la hatari," alisema Lwaitama.
Alisema waraka wa kanisa hilo hausemi mahali popote kuhusu kuwachagua viongozi wa dini yoyote na badala yake unahimiza kuhusu kuchagua viongozi waadilifu, jambo ambalo linapaswa kuhimizwa na watu wa imani na dini tofauti pasipo kusababisha tatizo lolote.
Akichangia hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, iliyowasilishwa bungeni juzi, Kingunge, alilitaka Kanisa Katoliki kuutoa waraka wake ambao umesambazwa kwa waamini wake na kudai kuwa umemsikitisha sana.
Katika hoja zake, Kingunge aliifananisha Tanzania na Lebanon, ambayo imekuwa na mapigano ya Wakristo na Waislamu kwa muda mrefu hivi sasa, kiasi cha kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha, kukimbia nchi yao pamoja na kupoteza mali zao.
Kanisa Katoliki limekuwa na utamaduni wa kutoa nyaraka mbalimbali kama mchango wake kwa maendeleo ya nchi. Mwaka 1989 lilitoa waraka kuhusu tatizo la rushwa, kisha. yalifuata machapisho na nyaraka mbalimbali yakiwamo yanayozungumzia haki juu ya ardhi, magereza, polisi rafiki na nyingine.
Mwaka 1995 lilitoa mfululizo wa vitabu vitano juu ya elimu ya demokrasia shirikishi. Mwaka 2000 kabla ya Uchaguzi Mkuu lilitoa mwongozo wa wahamasishaji katika kujenga ushiriki wa watu ulioitwa ‘Uchaguzi wa Kisiasa Kwanini Tunajali' na Oktoba 2004 kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita, lilitoa chapisho ‘Kwanini Tunajali; Ustawi Kwa Wote?'
Taarifa hii imeandaliwa na Joseph Sabinus, Naishock Piniel Deogratius Temba, Edward Kinabo na Datus Bornface.
Waraka wa Kanisa Katoliki: Kingunge alikoroga
 
kazi kwelikweli,

Mwaka huu mtahahaha huku na kule, lakini lengo ni moja, naona mambo mengine hata nyepesi nyepesi hayastahili!
 
hivi kumbe mnazo shule nyingi ehee, sasa kwanini mwalimu aliwanyang'anya hawa jamaaa? Pili, point of correction,mimi sina chuki ya kidini ya aina hiyo, what i was trying to show here, ni NAMNA HAYA MAMBO YANAVYOLISAMBARATISHA TAIFA. nina uhakika wakristo na waislam wakisambaratika, kuna kundi moja(silitaji) litaathirika sana.

Pia, sisi wakristo, tunatoa sadaka. television karibia zoote tatu tulizoanzisha tumechanga na kutoa sadaka. kama hauamini tembelea makanisani. kama unazungumzia radio, asee wakristo karibia kila mkoa kuna radio. na radio zetu sisi hatusambazi chuki kama zile za radio heri na kuran. jaribu kuangalia. hamuna shule nyinyi, mnapendelea biashara tena ya madawa ambayo siku hizi haifanyi kazi. shule za wakristo zimewasaidia sana. Hizo shule ulizo taja hapo zilianzishwa na misikiti? zilianzishwa na misikiti au na nani? tuache hili, JAMANI TUSHIRIKIANE TU, WALA TUSIFIKE MBALI HIVYO. MATENGANO HAYATATUFIKISHA POPOTE.

kwa wale wanaotembelea makanisani, na misikitini, wanajua namna wachungaji karibia wooote, ujumbe wa jumapili siku hizi ni kadhi na oic. sijui huko misikitini kwasababu sijawai kwenda. halitufikishi sehemu yoyote.

Hata sikuelewi unatetea nini na kupinga nini?. Nimekueleza kwa nini tokea kabla ya uhuru Wakristo wakawa na shule nyingi. Unadhani kama mambo yangewekwa sawa nasi tungekuwa mbali mno. Lakini kwa tangu wakoloni, mpaka Serikali sasa, mtoto mmoja ni Dekwa, anapewa kila kitu na bado analilia hata kile kidogo anachopata mtoto mwingine.

Unapozungumzia kusambaratika sijui kivipi. Lakini kama ni shule zote kurudishwa, hata sisi tutajua tunaendeleaje, kwani unataka sema kila nchi duniani shule ni za Wakristo tu. Sisi tunachotaka ni haki, wala hatutaki kupendelewa.

Kuwa na Radio kila mkoa, na TV tatu ni suala lile lile. Hawa walipendelewa tokea kabla ya uhuru na baada ya uhuru, utawalinganisha na jamii inayo simama yenyewe. Unauliza shule nilizotaja zilianzishwa na misikiti?, zilianzishwa na Waislam.

Jumapili zungumzie kadhi na OIC, hiyo ni haki yenu kwa kuwa kila mtu ana haki ya kufikisha ujumbe bila kuvunja sheria.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom