Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

hilo la msingi siasa za bungeni wasizilete uraiani tutaangamia...malalamiko yao wamalizane huko huko hadi futari???
 
ubaguzi ndio sera ya chama cha mapinduzi awamu hii walionywa kwenda kumjulia hali Lema alipokuwa gerezani kisongo raisi wao aliwaomya kujumuika na wapinzani kwa lolote lile

Si muliwakataza wabunge wenu kula la na wapinzani!
 
Ndugai ana hasira sana na wapinzani,hajui kama wapo kisheria bungeni!
Ale futari na maccm wenzake,aache unafiki
 
Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.

Source: EATV

Hivi kuna umbali gani kutoka hapo Bunge linapokaa na ilipo hospitali ya Rufaa Mirembe?

Nadhani kuna mtu amepoteza mawasiliano kati ya akili na matendo yake, anatenda kinyume lakini akili yake inamwambia yuko sawa sawa. Nashauri afya ya akili yake ipate matibabu haraka iwezekanavyo.
 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameonyesha kuumizwa na kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kutojumuika pamoja na wabunge wenzao katika masuala ya kijamii ikiwepo kususia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.




Ndugai%20Job%20.jpg

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai

Kufuatia jambo hilo Ndugai amewaomba viongozi na wabunge kwa pamoja kuachana na mambo ya kujitenda kwani yanaweza kuleta athari kubwa ambazo hakuna anayehitaji, na kudai kama kuna mambo ambayo yanakwaza basi viongozi hao wanapaswa kukaa pamoja na kumaliza mambo hayo.

"Tumekuwa tukiandaa baadhi ya hizi shughuli siku ile ya bajeti tulipata nafasi ya kupata futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo, mabalozi tulihudhuria pale na ilikuwa imeandaliwa kwa wema kwa kweli. Leo (jana) pia na mimi nimepata nafasi ya kuandaa kama nilivyowataarifu lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema lakini ngoja nikiseme hapa kidogo, kuna baadhi yetu wengine wamekatazana rasmi kutohudhuria shughuli kama hizi, sasa mimi sitaki kuingilia uhuru wao, wana haki kufanya hivyo kama wanaona ni sawa lakini mimi mwenzao ningependa kuwashauri tu hasa viongozi wanaofanya mambo hayo kutazama tena njia zao, yako mambo mengine ni ya kijamii tu, ukifika mahali kiongozi unaanza kuwazuia watu hata mambo ya kijamii ujue unaenda mbali kidogo" alisema Ndugai

Spika wa Bunge aliendelea kutoa malalamiko yake dhidi ya vitendo vya baadhi ya wabunge wa upinzani kususia shughuli hizo za kijamii ambazo zinawaweka pamoja na kusema

"Hili bunge linavyoendeshwa labda wabunge wa kambi mbalimbali mnaweza msielewe bunge hili linaendeshwa katika mawasiliano mbalimbali ya sisi kwa sisi endapo kuna jambo linakwaza mpaka linasababisha hata watu wasipate futari kwa pamoja basi ni vizuri viongozi wa pande zote tukakaa tuzungumze na kuondoa vikwazo hivyo kama vipo maana mimi sijui kama vipo lakini kama havipo ni vizuri tuwe tunajumuika kwa pamoja, maana sera hizo zikienea na hakika kabisa na pande zingine nazo zitaanza na hakika matokeo yake italeta mipasuko ambayo hakuna anayehitaji hapa" alisisitiza Job Ndugai

Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.

Source: EATV
Tatizo ni unafiki na utoto unaofanywa na wabunge wa CCM pia spika mwenyewe,wanaweza kwenda kujumuika ila kwenye kujadili hoja muhimu utasikia vijembe vya kijinga au kipuuzi kutoka CCM mmekula futari yetu bure nyie walafi,hatuwakaribishi tena ktk futari yetu nyie waroho mnakula sana na Spika naye atacheka au utasikia jamani mmevimbiwa pilau tumwambie waziri aandae tena,huo upuuzi ndio unawafanya wajitenge,mkijiheshimu na wao watajiheshimu
 
...kushiriki futari kinafiki na watu hawa wabaya na wanafiki ni kufanya dhambi zaidi...maana wao wala hawajui maana ya kusamehe.....unaniitia polisi na kunipiga ndani ya bunge alafu leo unaniita tule futari???huu unafiki hata Mungu hapendi....endeleeni na unafiki wenu huko huko ccm...
 
Mwezi mtukufu ndio unafaa kuitia wapinzani polisi wawapige kama mbwa kwa amri ya spika!!?
 
Nawapongeza sana wapinzani kwa kugoma kwenda, kuhuria kwa mtu uliye na kinyongo nae, anaetumia jazba badala ya busara, anaetumia kanuni kuadhibu wapinzani na wenzie akawaacha, anaengoza mhimili ulio huru kwa kupokea maagizo kutoka juu, kumuunga mkono mtu anayekunyanyasa huo ni unafiki
 
Alipigwa Mkwara mzito kuwa kama wapinzani wanasubiri na wanampenda basi ahamie CDM.....baada hapo amebadilika kabisa....anataka kuonyesha amebadilika na anafuata matakwa , remote iko magogoni!! Pia ameona kasi ya Tulia kutafuta jimbo mojawapo Mbeya huenda yakatokea yale ya.........zamu ya Jinsia!! Akabakia na Ubunge wake.....akiwa Speaker mstaafu ndani ya Bunge....aibu!!!
Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
 
NAUTAFAKARI UBONGO ULIOTOA AMRI MEYA AWEKWE MAHABUSU SAA 48

Katika mamlaka za Serikali za Mitaa (Municipal/Local Government), hapo yakizungumzwa majiji, manispaa na miji, kiongozi wa juu kabisa ni Meya.

Kwenye nchi ambazo mamlaka za Serikali Kuu na Serikali za Manispaa zimetenganishwa vizuri, Meya ni cheo ambacho hakichezewi. Meya ni Ofisa Mtendaji Mkuu kwenye jiji, mji au manispaa yake. Meya ni kiongozi mwenye mamlaka kamili ambayo hayaingiliwi na Serikali Kuu.

Hivi karibuni Meya wa New York, Bill de Blasio, alitangaza kuwa New York itaendelea na Mkataba wa Mazingira wa Paris ambao Rais wa Marekani, Donald Trump anaupinga.

Uamuzi wa Blasio uliungwa mkono na mameya wa majiji mengine ya Marekani kwa sababu waliona kuwa Mkataba wa Paris una manufaa makubwa kwenye maeneo yao, hivyo wameahidi kuendelea nao hata kama Rais wao anaukataa.

Hali hiyo inatokea Marekani kwa sababu Serikali za Manispaa haziingiliwi na Serikali Kuu.

Novemba 21, mwaka Jana, baada ya Trump kushinda Urais wa Marekani, Blasio aliwahutubia wakazi wa New York na kuwaeleza kuwa ataiongoza mamlaka ya Jiji la New York kupambana dhidi ya amri za Trump ambazo aliziita za kibaguzi.

Blasio alisema kuwa hakuna Muislam wa New York atakayesajiliwa na hakuna mhamiaji wa Marekani atakayetenganishwa na familia yake. Kauli hiyo ilikuwa kuonesha kuwa Meya anasimamia mamlaka yake.

Umeya ni cheo chenye nguvu. Kipindi cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kumfukuza kazi Mkuu wa Mkoa lakini alishindwa kumfukuza Meya wa Jiji la Dar, Kitwana Kondo ingawa kosa lao lilikuwa moja. Sababu ni kuwa Meya ni mamlaka nyingine. Meya haguswi kienyeji.

Tanzania na sheria zake, Serikali za Manispaa zipo kama matawi ya Serikali Kuu, ndiyo maana Mameya hawana nguvu dhidi ya viongozi wa Serikali Kuu.

Tulishashuhudia vyanzo vingi vya mapato ya Serikali za Manispaa vikihamishiwa Serikali Kuu. Mfano kodi za majengo na mabango ya matangazo barabarani. Serikali za Manispaa zimebaki kuungaunga vyanzo vingine.

Wakati hayo yakiendelea, natafakari kuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, yupo mahabusu kwa siku ya pili sasa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwamba kiongozi huyo awekwe mahabusu saa 48.

Kosa la Meya inaelezwa ni kuwaalika wana Chadema wenzake kukagua shughuli za halmashauri ambayo inaongozwa na chama hicho. Wana Chadema kutembelea ofisi za halmashauri inayoongozwa na chama chao imeonekana ni kosa.

Wakati huo mwaka huu, Rais Magufuli akiwa ndiye Mwenyekiti wa CCM, aliongoza kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (Nec) ya chama hicho, kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Ikulu ikapambwa kijani na njano, rangi za chama.

Ikawa sahihi kwa ofisi kuu ya umma (Ikulu) kufanya shughuli za chama, ila imekuwa dhambi kubwa kwa Manispaa ya Ubungo kupokea wana Chadema kukagua kama jukumu waliloomba kwa wananchi linatekelezwa ipasavyo.

Wana Chadema wameitwa wavamizi na mwenyeji wao, yaani Meya, amewekwa korokoroni kwa saa 48. Uamuzi ni wa Mkuu wa Wilaya. CCM wao walionekana wenyeji wa Ikulu kwa sababu Rais ni wa chama chao.

Tukio la Meya Jacob kuwekwa mahabusu halitoshi kulaaniwa, kwani ni kichekesho kikubwa cha siasa za Tanzania.

Ndimi Luqman MALOTO
Hapo Maloto Luqman amenena haswa. Tanzania Meya anakuwa MSTAHIKI MEYA pale tu anapokuwa wa CCM. akiwa kutoka upinzani, tena mwenye kuchapa kazi kama huyu wa Ubungo, ambaye amediriki kufanyia kazi tetesi za "BASHITE" , Meya, kwa CCM, ni kama toilet pepa iliyotumika.
 
Akale mafutari na wale waliumsaidia kufukua kaburi
 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameonyesha kuumizwa na kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kutojumuika pamoja na wabunge wenzao katika masuala ya kijamii ikiwepo kususia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.




Ndugai%20Job%20.jpg

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai

Kufuatia jambo hilo Ndugai amewaomba viongozi na wabunge kwa pamoja kuachana na mambo ya kujitenda kwani yanaweza kuleta athari kubwa ambazo hakuna anayehitaji, na kudai kama kuna mambo ambayo yanakwaza basi viongozi hao wanapaswa kukaa pamoja na kumaliza mambo hayo.

"Tumekuwa tukiandaa baadhi ya hizi shughuli siku ile ya bajeti tulipata nafasi ya kupata futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo, mabalozi tulihudhuria pale na ilikuwa imeandaliwa kwa wema kwa kweli. Leo (jana) pia na mimi nimepata nafasi ya kuandaa kama nilivyowataarifu lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema lakini ngoja nikiseme hapa kidogo, kuna baadhi yetu wengine wamekatazana rasmi kutohudhuria shughuli kama hizi, sasa mimi sitaki kuingilia uhuru wao, wana haki kufanya hivyo kama wanaona ni sawa lakini mimi mwenzao ningependa kuwashauri tu hasa viongozi wanaofanya mambo hayo kutazama tena njia zao, yako mambo mengine ni ya kijamii tu, ukifika mahali kiongozi unaanza kuwazuia watu hata mambo ya kijamii ujue unaenda mbali kidogo" alisema Ndugai

Spika wa Bunge aliendelea kutoa malalamiko yake dhidi ya vitendo vya baadhi ya wabunge wa upinzani kususia shughuli hizo za kijamii ambazo zinawaweka pamoja na kusema

"Hili bunge linavyoendeshwa labda wabunge wa kambi mbalimbali mnaweza msielewe bunge hili linaendeshwa katika mawasiliano mbalimbali ya sisi kwa sisi endapo kuna jambo linakwaza mpaka linasababisha hata watu wasipate futari kwa pamoja basi ni vizuri viongozi wa pande zote tukakaa tuzungumze na kuondoa vikwazo hivyo kama vipo maana mimi sijui kama vipo lakini kama havipo ni vizuri tuwe tunajumuika kwa pamoja, maana sera hizo zikienea na hakika kabisa na pande zingine nazo zitaanza na hakika matokeo yake italeta mipasuko ambayo hakuna anayehitaji hapa" alisisitiza Job Ndugai

Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.

Source: EATV

So what
 
Naona imemuingia na itakuwa chakula kimebaki na kuwadodea.

Nimegundua mnafiki hana umri wala jinsia
 
Back
Top Bottom