Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
1,025
Reaction score
475
Akitolea ufafanuzi kombora lililorushwa na David Kafulila, Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta ameikejeli kambi ya Upinzani kuwa ni wanafiki na waliojaa kauli nyepesi na za Ujanja ujanja na kazi waliyotumwa bungeni ni kufanya wanachokifanya sasa, hivyo wabunge wa CCM wawapuuze na kuwatazama kama walivyo kwani wananchi wanatazama na wataamua kwa wanayoyafanya.

Inashangaza kuona Sitta anaobuka na kauli hizi huku maji yakiwa shingoni kwa upande wake katika uwanja wa siasa. Akizungumza kwa mbwembwe huku akizomewa pia na baadhi ya Wabunge pale aliponukuu mfano wa hoja ya Posho

Sitta amesikika dhahiri akijikinga katika mwavuli huu kwa kuhoji inakuwaje leo wabunge wa Upinzani ambao wengine walikuwapo miaka kadhaa iliyopita bungeni na wamekuwa wakilipwa posho hizo kwa miaka mitano iliyopita leo wanziona si halali, warudishe posho zote ndio waseme kauli zao hizo za kinafiki alisisitiza Sitta.

Awali kigwangala nae aliangukia pua baada ya kuataka kuota muongozo kwa Mbunge wa Viti maalum CDM aliyeponda utitiri wa Vihiyo waliojaa MSD kuwa ndio kiini cha tatizo la upungufu mkubwa wa madawa kwa sasa Nchi.
 
Sita kaanza mbio za kujikomba CCM ili wasahau au wamsamehe kuhusu kuanzisha CCJ.

Sikutarajia mtu ninaye mheshimu kama Sita kumwaga upupu namna hii.
 
Huyo naye anazeeka vibaya kwishney na yeye.

Akitolea ufafanuzi kombora lililorushwa na David Kafulila, Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta ameikejeli kambi ya Upinzani kuwa ni wanafiki na waliojaa kauli nyepesi na za Ujanja ujanja na kazi waliyotumwa bungeni ni kufanya wanachokifanya sasa, hivyo wabunge wa CCM wawapuuze na kuwatazama kama walivyo kwani wananchi wanatazama na wataamua kwa wanayoyafanya.

Inashangaza kuona Sitta anaobuka na kauli hizi huku maji yakiwa shingoni kwa upande wake katika uwanja wa siasa. Akizungumza kwa mbwembwe huku akizomewa pia na baadhi ya Wabunge pale aliponukuu mfano wa hoja ya Posho

Sitta amesikika dhahiri akijikinga katika mwavuli huu kwa kuhoji inakuwaje leo wabunge wa Upinzani ambao wengine walikuwapo miaka kadhaa iliyopita bungeni na wamekuwa wakilipwa posho hizo kwa miaka mitano iliyopita leo wanziona si halali, warudishe posho zote ndio waseme kauli zao hizo za kinafiki alisisitiza Sitta.

Awali kigwangala nae aliangukia pua baada ya kuataka kuota muongozo kwa Mbunge wa Viti maalum CDM aliyeponda utitiri wa Vihiyo waliojaa MSD kuwa ndio kiini cha tatizo la upungufu mkubwa wa madawa kwa sasa Nchi.
 
Kwa hakika the OLD MAN IS IN COMMA, may be unafiki huu can do him good a bit of political relief
 
Kiukweli binafsi huwa simuhusudu mzee SIX japo natoka wilaya moja na yeye, kauli zake huwa siziamini hata chembe. Sifa zimemtawala mzee wetu huyu.
 
Samwel Sitta, mwanzilishi na mfadhili mkuu wa CCJ ni mnafiki mkubwa sana. Alizuga watanzania wengi wakamuona kuwa ni kamanda vita dhidi ya ufisadi kumbe yeye mwenyewe ni fisadi papa, hivi kutumia zaidi ya Tsh 500,000,000/- kujenga ofisi ya spika wa bunge nyumbani kwao Urambo kama siyo ufisadi ni nini?Hivi anaweza kuwaeleza walipa kodi wa nchi hii ofisi ile ina matumizi kwa sasa?Huyu mzee ni mnafiki wa kiwango cha juu kwani ni yeye alilizima kihuni sakata la Richmond bungeni.Kifupi huyu SAMWEL SITTA AOGOPWE KAMA UKOMA
 
Kiukweli binafsi huwa simuhusudu mzee SIX japo natoka wilaya moja na yeye, kauli zake huwa siziamini hata chembe. Sifa zimemtawala mzee wetu huyu.

Mzee is political saturated. Anatafuta agenda za kupamba kurasa za magazeti. Hizi siasa za magazeti ndio zianawatoa roho viongozi wapenda ujiko wababaishaji wa utekelezaji. Mifuko kumi ya Cement anataka media coverage vyombe vyote wawepo na waandishi wa Blog.

Huu ndio mwisho
 
jamani kadri magamba yanavyozidi kuwa na umri mkubwa ndivyo na akili inazidi kuwapungukia
 
Hata kama aliyosema ni kweli angekaa kimya kunusuru hadhi yake...shauri yake
 
Sita kama kuna mtu wa kuogopwa yule ni mnafiki kuliko wote bungeni huwa anacheza na popularity
 
hata kama ni ukweli angekaa kimya kunusuru hadhi yake...atajiju
 
CCM hakuna mzima hata kidogo .Yeye anadhani anakisaidia Chama mwache atajionea .Watafute hoja nzito waweze kuhalilisha posho Maalim kesha waambia hawasikii.Kwani kuwemo miaka 5 bungeni ndiyo sababu ya kutoipinga posho ? Huyu mzee eti naye ana uchungu na Nchi.Huyu ana uroho wa madaraka na si lolote .CCM ndiyo walivyo unafiki means what ? Watu kusema ukweli ?Kesha shusha heshima yake kwenye jamii hata wale waliokuwa wanamkubali basi wameona aibu .Hakuna kitu
 
Kipenzi cha CDM Sitta leo kawageuka anawaita CDM wanafiki!
 
CCM hakuna aliyena afadhali wote ni Mijmbazi inayotuibia Kodi na Rasilimali Zetu.
 
Hakuna zaidi ya ubabaishaji huu Rev. Ila jioni itabidi bibi kiroboto akalie kiti na kama hayupo Dodoma basi uovu mwingi leo utapata nafasi ya kuanikwa bila hiyana
Leo tena kipenzi chenu CDM mnamkataa? Magwanda bana
 
Back
Top Bottom