Wosia wa Le Mutuz: CCM/Serikali Imejisahau Haisikilizi, Ikosolewe. Wabunge Wasisifu Viongozi kwa Kutimiza Wajibu Wao. Upinzani Sio Uadui, JF Keep Up!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
NIPASHE YA JANA 04/06/2023
Screen Shot 2023-06-05 at 7.31.45 AM.png
Screen Shot 2023-06-05 at 7.32.15 AM.png

Kama nilivyoahidi wiki iliyopita Wosia mzito wa William Malecela (Le Mutuz) kwa CCM, Wapinzani, Serikali na kwa JamiiForums uzingatiwe na kutekelezwa ili tuendelee kumuishi kuwa wiki hii, nitawaandikia kile alichokisema mtoto wa Mzee Malecela, hayati William Malecela kwa jina maarufu Le Mutuz katika mahojiano yetu na mimi ambayo hayakupangwa, ni mtu mnakutana tuu unampiga maswali bila kumtayarisha, kiuandishi intervyuu hii inaitwa “impromptu’

Kwa kawaida sisi waandishi wa habari tunapotaka kufanya mahojioano ya kihabari na mtu yoyote, huwa tunamuandaa na wakati mwingine hata kumtumia maswali ili aandae majibu.

Sisi waandishi pia tumegawanyika, wako waandishi wa maswali rahisi rahisi na waandishi wa maswali magumu, ikitokea mwandishi wa maswali magumu umekutana na mtu bila kupanga ukampiga maswali magumu na akakujibu kwa ufasaha kama hapa Le Mutuz, hiyo maana yake Le Mutuz ni akili kubwa, kuna viongozi wengine akisikia tuu anatafutwa na waandishi wa maswali magumu, anaingia mitini, ama kwenye press conference, mwandishi wa maswali magumu ukiuliza swali gumu, kiongozi analikwepa kiana.

Hivyo hii interview na William Malecela, Le Mutuz nimeiita wosia kwasababu hakujiandaa na akatema nondo nzito. Mahojioano hayo yako kwenye mtandao wa YouTube

Kwa faida ya wengine, unaweza kusikia kitu kwa masikio, na usielewe, hivyo hapa nakuletea sehemu mahojiano hayo kwa maandishi kwa faida ya wasomaji wa makala zangu. Kwenye wosia, nitaweka msisitizo kwa bold.
PM ni Pascal Mayalla na WM ni William Malecela
PM: “Katika pita pita yangu, nimekutana na mwana JF wenzetu atajitambulisha”
WM: (anacheka huku anafuna bigijii “Ha ha ha, Naitwa William John Samwel Malecela ni member wa JamiiForums, ni mmoja wa waanzilishi, I have been a member toka tulipoianzisha and I love it"
PM:”Kuna mtazamo mtandao wa jamiiforums jf, kazi yake ni kulalamika tuu, kuikosoa serikali, hauelezei mazuri yoyote ya serikali, wao kazi yao ni kuvurumisha tuu makombora na ukosoaji, kuna ukweli kuhusu hili?”.

Wosia kwa serikali: serikali inatakiwa kufanya mema wakati wote,
WM: “Naomba kusema serikali yetu kwa muda mrefu imekuwa ni serikali ya chama kimoja, sasa ukafika wakati tukaingia kwenye vyama vingi, wakati wote wa mfumo wa chama kimoja, wananchi walikuwa na madukuduku ya kutoa matatizo yao na serikali, haikuwepo nafasi, tulipoingia vyama vingi wananchi wamepata nafasi ya kukosoa serikali, Jamiiforums hakipawi kuwa chombo cha kusifia serikali kinatakiwa kuwa chombo cha kukosoa serikali. Serikali kisheria by the law, inatakiwa kufanya mazuri wakati wote.

Wosia kwa Wabunge: Wasipoteze muda kuwasifu viongozi wao kwa kutimiza wajibu wao.
WM:
“hivyo hakuna sababu ya sisi wananchi kuisifia serikali kwa mazuri inayoyafanya, kama juzi mbunge mmoja alipouliza Bungeni, haelewi ni kwa nini wabunge wengi wanapoteza muda wao kuwasifia viongozi wa vyama vyao Bungeni kwa mambo walioyafanya nje ya Bunge, huo ni wajibu wao.

Wosia kwa Jamiiforums, Mitandao, na Makundi Sogozi
WJ: “
Jamiiforums inatakiwa kuwa chombo cha kuikosoa serikali, kuisaidia serikali kwasababu serikali ni kubwa mno haiwezi kujiona kwenye kila kona ya mwili wake, jamiiforums inaisaidia serikali kuona mapungufu yake. lakini jamiiforums sio mtandao wa Chadema, nimesikia hizi habari siku nyingi kwamba jamiiforums ni mtandao wa Chadema, hapana!. Mimi ni CCM, nimesema and I have said it mara nyingi commitment yangu ni kuhakikisha kuwa CCM, inatawala kwa miaka 50 ijayo”.

PM: “Watanzania wameamka, hakuna chama cha kutawala milele!”.

Wosia kwa CCM: CCM ina tatizo la viongozi kwa viongozi wananchi hawana tatizo na CCM.
WM
: “Nimesema hivii, baada ya mkutano wa Jangwani nikashuhudia jinsi wale wananchi waliomiminika pale uwanjani, nikamwambia Mwenezi wa CCM Nape, tatizo la CCM ni sisi viongozi kwa viongozi “

WM: ”pamoja na mabaya yote yanayosemwa kuhusu CCM, CCM bado inapendwa na wananchi wa kawaida, umati wa watu uliojitokeza Jangwani bila kulazimishwa ni ushahidi wananchi hawana tatizo na CCM”

Wosia kwa CCM/Wapinzani: siasa sio uadui
WM:
“Siasa sio ugomvi, nimelithibitisha hilo kwenye mechi ya wabunge wa Yanga na Wabunge wa Simba, I was there, siasa sio ugomvi, siasa inatakiwa kukosoana na kuelezana ukweli”.

Wosia kwa CCM: CCM ijifunze kusikiliza).
WM:
“Ninasema CCM ina uwezo wa kutawala miaka 50 ijayo kama CCM itajifunza kusikiliza, CCM haisikilizi!.

Wosia: CCM wa introduce time limit kwa uongozi ndani ya chama ili kuleta akili mpya, mawazo mapya.
WM:”Jana nimeshiriki kugombea level ya kata, wilaya na mkoa, I was very shocked kukuta watu walioshika vyeo kwa miaka 20, bado wanagombea, hawataki kutoka!, hilo ni tatizo kubwa la CCM, CCM lazima tufike mahali tuwekeane limit baada ya miaka 10 au 15, usigombee tena, tupishe wengine, tulete akili mpya”.

Wosia kwa Jamiiforums, kuendelea kuisaidia serikali.
WM:
“Jamiiforums, keep on helping the government, inaendelea kuisaidia serikali”.

Wosia kwa CCM, imekaa madarakani kwa muda mrefu sana unajisahau
WM:”
Serikali inafika mahali inalala usingizi, serikali ni kubwa mno, na tumetawala kwa muda mrefu sana. Watu wenye akili nyingi wanasema, ukikaa madarakani kwa muda mrefu sana, unafika mahali unajisahau, CCM kuna areas nyingi tumeisha anza kujisahau, lakini we are alright, sawa Bwana Paskali!”.

Alimalizia William Malecela, Le Mutuz. Ni maneno makubwa mazuri, mazito aliotuachia.

RIP William Malecela Le Mutuz, wa kukuishi, watakuishi, wasipotokea, wewe umetiza wajibu wako, mwendo umeumaliza kikamilifu!.

Wasalaam
Paskali.
 
Hapo kwenye kuleta akili mpya inasaidia sana kuondoa watu kujijengea mizizi hadi wanageuka wao ndio kama dola au wanaotawala gizani.

Huko kwa watendaji ni sawa lakini wanasiasa kutokuwa na limit ina matatizo mengi. Bora wangesema baada ya miaka 10 usigombee at least for 5 years ndio uruhusiwe.

Kuna wazee wanagombea kila mara au kuteuliwa wakati walishatumikia taifa miaka mingi.
 
Naamini alikuwa akitoa hayo mawazo yake kwasababu alikuwa nje ya hilo dude linaloitwa CCM, lakini kama angepata nafasi ya kuingia ndani yake kwa kushinda hizo nafasi alizokuwa akigombea, na kukuta bado wengine waliokuwa uongozini wanazitolea macho, asingetoa maoni yake kwa uhuru kama alivyofanya.
 
Back
Top Bottom