Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

Wapinzani wanataka utawala wa Kabila moja; wameamua kupiga kura zao kihivyo. Hawajali maendeleo au umoja, wanayaka ukabila. Yeyote ambaye hataki ukabila, anajikita kwenye taifa, hawampi kura - angalia Binti wa Sokoine alivyotemwa, Mwanri na Waziri Mbarawa.

Watasusia watapinga na kubeza kila kitu; lakini ni wachache. Maeneo yaliyosahaulika ni wengi zaidi, wawaacheni wajifurahishe.
Nani ale futari ya kinafiki iliyoandaliwa na mnafiki.
 
Wakati Ndugai akiwa matibabu kule India, na Tulia Ackson akikalia kiti, uadui bungeni ulikuwa mkubwa kiasi kwamba hata kusabahiana kati ya wabunge wa CCM na wale wa upinzani ikawa hakuna. Nakumbuka kuna wakati wabunge wa Upinzani walifunga plasta mdomoni. wakati huo Ndugai alionekana kukerwa na hali hiyo na aliporudi alikuja kama mkombozi. alikusudia kabisa kuondoa chuki hizo. kilichokuwa kinatakiwa ni kuwa na balansi. kutenda iliyo haki. hicho tu. hata mtoto mdogo kama unamwadhibu kwa kutenda kosa, lakini ukamwonesha upendo, atalia lakini bado atakukimbilia miguuni pako. lakini ukimwonesha chuki, atakukimbia.

Lakini inaonekana Ndugai naye anarudia kufanya yaleyale ya Tulia Ackson. Maana ukiangalia alivyomwadhibu Mnyika, tena akamwacha Kibajaji, alivyowashughulikia akina Mdee na Bulaya, na hiyo timua timua ya wabunge wa upinzani, inashangaza kwamba anao mshipa wa kushangaa kwamba wapinzani wanaanza kususa. kuna haja gani ya kuwa wanafiki? kama hawawezi ku-protest kwa njia za kawaida, wata-protest kwa njia yoyote ile. Na huo ni mwanzo tu, Wapinzani komaeni. Mwezi Mtukufu ni kwa ajili ya Haki, siyo Unafiki. Unafiki ni dhambi kubwa sana.
 
acha naye aumie kwani upendepeo wake na harrassment action zakehuwa zinawaumiza wapinzani
 
Ndugai ndo kalea huo ubaguzi. Asifanye propaganda za kujisafisha kwa Watanzania. Tumeona mengi aliyowatendea wapinzani isivyo bungeni. Aanze yeye kujirekebisha, hana hata hofu ya Mungu?
 
Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
Hizo sheria kwenye futali zimo?kama ndio basi ndo sababu
 
Ndugui amepooza akili siku hizi.maana sio kwa kujipendekeza kule..hebu fikiria anavyowatreat wapinzan pale bungen utathan yeye ni spika wa wabunge wa ccm tuu,, hebu angilia adhbu ya mdee na bulaya ilivyopitishwa kwa ghadhabu. Mnyika alivyoondolewa kama jambz tena spika anasema toa hilo toa hilo kana kwamba si binadamu na si kiongozi na mwakilishi wa watu...wapinzani wanabaguliwa nje ya bunge, na ndani ya bunge..nan hakusikia agizo la mwenye nchi alibyomwamuru supika awashughulikie wapinzani wakiwa bungeni na wakiwa nje yeye atawashughulikia..katika nchi hii yanayofanyika kama kungekuwa na uwezekano ni yakuihama tuuu.maana kuna watu wamejimilikisha imekuwa mali yao
 
Mimi nashauri 2020 apite Magufuri hawa wabunge wa ccm wapigwe chini wote ....Da aliye waloga wa Tz kuichagua ccm alishakufa na dawa
 
apeleke uchawi wake huko.

Huyu Ndugai ni bingwa wa bias leo anajifanya mwema sana mnafiki mkubwa huyu.

"Ni marufuku wabunge wa CCM kwenda kumsabahi Lema huko Magereza" By Mwenyekiti wa CCM
Kwani inadhani Chadema mkiacha kula futari ya W.mkuu kutatokea mabadiriko ? Lowasa atabaki kuwa FISADI tu.
 
Hakuna dhambi mbaya Duniani kam kuwa mnafiki. Nibora ujuoneshe jamii ikujue wakati wa kumuaga mzee Ndesambulo hamkutokea kumuangalia lema gerezani na lijualikali hamkutokea kwa amli mliyopokea kumpa dakika mbinge wa upinzani ni kosa hivyo chuki mezijenga wenyewe.
Mh. Spika jitafakiri umekosea wapi kaa jadiliana na wenzako kwa maana funga zetu zitakua hazina swawabu kama tutakua wanafiki.
voice of voiceless people
 
NAUTAFAKARI UBONGO ULIOTOA AMRI MEYA AWEKWE MAHABUSU SAA 48

Katika mamlaka za Serikali za Mitaa (Municipal/Local Government), hapo yakizungumzwa majiji, manispaa na miji, kiongozi wa juu kabisa ni Meya.

Kwenye nchi ambazo mamlaka za Serikali Kuu na Serikali za Manispaa zimetenganishwa vizuri, Meya ni cheo ambacho hakichezewi. Meya ni Ofisa Mtendaji Mkuu kwenye jiji, mji au manispaa yake. Meya ni kiongozi mwenye mamlaka kamili ambayo hayaingiliwi na Serikali Kuu.

Hivi karibuni Meya wa New York, Bill de Blasio, alitangaza kuwa New York itaendelea na Mkataba wa Mazingira wa Paris ambao Rais wa Marekani, Donald Trump anaupinga.

Uamuzi wa Blasio uliungwa mkono na mameya wa majiji mengine ya Marekani kwa sababu waliona kuwa Mkataba wa Paris una manufaa makubwa kwenye maeneo yao, hivyo wameahidi kuendelea nao hata kama Rais wao anaukataa.

Hali hiyo inatokea Marekani kwa sababu Serikali za Manispaa haziingiliwi na Serikali Kuu.

Novemba 21, mwaka Jana, baada ya Trump kushinda Urais wa Marekani, Blasio aliwahutubia wakazi wa New York na kuwaeleza kuwa ataiongoza mamlaka ya Jiji la New York kupambana dhidi ya amri za Trump ambazo aliziita za kibaguzi.

Blasio alisema kuwa hakuna Muislam wa New York atakayesajiliwa na hakuna mhamiaji wa Marekani atakayetenganishwa na familia yake. Kauli hiyo ilikuwa kuonesha kuwa Meya anasimamia mamlaka yake.

Umeya ni cheo chenye nguvu. Kipindi cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kumfukuza kazi Mkuu wa Mkoa lakini alishindwa kumfukuza Meya wa Jiji la Dar, Kitwana Kondo ingawa kosa lao lilikuwa moja. Sababu ni kuwa Meya ni mamlaka nyingine. Meya haguswi kienyeji.

Tanzania na sheria zake, Serikali za Manispaa zipo kama matawi ya Serikali Kuu, ndiyo maana Mameya hawana nguvu dhidi ya viongozi wa Serikali Kuu.

Tulishashuhudia vyanzo vingi vya mapato ya Serikali za Manispaa vikihamishiwa Serikali Kuu. Mfano kodi za majengo na mabango ya matangazo barabarani. Serikali za Manispaa zimebaki kuungaunga vyanzo vingine.

Wakati hayo yakiendelea, natafakari kuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, yupo mahabusu kwa siku ya pili sasa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwamba kiongozi huyo awekwe mahabusu saa 48.

Kosa la Meya inaelezwa ni kuwaalika wana Chadema wenzake kukagua shughuli za halmashauri ambayo inaongozwa na chama hicho. Wana Chadema kutembelea ofisi za halmashauri inayoongozwa na chama chao imeonekana ni kosa.

Wakati huo mwaka huu, Rais Magufuli akiwa ndiye Mwenyekiti wa CCM, aliongoza kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (Nec) ya chama hicho, kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Ikulu ikapambwa kijani na njano, rangi za chama.

Ikawa sahihi kwa ofisi kuu ya umma (Ikulu) kufanya shughuli za chama, ila imekuwa dhambi kubwa kwa Manispaa ya Ubungo kupokea wana Chadema kukagua kama jukumu waliloomba kwa wananchi linatekelezwa ipasavyo.

Wana Chadema wameitwa wavamizi na mwenyeji wao, yaani Meya, amewekwa korokoroni kwa saa 48. Uamuzi ni wa Mkuu wa Wilaya. CCM wao walionekana wenyeji wa Ikulu kwa sababu Rais ni wa chama chao.

Tukio la Meya Jacob kuwekwa mahabusu halitoshi kulaaniwa, kwani ni kichekesho kikubwa cha siasa za Tanzania.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Wakati Ndugai akiwa matibabu kule India, na Tulia Ackson akikalia kiti, uadui bungeni ulikuwa mkubwa kiasi kwamba hata kusabahiana kati ya wabunge wa CCM na wale wa upinzani ikawa hakuna. Nakumbuka kuna wakati wabunge wa Upinzani walifunga plasta mdomoni. wakati huo Ndugai alionekana kukerwa na hali hiyo na aliporudi alikuja kama mkombozi. alikusudia kabisa kuondoa chuki hizo. kilichokuwa kinatakiwa ni kuwa na balansi. kutenda iliyo haki. hicho tu. hata mtoto mdogo kama unamwadhibu kwa kutenda kosa, lakini ukamwonesha upendo, atalia lakini bado atakukimbilia miguuni pako. lakini ukimwonesha chuki, atakukimbia.

Lakini inaonekana Ndugai naye anarudia kufanya yaleyale ya Tulia Ackson. Maana ukiangalia alivyomwadhibu Mnyika, tena akamwacha Kibajaji, alivyowashughulikia akina Mdee na Bulaya, na hiyo timua timua ya wabunge wa upinzani, inashangaza kwamba anao mshipa wa kushangaa kwamba wapinzani wanaanza kususa. kuna haja gani ya kuwa wanafiki? kama hawawezi ku-protest kwa njia za kawaida, wata-protest kwa njia yoyote ile. Na huo ni mwanzo tu, Wapinzani komaeni. Mwezi Mtukufu ni kwa ajili ya Haki, siyo Unafiki. Unafiki ni dhambi kubwa sana.
Hili bunge linazidi kupoteza muelekeo kisa maagizo kutoka juu
 
Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
sawa basi kulen futari yenu
 
Akumbukumbuke pia anavyobania dakika kwa wabunge wa upinzani, kuwaitia askari watolewe nje na kuruhusu waitwe wezi
Na ndio hio bigotry ambayo wapinzani wanamrejeshea. Asilalamike
 
Back
Top Bottom