Wapi alipo Nurjehan aliyefaulu mtihani wa kitaifa na professor issa shivji 1960?

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
NURJEHAN ALIYEOONGOZA MITIHANI AKIWA NA PROF. SHIVJI MIAKA YA 1960s YU WAPI?

Jina la Nurjehan Walli limekuwa maarufu sana katika mitandao ya kijamii baada ya picha yake kuonekana akiwa na Issa Shivji wakati wawili hao walipoongoza mitihani adhimu ya Senior Cambridge Examinations (sasa Form Four) mwanzoni mwa miaka ya 1960s. Wakati huo Nurjehan alitokea Agha Khan Girls Secondary School (Zanaki Girls Secondary School) na Issa alitokea Khan Boy's Secondary School (sasa Tambaza High School).

Wapo watu waliomuuliza Askofu Mwamakula kutaka kujua aliko Nurjehan kwa sasa. Askofu ameamua kujibu swali kwa upana zaidi pasipo kuingilia maisha binafsi ya familia ya Walli. Prof. Issa Shivji sasa hivi ana umri miaka 77 na kwa demografia hiyo, tunaweza kukadiria kuwa Nurjehan atakuwa na umri wa miaka kati ya 76 hadi 78 kama bado atakuwa hai. Lakini kwa vyo vyote vile atakuwa hai kwa kuwa yeye anatoka katika jamii ya watu wanaoishi miaka mingi.

Utafiti wetu umebaini kuwa Nurjehan Walli ni majina ya watu wa jamii ya dhehebu la Ismailia. Sensa ya jamii ya Waismalia ya mwaka 1960 inatujulisha kuwa kulikuwa na familia ya Walli ambayo ilikuwa ikiishi Tanga. Hatuna uhakika kama familia hiyo ilikuwa na nasaba ye yote na Nurjehan Walli.

Waismalia ni madhehebu katika Uislamu lakini sehemu kubwa ya nasaba au jamii hizo asili yake ni nchi za Kiajemi (hasa Pakistan) na nchi jirani za Indonesia na Thailand. Majina hayo ya Walli ni maarufu sana katika nchi hizo. Hawa si Wahindi, ni Waajemi. Na kama wapo wanaoishi India ni kwa sababu ya ujirani tu. Dini yao au dhehebu lao kuu ni Ismailia na wengi kwa hapa Tanzania ni sehemu ya Uhalifa wa Agha Khan. Ikumbukwe kuwa Agha Khan sio taasisi ya Kihindi, bali ni taasisi ya Kiajemi au Ki-Urdu kutoka Pakistan.

Tofauti kubwa kati ya Waismalia na Wahindi ni dini kwani Wahindi ni Wahindu na Waismalia ni Waislamu. Tofauti nyingine ni kuwa Waismalia ni watu ambao wanaweka msisitizo sana kwa elimu (academic) wakati Wahindu msisitizo wao uko katika dini yao na biashara. Inafaa pia kukumbuka kuwa Agha Khan ni moja ya taasisi zinazoongoza duniani katika kutoa elimu bora.

Kama ilivyo familia ya Shivji, familia ya Walli pia ni miongoni mwa Waajemi ambao walifika katika nchi hii kabla hata haijaitwa Tanganyika na wakawa sehemu ya jamii ya Waasia. Ndio maana Issa alizaliwa Kilosa. Wakati Uhuru wa Tanganyika unapatikana, familia hizi zilikuwa ni sehemu ya raia wazawa wa Tanganyika huru.

Hata hivyo, wapo baadhi ya Waasia (Waajemi na Wahindi) walioondoka Tanganyika baada ya biashara na mali zao kutaifishwa pale Azimio la Arusha lilipozaliwa. Ndicho kipindi ambacho pia Shule mbili za Agha Khan zikataifishwa na kuitwa Zanaki na Tambaza. Tutaongelea wakati ujao juu y Shule za Wahindi zilizotaifishwa.

Familia ya Issa Shivji ni miongoni mwa familia zilizobaki nchini na kuwa sehemu ya mfumo wa kijamii, kielimu, kiuchumi na kisiasa na kwa sababu hiyo wameendelea kuheshimiwa sana katika nchi hii kama wazawa sawa na Wahehe, Wangoni, Wahaya, nk. Ukiwatenga Waajemi wa nchi hii itabidi uwatenge pia Wangoni, Wataita, Wamanyema, Wasukuma, Wahehe, nk kwani wote walihamia nchi hii katika miaka hiyo hiyo ya 1880s. Mwenyeji hasa wa nchi hii ni Mgogo asiyechanganyikana na Muhehe.

Wengi wa Waasia walioondoka hawakurudi Uajemi, bali walikwenda kuishi Uingereza na Canada. Ndugu zao wengi walibaki nchini na ni Watanzania halisi na uraia wao hauwezi hata kidogo kutiliwa shaka. Wakati nasoma Azania tulisoma nao wachache. Namkumbuka mtu mmoja tulikuwa naye Darasa moja pale Azania aliitwa Zulfika ila akahamia Mzizima Secondary School ambayo inamilikiwa na Agha Khan.

Je, Nurjehan Walli yuko wapi sasa? Hili ni swali ambalo nalirudisha kwa jamii au ikimpendeza, Prof. Issa Shivji anaweza kusaidia kujibu hili. Je, nini kimekushangaza? Je, nini moani yako?

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 19 Julai 2013; 18:26 pm.

Screenshot_20230722-085405.png
 
View attachment 2695849
Asante, leo ndio nimejua kumbe Prof. Shivji alisoma Tambaza!. Ndio Shule yangu!.
Tambaza imetoa vipanga kibao!.
Miaka yetu kuna kipanga akiitwa Mustafa Kudra, alipiga A 11!. Mwingine aliitwa Elhanan Elirehema Lema, huyu alipiga A 10!. Tambaza tulikuwa na A 7 kibao!, mimi mwenyewe nilikuwa na A's kadhaa, nikaenda Ilboru.
P
 
Miaka yetu kuna kipanga akiitwa Mustafa Kudra, alipiga A 11!. Mwingine aliitwa Elhanan Elirehema Lema, huyu alipiga A 10!. Tulikuwa na A 7 kibao!.
P
Hadi Mpwayungu Village nae eti product ya Tambaza yetu.
 
Asante, leo ndio nimejua kumbe Prof. Shivji alisoma Tambaza!. Ndio Shule yangu!.
Tambaza imetoa vipanga kibao!.
Miaka yetu kuna kipanga akiitwa Mustafa Kudra, alipiga A 11!. Mwingine aliitwa Elhanan Elirehema Lema, huyu alipiga A 10!. Tambaza tulikuwa na A 7 kibao!, mimi mwenyewe nilikuwa na A's kadhaa, nikaenda Ilboru.
P
Mitihani si wanatunga walimu wenu wenyewe hizo shule
 
Asante, leo ndio nimejua kumbe Prof. Shivji alisoma Tambaza!. Ndio Shule yangu!.
Tambaza imetoa vipanga kibao!.
Miaka yetu kuna kipanga akiitwa Mustafa Kudra, alipiga A 11!. Mwingine aliitwa Elhanan Elirehema Lema, huyu alipiga A 10!. Tambaza tulikuwa na A 7 kibao!, mimi mwenyewe nilikuwa na A's kadhaa, nikaenda Ilboru.
P
Hongera mkuu!

Na wewe ni Mzalendo halisi kama Profesa Issa Shivji?
 
Asante, leo ndio nimejua kumbe Prof. Shivji alisoma Tambaza!. Ndio Shule yangu!.
Tambaza imetoa vipanga kibao!.
Miaka yetu kuna kipanga akiitwa Mustafa Kudra, alipiga A 11!. Mwingine aliitwa Elhanan Elirehema Lema, huyu alipiga A 10!. Tambaza tulikuwa na A 7 kibao!, mimi mwenyewe nilikuwa na A's kadhaa, nikaenda Ilboru.
P

Kaka kumbe umepita Ilboru, jaman kusoma Ilboru na yale Majengo, na baridi ni hatari.

Ilboru ya zaman ilikuwa vipanga kweli kweli, hongera Kaka.
 
Back
Top Bottom