DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,094
- 1,691
- Haina uhalisia
- Kauli yake itawafanya watu wengi waogope mazoezi
- Hatuna vituo vya kutosha vya kufanya uchunguzi kama huo
- Ni gharama kufanya chunguzi
- Watu wangapi umewasikia wakifa kwa sababu ya kufanya mazoezi?
- Madhara yake hutokea kwa nadra sana.
Kumekuwa na elimu nyingi zinazotolewa na daktari anayeitwa Prof. Janabi, ambazo zinasaidia jamii. Bahati mbaya baadhi ya mafunzo yake, ambayo yanaaminika sana na jamii huwa na makosa ya kitabibu.
Watu wengi wamesikiliza clip yake ya mwaka jana inayowashauri watanzania kwamba wanapaswa kuonana na daktari wao kuchunguza afya za mioyo yao kabla ya kuanza mazoezi yoyote. Clip hii ya mwaka jana, ime trend sana baada ya Manager wa TANROAD Mkoa wa Ruvuma kufariki wakati akifanya mazoezi.
Ni muhimu kutambua kwamba madaktari huwa hawajui kila kitu, hivyo kwa Wizara ya Afya na Janabi mwenyewe, ni vyema akawa anatoa masomo kwa maeneo aliyobobea nayo, kwani akikosea kufundisha vitu ambavyo hana ujuvi navyo, bado jamii itamuamini maana haijui kitu.
Ni kweli kwamba mwongozo wa kila mtu kufanyiwa uchunguzi wa moyo au afya na daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi, ulikuwapo miaka hadi miaka ya karibuni ulipobadilishwa hasa kwa watu ambao wanajitambua kuwa na afya njema sawasawa na maelezo yangu hapo chini. Andiko hili halimaanishi kuwa uchunguzi wa moyo kabla ya kuanza programu ya mazoezi sio muhimu kwa watu wote, lakini thread hii inasema sio muhimu kwa watu wengi.
Kwa nini watu wanapaswa kuchunguzwa moyo kabla ya kuanza programu ya mazoezi?
Mapendekezo ya kimapokeo katika jumuiya ya afya yalikuwa kwamba kila mtu anapaswa kuchunguzwa na daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi. Hii ilikuwa inaongozwa na nadharia, kwamba unapoanza kufanya mazoezi ya wastani au mazito, kuna hatari kidogo ya kuongezeka kwa mashambulizi ya moyo au matatizo ya moyo.
Kwa hivyo uchunguzi wa moyo ungekuwa kuhakikisha kuwa mtu hana ugonjwa wa moyo ambao labda hajui - au kwamba hafanyi matibabu ya ugonjwa wa moyo alionao kwa sababu hana dalili zozote za kumtisha kwa kuwa hafanyi mazoezi, lakini dalili zitajitokeza au kuongezeka mara tu atakapoanza kufanya mazoezi.
Lakini miongozo hii ya huko nyuma imebadilika sana. Imegundulika kwamba kupendekeza kila mtu afanyiwe kwanza uchunguzi wa daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi kunaweza kunatengeneza vikwazo vinavyowazuia watu wengi kufanya mazoezi.
Hivyo nchi nyingi tunakonakili miongozo yao mfano kutoka American College of Sports Medicine wamerekebisha miongozo yao kuakisi hili. Lengo ni kuhakikisha kunakuwa na usalama wa mgonjwa na kutotengeneza kikwazo chochote cha kufanya mazoezi.
Je, nani anapaswa kuchunguzwa moyo kabla ya kuanza mazoezi?
Kwa miongozo ya sasa ni kwamba unapaswa ujiulize maswali matatu ya msingi kabla ya kuanza kufanya mazoezi.
Swali la kwanza: je, wewe kwa kawaida ni mtu wa kukaa tu (physically inactive)? Ikiwa inaamamisha shughuli zako za kila siku zinahusisha kukaa tu, unaweza kutaka kuonana na daktari kabla ya kuanza programu ya mazoezi ya kawaida wastani (si madogo).
Swali linalofuata: Una dalili za matatizo ya moyo? Au una matatizo mengine ya kiafya ambayo yanaweza kukufanya uwe na matatizo ya moyo? Kwa mfano, shinikizo la damu, ugonjwa wa figo, ugonjwa wa kisukari, na ugonjwa wa mapafu ni hali zote ambazo zinaweza kukuweka kwenye matatizo ya moyo.
Swali la mwisho: ni shughuli gani unataka kushiriki? Je, ni za nguvu kubwa, kama kukimbia? Ikiwa mpango wako wa mazoezi unahusisha mazito, unaweza kuonana na daktari kwanza, hususani kama umekuwa mtu wa kukaakaa tu.
Ukijibu "ndiyo" kwa mojawapo ya maswali hayo juu, kwa hakika unapaswa kupima moyo kwanza kwani unaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata tatizo la moyo wakati wa mazoezi.
Watu wanapaswa kujua nini kuhusu hatari ya mshtuko wa moyo au masuala mengine ya moyo wakati wa mazoezi?
Uwezekano wa kuwa na mshtuko wa moyo au tatizo la moyo wakati wa mazoezi ni mdogo sana. Hata tukio la juzi la Songea, ni kati ya matukio machache ya kuhesabika.
Hivyo inashauriwa, unapaswa kuanza mazoezi madogomadogo na polepole kila wakati. Usianze ghafla mazoezi makubwa, kama kukimbia umbali, mrefu kwa muda, na kadhalika. Kwa wale wenye uwezo wanaweza mtafuta mkufunzi kama mfiziotherapia anayeweza kusimamia programu zao za mazoezi anayeweza kukusaidia kujenga nyongeza za kiwango cha mazoezi kwa usahihi.
Ikiwa huna dalili au dalili za matatizo yoyote, lakini bado huna uhakika kuhusu afya ya moyo wako, nenda kituo cha afya umwone daktari. Yeye anaweza kukusaidia kujua kama unaweza kufaidika na upimaji wowote unaohusiana na magonjwa ya moyo kabla ya kuanza programu yako ya mazoezi.