Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

Wapinzani wamuumiza Spika wa Bunge

Samba la mbowe mwekezaji wa mazao ya chakula, tena la chakula linaharibiwa vileeeee!!

Aisee,the whole Tz will be Kibiti,you will tell me one day
 
Heri ya Mchawi kuliko mnafiki maana Mchawi haonekani!!! Napita tu!!!!
 
Kwahiyo wabunge wakale futari ya kinafiki wakati wananchi wao umewatangazia rasmi hawatapata maji
 
Alikua ameweka sumu nini mbona ghafla wapinzani wamemuumiza kutokula futari angesema anaumia wapinzani kuwatoa Bungeni coz wanawakikisha Wananchi leo anaumia wapinzani kutokula futari kunanamna hapo sio bure
 
Na bora hata hawakwenda angewafukuza huko huko kwenye futari
 
Namchukia sana huyo kiumbe [emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameonyesha kuumizwa na kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kutojumuika pamoja na wabunge wenzao katika masuala ya kijamii ikiwepo kususia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.




Ndugai%20Job%20.jpg

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai

Kufuatia jambo hilo Ndugai amewaomba viongozi na wabunge kwa pamoja kuachana na mambo ya kujitenda kwani yanaweza kuleta athari kubwa ambazo hakuna anayehitaji, na kudai kama kuna mambo ambayo yanakwaza basi viongozi hao wanapaswa kukaa pamoja na kumaliza mambo hayo.

"Tumekuwa tukiandaa baadhi ya hizi shughuli siku ile ya bajeti tulipata nafasi ya kupata futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo, mabalozi tulihudhuria pale na ilikuwa imeandaliwa kwa wema kwa kweli. Leo (jana) pia na mimi nimepata nafasi ya kuandaa kama nilivyowataarifu lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema lakini ngoja nikiseme hapa kidogo, kuna baadhi yetu wengine wamekatazana rasmi kutohudhuria shughuli kama hizi, sasa mimi sitaki kuingilia uhuru wao, wana haki kufanya hivyo kama wanaona ni sawa lakini mimi mwenzao ningependa kuwashauri tu hasa viongozi wanaofanya mambo hayo kutazama tena njia zao, yako mambo mengine ni ya kijamii tu, ukifika mahali kiongozi unaanza kuwazuia watu hata mambo ya kijamii ujue unaenda mbali kidogo" alisema Ndugai

Spika wa Bunge aliendelea kutoa malalamiko yake dhidi ya vitendo vya baadhi ya wabunge wa upinzani kususia shughuli hizo za kijamii ambazo zinawaweka pamoja na kusema

"Hili bunge linavyoendeshwa labda wabunge wa kambi mbalimbali mnaweza msielewe bunge hili linaendeshwa katika mawasiliano mbalimbali ya sisi kwa sisi endapo kuna jambo linakwaza mpaka linasababisha hata watu wasipate futari kwa pamoja basi ni vizuri viongozi wa pande zote tukakaa tuzungumze na kuondoa vikwazo hivyo kama vipo maana mimi sijui kama vipo lakini kama havipo ni vizuri tuwe tunajumuika kwa pamoja, maana sera hizo zikienea na hakika kabisa na pande zingine nazo zitaanza na hakika matokeo yake italeta mipasuko ambayo hakuna anayehitaji hapa" alisisitiza Job Ndugai

Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.

Source: EATV

JAZA UJAZWEEE HIOOO
 
KUNA MAMBO HUFANYWA NA SPIKA NA WASHIRIKA WAKE HATA ANGEKUWEPO FOROJO GANZE ANGEKANA KWAMBA KULE SHIMONI HAWAKUAMBIWA NA SHETANI WAFANYE HAYA WANAYOFANYA MFANO YULE SLOWLY KUWA NDUMILA KUWILI NA MNAFIKI.
 
Alafu vitendo wanavyowafanyia upinzani avitwasandia chama tawala kuongeza wabunge bali wanajenga chuki mfano Mbunge wa jimbo langu hawezi kutolewa Bungeni na Ndugai akadhani nitampenda Ndugai never
 
Kwakweli wanaCCM wana phd ya Unafiki.... Ndugai ina maana hajui kuwa Wapinzani wanaonekana na wahaini....


Kwanini wahaini wajumuike na Wazalendo ( CCM)....


Ndugai hao CCM wenzako wanakutosha
 
WanaCCM wana phd ya Unafiki.....


Ina maana Ndugai hajui kuwa awamu hii ya Tano kuwa mpinzani ni sawa na kuwa Mhaini.......... Muda wowote unaenda kula sero.



Nyie wazalendo (CCM) andaeni futari zenu mjipongeze.
 
Back
Top Bottom