Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Nafikiri mzee sitta ameona spidi ya EL ni kubwa hivyo anajikomba walau aendelee kupata mkate wake wa kila siku.
 
Kwani kasema uongo? Ni kweli wabunge wa CDM ni wanafiki.

Samwel Sitta ndiyo MNAFIKI nambari wahedi!

Asitake kuwakoroga Watanzania ambao walikuwa wakimweheshimu kama Spika aliyeongoza Bunge lililopita kwa umahiri mkubwa. Lakini kwa kauli yake hii ya jana huyu mzee sasa anataka Watanzania waanze kumvua nguo moja baada ya nyingine mpaka ajikute akiwa mtupu!

Unafiki wa KWANZA kabisa wa Sammy Sitta ni YEYE KUHUSIKA NA KUANZISHWA KWA CHAMA CHA CCJ(Chama Cha Jamiii)ambacho amekiri kuhusika. Sasa tumwulize yeye Sitta kama hiyo CCJ ingelikamilika na kuanzishwa rasmi ina maana na yeye angelijiita MNAFIKI? Maana angelikuwa upande wa upinzani na siyo CCM!

Kwanza alitakiwa awaambie hao Chama Cha Magamba kuwa ndiyo WANAFIKI WAKUBWA KWA KUMNYIMA YEYE USIPIKA kwa kisingizio cha kutaka kuwa na Spika MWANAMKE! Mbona hajawauliza hao CCM kwanini walimpa fomu za kugombea Uspika wakti yeye ni MWANAMME??

Mimi nampa SS ushauri wa bure kabisa. Hebu na anyamaze tu maana hata hao CCM anaowapigia debe kwa sasa wanasubiri muda tui ili waendelee kumsulubu kama walivyofanya wakti wa kumchagua Anne Makinda. SS anatakiwa ajibu tuhuma za kutaka kuanzisha CCJ akiwa ndani ya CCM.

Kwa hili SS amechemka.
 
Waungwana, it is a pity that kwa mtu aliyetumainiwa kama Samwel Sitta kutoa kauli kama zile dhidi ya upinzani. Pamoja na kuwa yupo CCM , lakini alionekana kusema ukweli hata kama utawaudhi wenzake wa CCM. jana sikuamini kauli zake alizozitoa bungeni. Mheshimiwa Sitta, umetuvunja moyo. Ilikuwa inatia moyo kuwa pamoja na kuwa uko CCM, pale penye ukweli ulikuwa unautetea hata kama unatoka kwa wapinzani. Labda kukaimu nafasi ya Waziri mkuu bungeni kumetengua msimamo wako wa kutetea haki, wanyonge etc. TUMEKWISHA, KAMA NI NDIVYO ULIVYO, BASI EL ATAUKWAA URAIS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Maana bila wewe hakuna tena CCM wa kutetea wanyonge. I stand to be corrected.
 
Akitolea ufafanuzi kombora lililorushwa na David Kafulila, Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta ameikejeli kambi ya Upinzani kuwa ni wanafiki na waliojaa kauli nyepesi na za Ujanja ujanja na kazi waliyotumwa bungeni ni kufanya wanachokifanya sasa, hivyo wabunge wa CCM wawapuuze na kuwatazama kama walivyo kwani wananchi wanatazama na wataamua kwa wanayoyafanya.

Inashangaza kuona Sitta anaobuka na kauli hizi huku maji yakiwa shingoni kwa upande wake katika uwanja wa siasa. Akizungumza kwa mbwembwe huku akizomewa pia na baadhi ya Wabunge pale aliponukuu mfano wa hoja ya Posho

Sitta amesikika dhahiri akijikinga katika mwavuli huu kwa kuhoji inakuwaje leo wabunge wa Upinzani ambao wengine walikuwapo miaka kadhaa iliyopita bungeni na wamekuwa wakilipwa posho hizo kwa miaka mitano iliyopita leo wanziona si halali, warudishe posho zote ndio waseme kauli zao hizo za kinafiki alisisitiza Sitta.

Awali kigwangala nae aliangukia pua baada ya kuataka kuota muongozo kwa Mbunge wa Viti maalum CDM aliyeponda utitiri wa Vihiyo waliojaa MSD kuwa ndio kiini cha tatizo la upungufu mkubwa wa madawa kwa sasa Nchi.

Busara imehama tayari, tulimtegemea sana huyu mzee atuvushe kidogo kutoka makucha ya CCM ingawa kuyakemea, sasa looooo, mvi za bure. Yeye kwa busara????? zake tulitegemea awajenge wapinzania ili waikosoe serikali na kuisukuma iwatumikie watu, sasa anaukandia upinzani. Hajui kuwa kama sio kuwa na vyama vingi asingelikuwa na wzo la kuunda CCJ. SHAME UP ON YOU MZEE WETU
 
Busara imehama tayari, tulimtegemea sana huyu mzee atuvushe kidogo kutoka makucha ya CCM ingawa kuyakemea, sasa looooo, mvi za bure. Yeye kwa busara????? zake tulitegemea awajenge wapinzania ili waikosoe serikali na kuisukuma iwatumikie watu, sasa anaukandia upinzani. Hajui kuwa kama sio kuwa na vyama vingi asingelikuwa na wzo la kuunda CCJ. SHAME UP ON YOU MZEE WETU

Adui muombee Njaa, Mzee kawekwa katika Wizara ambayo ulaji wake ni kwa dhiki sna tofauti na alivyokuwa Bungeni. Majaaliwa yake kisiasa yapo njia panda. Haishangazi kuona anatoa kauli kama hizi walau apate mahala pa kuganga njaa.

Ila heshima yazidi mali, taswira aliyoijenga hata watanzania wote kwa ujumla wao wakasimama nyuma yake wakati anahujumiwa kuondolewa katika kiti, leo naichezea kwa kufurahisha wanasiasa walafi. Hapa ndio utagundua wanasiasa wengi wa CCM wana hoja za kufikiri kwa tumbo kuliko kutumia bongo
 
Kusema kweli nashindwa kuelewa serikali na Wabunge wa CCM. Nashindwa kwa sababu wanakitayarishiria CCM safari ya kwenda kuzimu kama ilivyo kwa KANU na Vyama vingine vinavyojiita vyama Ukombozi . Sijui ni ukombozi gain waliofanya hasa CCM. Maisha ni magumu, heri enzi ya Mkoloni kwani hao wazee waliopambana na ukoloni wametuhadaa sana. Wao walikuwa wanasomeshwa Bure na wakoloni, wanapata matibabu Bure tena kwa kulazimishwa na hao wakoloni.
Anayewalaani wakoloni ni ADUI YANGU NAMBA 1 Kama CCM ilivyokuwa ADUI yangu No 1 !
Jana nilikuwa naangalia Bunge Hongera Kafulila Pia Hongereni Wabunge wote wa Upinzani kwa kumpa moyo mwenzenu wa Upinzani ila nina wasiwasi na wabunge wa CUF.
Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni yaani Samweli Sitta amethibitisha unafiki wake kwa vitendo:-


  1. Kwa kipindi hiki anapokaimu uwaziri mkuu ameonyesha jinsi gani alivyo mtu wa Visasi,
  2. Hana tofauti na Muimba Mipasho
  3. Uadilifu anaomshupalia lowasa ni upi ? wakati jana Mchango wa Kafulila ulikuwa na asilimia 100 za ukweli kuhusu Uadilifu wa Serikali ambapo serikali hii ya CCM haina. Na sita alivyomjibu lowasa kuhusu maamuzi magumu alisema yawe adilifu.
  4. Bunge si Jukwaa la Mkutano wa Hadhara! Sita unaposema kuwa wabunge wengine walikuwapo kipindi cha nyuma warudishe posho za kipindi hicho ndio wasimamie mgomo wa posho si kitendo cha kizalendo. Upambanaji wako dhidi ya Ufisadi uko wapi! Bwana Sita. Hivi Posho sio sehemu ya Ufisadi! Huo unafiki wa wapinzani ni upi?
  5. Hao wananchi watakaopembua ukweli na uongo unaowasemea ni wa nchi gani? Kama ni ya Tanzania wanataka ukweli gani mwingine zaidi ya kusema CCM imechoka na ipumzishwe sasa,
  6. Nafikiri tusubiri uchaguzi mdogo wowote utakaofanyika hapa nchini ndio utaujua vizuri ukweli unaoutaka .
  7. Ndio Maana hata kesi za kupinga matokeo ya Uchaguzi zinacheleweshwa kwa makusudi kwa sababu mnajua hamkushinda kihalali na uchaguzi ukirudiwa mtalia. Mwaka 2005 katika kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi zilikuwa zinaamuliwa mapema kwa sababu mtanashati wenu(kikwete) watu walikuwa na Imani naye.
  8. WATANZANIA WANAJUA KUWA ULIAHIDIWA UWAZIRI MKUU 2005 WENZAKO WAKAKUZUNGUKA NDO MAANA UNAONGEA TU BAAAA BAAA BAAAA KAMA BATA! HUNA HOJA,HUNA UZALENDO WOWOTE, WEWE NI MNAFIKI !
 
Hawai magamba ipo siku na wao watakuwa wapinzani,Sitta umejishushia heshima yako na sasa nimeamini magamba hamna watetezi wa kweli
 
Utawala huu wa sasa uliwahi kumfikiria Sitta kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu. Ni Mungu tu alituepusha na balaa hili nadhani. Sitta hana msimamo kwa lolote. Ingawa mnanipinga sana lakini ukweli mmoja lazima niuseme mara kwa mara. Baadhi ya makabila hapa duniani hayana kitu kinaitwa MSIMAMO, UJASIRI na MAAMUZI.
 
Mnafiki ni yemwenyewe Sitta maana anajifanya yupo CCM huku pembeni ananzisha CCJ
Anajifanya anapambana na Ufisadi kumbe ni mroho wa madaraka na posho
shame on you SIX wananchi wa Urambo mtaendelea na maisha yenu hayo hayo ya ufukara, bahati nzuri nimefika Jimbo la Urambo
 
urais mtamu, lazima wakati mwingine ujifanye hamnazo kutetea vitu ambayo vipo waziwazi kabisa. hakuna mtu yeyote mzalendo anaweza kupingana na kauli ya Mh Kafulila.

Alichosema Kafulila ni ukweli na kawaida ukweli unachoma sana.
 
samwel 6 hana maana tena, sina haja ya kuremba maneno hapa. nilikuwa namuona ni m2 mwenye kupenda ukwel, kumbe ni mnafiki tu.
 
Watanzania hatuaminiki, ni vigeugeu na tusio na dira njema kwa muendelezo mwema wa taifa letu Tanganyika zaidi ya ubinafsi. Kwa matokeo ya sasa juu ya mzee SIX...analinda mifereji yake imtoleayo asali na maziwa, ya kwamba kwa namna yoyote iwayo TOPE & MICHANGA isiingie katika mitiririko ya mifereji yake.
Ni muendelezo wake mzee wetu SIX wa kutoonyesha uzalendo kwa taifa lake kiuthabiti, zaidi ya ngonjera pevu za ufisadi,ufisadi,ufisadi zisizo na ncha.
 
Jana nilimshangaa sana samweli sita kwa kweli kauli alizotoa bungeni juu ya swala la kafulila ukweli alapaswa afikiri kabla ya kuongea maneno yale. kwanza ameingia kwenye orodha ya viongozi wanaotetea posho jamani sita toka aanze kula pesa za walipa kodi toka awamu ya kwaza mpaka leo bado anazitolea macho huyu ni kiongozi hatari anayetoa kauli akiwa na jazba na ufinyu wa mawazo kwa kauli ya jana amejimaliza kisiasa
 
Swali langu kwa Mh. Sitta: anaamini CCM ni chama safi na chenye/dhamira ya kweli ya kuwakomboa Watanzania? Kama jibu ndio, ni kwa nini aliasisi chama kingine (CCJ)? Na kama jibu ni hapana, kwanini bado yuko CCM?
 
Jana nilimshangaa sana samweli sita kwa kweli kauli alizotoa bungeni juu ya swala la kafulila ukweli alapaswa afikiri kabla ya kuongea maneno yale. kwanza ameingia kwenye orodha ya viongozi wanaotetea posho jamani sita toka aanze kula pesa za walipa kodi toka awamu ya kwaza mpaka leo bado anazitolea macho huyu ni kiongozi hatari anayetoa kauli akiwa na jazba na ufinyu wa mawazo kwa kauli ya jana amejimaliza kisiasa

Hapo in red naongezea...TENA HANA UZALENDO WA DHATI KWA TAIFA LAKE LA TANGANYIKA.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kumbe jamaa si lolote si Chochote, ni mwimbaji wa Mipasho tu. Jana ndio nilimdharau mpaka mwisho. Anapodai kwamba kama wale wabunge wa Upinzani waliokuwepo kwenye bunge lilillopita waanze kurudisha posho walizopewa kwenye kikao kilichopita. Inamaana kama serikali ikiamua kuzifuta posho nayeye atazirudisha zile alizochukua kwenye bunge lililopita? Aache U-makalio!
 
Back
Top Bottom