Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

nashangazwa sana na kitendo cha wapinzani wengi kutokubali kukosolewa
kitendo cha waziri sita kukosowa wapinzani na kuwaita wanafiki nakubali kabisa,
nafikiri sita ni mtu mzima na hawezi kukurupuka na kutoa maneno kama hayo bungeni,
samweli sita amekaa na kutafakari vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wapinzani na kuona ni unafiki,
mfano mzuri ni huu wa zito kusafiri na kikwete ndege moja na kulala hoteli moja huko juba,
kinachomshangaza sita ni hiyo process nzima je zitto anavyokaa na kusafiri na kikwete wanaongea nini na kikwete anapata information gani
kutoka kwa zitto,na je chadema kwa ujumla wanaonaje hilo swala,
je zitto alitumwa na wenzake akakae na kikwete?walikubaliana au anajifanyia maadam anamwona kikwete anamchekea?ni haki kwa makamanda wa upinzani kufanya vitendo kama hivyo?
vitendo vingine vilivyomshangaza sita ni hali halisi ya wapinzani hasa bungeni,mfano mzuri ni wa mbunge mzee cheo kwenda na timu ya ccm
uk kudai serikali ya uk ilipe hela za rada kwa ccm,kumbuka cheo ni mpinzani,sasa tuite nini hiyo process kama sio unafiki?je cheo alichukuliwa na ccm kwenda kuwakilisha wapinzani wa tanzania kudai hiyo hela aliwasiliana na wenzake?na kama kweli ni mpinzani kwa nini alikubali?aliweka maslahi ya nani mbele?
kitendo kingine ni kile kinachofanywa na mrema mbunge aliyekuwa anaaminika na watanzania kuwa anaweza kututoa hapa tulipo,
je mambo anayofanya sasa hivi mrema kujipendekeza kwa ccm sio unafiki?
MR SITTA AMEKAA NA KUONA HUO NI UNAFIKI NA AME-GENERALIZE KILA KITU NA KUWEKA PEUPE
tukumbuke sita alisaidia sana upinzani kufika hapo ulipo
tusiwe watu wa kukurupuka tujifunze kusikia,kufikiri na kuchukua hatua!!!!!!!!
mimi binafsi nimekaa na kufikiri sana tangu jana na hilo ndio jibu langu,weka la kwako!!!!!
 
Nafikiri tunahitaji kujua maana halisi ya neno "Unafiki".
 
Pia nafiri kukubali au kutaka maendeleo lazima tukubali kukosolewa, tunataka siasa safi na sio majungu.
 
hivi mnafiki ni nani anayetetea maslai ya wananchi au anayeanzisha chama akiwa ndani ya chama ni sawa na mtu yuko ndani ya kanisa anaanzisha kanisa tena

NI CCM WOOOOOOOOOOOTE + some few foxes wanaochekelea kuwaona waTz waliokosa MATUMAINI YA HUDUMA BORA etc! Nimeendelea na ninaendelea kuwatambua.
 
06_11_50pyc2.jpg
Hili ndilo bunge linaloongozwa na mama Kiroborobo aka Spika Semamba wa Chama cha zidumu fikra za mwenyekiti
A.k.a bi kiroboto
 
Mwanasiasa yeyote yule wa kweli kabisa na wa dhati ni lazima awe mnafiki...
Ndio maana uki observe, Great leaders katika history sio Wanasiasa - ila tu
huongoza kwa misingi ya mwanadamu wakiwa guided na Siasa lakini sio kua
controlled by Siasa...

Mtu yeyote anaetetea maslahi ya wananchi na hana nguvu/uongozi wowote
ni wa kumuogopa zaidi kama huo utetezi ulianza baada ya kutaka kugombea
nafasi au kiti fulani... ila mtu anaetetea maslahi ya wananchi na kutafuta nafasi
ya kuwawa kilisha na akawakilisha kweli... then huyo sio mnafiki...

Na mtu ambae anaanzisha chama ndani ya chama... yupo kati ya makundi mawili

  1. Ni a committed Mwanachama na yuko kwa ajili ya wananchi... bada ya kugundua chama chake hakina malengo mazuri na kafanya kila jinsi (kabla ya kuondoka.. ) kurekebisha hayo madhaifu na imeshindikana... hivyo basi anaamua kuanza cham kingine ili aweze fanikisha malengo kwa wananchi...
  2. Ni mwanachama committed lakini kila akitaka apande ngazi ili makulaji yaongozeke bado hakubaliki na fellow members... impatience inamkimbiza na kumfanya aanzishe Chama... kwa manufaa yake sio wananchi... ila tu hujifanya hivyo...
Hivyo hio statement yako ni ya kuitafakari kwa ukaribu... sio Black and White...
 
kama tukikataa kukosolewa basi tutaonekana wendawazimu wanaovaa nguo!
haswaa nakubaliana na wewe rosemarie, tunavoendelea kulalama basi tutakuwa sawa na mwalimu anaefundisha wanafunzi kuwa 1+1=11, na akiambia hajui au kakosea anatukana.
 
Kwani kasema uongo? Ni kweli wabunge wa CDM ni wanafiki.
Wa CUF, NCCR je Vp Wabunge wa CCM wanao justify matumizi ya Bajaji ambulance as the best option available? Vp wanapotisha Bajeti ya wizara ya Nishati kinafiki wakati wanjua fika haiaddress issue muhimu ktk upatikaji wa umeme?If I may ask unajua maana ya mtu mnafiki?
 
Jamani madaraka matamu Sitta hakufikiria kama ccm wammwaga mapema sasa anaona Anna Makinda kamnyakulia kiti chake,anataka afanye kila anavyoweza arejee,ccm alikua anapeta huko aliko sasa pesa yakujiachia kama alivyokua kwenye shamba la bibi <CCM> haipo ndio mana anaumbuka sasa kesha Chamba upupu wacha umuwashe.
 
nashangazwa sana na kitendo cha wapinzani wengi kutokubali kukosolewakitendo cha waziri sita kukosowa wapinzani na kuwaita wanafiki nakubali kabisa,nafikiri sita ni mtu mzima na hawezi kukurupuka na kutoa maneno kama hayo bungeni,samweli sita amekaa na kutafakari vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wapinzani na kuona ni unafiki,mfano mzuri ni huu wa zito kusafiri na kikwete ndege moja na kulala hoteli moja huko juba,kinachomshangaza sita ni hiyo process nzima je zitto anavyokaa na kusafiri na kikwete wanaongea nini na kikwete anapata information ganikutoka kwa zitto,na je chadema kwa ujumla wanaonaje hilo swala,je zitto alitumwa na wenzake akakae na kikwete?walikubaliana au anajifanyia maadam anamwona kikwete anamchekea?ni haki kwa makamanda wa upinzani kufanya vitendo kama hivyo?vitendo vingine vilivyomshangaza sita ni hali halisi ya wapinzani hasa bungeni,mfano mzuri ni wa mbunge mzee cheo kwenda na timu ya ccmuk kudai serikali ya uk ilipe hela za rada kwa ccm,kumbuka cheo ni mpinzani,sasa tuite nini hiyo process kama sio unafiki?je cheo alichukuliwa na ccm kwenda kuwakilisha wapinzani wa tanzania kudai hiyo hela aliwasiliana na wenzake?na kama kweli ni mpinzani kwa nini alikubali?aliweka maslahi ya nani mbele?kitendo kingine ni kile kinachofanywa na mrema mbunge aliyekuwa anaaminika na watanzania kuwa anaweza kututoa hapa tulipo,je mambo anayofanya sasa hivi mrema kujipendekeza kwa ccm sio unafiki?MR SITTA AMEKAA NA KUONA HUO NI UNAFIKI NA AME-GENERALIZE KILA KITU NA KUWEKA PEUPE tukumbuke sita alisaidia sana upinzani kufika hapo ulipotusiwe watu wa kukurupuka tujifunze kusikia,kufikiri na kuchukua hatua!!!!!!!!mimi binafsi nimekaa na kufikiri sana tangu jana na hilo ndio jibu langu,weka la kwako!!!!!
Think twice... you can do better.
 
Kama sitta angekuwa wa imani ya malaria sugu angesema mashambulizi haya dhidi ya sitta ni udini..... tafadhali Malaria sugu pitia thread hii na kisha uone na kutambua kwamba linapokuja suala la kitaifa Jamiiforums haiangalii mtu kwa dini yake.
 
CCM ni wanafiki na pia ni matapeli na wezi wa mali za watanzania! Nani anafadhali?
 
CCM ni wanafiki na pia ni matapeli na wezi wa mali za watanzania! Nani anafadhali?


hivi kama jirani yako ni jambazi na unajua halafu akaja kukupa ushauri,utaukataa kwa sababu ni jambazi au utauangalia kwa upana?
 
Mmh! Je vipi kuhusu yeye ambaye alitaka kuanzisha chama? Huyu si mpinzani? Mch. Msigwa jana alipata kuhoji!
 
Katika Sakata hili lote anayefaidika ni Mtoto wa Mkulima Pinda. Baada ya kukacha vipindi viwiili mfululizo vya maswali na majibu papo kwa papo na baada ya kupima upepe na kuona kutakuwa na mijadala mizito katika Wizara ya ofisi ya makamu wa Rais. Wizara ya Afya na baadaye madini. Pinda akabuni safari na kumuingiza King Sitta. Tumeona Sitta alivyo bore kuhusu Muungano na Jana tumeshuhudia jinsi alivyo likoroga kuhusu wizara ya Afya.

Sitta jana ameonekana choo na ikija malizika wizara ya madini atakuwa ananukaa MAVI. Nilishangaa kabisa jinsi Sitta alivyotetea ulegevu wa serikali kukusanya kodi/mapato kwa hoja nyepesi ya posho na unafiki. Sitta amejichimbia kaburi mwenyewe.

Lakini pia nimushukuru mh. David Kafulila. Hivi nyinyi watu Kigoma mna kitu gani cha zaidi mnachotuzidi watanzania wengine? Aliianza Dr. Kaborou, akaja Zitto na sasa Kafulila. Watanzania tungeweza kuchagua wabunge MAKINI kama wenzetu wa Kigoma nchi hii tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana. Ninapata impression kwamba watanzania labda tuanze kufikiria kumtafuta rais kutoka Kigoma na hiii sio kwamba nampigia chapuo Zitto au Kafulila.

Mh. Kafulila alisema kweli leo miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika budget ya wizara ya afya inakuwa tegemezi kwa 98%. 2% tu ndiyo pesa zetu za ndani! halafu wabunge wa CCM jamani mnashindwa kuona huu UKWELI ULIO WAZI kwamba kwa mwendo huu yule aduai No. 1 aliyetufanya tumfukuze mkoloni adui MARADHI hatutaweza kumshinda.

Sijui ni watanzania wangapi waliona au kusikiliza hii hoja ya Kafulila v wabunge wa CCM, sidhani kama kuna mwananchi angekubaliana na utetezi wa Sitta na wabunge wengine wa CCM.

Mh. Kafulila umeingia kwenye historia ya nchi hii utakumbukwa daima kama mtetezi wa wanyonge wa Tanzania. Na pia tunashukuru Mungu kwani sasa tumemfahamu Sitta ni nani, kweli Mungu huwapigania waja wake.
 
Tukiangalia kwa mapana yamkini Sitta yuko sahihi kusema wabunge wa upinzani ni wanafiki, mtoa hoja wa kwanza ambaye ni Zitto kwa niaba ya chama chake cha CHADEMA alitaka posho zifutwe lakini zipelekwe jimboni kwake badala ya kurudushwa hazina ili zipangwe upya. Ni nani kati yetu ana uhakika kwamba fedha hizo zingetumika kwa makusudio ya maendeleo wakati Akaunti ya benki ya mfuko wa maendeleo wa jimbo la Zitto iko kwa jina lake?
 
Hoja ya mzee Sitta haina mashiko kwani amesahau kuwa kwenye bunge la 9 tulikuwa na wabunge wa upinzani wachache ambao ndo watetezi wakuu wa wananchi hivi sasa, na leo namba yao imeongezeka bungeni na ndo mda muafaka wa kufuta uozo wote ambao bunge lilishafanya.
Hivi Sitta anadhani posho ambazo ni wizi wa fedha za umma uendelee kwakuwa awamu yake haukugundulika?
 
Back
Top Bottom