Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

serikali yetu imejawa na mafisadi mno katika kila ilan ya chama viongozi hujiwekea mikakati yao kwa ajili ya maendeleo ya taifa.hii inaonyesha dhahiri kuwa mweshimiwa sitta ana ufinyu wa uelewa,haiwezekani mtu akahisi kunya leo alafu umwambie kwanini hujanya jana,viongozi kama hawa 2napaswa kuwaondoa bungen kabisa ni bora akapalilie 2mbaku kwao huko kuliko kuongea pumba mbele ya hadhira
 
Sitta anapata wapi ujasiri wa kuita mtu yeyote (hata kama si mbunge) mnafiki? Na asema haya kama ccm card holder or ccj card holder?
Kufanya kosa sio kosa, bali kuridia kosa ni kosa. Kama wabunge wamekuwa wanachukuwa posho isivyo halali kwake Sitta anaona waendelee tu maana wakisitisha watakuwa wanafiki?

Wanasema, ukitaka kumjua mtu vizuri basi mmpe madaraka.Sitta kapewa cheo cha kukaimu shughuli za serikali Bungeni na bila kupoteza muda anaonekana kutumia fursa hiyo kujijenga kama alivyojengea hekalu jimboni kwake wakati akiwa Speaker!
 
Kwani Sitta ni nani jamani,si amekuwa historia ,haitajiwi hata kujadiliwa humu,Sitta ni sawa na Maalimu Seifu kelele zote ni kutaka cheo,na JK kamvika kilemba cha ukoka,sasa anabweka hovyo kama vile mbwa aliyesikia miluzi mingi,hajui afanye nini,miluzi imempoteza kabsa sasa naye ni NDIOOOOOOOO,papapa kwenye meza pale mjengoni
 
Ndugu msijali kwa wanayoyafanya yamekuwa dhahiri hata kwa mtoto mdogo anauona upendeleo na double standards.Lakini kubwa linalotupa moyo ni kuwa watz wameona na kuelewa sana sana viongozi wa bunge wanazidi kuichimbia kaburi CCM na serikali yake either by intention au bila kujijua.
 
Sitta mbona ha eleweki? Mara awe jasiri mara awe upande wa ma gamba afu mi namu shangaa coz magamba wenyewe anao wa tetea hawa mtaki mi naona ana zeeka vibaya.
 
Kuna mtu humu alikuwa na signature inayosema " MITANZANIA NDIVYO ILIVYO" Hivi ni uzee au kufilisika kisiasa? Sitta na CCM yake wanataka suala la posho liwe la kibinafsi na wala sio la kisheria. Wanataka WABUNGE wasiotaka posho waache wanaotaka wachukue. Huu ni utoto, hivi hapa unataka ku-achieve nini? Wakikataa posho wabunge wa chadema tu lengo la kuokoa pesa ya mlala hoi inayoishia kutumiwa na vimada litatimia? Na Labda nimuulize Sitta, Hivi wakati Dr Slaa anapiga kelele bungeni msimu uliopita kuwa mshahara wa mbunge ni mkubwa mno kulinganisha na uwezo wa nchi hakuishiwa kubezwa na CCM? Hapa nani mnafiki SITTA AU SLAA? Maskini msomi kama Sita ananaswa kwenye mtego wa kitoto. Anasemema warudishe kwanza posho za nyuma ndio wadai kufutwa za sasa. Kwani kurudisa posho za miaka mitano iliyipita ndio kunaifanya hoja ya kufuta posho mbalimbali iwe na nguvu ya kisheria? Kweli mitanzania ndivyo ilivyo
CDM ukweli huwa unakusumbueni sana! Je hakuna wabunge ambao miaka mitano illiyopita waliramba posho? Wazee wa Magwanda kubalini hili kweli kuna Unafiki hapa! Mlitaka Sitta asemeje? Tanzania tuna Wapinzani Wanafiki hasa wavaa magwanda! ambao kwao wakiambiwa ukweli hugeuka kuwa maadui wa aliye wasema kwa uovu wao!
 
Pamoja na yote tatizo kubwa liko kwenye spika,naibu wake na wenyeviti wa vikao maana maamuzi wanayotoa! ngumi zitapigwa bungeni hivi karibuni.mlioko Dar na Dodoma waonesheni kwa vitendo watu hawa-chomeni hata gari ya mmoja wao watambue nchi ina hasira kupita kiasi sasa.Tungetamani pamoja na hizo posho za wabunge hata kodi tunazokatwa mwezi huu zimalize mgawo wa umeme then watu kama Sita wanaongea upupu bado wanapata watu kama Ndugai kuwakingia kifua!!aggrrr
 
hatuna speaker, naibu wa spika raisi, waziri mkuu wala mwanasheria mkuu. Waliopo ni wawakilishi, yaani wanakaimu tu.
 
Magamba jamani kila siku nasema ni janga kubwa kwa taifa hili! laaana tupu
 
Magamba ni ajali tena mbaya sana!I realy hate them all ccm MPs
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema mambo mengi ya wapinzani ni ya kinafiki na wamekuwa wakiibeza Serikali kwa kauli nyepesi nyepesi. Sitta alitoa kauli hiyo jana bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijaribu kutuliza Bunge lililokuwa limechafuka baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), kudai kuwa Serikali iliyoko madarakani ni legelege na imeshindwa kukusanya kodi. "Nawasihi wenzangu hasa wa CCM, hawa wapinzani hii (kupinga mambo) ndiyo kazi yao, wanabeza kila tunachofanya kwa lugha nyepesi nyepesi na mambo mengi wanayozungumza ni unafikinafiki hivi, sisi tuwaachie wananchi wawahukumu.

Kauli hiyo ilisababisha baadhi ya wabunge hasa wa upande wa upinzani kusimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti na wengine wakizomeana, huku Sitta ambaye ni Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, akiwa amesimama akiomba kuendelea. "Subirini nitoe mfano ... wanazungumza posho za vikaoni ni kuibia wananchi na baadhi yao wamekuwa wabunge kwa miaka mitano iliyopita na walikuwa wakizichukua, kama kweli ndivyo hivyo, basi warudishe," alisema Sitta.

Kauli hiyo ilisababisha wabunge zaidi, karibu 10 wakiwamo wa CCM kusimama kuomba Mwongozo wa Mwenyekiti, lakini Mwenyekiti Jenista Mhagama akaahirisha shughuli za Bunge kwa mapumziko ya mchana, kwa kuwa muda ulikuwa umefika, huku akiwaacha wabunge wakipiga kelele za kuomba Mwongozo. Kabla ya kuibuka tafrani hiyo, Kafulila aliyekuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alisema tangu Uhuru moja ya maadui waliopigwa vita ni maradhi; lakini akashangaa bajeti ya Afya ni ndogo na kuongeza kuwa inatokana na Serikali legelege kushindwa kukusanya mapato. "Miaka 50 ya Uhuru asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo ya afya inategemea fedha za nje, tatizo hamkusanyi kodi na Nyerere (Baba wa Taifa) alisema Serikali legelege inashindwa kukusanya kodi," alisema Kafulila.

Kauli hiyo ilipingwa na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangala (CCM) aliyesema Kafulila alitumia neno la kuudhi kwa kuiita Serikali ya CCM legelege. Dk. Kigwangala alifafanua kuwa Kafulila hakuwa na taarifa sahihi, kwa kuwa katika miaka mitatu iliyopita, Serikali ilikuwa ikikusanya karibu Sh bilioni 200, lakini mpaka mwaka huu, makusanyo yaliongezeka na kufikia karibu Sh bilioni 400. Baada ya ufafanuzi huo, Mwenyekiti wa Bunge, Mhagama alimtaka Kafulila kufuta usemi, lakini mbunge huyo alipinga akisema ni kauli ya Baba wa Taifa, ambaye kila mtu anamuenzi bila kujali anatoka chama gani.

"Tunapoteza muda kujadili suala ambalo liko wazi, mwaka 2005/06 Serikali ilikuwa ikikusanya wastani wa Sh bilioni 260 lakini dola moja ilikuwa sawa na Sh 1,000. "Leo mnakusanya karibu Sh bilioni 400 kwa mwezi, dola moja ni Sh 1,600 ni hesabu rahisi, hakuna kilichoongezeka ... sifuti usemi, niko tayari kufia ukweli huu," alisema Kafulila na kusababisha Sitta kuamka na kuwaita wapinzani wanafiki huku akiwataka CCM kuwavumilia. Hata hivyo, Mwalimu Nyerere alisema chama legelege huzaa Serikali legelege na pia aliwahi kusema "Serikali corrupt (inayokula rushwa) hushindwa kukusanya kodi," na si Serikali legelege hushindwa kukusanya kodi.

Awali, kabla ya tafrani hiyo, Kafulila alimtaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, ikibidi ajiuzulu kuliko kukubali kuwasilisha bajeti ya fedha ndogo bungeni huku ikitegemea fedha nyingi za wahisani. Alisema hiyo inatokana na wabunge na familia zao kuwa na uwezo wa kutibiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi, ndiyo maana hawawekezi katika hospitali za vijijini. Wakati akisema hayo, mmoja wa wabunge ambaye hakufahamika lakini mwanamke, aliwasha kipaza sauti akasema: "Pamoja na wewe (Kafulila) na Mbunge wa Mpanda Mjini Chadema (Said Arfi ambaye alilazwa India hivi karibuni)."

Hata hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, alisimama na kupinga kauli ya Kafulila, akisema: "Hili ni Bunge Tukufu, tuzungumze kwa heshima." Mbunge mwingine mwanamume akawasha kipaza sauti na kuhoji: "Nani ana heshima?" Nagu akaendelea kufafanua kuwa mwanawe ni daktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ni ya Serikali na hata baba yake mzazi alilazwa katika hospitali ya Katesh ambayo ni ya vijijini. Hata hivyo, sauti ile ya kiume iliendelea kumkatisha Nagu na safari hii Mbunge huyo alisema, "so what(kwa hiyo?"

Kutokana na kauli hizo za kukatishana, Mhagama alisimama na kusema ameisikiliza sauti ya mmoja wa wabunge wanaotoa kauli hizo za kejeli huku akimkatisha waziri aliyekuwa akizungumza na kubaini kuwa sauti hiyo inafanana na ya Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema). Alionya kuwa wanachofanya wabunge kuwasha vipaza sauti holela ili kuzuia hoja za wenzao kusikika au kuwakatiza, ni kinyume na Kanuni za Bunge na akifuatilia anaweza kuwabaini na kuwachukulia hatua.

Habari leo
 
Bado nakumbukumbu ya kurushiana makombora kipindi cha kampeni mwaka jana kati ya Dr. Slaa na Sitta aliyekuwa Spika wa bunge. Moja ya kombora la Dr. Slaa ni hili kwamba Samweli Sitta ni Mnafiki sana. Sasa ukweli huo unajidhihirisha anavyojikanyagakanyaga na kukosa hoja ya kutetea madhara ya uongozi wake bungeni kuongeza posho kiholela na leo yanamtokea puani. Kwa aibu ya kukosa hoja anaibuka na shambulizi ya kuwahamasisha wabunge wa CCM eti wawadharau na bila hata kupima kwa akili timamu kuwahadaa watanzania kwamba wananchi wenyewe waamua juu ya hilo. Kwa hoja hiyo Sita ana pakutokea?
 
kauli ya SITTA Kuhusu posho ni dhahiri anamtukana kiongozi mwenzie wa serikali MAKAMU WA RAIS WA ZNZ seif kuwa ni MNAFIKI kutetea posho zifutwe..hii mijitu bwana.ye ndio MNAFIKI no1
 
06_11_50pyc2.jpg


Hili ndilo bunge linaloongozwa na mama Kiroborobo aka Spika Semamba wa Chama cha zidumu fikra za mwenyekiti
 
Hivi ni kwanini linapokusiwa suala la posho wabunge huwa ni wakali kama nyuki? Je kuna maslahi gani kwa mwananchi wa kawaida? Mbona yanapogusiwa mambo ya unaafuu wa maisha ya mlala hoi sioni wakipigania kwa lengo la kumwinua huyu mtz. Tumeona bei ya mafuta ilivyopitishwa kirahisi bila hata kufikiri maisha ya mtz eti kwa sababu wao wamepata unaafuu ktk dizel na petrol. Nilidhan mtu kama SITA asingeweza kutoa kauli kama hii. 2naona wapinza wanyojitahid kututetea wanyonge. 6 unapotea take care....
 
Back
Top Bottom