Wapi nitapata soko la kuuza mkaa mbadala? Ujuzi wa kuzalisha ninao, mwenye kujua soko anijuze tafadhali

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Feb 6, 2022
276
792
Hello wapendwa! Nina ujuzi wa kutengeneza mkaa mbadala wa kupikia!

Lakini tatizo sijui wapi nitapata wateja!

Naomba mawazo nifanyeje ili nipate wateja ili nianze kuzalisha bidhaa hii.

Ujuzi ninao, vifaa na mashine zipo lakini shida ni wapi nitauza hii bidhaa!

Kwasasa napotaka kuanza kuzalisha Sina uwezo wa kumwajili afisa masoko! Lakini kama kuna vijana wenzangu mliosomea masoko hamna kazi leteni mawazo tufanye kazi pamoja tuunde kikundi cha pamoja!

Mwenye kujua wapi naweza peleka bidhaa hii anijuze!

Ni mkaa mbadala safi ambao hauishi haraka, unatumika kidogo tu kupikia, unatumika kwenye jiko la mkaa wa kawaida hata mafiga matatu unaweza kutumia!

Naomba anaejua wapi naweza pata soko la mkaa huu anijuze au tuwasiliane
IMG_20230626_095456_975.jpg
 
Kwahiyo ndugu yetu ulienda kujipa ujuzi wa kutemgeneza kitu usichokuwa na uhakika wa soko lake?

Kila la kheri, Mungu akuongoze kufanikisha ndoto yako
 
Kwahiyo ndugu yetu ulienda kujipa ujuzi wa kutemgeneza kitu usichokuwa na uhakika wa soko lake?

Kila la kheri, Mungu akuongoze kufanikisha ndoto yako
Ni katika harakati za maisha mkuu! Nilifulia hela ya gesi siku hiyo nyumbani nikapata wazo la kuunda mkaa mbadala! Nilipofanikiwa ndipo nikaona nianze kuzalisha kwa ajili ya kuuza ....tatizo wapi nitapata soko ndiyo changamoto!

Ikumbukwe Mimi pia ni fundi umeme! Hivyo nimeunda mota ambazo zitaniwezesha kuzalisha kilo 100 hadi 200 kwa siku! Lakini sijajua Nikishatengeneza huu mkaa nitaupeleka wapi? Ndiyo maana naomba ushauri
 
Ni katika harakati za maisha mkuu! Nilifulia hela ya gesi siku hiyo nyumnani nikapata wazo la kuunda mkaa mbadala! Nilipofanikiwa ndipo nikaona nianze kuzalisha kwa ajili ya kuuza ....tatizo wapi nitapata solo ndiyo changamoto!

Ikumbukwe Mimi pia ni fundi umeme! Hivyo nimeunda mota ambazo zitaniwezesha kuzalisha kilo 100 hadi 200 kwa siku! Lakini sijajua Nikishatengeneza huu mkaa nitaupeleka wapi? Ndiyo maana naomba ushauri
Naomba kujua uko mkoa gani na huo mkaa unaotengeneza unatumia malighafi gani na kiwango cha uzalishaji kwa siku ni kg ngapi?
 
Mkuu hongera sana.

Zungukia mashule hasa ya bweni na taasisi za elimu.

Pia hebu tuambie unauzaje kwa kipimo na kipimo kina ujazo gani
 
Naomba kujua uko mkoa gani na huo mkaa unaotengeneza unatumia malighafi gani na kiwango cha uzalishaji kwa siku ni kg ngapi?
Niko dar mkuu, Natumia malighafi za matakataka tu!

Kwenye uzalishaji hakuna shida, hata benki wako tayali kunipa mkopo! Tatizo kubwa ni wapi nitauza mkaa huu ...simu yangu ni 0711756341
 
Ni mkaa mbadala safi ambao hauishi haraka, unatumika kidogo tu kupikia, unatumika kwenye jiko la mkaa wa kawaida hata mafiga matatu unaweza kutumia!
1).Jaribu kutafuta wahitaji wa mkaa(mamantilie/shule) anza na kuuza 50% off(nusu bei) mfano kilo 10 bei yako 5,000 wewe uza kwa 2,500 hii kwa kuvutia wanunuzi.

2). Jaribu kutembeza mitaani kwa bei nafuu au ajiri vijana watembeze mfano kilo 5 unauza kwa 3,000. Wewe waambie vijana unauza kwa 2,000 wao waweke 2,300 hio 2,000 yako na hio 300 itakuwa yao.

3). Anza kuwauzia Ndugu na majirani kwa bei rafiki kumbuka hii kuuza bei rahisi ni kwa muda tu ili upate wanunuzi. Hata ukifanikiwa usiweke sawa na bei ya mkaa halisi wewe weka discount flani.

Nakutakia mafanikio mema.
 
Natarajia kuuza kilo moja kati ya tsh (1000~2500) kwa kilo moja Bei itategemea na mkaa unaenda wapi kwa pakeji gan!
Kilo moja kwa familia ya watu watano unaweza pikia hata siku 3!

Mkaa kidogo moto, moshi kidogo sana! Moto mwingi! Chakula kitamu!
Anza kututengenezea sisi wenye mahaba na mazingira.

Naupata espi huo mkaa?

Au umekuja kunadi bidhaa ambayo ya kusadikika?
 
Mbona hiyo kazi rahisi sana,tengeneze mkaa wako wa kutosha, beba jiko lako la mkaa sufuria na maharage, nenda kakae sehemu zenye mchanganyiko mwingi wa watu, mfano inje ya stend ya magufuri, kaliakoo, anza kupika kwa vitendo huku ukiwa unanadi kwa mdomo au vipaza sauti

Yaani uwe alwatani, pembeni unao mka wako wa kuuza, pamoja na vipeperushi vyako unapatikana wapi, walahi ndani ya miezi 2, utakuwa umezidiwa na wateja au utakuwa na mauzo ya milion 1 kwa siku

Maana ya matangazo ya biashara ni kujitoa ufahamu
 
Anza kututengenezea sisi wenye mahaba na mazingira.

Naupata espi huo mkaa?

Au umekuja kunadi bidhaa ambayo ya kusadikika?
Njoo uone mkuu au nipigie 0711756341 nimezalisha kidogo natumia nyumbani! Kwasasa nina kilo elfu 1000 zipo tu sijui hata pa kuzipeleka!

Kiufupi ni kama ka kiwanda maana nimeunganisha na mota za umeme kuchanganyia!
 
1).Jaribu kutafuta wahitaji wa mkaa(mamantilie/shule) anza na kuuza 50% off(nusu bei) mfano kilo 10 bei yako 5,000 wewe uza kwa 2,500 hii kwa kuvutia wanunuzi...
Msomi huyo
Kazi ya kimachinga hawezi ndo maana anatafuta soko ambapo atakuwa anauza mkaa wake akiwa ofisini tena na kiyoyozi juu.

Nimemuuliza tunaupata wapi mkaa tukaununue. Maana yake angekuwa ameusambaza kwenye maduka na masokoni lakini kumbe hata kuutengeneza bado
 
Back
Top Bottom