Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,304
Hii jee X-paster unaijua ya Bi fatma Binti Issa
(inasemwa aliimba kwa kuwa watu walimsema ana 'uso wa basi' na anakunywa pombe)
Haya maumbile yangu
Chuki binafsi na choyo, nyoyoni za wasumbua
Kutwa kazi yenu hiyo, zimewajaa shakawa
Kwangu yepi muonayo, mageni msoyajua?
Kufanya niyapendayo, kwenu kosa limekuwa.
Hilo haliwezikani, na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni, muache kunichungua
Msijitie shidani, haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani? Mie la kulaumiwa?
Nami ni mja mwenzenu, hata mkinichukia
Aibu yangu ndo yenu, kama mtafikiria
Kama baya kwenu nyie, kwangu nna ona sawa
Nawambia msikie, msio fahamikiwa
tena hadi msikie, kukaa kujizuzuwa
Lilobaki mniachie, sitaki kudhulumiwa
Wengi wamenihasimu, na thamani kunitoa
Mwapita kumwaga sumu, kila ovu kutupiwa
Bure mnanituhumu, ya fitina kuyagawa
Nami ni mwanadamu, si vyema kunibagua
(inasemwa aliimba kwa kuwa watu walimsema ana 'uso wa basi' na anakunywa pombe)
Haya maumbile yangu
Chuki binafsi na choyo, nyoyoni za wasumbua
Kutwa kazi yenu hiyo, zimewajaa shakawa
Kwangu yepi muonayo, mageni msoyajua?
Kufanya niyapendayo, kwenu kosa limekuwa.
Hilo haliwezikani, na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni, muache kunichungua
Msijitie shidani, haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani? Mie la kulaumiwa?
Nami ni mja mwenzenu, hata mkinichukia
Aibu yangu ndo yenu, kama mtafikiria
Kama baya kwenu nyie, kwangu nna ona sawa
Nawambia msikie, msio fahamikiwa
tena hadi msikie, kukaa kujizuzuwa
Lilobaki mniachie, sitaki kudhulumiwa
Wengi wamenihasimu, na thamani kunitoa
Mwapita kumwaga sumu, kila ovu kutupiwa
Bure mnanituhumu, ya fitina kuyagawa
Nami ni mwanadamu, si vyema kunibagua
Last edited by a moderator: