Unstoppable
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,046
- 384
Kutoa hoja ya msingi wakati wewe mwenyewe huchukui jukumu la kuishi maisha hayo ni Unafiki! tumewaona kina Seif Sharrif hhamad hapa wakipiga vita wagonjwa kupelekwa India kwa matibabu lakini siku aloumwa yeye aligeuka na kudai ni haki yake kama kiongozi na akaitumia sheria alokuwa akiipiga vita kama ushahidi wa haki yake. Huu ni Unafiki!.
Tazama wabunge wa CUF Zanzibar wanapiga vita Muungano lakini wanapokea misaada yote toka bara na bado wanajiandikisha kuchaguliwa kuwa wabunge ktk bunge la Jamhuri na wamefikia hadi kurekebisha katiba kukidhi matakwa yao wao wenyewe ya kiuongozi hali wakiwa bungeni kila siku ugonvi ni muungano. Unapinga Muungano wakati huo huo unasaini muafaka wa kiutawala unaotuunganisha! huu ni Unafiki!..
Kwa hiyo Sitta anapozungumzia kambi ya Upinzani ni wanafiki hajakosea kabisa na imefanywa makusudi kabisa kuwanyima Chadema mamlaka ya kuchagua viongozi wake. Ndio maana tumeona wenyeviti wa kamati tofauti wakichaguliwa na CCM toka kina Mrema, Cheyo, Zitto na wengineo wakipewa dhamana ili Unafiki wao ujitokezee!
Inawezekana unalosema ni sahihi. Sasa solution ni nini? Mapendekezo/ where do we go from here? Je name calling itamaliza tatizo? Argument ni nzuri kama ikiwa constructive ili tufikie goal yetu (kuwaondolea kero wananchi).
Lakini hii imeishia kwenye jazba na miongozo tu. As I see it, unapotaka soln ya kitu unaanza kwanza na neutral discussion bila kufanya character assassination, then ukishapata jibu au mkisha exhaust all options wakati wakufunga mjadala ndio unaweza ukatoa yaliyoko moyoni. Lakini ukianza na character assassination hamuezi kuwa na substance kwenye mazungumzo.
Na hii sio kwa CCM tu bali na Upinzani pia. I should also say; Sitta pamoja na mapungufu yake nilikua namuona mkomavu flani hivi kwenye haya mambo, lakini kaniangusha sana. Huwa anamisimamo yake peke yake hata kama hayuko sahihi. Lakini anaanza kunistua sasa. Labda amejikwaa sijui ngoja tuone.