Wapi AshaDii?

Wapi AshaDii?

Status
Not open for further replies.
Boss and Kaizer

pata mashairi kwanza ....audio will be with you shortly

[h=6]Rabi sinipe mapenzi, hakuna wakuamini
Wapendwa wenye ujuzi, ni wachache duniyani
Pendo la kisikuhizi, kuhadaana nyoyoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Niwingi udanganyifu, kweli hakuna nyoyoni
Ambao wathibitifu, ni tabu kuwabaini
Kitu nnacho khofu, kuja vunjiwa thamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Wanaopenda wapende, mimi siye asilani
Nimejitowa upande, singii mwao kundini
Moyo nimepiga konde, siwezi kutamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Nimefunga moyo wangu, usinitie taabuni
Kuteswa na walimwengu, wasojuwa pendo ni nini
Haiwi fakhari kwangu, kujinasa mtegoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
[/h]
 
Ooh so nice to have you back AshaDii,

U can see, for yourself that apart from the love from me and maself and I, there is a 'plethora' of good samaritans here, with all good will and best wishes for you

"Oooh Rabbi, sinipe mapenzi" (Gaijin hebu do ze nidiful)

I am short of words hapa wajameni.

FF, vipi umemtayarishia nini mdogo wako leo (Vyangu ni vya chumbani zaidi)
Subira yavuta heri shemeji......subira yavuta heri...naburudika na leo tenaaaaa....thanx gaijin
 
ewaaa umemwona bibie ee Gaga....salamu zangu sijui kama ulizifikisha lakini....how is ur sunday
My sunday iko poa upweke tu nimetulia ndani hata mapazia sijayanyanyua kama usiku vile....bora karudi naona malalamiko yatapungua....
 
Boss and Kaizer

pata mashairi kwanza ....audio will be with you shortly

Rabi sinipe mapenzi, hakuna wakuamini
Wapendwa wenye ujuzi, ni wachache duniyani
Pendo la kisikuhizi, kuhadaana nyoyoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Niwingi udanganyifu, kweli hakuna nyoyoni
Ambao wathibitifu, ni tabu kuwabaini
Kitu nnacho khofu, kuja vunjiwa thamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Wanaopenda wapende, mimi siye asilani
Nimejitowa upande, singii mwao kundini
Moyo nimepiga konde, siwezi kutamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Nimefunga moyo wangu, usinitie taabuni
Kuteswa na walimwengu, wasojuwa pendo ni nini
Haiwi fakhari kwangu, kujinasa mtegoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Ukipata audio yake tutafutie na hii:

Kama nitahirishwa, penye viwili teuwa
Mali nikiamrishwa, au bahati chukuwa
Sitongoja kuonyeshwa, bahati nitanyakuwa
Bahati ni kitu bora, kiumbe akijaliwa

Ukiwa nayo bahati, juwa umefanikiwa
Utatumia wakati, bila pingamizi kuwa
Ukitamka lolote, wenzako huona sawa
Bahati kitu adhimu, mja akitunukiwa

Iwapo bahati huna, umekisha vunjikiwa
Utahangaika sana, la kufanya hutojuwa
Dunia itakubana, huwezi kujikunjuwa
bahati ni kitu bora, kiumbe akijaliwa

Pindi ukipewa mali, bahati ukufutiwa
Ijae shehena meli, yako umesabiliwa
Itapotelea mbali, bila ya wewe kujuwa
Bahati ni kitu bora, kiumbe akijaliwa
Ijapokuwa fukara, yake huenda muruwa.
 
My sunday iko poa upweke tu nimetulia ndani hata mapazia sijayanyanyua kama usiku vile....bora karudi naona malalamiko yatapungua....

kwa wale walalamishi wanaofikia kumfananisha na bibie FF......

Hapo bold, nimesoma kati kati ya mistari...
 
and this is special dedication to FaizaFoxy

Na watende wao, kina mwafulani, wawe furahani
Kitenda wenzao, haya mambo gani?, huteta pembeni
Yale yaso yao, yote mitaani, huwa vikaoni
Ajabu ya watu hao, ajabu yakini, yao hawaoni

Na watende wao kitenda wenzao, ati huwa mwao kitenda wenzao

Duni utu wao, hawana mizani, hawa watu gani
Huacha ya kwao, haya hawaoni, wapo mitaani
Lile liso lao, kwatu mikononi, mbuga miguuni
Kutwa kucha na vikao, wamo dadisini, kuwa fitinini

Tena kwa matao, vingi huvibeza, bila ya kuwaza
Wapendacho wao, kikiwapendeza, sifa hueneza
Mikononi mwao, chongo ni kengeza, huipa na tunza
Zile ila zao, ukiwasemeza, kimya huzimeza

Yule aso hili, huwa ana lile, ndio maumbile
Kamili jalali, zake sifa tele, hazishi milele
Kiumbe thakili, toka hapo kale, toka zama zile
Wambili ni wa mbili, la mwisho si mbele,


 
Last edited by a moderator:
And this is special dedication to X-Paster



Wache waseme sina budi nawe,
si khofu lawama, sababu ya wewe
Ungekuwa nyoka, hadi uniume,
seuze tausi ,wache walalame

Ungekuwa nyoka, sumu yako dawa
Damu husafika, maradhi hupoa
Uzuri hakika, wewe umepewa
Siwezi kwepuka, liwe litokuwa

Nimefunga nia, katu sibadili,
Hapana hatia, kupenda jamali
sioni hatia, pasiwe suali
mimi meridhia, yeye mekubali

 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 3D.
Hizi nyimbo za zamani wadada uzitumia sana kwenye kuboresha mahusiano yao ya kwenye ndoa, na wengine uzitumia kutongozea. ah ah ah ah ah!

Si unajuwa wakati mwingine kuna raha yake ukitongozwa na Mkeo au mume kumtongoza tena mke wake.

Leo mimi nina kazi moja tu: kuiba ujuzi.
 
Leo mimi nina kazi moja tu: kuiba ujuzi.

Wewe basi nakupatia hii


Alinidhani bandia ndani ya mikono yake
Akichoka nichezea anache nifedheheke
Nami sikufikiria kama nitarudi kwake
Sitarudi abadan ni kheri niangamie


Lakini leo karudi, kama jambo halikuwa
Na macho yake shahidi, kuja kuniangukia
Kaja niomba nirudi, mapenzi kuyachukua
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie ?

Na koja la asumini, kaniletea tamasha
Mapenzi ya utotoni, leo kaja yakumbusha
Yana mwenda mdomoni, ya furaha na bashasha
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie?

Zikapita samahani, nyoyo tukazisafisha
Vifundo vilivyo ndani, vyote tukaviondosha
Raha iliyoje jamani, mapenzi kuyarudisha
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie?

 
Last edited by a moderator:
Wataka tena zabiiibu , umekumbuka utamuuuuu ....halohalo hata kama umetubu kukupatena haramu........halooooooo nimeipenda hii
ABDALLA ISSA-LEO TENA



​

Nadhani nyimbo hii, ilikuja kujibiwa na Mkongwe wa Nyimbo za Taarab, mwenye asili ya kisomali Asha Abdow a.k.a Malika Ikienda kwa jina la "Uwi Tena."
 
Last edited by a moderator:
And this is special dedication to X-Paster



Wache waseme sina budi nawe,
si khofu lawama, sababu ya wewe
Ungekuwa nyoka, hadi uniume,
seuze tausi ,wache walalame

Ungekuwa nyoka, sumu yako dawa
Damu husafika, maradhi hupoa
Uzuri hakika, wewe umepewa
Siwezi kwepuka, liwe litokuwa

Nimefunga nia, katu sibadili,
Hapana hatia, kupenda jamali
sioni hatia, pasiwe suali
mimi meridhia, yeye mekubali
Alafu basi hizi nyimbo zote ninazo, wakati mwingine ushinda kutwa nikisikiliza.

Thanks for dedication.
 
Gaijin nimetafuta hii Insha'Allah Tutaonana ya Sabaha Salum, sijaipata. Ilikuwa hiwe ndio dedication yako
 
Gaga kuna hii unaweza kuipenda


Huna muamana, mtu wa tamaa
Nenda haja sina, tele wamejaa

Nimeshakujua mtu wa tamaa, huna muamana
Bora ulivyokataa, wala haja sina tena
Tele wamejaa, wasi wasi sina

Wema na fadhila, umenionyesha ahsante sana
sikusahau maisha, kwa vitendo si kwa jina
Unasikitisha, maarifa huna

Nilihadaika nikakudhania, mtu wa dhamana
dhamiri na yako nia, nimeifahamu sana
Maneno uno nambia, yote ukweli hayana
Bora shika njia, hatuto wezana

Mimi na wewe....
Huna muamana, mtu wa tamaa
Nenda haja sina, tele wamejaa

Kaa ukijua tamaa maradhi, vigumu kupona
Unajivunjia hadhi, ujuulikane kimwana
Nenda nimeridhi, wala sikununa

Bibi kwa heri...
Huna muamana, mtu wa tamaa
Nenda haja sina, tele wamejaa

 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 3D.
Wewe basi nakupatia hii


Alinidhani bandia ndani ya mikono yake
Akichoka nichezea anache nifedheheke
Nami sikufikiria kama nitarudi kwake
Sitarudi abadan ni kheri niangamie


Lakini leo karudi, kama jambo halikuwa
Na macho yake shahidi, kuja kuniangukia
Kaja niomba nirudi, mapenzi kuyachukua
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie ?

Na koja la asumini, kaniletea tamasha
Mapenzi ya utotoni, leo kaja yakumbusha
Yana mwenda mdomoni, ya furaha na bashasha
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie?

Zikapita samahani, nyoyo tukazisafisha
Vifundo vilivyo ndani, vyote tukaviondosha
Raha iliyoje jamani, mapenzi kuyarudisha
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie?

Aisee kila watu na fani zao (zenu). Thanks for the song. Ngoja niurudie-rudie leo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom