Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na waraka wa maaskofu.

Labda watuambie kwamba Yesu aliwaelekeza wafuasi wake wamtumikie kaisari wa aina ipi??? Yeye alisema ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Alijua kwamba kuna kila aina ya kaisari duniani hivyo Yesu alijua pia namna ambavyo kaisari huwa anapendwa kwa uoga na si upendo wa dhati kwani hawezi kumfurahisha kila mmoja.

Siitetei serikali mbovu ila natetea UMOJA wa kitaifa usio na itikadi za kiimani wala kinasaba.

Hata kama tuna matabaka tofauti ktk kuabudu lakini hicho si kigezo cha kuchochea ubaguzi wa kifikra.
 
Hii mikakati ya kanisa sasa inajitokeza ,ninavyowasoma wakatoliki wanakasumba mbaya sana ,kuwa hapa duniani ni wao tu na wanao uhuru wa kumuua yeyote yule ambae si mkatoliki,ukisoma kitamu cha mauaji ya Mwembe Chai utaona mwandishi ni jinsi gani ameweza kuonyesha msimamo wa wakatoliki na makanisa mingine ,inaonyesha wakifanikiwa kuwaweka pembeni Waislamu watawageukia wenzao.
hapo basi mkuu nahisi itakuwa hatari,wapo in-direct hali hii jee....!!!!! tuyaone..
 
Swwali kubwa ni kwamba, wy now? Jibu ni kwamba kuna ombwe (vacum) la kiutawala
 
Swwali kubwa ni kwamba, wy now? Jibu ni kwamba kuna ombwe (vacum) la kiutawala

Hilo ndilo ulilo sahau blame on Kikwete! kunya anye mwingine kuzoa azoe JK una lako jambo wewe!
 
Na wewe Halisi acha udini, hiyo "siri nzito" ipo wapi? wakati content ya habari inaonyesha waraka umesambazwa, unauzwa na kugawiwa bure!

Umeileta habari kishabiki shabiki na ki udini udini shame on you!

We Masatu, wewe!!! shame on you!, huo udini udini upi? Nakuaminia mkuu wewe ni mtu mweledi unayeweza kujua katika hiyo thread hakuna hata nukta moja ya neno niliyoweka, sasa hapo unanihukumu kwa lipi? na huo udini upi na dini ipi? Halafu tukirejea kwenye source ya habari husika utaona kwamba hata wao kichwa cha habari kimelenga kuwafahamisha wasomaji wao wengi na hata hapa JF unaona wengi ni wale ambao hawajawahi kusoma hiyo ILANI na waliosoma pengine wapo ambao hawajapata vionjo vyake. Mfano ni Mbunge aliyechangia bungeni huku akiwa hajawahi kuusoma waraka husika. Tafadhali tafakari kwanza.
 
''The maximum amount of posts on this page can display has been reached. Posts will now start to disappear from oldest to newest''
​

Hii kitu inanikera sanaaaaaaa!! Naomba mods muangalie jinsi ya kurekebisha hili, yaani hata post ya kwanza sijasoma inaniambia habari za kuexceed max ammt of posts, sasa nitachangiaje?
 
Hilo ndilo ulilo sahau blame on Kikwete! kunya anye mwingine kuzoa azoe JK una lako jambo wewe!

Sasa NIMEKUELEWA uko right. Unaweza kuendelea na mjadala
 
Mkuu Halisi.
usirudi nyuma,endelea kutupa vitu,mimi binafsi hii kitu ndo kwanza naipata.. tupo pamoja na wewe..Amani ya bwana iwe nawe mkuu..
 
Halisi,

..nadhani ulichokosea ni jinsi ya kuwasilisha thread yako.

..ungeweka bayana kwamba heading ya thread yako inawa-quote gazeti la raiamwema.

..nadhani raiamwema wameamua ku-sensationalize tu, lakini mambo yote yaliyopo ndani ya habari yao yamekuwa yakizungumziwa mitaani kwa muda mrefu tu.

..halafu ni siri gani hiyo inayowekwa ktk maandishi na kuandaliwa waraka? binafsi nimeshangazwa na jinsi raiamwema walivyoitoa habari hii.

..kwa maoni yangu waraka wa Kanisa Katoliki ungekuwa mzuri na INCLUSIVE kama ungeepuka suala la mahakama ya Kadhi.

..nadhani kwa kulitumbukiza suala hilo[mahakama ya kadhi] ktk waraka wao Maaskofu, na walioandaa waraka huo, wameshindwa kuisoma hali ya kisiasa na kijamii iliyoko Tanzania sasa hivi.
 
Duh! sasa hili kanisa karibu litachukua nchi!!

Tungekuwa wote tunajadili kitu tunachokielewa ingekuwa vizuri. Lakini baadhi yetu tunajadili hoja kutoka 'secondary sources' au maoni ya wengine. Ni kitu cha hatari sana kufanya hivyo na always tutakuwa kwenye matatizo.

Nilichogundua ni kwamba baadhi ya wachangiaji wamehamasishwa kupotosha ukweli ulioelezwa kwa kuleta hisia zao na 'inferiority complex' yao. Na ni kitu cha ajabu kabisa mtu mwenye akili timamu kufanya hivyo!
 
Hii mikakati ya kanisa sasa inajitokeza ,ninavyowasoma wakatoliki wanakasumba mbaya sana ,kuwa hapa duniani ni wao tu na wanao uhuru wa kumuua yeyote yule ambae si mkatoliki,ukisoma kitamu cha mauaji ya Mwembe Chai utaona mwandishi ni jinsi gani ameweza kuonyesha msimamo wa wakatoliki na makanisa mingine ,inaonyesha wakifanikiwa kuwaweka pembeni Waislamu watawageukia wenzao.

huna hoja hapo labda sema kingine
 
MagobeT,

..nimeona wengi wamechangia kwa kufuata heading ya thread na siyo content ya thread.

..nina mashaka sana kama taasisi secular, mfano CHUO KIKUU, wakiandaa waraka wa uchaguzi, watakuja na kiti tofauti sana na huu waraka wa Kanisa Katoliki.

..misikiti na makanisa ndiyo ina mtandao mkubwa mpaka vijijini inayoweza kui-challenge CCM. vyama vya upinzani vimeshindwa kuwaelimisha wananchi haki zao za kiraia na wajibu wao wakati wa uchaguzi.

..binafsi nategemea waraka huu wa Kanisa, na mwingine tunaotarajia utatolewa na Waislamu, utasaidia kuwaelimisha wapiga kura kabla ya uchaguzi 2010.
 
Hebu give us a break mazee..Sisi wakatoliki tumewakosea nini? Kama imani na nyie mnazo zenu..kama elimu ya uraia wote sasa wanataka kutoa..au mtuambie mnalo jingine au ndo kijiba cha roho? chawachoma kotekote?
 
Waislam wakitoa waraka anaweza kufungwa mtu au hamlijui hilo ? Bora tuende hivihivi kila mtu akili kichwani mwake ,labda ndugu zetu wakubwa wa Kikiristu wameshajipima nguvu na wanaweza kukabiliana na kupambana na yeyote yule atakaejaribu kuwasimamisha hivyo wakati muwafaka umefika wa kuanza kugonga gonga hodi hadi ikulu.
 
Halisi,

..nadhani ulichokosea ni jinsi ya kuwasilisha thread yako.

..ungeweka bayana kwamba heading ya thread yako inawa-quote gazeti la raiamwema.

..nadhani raiamwema wameamua ku-sensationalize tu, lakini mambo yote yaliyopo ndani ya habari yao yamekuwa yakizungumziwa mitaani kwa muda mrefu tu.

..halafu ni siri gani hiyo inayowekwa ktk maandishi na kuandaliwa waraka? binafsi nimeshangazwa na jinsi raiamwema walivyoitoa habari hii.

..kwa maoni yangu waraka wa Kanisa Katoliki ungekuwa mzuri na INCLUSIVE kama ungeepuka suala la mahakama ya Kadhi.

..nadhani kwa kulitumbukiza suala hilo[mahakama ya kadhi] ktk waraka wao Maaskofu, na walioandaa waraka huo, wameshindwa kuisoma hali ya kisiasa na kijamii iliyoko Tanzania sasa hivi.

Hata hilo la Mahakama ya Kadhi limechukuliwa 'out of context'. Waraka unasema hivi kwa sehemu hiyo:

2) Marekebisho ya Katiba
......
Katiba inamilikiwa na watu na ni ya watu katika anuwai (diversity) na katika upokeaji wa watu wenye tofauti mbalimbali (plurality). Kwa kuwa taifa ni kitu kinachoishi ni jambo la kiasili na la muhimu hivyo ni sharti kuruhusu mapitio ya vipindi kwa vipindi yafanyike ili kuwapa watu fursa keleza maoni yao.

.......
Kuhusiana na swala hili tungependa masuala haya yapewe kipaumbele:

.......

- Kuheshimu Kanuni ya kuwa Serikali haina dini na kutoruhusu taasisi za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi (mfano, Mahakama ya Kadhi na uanachama wa OIC).

Maelezo:

...... inaonyesha maneno niliyoacha!
 
ndio kuamka kwenyewe huko sema sio sasa mnajigawa muungane na viongozi wa kiislamu hili muwajibishe viongozi sio kuanza kutengana kwamba dini hii inapendelewa kushinda hii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom