Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,304
moyoni sina nafasi, kuweka nongwa na chuki
wala siweki kisasi, kufanya hivyo sitaki
kugombana nna hisi, napotoka siongoki
Ila nitavumilia, wala hasama siweki
nguzo nilotegemea, ya mola haitenguki
Sina chuki kwa waovu, seuze kwa marafiki
siachi uvumilivu, kuikabili mikiki
subira ni uerevu, sikatai nasadiki
Wamo katika dunia, waongo na wanafiki
Wamo wenye nia mbaya, wenzao kuwahiliki
wachache walobakia, wakweli wapenda haki
wala siweki kisasi, kufanya hivyo sitaki
kugombana nna hisi, napotoka siongoki
Ila nitavumilia, wala hasama siweki
nguzo nilotegemea, ya mola haitenguki
Sina chuki kwa waovu, seuze kwa marafiki
siachi uvumilivu, kuikabili mikiki
subira ni uerevu, sikatai nasadiki
Wamo katika dunia, waongo na wanafiki
Wamo wenye nia mbaya, wenzao kuwahiliki
wachache walobakia, wakweli wapenda haki
Last edited by a moderator: