Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
500
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameonyesha kuumizwa na kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kutojumuika pamoja na wabunge wenzao katika masuala ya kijamii ikiwepo kususia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Ndugai%20Job%20.jpg

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai

Kufuatia jambo hilo Ndugai amewaomba viongozi na wabunge kwa pamoja kuachana na mambo ya kujitenda kwani yanaweza kuleta athari kubwa ambazo hakuna anayehitaji, na kudai kama kuna mambo ambayo yanakwaza basi viongozi hao wanapaswa kukaa pamoja na kumaliza mambo hayo.

"Tumekuwa tukiandaa baadhi ya hizi shughuli siku ile ya bajeti tulipata nafasi ya kupata futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo, mabalozi tulihudhuria pale na ilikuwa imeandaliwa kwa wema kwa kweli. Leo (jana) pia na mimi nimepata nafasi ya kuandaa kama nilivyowataarifu lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema lakini ngoja nikiseme hapa kidogo, kuna baadhi yetu wengine wamekatazana rasmi kutohudhuria shughuli kama hizi, sasa mimi sitaki kuingilia uhuru wao, wana haki kufanya hivyo kama wanaona ni sawa lakini mimi mwenzao ningependa kuwashauri tu hasa viongozi wanaofanya mambo hayo kutazama tena njia zao, yako mambo mengine ni ya kijamii tu, ukifika mahali kiongozi unaanza kuwazuia watu hata mambo ya kijamii ujue unaenda mbali kidogo" alisema Ndugai

Spika wa Bunge aliendelea kutoa malalamiko yake dhidi ya vitendo vya baadhi ya wabunge wa upinzani kususia shughuli hizo za kijamii ambazo zinawaweka pamoja na kusema

"Hili bunge linavyoendeshwa labda wabunge wa kambi mbalimbali mnaweza msielewe bunge hili linaendeshwa katika mawasiliano mbalimbali ya sisi kwa sisi endapo kuna jambo linakwaza mpaka linasababisha hata watu wasipate futari kwa pamoja basi ni vizuri viongozi wa pande zote tukakaa tuzungumze na kuondoa vikwazo hivyo kama vipo maana mimi sijui kama vipo lakini kama havipo ni vizuri tuwe tunajumuika kwa pamoja, maana sera hizo zikienea na hakika kabisa na pande zingine nazo zitaanza na hakika matokeo yake italeta mipasuko ambayo hakuna anayehitaji hapa" alisisitiza Job Ndugai

Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.

Source: EATV
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,125
2,000
Source ya yote haya ni wewe Spika Job Ndugai mwenyewe..

Wewe ndio unaeleta huu mgawanyiko bungeni na mpaka wabunge wa upande mwingine wameamua kuwa wapinzani kwelikweli..

Acha kulia lia..
Be fair kwa wote.

Am sure (kwa mfano) kama Mkiti Mussa Zungu angekuwa ameandaa futari na kuwakaribisha wabunge, wote wangeudhuria..!!

So Ndugai angalia nyendo na matendo yako kwa wapinzani na hasa Chadema then jiulize why??
 

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,205
2,000
Sijawahi kuona mbunge wa ccm ametolewa nnje
Wala sijawahi kuona mbunge wa ccm akitukana n'a kuchukuliwa hatua bila shaka adhabu zote pâle bungeni ni kwa ajili y'a wapinzani tu
Kwa mtindo huu kuna haja gani kuhudhururia kwenye futari za majaliwa n'a spika ndugai au tulia Akson ?

Éden kimario
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,602
2,000
Kwani ni lazima kwenda kula hayo mafutari?

Wajiulize ikiwa kutokwenda kula futari inawaumiza roho namna hii inakuwaje pale unapotuzuia kumuaga kipenzi chetu, shujaa wetu, baba yetu, kiongozi wetu (katika muktadha huo huo wa "kijamii") MZEE NDESAMBURO kwenye uwanja wenye hadhi na heshima kwa jamii UWANJA WA MASHUJAA?
 

1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
8,963
2,000
Source ya yote haya ni wewe Spika Job Ndugai mwenyewe..

Wewe ndio unaeleta huu mgawanyiko bungeni na mpaka wabunge wa upande mwingine wameamua kuwa wapinzani kwelikweli..

Acha kulia lia..
Be fair kwa wote.

Am sure (kwa mfano) kama Mkiti Mussa Zungu angekuwa ameandaa futari na kuwakaribisha wabunge, wote wangeudhuria..!!

So Ndugai angalia nyendo na matendo yako kwa wapinzani na hasa Chadema then jiulize why??


Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
 

steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,937
2,000
yaani waende halafu waanze kuwabagua huko kwenye futari kama wanavyobaguliwa bungeni ktk uchangiaji wa masuala mbalimbali,wapo sahihi kabisa,naamini wangekwenda zama za makinda au marehemu sitta,ila sio huyu mwenye hulka za jazba,unafiki,mihemko,kukosa busara ya uongozi,kutopenda kusikiza wengine hasa kama si wa upande wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom