Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Watuambie kama Zanzibar ni nchi au si Nchi au hawakugusia mambu ya Muungano ?
 
ndio kuamka kwenyewe huko sema sio sasa mnajigawa muungane na viongozi wa kiislamu hili muwajibishe viongozi sio kuanza kutengana kwamba dini hii inapendelewa kushinda hii.

Mzee wewe umeongea la maana..Kinachotakiwa ni ku-harmonize hizi efforts kama kweli nia ni kuwasaidia wananchi wanyonge nadhani hakutakuwa na migongano isiyo ya lazima.. Najua itakuwa ngumu kwa kuanzia maana watu kwenye mambo ya dini huwa wanaacha kuwa sober kidizaini, watu hata ambao hukuwategemea..lol
 
MagobeT,

..suala la OIC na Kadhi halijadiliki sasa hivi bila watu kukimbilia majoho yao ya udini-udini.

..waraka huu utawatenga Waislamu kwasababu ya hoja hiyo ya Kadhi na OIC.

..hata Wapalestina na Waisraeli wanapofanya mazungumzo hatima ya mji wa Jerusalem huachwa kando kwanza.
 
Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na waraka wa maaskofu.

Labda watuambie kwamba Yesu aliwaelekeza wafuasi wake wamtumikie kaisari wa aina ipi??? Yeye alisema ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Alijua kwamba kuna kila aina ya kaisari duniani hivyo Yesu alijua pia namna ambavyo kaisari huwa anapendwa kwa uoga na si upendo wa dhati kwani hawezi kumfurahisha kila mmoja.

Siitetei serikali mbovu ila natetea UMOJA wa kitaifa usio na itikadi za kiimani wala kinasaba.

Hata kama tuna matabaka tofauti ktk kuabudu lakini hicho si kigezo cha kuchochea ubaguzi wa kifikra.

Mtu yeyote anayeshindwa kusoma na kuelewa lengo zuri la waraka nashindwa hata kumwelewa! Ninachoona mimi ni chuki inayopikwa dhidi ya Kanisa Katoliki.

Hakuna 'justification' yoyote ya kupinga kilicho kwenye waraka 'unless' anayefanya hivyo ana tatizo au hoja yake binafsi na siyo yaliyosemwa kwenye waraka! Kweli mtu mwenye akili timamu achukie na aendelee kupotosha ukweli unaotetea utaifa, unaopiga vita viongozi kuchaguliwa kwa misingi ya dini, chama au kabila na siyo maadili, utu na uwezo wa kuongoza!

Hapa wachangiaji wenzangu mnaniacha hoi kabisa! Kwa hiyo, mlitaka Kanisa liseme: chagueni watu kwa kufuata dini ya mtu, chama chake au kabila lake na asiye mwadilifu na asiye na sifa za uongozi? Hivyo ndivyo mnavyohamasishwa kufanya?
 
Tatizo la sisi Waafrika ni ROHO MBAYA yani ndivyo tulivyo wala hakuna mwafrika mwenye udini Ila roho mbaya ndiyo inajificha ktk miavuli ya udini,ukabila kwa kuamusha hamasa watu wako ili wapate kuiunga roho mbaya na hili nalo ndilo tatizo kuu letu mpaka tukafika sisi ndivyo tulivyo.

kwa asilia na kwa asilimia kubwa sisi waafrika hatupendi mamba ama fikira nzuri zitoke kwa jirani wengi watajitahidi kwa kila hila ,mali ili wazifupishe safari njema.

Tumeona enzi zile kuteuliwa tu kuingia kidato cha kwanza ilikuwa kizaa zaa kijijini na sio kwa heri bali kwa chuki na fitina kuu.

Sisi ndivyo tulivyo ni wanafiki wakuu hatuna atom za kuzipa jitihada halali za maendeleo zinazofanywa na watu/viongozi wetu bali tupo kuziweaken tu ili tuendelea kubaki ndivyo tulivyo.Mfano Haiwezekani kabisa Rais JK hajafanya mambo mazuri,huyu jamaa kafanya mambo mazuri tu mengi na mabaya ambayo mwanadamu hawezi kuyakwepa.

Pili juhudi za KANISA ni juhudi sahihi ambazo kila vikundi vya dini vingeiga na kuendeleza libeneke lilelie lakini badala yake vinaanzishwa vikundi vya kuyapinga yaliyo sahihi na kama hayako sahihi hao wanaopinga wangeiliita kanisa wakaketi na wakatoa kitu kilicho bora zaidi.Lakini kwa vile ndivyo tulivyo hatuna tabia ya kuiga mema bali uzoefu unaonyesha tuna tabia ya kupinga mema na kuiga maovu.

Naomba niludie tena Afrika hakuna mtu mwenye UDINI ila ni roho mbaya ya watu husika kuificha roho mbaya nyuma ya pazia la udini/ukabila n.k.
 
Mashehe, Maaskofu, Mapadri, Wachungaji, Ma-Rabi, n.k.. wakiungana kuhamasisha waumini/wafuasi wao kuchagua viongozi wanaofaa, itakuwa njia mojawapo madhubuti ya kuwafanya viongozi wetu waanze kuwajibika, kwani pungufu ya hilo ni kuwang'oa wababaishaji nyakati za uchaguzi!
 
Mkiambiwa kuwa Tanzania kuna udini (ili tiba ya ugonjwa huu itafutwe) mimacho na mipovu inawatoka. Maoni ya baadhi ya wachangiaji hapa yanaoenyesha kuwa waafrika (ambao ni wadini ila wakiambiwa ukweli kuwa wao ni wadini wanakataa) ndivyo walivyo.
 
Na hao hao viongozi wa dini pia wawe wa kwanza kuwalaani na kuwakumbushia dini zao zinakataza wizi na utapeli viongozi wanaofuata dini zao.sio mbaya padri akimkumbushia mstari wa dini kiongozi wa nchi ambaye mkristow wakati anapofanya kosa kama (ufisadi) na pia sio mbaya kwa shekhe kufanya hivyo hivyo kwa kiongozi wa nchi ambaye ni muislamu.na wakiowaona viongozi kwenye majumba yao ya ibada ijumaa na jumapili wawakumbushie uongozi bora huko vipi na yapi dini zinakataza labda viongozi wetu wanaweza kumuogopa mungu.manake maovu yanayofanywa na viongozi wetu nchini mtu unaweza kujiuliza kama wana dini au la.
 
Hii mikakati ya kanisa sasa inajitokeza ,ninavyowasoma wakatoliki wanakasumba mbaya sana ,kuwa hapa duniani ni wao tu na wanao uhuru wa kumuua yeyote yule ambae si mkatoliki,ukisoma kitamu cha mauaji ya Mwembe Chai utaona mwandishi ni jinsi gani ameweza kuonyesha msimamo wa wakatoliki na makanisa mingine ,inaonyesha wakifanikiwa kuwaweka pembeni Waislamu watawageukia wenzao.
kwa wakatoliki inashangaza kwa sababu wao wenyewe hawana mfumo wa kuchaguana.sasa hiyo democrasia wanaijuaje wakati wao wenyewe hawana ndani ya dini yao.Huu ni unafiki Hata hivyo nadhani tatizo ni serikali kwa sababu ilitakiwa kutolewa kauli ya kukemea hilo kwani viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa ni kuhatarisha amani ya nchi wao wahubiri neno la mungu.ya kaisari wamuachie kaisari.
 
Mkiambiwa kuwa Tanzania kuna udini (ili tiba ya ugonjwa huu itafutwe) mimacho na mipovu inawatoka. Maoni ya baadhi ya wachangiaji hapa yanaoenyesha kuwa waafrika (ambao ni wadini ila wakiambiwa ukweli kuwa wao ni wadini wanakataa) ndivyo walivyo.

Ngoja ni kwambie kama yule waziri Sumari alivyomwambia Dr Slaa; "nawewe nawe tafuta hoja nyingine." Kila post yako lazima sentensi hiyo iwemo. Kwenye huo waraka hebu tuambie udini uko wapi? Mwizi hudhani kila mtu ni mwizi. cheating spouse hufikiri na mwenzie ni cheater. Sasa wewe kwasababu una udini unadhani watanzania wote wana udini.
 
Watuambie kama Zanzibar ni nchi au si Nchi au hawakugusia mambu ya Muungano ?

Wewe naye sasa uambiwe nini usichofahamu? Zanzibar si nchi ni mkoa ulioko ndani ya Tanzania. Kama mnataka iwe nchi ni kuondoka ndani ya Muungano. Vinginevyo zoeeni kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Waislam wakitoa waraka anaweza kufungwa mtu au hamlijui hilo ? Bora tuende hivihivi kila mtu akili kichwani mwake ,labda ndugu zetu wakubwa wa Kikiristu wameshajipima nguvu na wanaweza kukabiliana na kupambana na yeyote yule atakaejaribu kuwasimamisha hivyo wakati muwafaka umefika wa kuanza kugonga gonga hodi hadi ikulu.

nah...wewe tutakuita "terrorist" au hujui hilo......tena ile sheria ipo..wee jaribu uone...........
 
kwa wakatoliki inashangaza kwa sababu wao wenyewe hawana mfumo wa kuchaguana.sasa hiyo democrasia wanaijuaje wakati wao wenyewe hawana ndani ya dini yao.Huu ni unafiki Hata hivyo nadhani tatizo ni serikali kwa sababu ilitakiwa kutolewa kauli ya kukemea hilo kwani viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa ni kuhatarisha amani ya nchi wao wahubiri neno la mungu.ya kaisari wamuachie kaisari.


Nani kakwambia hatuchaguani? Mkikosa hoja mnaanza vioja na kuleta komedi humu jamvini. Unasema demokrasia kwenye dini? Hivi una akili timamu weye? Yaani unataka tuanze kuyapigia kura maagizo ya Mungu? Kafanye hivyo kwenye dini zenu za porini period!
 
Ngoja ni kwambie kama yule waziri Sumari alivyomwambia Dr Slaa; "nawewe nawe tafuta hoja nyingine." Kila post yako lazima sentensi hiyo iwemo.

Hayo mamlaka uliyojipatia ya kunichagulia cha kuandika hapa yaishie hapo kwenye kibodi yako ......... Asante.

Kwenye huo waraka hebu tuambie udini uko wapi? Mwizi hudhani kila mtu ni mwizi. cheating spouse hufikiri na mwenzie ni cheater. Sasa wewe kwasababu una udini unadhani watanzania wote wana udini.

Unahitaji miwani kuona nilichoandika? nilichoandika hapa ni.....

Maoni ya baadhi ya wachangiaji hapa .....

Waafrika ndivyo ....... kila mara .... kila mwaka .....bila kubadilika ....
 
Waislam wakitoa waraka anaweza kufungwa mtu au hamlijui hilo ? Bora tuende hivihivi kila mtu akili kichwani mwake ,labda ndugu zetu wakubwa wa Kikiristu wameshajipima nguvu na wanaweza kukabiliana na kupambana na yeyote yule atakaejaribu kuwasimamisha hivyo wakati muwafaka umefika wa kuanza kugonga gonga hodi hadi ikulu.

Mwiba,
Tunalifahamu sana hilo. Ni kweli waislamu mkitoa waraka anaweza afungwe mtu. Kama huo waraka utakuwa unahamasisha waislamu kuwakata vichwa makafiri (wasio waislamu), unafikiri kwa nini asifungwe mtu hapo?
 
duh mbona walisema ni chaguo la mungu? yetu macho

inawezekana kweli alikuwa chaguo la Mungu lakini akakengeuka baadae, soma biblia yako utawaona wengi tu
Sauli,Samson,Solomon, Juda iskariote na wengine wengi tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom