Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Utatishaje sauti ya umma? Nani anauwezo huo? Serikali kama imechemsha imechemsha tu.
 
Kama hii ni kweli au kama kweli ni hii, basi itakuwa The begining of the end and the end of the begining. Longo live Tanzania.
 
CCM na viongozi wao na hata Serikali JK na uzoefu wake wote wa kuwa madarakai anasahau kwamba wakatoliki ndiyo wamekuwa walinzi wa Nchi hii kwa miaka mingi.Nikiwa na maana kwamba kuanzia Usalama wa Taifa na kwingineko , akina Membe Mseminary , Pinda Mseminary , Mkapa Mseminary na wako wengi kwenye system na hivyo kufanya uhalifu dhidi ya kanisa katoliki si rahisi na hawa watu wote wako very royal kwa uongozi wa Kanisa katoliki.Kumbe ile misaada ilikuwa tisha toto sasa mbona kuna kuumbuka mtu hapa ?

Mkono means what ? Umkamate Kilaini ama Pengo au uvunje makanisa ?

Hapa JF Waseminarist ni lukuki. Hata Kikwete , Dk, Slaa , Dk Chami and so many more ni X seminarians . Ukija kwenye system serikalini, mashirika ya umaa, academics, waandishi etc wako kibao na wako juu. Nothing can be done if they put their voice. God bless Tanzania .
 
Pakacha upo wapi unahitajika utowe ushauri wako
 
Kanisa Katoliki TZ "ituchagulie Marais wanaofaa!"

Yaliyoandikwa katika 'RAIA MWEMA' wiki hii yanadhihirisha maneno ya Padre Sivalone kwamba Tanganyika na Tanzania zimekuwa/zinatawaliwa na kufuata Mfumo Kristo, hususan chini ya kanisa katoliki. Hebu angalia:
(1) Tokea Uhuru tumekuwa na Marais 4 - WAWILI WAKATOLIKI akiwemo aliyedumu miaka 22 madarakani!
(2) VATICAN ni dini pekee yenye "status ya Ubalozi" kuwakilisha maslahi ya wakatoliki na amri za Papa
(3) Kanisa hilo ndio pekee bado lina WAZUNGU WENGI ktk mission centres zao - Msimbazi DAR, Kipalala, Peramiho-Ruvuma, Ndanda-Masasi, Mtwara Parish- Shangani, na kwk.
(4) Papa alialikwa TZ kuzuru kwa gharama ya Watanzania wote - hakuna wasio wakristo waliolalamika "ujio huo mtaka-tifu"
(5) Serikali eti haina dini lakini inapumzika (ofisi zote za Serikali zinafungwa kwa lazima) Jumapili (kwa wakatoliki) na Jumamosi (kwa wasabato et la).
(6) Wakati wa Xmas ofisi zote za serikali zinapambwa na "merry xmas' flyers na kuchapisha makadi ya salaam kedekede pamoja kuangusha miti ya xmas ovyo bila kujali mazingira. Dar A/P xmas carols tokea Dec 1 hadi Jan 31!
(7) Nyerere anapigiwa debe awe "saint" KWA KUITAWALA TANGANYIKA NA TANZANIA KWA MAELEKEZO YA KANISA KATOLIKI kwani ki-dini kafanya nini cha ajabu kustahili kupewa 'utaka-tifu'??

Naam, jibu tumelipata kutoka kwa wakatoliki wenyewe - nchi hii yao, wengine tulie tu .... sasa tunamngojea nominee wa urais 2010 'mkatoliki wa 3' !!
 
Kanisa Katoliki limesimama Kama Vyama vya Siasa, Maana kuna haja hata baadhi ya vyama kuchukua yake mazuri yaliomo kwenye Ilani yao na mkakati yao kwa ajili ya uchaguzi na kuona kuwa wapo makini kiasi hicho
 
Katika thread zote ambazo nimewahi kusoma, sijawahi kusoma pumba kama za thread hii. Moderator angalia wapi unaweza kuizika mapema.
 
Moderator hana haja ya kumtupa nje ya forum. Acha tumpe shule na wenzake wenye ufinyu wa elimu kama yeye.

Ndugu yetu mtoa pumba, ilishawahi kujadiliwa hapa kwamba hakuna nchi duniani ina uhusiano na kitu kinachoitwa nchi ya Vatican. Nchi ya Vatican haijawahi kutoa ubalozi. Kilichopo ni kitu kinaitwa ubalozy wa Papa.

Kuna jamaa alieleza hapa JF tukashangaa lakini tukaelewa. Nimetafuta thread ile lakini siioni ila si unajua siku hizi unaweza kugoogolize na kupata. Tumeipata sasa kazi mwenyewe kusoma. Kama huna uvivu wa kusoma basi usikamatwe na uvivu wa kuelewa.
---------
Click hapa kwenye mabano (Miaka 80 ya Uhuru wa Vatican,, Je ?Ubalozi? unaeleweka?) au soma kila kitu hapa chini:
--------
Miaka 80 ya Uhuru wa Vatican,, Je ‘Ubalozi’ unaeleweka?

Tuesday, 10 February 2009 11:50 administrator

VATICAN City State au kwa kifupi Vatican ni nchi yalipo makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani. Kesho inatimiza miaka 80 ya uhuru iliyoupata kutoka Italy.
Makala hii inatumia fursa hii kufafanua kilichozoeleka kuitwa ”Ubalozi wa Vatican”. Mwisho tutaona kuwa kumbe hawa si mabalozi wa Vatican. Je ni mabalozi wa nini? Nakushauri msomaji tuwe pamoja hadi mwisho.
Si ajabu kukutana na swali kuwa ni nini maslahi ya Ubalozi wa ‘Vatican’ hapa nchini wakati ni nchi ya kidini yaani Kanisa Katoliki.
Je, ni kweli Wakatoliki hatuulizi swali hili? Kwamba muuliza swali akificha jina basi tusidhani kwamba ni mkatoliki?
Hapana. Balozi wa ‘Vatican’ nchini Australia, Askofu Mkuu Charles Daniel Balvo anasimulia kwenye Sheria za Kanisa zinazohusu wawakilishi wa Papa ndani ya kitabu kiitwacho New Commentary on the Code of Canon Law kilichotolewa mwaka 2003 kwa ushirikiano wa Beal, Corriden na Green.
Ameeleza kwamba wakati wa Mtaguso (Vatican II) maaskofu walitaka ufafanuzi zaidi kuhusu kazi za mabalozi hawa baadhi wakipendekeza kuwa mpango wa kuendelea kuwa na mabalozi hauendi na wakati, hivyo ufutwe {Ukurasa. 491, aya ya sita}.
Mtaguso ni mkutano wa maaskofu wote duniani. Hapa nchini, Placidus Gervasius Nkalanga, Askofu Mstaafu wa Bukoba ndiye aliye hai aliyekuwa tayari ni askofu wakati wa Mtaguso. Kipindi hicho alikuwa ni Askofu Msaidizi wa Bukoba wakati Jimbo hilo likiongozwa na Laurian Kadinali Rugambwa.
Kanisa Katoliki ni dhehebu pekee ambalo makao yake makuu ni nchi (Sovereign territory). Kiongozi wa Kanisa (Papa) ndiye Mkuu wa nchi hiyo. Tujikumbushe nchi hiyo ilivyozaliwa.
Kanisa halikumiliki mali wala ardhi, hadi ilipofika mwaka 321BK umiliki uliruhusiwa. Wapo waliotoa majengo na ardhi kuwa mali ya Kanisa. Mnamo karne ya 16 Papa alipewa hata maeneo ambayo ni nchi azitawale. Nchi hizo zilizoitwa Papal States zilienea katikati ya Italy na mbili ndani ya Ufaransa yaani Venaissin na Avignon.
Dunia ilibadilika, Marekani ikajitawala (1776) na mapinduzi Ufaransa yalifuata miaka 15 baadaye. Mapinduzi hayo yaliteka zile Papal State mbili kuzifanya zisiwe tena miliki ya Papa.
Baada ya Ufaransa, huko Italy lilianza vuguvugu la kuunganisha tawala za Italy kuwa tawala moja. Papal States zilitekwa na hadi mwaka 1860 zilishamezwa na Italy mpya kasoro eneo la Roma alimoishi Papa.
Mwaka 1861 Italy mpya iliitangaza Roma kuwa Mji Mkuu na kuuteka Septemba 20, 1870. Hii ndiyo siku iliyofuta Papal States zilizodumu kwa karne kadhaa na mwaka uliofuata, Italy ilimtaka Papa kuwa chini ya mamlaka yake, japo haikumzuia kuteua mabalozi wanaomuwakilisha duniani.
Ilishindikana Papa kuwa chini ya Italy ikabidi abaki ndani ya eneo la Vatican yeye na waliomrithi wakijulikana kama mfungwa ndani ya Vatican. Hali ilibaki hivyo kwa miaka 60.
Hatimaye Februari 11, 1929 makubaliano yalifikiwa kwa jina la Mkataba wa Lateran. Eneo la Vatican likageuzwa kuwa nchi inayojitegemea (sovereign territory) chini ya Kanisa Katoliki.
Vatican ni nchi ndogo iliyozungukwa na jiji la Roma. Mpaka wa Tanzania unazidi kilomita 4,247 wakati unaoizunguka Vatican haufiki kilomita nne. Jijini Mwanza safari ya kutoka Benki Kuu hadi Mkuyuni inazidi ya kuizunguka Vatican.
Dar es Salaam kwenye barabara ya Morogoro, safari ya Fire au Zimamoto hadi daraja la Manzese pia ni zaidi ya kuizunguka Vatican.
Si rahisi kuuelewa ubalozi kwa sababu tu kuna nchi ya ”Vatican”. Ni lazima kujua taasisi iitwacho Holy See.
Sheria ya Kanisa inaifafanua ”Holy See” kwamba ”Holy See” ni Papa na idara zote za Roman Curia katika kuendesha Kanisa zima duniani (Can. 361).
Tayari tuna ufafanuzi kuhusu Vatican kama nchi na Holy See kama kikundi cha viongozi. Inawezekana kufafanua ubalozi katika hatua hii. Lakini pia tujadili hali inayoitwa Sovereignty. Sina hakika UHURU ndiyo tafsiri fasaha kwa neno hili.
Nadharia za Sovereignty zinakubaliana kwamba ni hali ya kuwa na mamlaka ya mwisho kuendesha serikali, nchi au watu. Mihimili kama serikali (executive), bunge(legislative) na mahakama (judiciary) hugawana uhuru huu wa ndani (Internal sovereignty). Majimbo ya Marekani yana uhuru huu wa ndani ambapo si lazima yafanane uendeshaji.
Uhuru wa kimataifa (External sovereignty) ni hali ya kutambulika na mataifa mengine pia kukidhi vigezo vya sheria za kimataifa (International laws).
Uhuru huu (Sovereignty) unaviweka wapi vyombo viwili, nchi ya Vatican na kingine kikiwa Holy See?
Vatican ina ardhi kama Tanzania japo ni ndogo. Tanzania ina haki ya kuweka mabalozi nchi za nje. Haki hii inaenda kwa Vatican City pia. Ni wazi ubalozi wao yabidi uitwe ”Ubalozi wa Vatican” (Vatican Embassy) na si vinginevyo.
Jambo la msingi kutambua ni kwamba, Holy See ndiyo inayosimamia mahusiano ya kidiplomasia kwa mujibu wa sheria za kimataifa, pia kupokea na kutuma mabalozi na wala si Vatican City State. Hivyo kuanzia sasa halitatumika tena neno “Ubalozi wa “Vatican” badala yake neno “Holy See” litatawala makala hii.
Ni haki kudadisi kwa nini Vatican isitoe mabalozi, jukumu hilo lifanywe na Holy See. Turejee neno Sovereignty tukiiangalia Holy See, uongozi wa Kanisa tangu kale. Papa au Holy See wameteua wawakilishi tangu karne ya nne.
Holy See imetambulika bila kuingiliwa kabla ya karne ya 16. Tumeona ilivyopata nchi zake, yaani Papal States. Ilipokuzwa dhana ya uhuru (Sovereign State), Holy See iliendelea kutambulika tayari ikiwa na Papal States. Ferdinando Cardinal d'Adda amekuwa balozi wa Papa (Holy See) nchini Uingereza Machi 03, 1687.
Kuepusha magomvi, mwaka 1815, Ulaya walikubaliana kuipitia upya ramani ya bara hilo katika mkutano wa Vienna (Congress of Vienna-1815). Kifungu (article) cha nne cha maamuzi kilimpa Nuncio au mwakilishi wa Papa (Holy See) hadhi kubwa ya kidiplomasia (dean) katika nchi anayopelekwa.
Papal States zilipofutwa na Italy (1870-1928), mapapa hawakuwa tena na nchi. Wala Vatican walimoishi haikuwa nchi. Kipindi chote hicho (miaka 60), Holy See imeendelea kutambuliwa uhuru wake (Sovereignty) na kupokelewa mabalozi wake walioteuliwa na Papa.
Pia mwaka 1961 Umoja wa Mataifa ulitoa makubaliano mapya ya kidiplomasia (Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961). Wawakilishi wa Papa wametajwa kwenye vifungu 14(1)(a) na 16(3). Balozi za Holy See huitwa Apostolic Nunciature of the Holy See.
Kuzaliwa kwa Vatican kuliiongezea Holy See chombo kingine huru (Sovereign) kwa vigezo vya kimataifa. Holy See ina umri wa karne nyingi. Vatican ndiyo kwanza inafikisha miaka 80. Hivyo, Holy See ni mzoefu mzuri duniani kwa masuala ya ubalozi kama si mmoja wa waanzilishi. Uhusiano wake (Nunciature) nchini Iraq ulianza Disemba 17, 1832 na Askofu Mkuu Henri-Marie Amanton akiwa mwanzilishi katika hadhi ya Apostolic Delegate. Holy See duniani ina ubalozi kwenye nchi 173, baadhi ni Iran, Yemen, Sudan, Morocco, Brazil n.k.
Holy See ina mahusiano maalum kwa Palestina na Russia. Pia ina mahusiano ya kibalozi na taasisi isiyo na nchi, lakini inatambulika huru iitwayo Sovereign Military Order of Malta (SMOM).
Vatican na Holy See ni vitu viwili tofauti vilivyo huru. Holy See imeteua mabalozi karne nyingi na imeendelea hivyo hata baada ya kuzaliwa Vatican City State.
Kwa uhuru (Sovereignty) uliopo Holy See na Vatican City State kila moja zaweza kutoa pasi za kusafiri (passport). Udogo wa Vatican na shughuli za Holy See havileti mazingira ya utoaji pasi mara kwa mara. Inapotokea, Holy See hutoa pasi maalum (Diplomatic passport).
Vatican City kama nchi yaweza kutoa pasi za kawaida (normal passports) japo yaelekea hilo limekabidhiwa kwa Holy See pia. Mahujaji kwenda Vatican hupata viza ya Italy kwenye ubalozi wa Italy.
Vatican City haijatangaza utaratibu wa kuteua mabalozi wakati utaratibu wa Holy See umo kwenye sheria za Kanisa, mabalozi wakiwa aina ya wawakilishi wa Papa au Papal Legates (Can. 363-367).
Hivyo ni vigumu kuhoji kwa nini nchi iwe na ubalozi wa Holy See. Yapo mawazo yanayofananisha kwa kuuliza ‘Mbona tuna ubalozi wa Vatican ambayo ni nchi ya kidini’?
Jibu la kwanza ni kwamba, hakuna ubalozi wa Vatican ila kuna ubalozi wa Holy See. Jibu la pili linahitaji msaada wetu tulio wakatoliki. Hata Vatican na Holy See zisitambuliwe kimataifa, bado mwakilishi huyu (Nuncio) anahitajika penye wakatoliki (Can. 362).
Nafasi yake kwa wakatoliki haitaathirika na kutotambuliwa huko. Masuala yetu atayafikisha kwa Papa kama kawaida. Itakayopotea ni hadhi yake ya kiubalozi tu.
Yeye ni sehemu ya utaratibu wa Kanisa. Nchi kuikubali hali yake ya kibalozi si suala la wakatoliki wala watanzania. Ni suala la Umoja wa Mataifa chini ya mkataba wa Vienna wa mwaka 1961.
Hivyo, swali hili halina tija kuwauliza wakatoliki au viongozi wa nchi ya Tanzania. Swali hili mahala pake ni Umoja wa Mataifa unaoweza kulijadili kwa uthabiti wa hoja itakavyojengwa.
Kila la heri Vatican City State kufikisha miaka themanini.

http://www.changamoto.co.tz/index.p...a-joseph-misango&catid=37:getaways&Itemid=154--------
 
...
(6) Wakati wa Xmas ofisi zote za serikali zinapambwa na "merry xmas' flyers na kuchapisha makadi ya salaam kedekede
Hata template ya JF huwa na mapambo ya X-Mass, lakini bado kila siku utaona member wapya wanajiunga JF, Wamisheni na Wanyenyekevu. Nilitegemea Wanyenyekevu hawatajiunga, lakini wanajiunga halafu wanakuja kutusumbua humu kwa malalamiko kama hili ulilolileta !!
 
Mzee Mwanakijiji,

Naona wanajf wote waliochangia hii mada hawajakuelewa unachotaka wakielewe. Nyaraka hizo mbili hakuna hata moja inayosema DINI fulani siyo nzuri kati ya tunazozijua. Vita unapigwa UFISADI, sasa sijui kama kuna dini inayopendekeza ufisadi ambayo wanaona inapigwa vita hata kutoa laana!

Wan JF tafakari yaliyomo kwenye nyaraka kabla hujachangia ili usitupotezee muda kwa kwenda nje ya mada. Mimi ninaamini 'oposition' kwenye mada hii zingekuwa UFISADI NI MZURI na kuupamba, kuuremba na kuukumbatia siyo kuagiza TEC wakaanzishe Chama, sidhani kama huko ndio wanakoelekea.
 
Kama hii ni kweli au kama kweli ni hii, basi itakuwa The begining of the end and the end of the begining. Long live Tanzania.[/Q

Put it this way: "PEOPLE ARE BORED OF STABILITY!!!

You have said it all Mkuu. They want to taste something bitter, and there after they will know that what they had was sweeter than nothing. Tunafanya ujinga huku tukiangalia. I never imagined kama tutafika kujadili ujinga huu wakati Taifa lina mamilioni ya mambo ya kujadili. Sijui hii ndio distraction au........
 
Hapa kanisa linataka tumia kero kukidhi mahitaji yake, imechukua mambo yanayo wagusa wananchi ili kutimiza agenda wanayoijua wenyewe...wanasiasa wanatupiga changa la macho, makanisa nayo yanapanga kutuhadaa, wana create nafasi ya kujinufaisha au kwa vile DECI imepigwa stop, wamishionari mmerudi na mbinu mpya? yaleyale mnagawa mitumba ili mlambe almasi.....kanisa limetupa chambo hapo au? Time will tell.

Programu hii ya kichungaji inahitaji uongozi mzuri na hatua madhubuti za ufuatiliaji. Hapo tutaweza kufanikiwa na kuleta matokeo katika maisha ya Jumuiya ya Kanisa na ya taifa letu.

Katika hatua ya utekelezaji wa programu hii tunapendekeza:

3) Katika kazi ya kuongoza mkutano (no. 1), wajumbe wa CPT na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi.
kanisa (CPT) na serikali , wawakili wa dini nyingine hawatakiwi au ni siri ya kanisa na serikali?

1) Ripoti za majadiliano hayo zitumwe Parokiani (Paroko na Halmashauri) kila baada ya miezi mitatu. Ripoti hizo zionyeshe mambo yaliyojadiliwa na maamuzi yaliyofikiwa. kwanini

1) Umuhimu wa uongozi wenye maadili katika kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini katika Tanzania.
Hao wafisadi siku zote wako nao kwenye nyumba za ibada, na ndio wachangiaji wakubwa wa shughuli zao za kiroho, ndio wanaokaa viti vya mbele kwenye mikutano yao ya kiroho, ndio kimbilio la viongozi wa nyumba za ibada kunapokuwa na matatizo. Leo eti wanawapiga vita hao mafisadi, walikuwa wapi siku zote kama siyo ku-take advantage ili kupitisha agenda yao?

kitega uchumi cha kanisa (DECI) kimeliza wangapi? kuna akina Kakobez,mama Rwakat n.k. Jamani makani yanatikiwa kuwa mfano, watu wamegeuza kanisa dili, ya kaisari wanampa mungu na ya mungu wanampa kaisari..
 
Unajua mlima Kilimanjaro ni mrefu kuliko yote duniani? Ila inategemea your bench Mark aka point of reference?

Point of reference yangu imenipelekea kuhoji hiyo busara ya Mkandara maana siioni asilani abadan na ndio maana nashangazwa unapomuweka ktk orodha ya watoa nondo. Au labda mzee unafanya masikhara na kumtia ujinga kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa?
 
Katika thread zote ambazo nimewahi kusoma, sijawahi kusoma pumba kama za thread hii. Moderator angalia wapi unaweza kuizika mapema.

Akimaliza homework tuliyompa ya kusoma mambo ya Vatican atujulishe kama ameelewa halafu ndipo tumpe nyingine kuhusu Mahakama ya Kadhi.

Tukimpatia kwa mkupua jamaa alivyo kilaza ataishia kuchanganyikiwa. Sina unajuwa hawa wakichanganyikiwa wanzaba vibao viongozi wastaafu wakati wa ibada zao.
 
Huo ni "MPANGOMZIMA" ni wa kichama wala si dini kwa vyovyote dini haiwezi kufanya kazi
Wakitaka kufanya kazi waanzishe "CHRISTIAN....PARTY" wananchi tutawachagua kwa maelezo yao yote waliyotoa
a) Elimu anato walei (sijui ni nani?) anaripoti kwa padre anawaelimisha wanaparoko ..common sense inakupa kwamba lazima awe na conlict of interest anatoa directive indirectly kwamba mchague mkiristo the whole issue ni nonsense..ni ubaguzi wa kijinga kwelikweli...lakini yakija kama ploitcal party (WAACHE UNAFIKI) tutawachambua kama tunavyofanya kwa DP ya mtikila..without any problem
b) Haya mambo ya kujificha kwenye "NYASI FUPI" huku unaonekani ni UNAFIKI.

Kama ungekuwa wewe, obviously ungefanya hivyo unavyodai. Lakini si hivyo kwa mpango huu. Niambie kama ulishahudhuria 'civic education' yeyote katika levels zilizotajwa na ukakuta madudu hayo unayosema.

Binafsi nimeshiriki na kinachotolewa ni hasa elimu ya jumla ya kujenga dhamiri ya mtu katika kuchagua kitu kwa kuzingatia mfano uwezo wa kuongoza na maadili ya kiongozi husika. Na njia inayotumika ni ile ya kuwawezesha wananchi wenyewe waweze kugundua matatizo yao na uyatafutia ufumbuzi.

Hatua zilizotajwa - jumuiya, kigango, parokia, taifa - ni hasa katika kupima 'effectiveness' yake: mfano, kama matatizo yatakayojitokeza yatafanana na au yatatofautiana na kwa nini na pia kutokana na hayo, muda ujao mambo gani yazingatiwe ili 'civic education' iende vizuri.

Lakini kwa vile unasoma miongozo hiyo 'with a bias' kwa vyovyote lazima upotoshe kusudi lake kama unavyofanya. Lakini kama msemaji mmoja alivyoeleza hapo juu hebu toa mstari/paragraph/chapter inayosema kuwa mpango huo unahamasiha Wakatoliki kuchagua viongozi kwa misingi ya udini (kutowachagua waislamu) katika uchaguzi ujao 2010.
 
Hapa kanisa linataka tumia kero kukidhi mahitaji yake, imechukua mambo yanayo wagusa wananchi ili kutimiza agenda wanayoijua wenyewe...wanasiasa wanatupiga changa la macho, makanisa nayo yanapanga kutuhadaa, wana create nafasi ya kujinufaisha au kwa vile DECI imepigwa stop, wamishionari mmerudi na mbinu mpya? yaleyale mnagawa mitumba ili mlambe almasi.....kanisa limetupa chambo hapo au? Time will tell.

Programu hii ya kichungaji inahitaji uongozi mzuri na hatua madhubuti za ufuatiliaji. Hapo tutaweza kufanikiwa na kuleta matokeo katika maisha ya Jumuiya ya Kanisa na ya taifa letu.

Katika hatua ya utekelezaji wa programu hii tunapendekeza:

3) Katika kazi ya kuongoza mkutano (no. 1), wajumbe wa CPT na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi.
kanisa (CPT) na serikali , wawakili wa dini nyingine hawatakiwi au ni siri ya kanisa na serikali?

1) Ripoti za majadiliano hayo zitumwe Parokiani (Paroko na Halmashauri) kila baada ya miezi mitatu. Ripoti hizo zionyeshe mambo yaliyojadiliwa na maamuzi yaliyofikiwa. kwanini

1) Umuhimu wa uongozi wenye maadili katika kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini katika Tanzania.
Hao wafisadi siku zote wako nao kwenye nyumba za ibada, na ndio wachangiaji wakubwa wa shughuli zao za kiroho, ndio wanaokaa viti vya mbele kwenye mikutano yao ya kiroho, ndio kimbilio la viongozi wa nyumba za ibada kunapokuwa na matatizo. Leo eti wanawapiga vita hao mafisadi, walikuwa wapi siku zote kama siyo ku-take advantage ili kupitisha agenda yao?

kitega uchumi cha kanisa (DECI) kimeliza wangapi? kuna akina Kakobez,mama Rwakat n.k. Jamani makani yanatikiwa kuwa mfano, watu wamegeuza kanisa dili, ya kaisari wanampa mungu na ya mungu wanampa kaisari..

Hayo una'critise' yako kwenye 'context' ya kuendesha hiyo 'programme'. Yaani, mfano, kama Parokia fulani wakianza kutoa mafunzo hayo wawaalike wana CPT (ambao ni wataalamu) ili kuweza kufafanua baadhi ya vipengere ambavyo wanaofuata mafunzo hayo wanaweza kuwa na maswali navyo.

Katika CPT kuna lawyers, economists, journalists, walimu, etc. Kwa hiyo, kama hao wapo, maswali yanayohusu uchumi yatajibiwa na wataalamu wa uchumi na yale ya sheria na wanasheria wenyewe. Ni katika 'context' hii.
 
Tukimpatia kwa mkupua jamaa alivyo kilaza ataishia kuchanganyikiwa. Sina unajuwa hawa wakichanganyikiwa wanzaba vibao viongozi wastaafu wakati wa ibada zao.
Si ajabu sasa hivi ameshaanza kutafuta ratiba za shughuli za wiki hii za viongozi wastaafu ili ahudhurie "akarekebishe microphone" !!! 😀
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom