Leo ikiwa ni Alhamisi hebu tuwakumbuke wabunge machachari enzi ya Bunge la Spika Marehemu Samwel Sitta!

Andre-Pierre

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
328
1,208
Leo ni alhamisi , huwa tunakumbuka mambo ya zamani kidogo. Mnalikumbuka Bunge la Spidi na Viwango chini ya uongozi wa Spika Marehemu Sitta?

Hebu leo tuwakumbuke wabunge waliokuwa machachari kwenye kuibua hoja zenye maslahi mapana ya Taifa.

Wabunge hao ni wale waliokuwepo katika uongozi wa Spika Samwel Sitta. Tukumbushane baadhi ya mikasa ya Bunge lile ambayo ilikuwa gumzo miaka ile.

Karibuni sana...
 
Mimi naanza na mkasa wa Zitto Kabwe! Alikuwa machachari miaka ile akiwa Chadema. Akatuhumiwa kuongea uongo bungeni. Basi aliyepata kuwa Mbunge wa Mchinga, Mudhihir M. Mudhihir akatoa muongozo wa namna Zitto anavyopaswa kushughulikiwa huku akimnyooshea mkono.

Zitto akala ban bungeni, siku chache baadae Mudhihir akapata ajali na kukatika ule mkono aliotumia kumnyooshea Zitto.
 
🤣 🤣 🤣 Mtoto kaoga dawa za hatari
 
Back
Top Bottom