Wapangaji nyumba za NHC Kariakoo walalamika notisi za kuhama bila mazungumzo, wadai NHC wamempa dili mwekezaji mpya kimyakimya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baadhi ya Wafanyabiashara na wakazi waliopanga kwenye majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation - NHC) mitaa ya Kariakoo wamelalamika kupewa ‘notisi’ ya miezi itatu wakitakiwa kuhama kwenye majengo hayo pasipokuwa na mazungumzo yoyote.

Wafanyabiashara hao waliopo kwene mitaa ya Kariakoo Kariakoo Jijini Dar es Salaam wamedai kuwa baada ya kusikia taarifa za kuwa wanatakiwa kuhama ili mwekezaji anayetambulika kwa jina la Baltazar aweze kuingia.

Wanasema baada ya kupatatetesi hizo walienda kwenye ofisi za NHC Ilala ambazo ndipo wanapofikisha malalamiko yao siku zote wanapokuwa na changamoto kuhusu majengo hayo.

Snapinsta.app_352828493_228235446636096_2798882471863222556_n_1080.jpg

Wanasema baada ya kushikia kwa mara ya pili kuhusu mwekezaji ambaye anataka kuwahamisha wapangaji wa maduku na wakazi wa kwenye Jengo namba 13/14H, walirejea Ofisi za NHC kupata ufafanuzi, wakajulishwa kwa mara nyingine kuwa hakuna mpango kama huo.

“Meneja wa HNC Ilala alituamba kuwa huyo Murtaza Hussein anayejiita mwekezaji ni tapeli tu na wao hawana mpango wa kuwekeza kama inavyoelezwa,” anasema mmoja wa wapangaji katika majeng hayo ya NHC, Kariakoo.

Inaelezwa kwa Juni 4, 2023 walifikishiwa taarifa rasmi ‘notice’ kuwa wanatakiwa kuondoka kwenye majengi hayo na kuwa barua zilieleza kuwa muda waliopewa unaanza Juni 2, 2023.

NHC11.jpg

Akaunti namba ya NMB inayodaiwa kuwa ni ya mwekezaji mpya aliyepewa dili na NHC kimyakimya, inadaiwa kuwa akaunti hii ndio inayotumika kufanya malipo kwa wapangaji wapya licha ya NHC kudai kuwa hawajapata mwekezaji mpya mpya.

Mpangaji mwingine ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake akaeleza kuwa “Awali walikuja kwenye jengo letu, aadaye wakatoa notisi kwenye majengo mengine, jumla ya waathirika kwa pande zote mbili ni zaidi ya watu 1000.

“Kilichokuwa kinashangaza ni kuwa hata tulipotoa taarifa kuhusu huyo mwekezaji Baltazar ambaye tiliambiwa ameshapokea hela za wapangaji wapya, hakukuw ana hatua zozote zilizochukuliwa na NHC.

“Tulivyopata barua zaidi ya watu 800 tulienda makao makuu ya NHC, wakasema tuunde timu ya watu 10, 10 watoke kwetu na 10 watoke kwao kwa ajili ya kufuatilia suala hilo.

“Kinachotushangaza hawatoa majibu ya kueleweka, wanakiri kuwa barua tulizopata ni za NHC, lakini tukiwauliza kuhusu mwekezaji wanadai hawajapata mwekezaji mpaka sasa.

risiti.jpg

Risiti za anayedaiwa anakusanya pesa kwa ajili ya kupangisha wapangaji wapya.

“Sasa mbona hawakutupa taarifa mapema? Huyo Baltazar tunasemkia taarifa zake hawamchukulii hatua? Wanasema hawajapata mwekezaji sasa kwa nini watuambie tuhame?

“Mpaka sasa hatujui kinachoendelea, kuna watu pale ndio makazi yao watahama ghafla hivyo waende wapi? Nani anayekuja kuwekeza kwa siri kiasi hicho?”

Pia soma: Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji


============

TAARIFA BAADA YA KIKAO CHA WAATHIRIKA WANAOTAKIWA KUHAMA, LEO JUNI 14, 2023
1. Muda tuliopewa sio rafiki hivyo tuongezewe muda
2. Baada ya ujenzi kukamilika tuhakikishiwe nafasi zetu

Kwenye hizo pointi zetu mbili kuu kutakuwa na sababu zake

ambazo tayari tunazo
3. Pia tumekubaliana kuchangisha fedha kwa sababu kuna gharama zitatumika kwenye kupambania haki yetu hivyo tumeamua michango itakusanywa na viongozi wa majengo waliochaguliwa katika kikao

4.Tumekubaliana gharama kwa kuanzia iwe kiasi cha shillingi elfu ishirini tu. 20000/= kwa kuanzia

14/16 TANDAMTI NA CONGO SAMEER
3/16 TANDAMTI NA CONGO ALLY
22/31 NARUNG’OMBE/SWAHILI -RASHID
23/31 TANDAMTI /SWAHILI SHAFIQ
12/16 TANDAMTI/NYAMWEZI NASSIR
13/16 NARUNG’OMBE/ NYAMWEZI- BENJAMIN
11/16 TANDAMTI /NYAMWEZI KARIM
13/14 MSIMBAZI/MKUNGUNI PRIVA
1/19 UHURU/CONGO ESTER
13/6 UHURU STREET MOHD HASSAN
14/6 UHURU/MSIMBAZI MBARAKA
13/19 UHURU - EDMOND
9/28 UHURU -ABDUL

Pia wenye ownership wamkabidhi copy za ownership anaepokea mchango kwenye jengo lako
Pia wenye construction wapeleke copy kwa anaepokea michango

Cha muhimu zaidi ni kwamba jumanne ya tarehe 13/06/2023 tufike makao makuu ya shirika la nyumba yaliyopo Kambarage House karibu na Aghakhan Hospital saa 7 kamili mchana tuwe pale bila kukosa tafadhali. Viongozi wahimize watu wa majengo yao wafike kwenye kikao.

NHC WATOA UFAFANUZI
Akifafanua madai hayo, Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Muungano Saguya anasema: Huko nyuma tuliboresha sera yetu ya ubia, Novemba 2022 ikizinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, lengo likiwa ni kuishirikisha Sekta inafsi katika kuboresha majengo mbalimbli yanayomilikiwa na NHC.

Hiyo haikuwa mara ya kwanza kufanya maboresho ya sera ilitokea 2006, 2008, 2016, ambapo bado kulionekana kuna maboresho ikiwemo mtu kukopea mikopo kwa majengo ya Shirika, kwenye umiliki pia kulionekana kuna changamoto.

Katika sera hii mpya kumekuja maboresho kadhaa mapya, NHC ikatangaza na kuboresha mchakato wa upangaji.

Kuna maombi mapya yakafanyika, walioomba mikataba yao ikapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hicho ndicho kinachoendelea kwa sasa.

Kuhusu notisi ni kweli tumewapa na tumewapa miezi mitatu, baadaye wabia watakaopatikana na kuweza kuingia.

Tumekutana nao jana (Juni 13, 2023), hata wao wamekubal kuwa mabadiliko lazima yafanyike kutokana na uhalisia, shida yao kubwa ni muda ambao wamepewa kuwa ni mfupi sana.

Hilo linazungumzika, kama ikibidi tunaweza kuongeza muda, wiki hii tutakutana na tutatoa taarifa kuhusu hilo.

Kuna wanaoweza kuwa na changamoto ya kuhama ndani ya muda huo wa miezi mitatu, wanaweza kuwasilisha maombi yao na kupewa ongezeko la muda.

Kuhusu madai kuwa kuna watu wamepewa majengo hayo kwa ajili ya kupangisha, hao ni wahuni na hakuna kitu kama hicho, wanapita wanakusanya hela Tsh. Milioni 2 hadi 12, tumeona risiti zikisambaa.

Tutashirikiana na vyombo vya Dola kuwatafuta wahuni wa aina hiyo, watu wasikubali kutoa hela, hakuna mwenye uhakika wa kupewa huo ubia, wanachukua hela za wapangaji.

Tumeona kuna madai ya kuwa kuna Mhindi amepewa nafsi hiyo ya kuwa mwekezaji, huo ni uongo, hakuna kitu kama hicho.

Pia, soma; Taarifa kwa umma kutoka NHC kuhusu utekelezaji wa sera ya ubia, Wapangaji walipewa Notisi ya siku 90
 
Baadhi ya Wafanyabiashara na wakazi waliopanga kwenye majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation - NHC) mitaa ya Kariakoo wamelalamika kupewa ‘notisi’ ya miezi itatu wakitakiwa kuhama kwenye majengo hayo pasipokuwa na mazungumzo yoyote.
watu pale ndio makazi yao watahama ghafla hivyo waende wapi? Nani anayekuja kuwekeza kwa siri kiasi hicho?”
Wekeni lawyer hodari mwaminifu !!
 
Hii nchi ukishakuwa na watu kwenye system na ukawa unajua namna ya ku-force baadhi ya mambo basi wewe umeshatoboa.

Huyo Balthazar ana watu huko huko NHC na sector zote na kwa sababu hao anaowatumia wanajua awamu hii hakuna mwenye meno ya kuwang'ata wanaacha mambo yawe yalivyo hao wapangaji watalalamika wee mwisho wataelewa.
 
Hii nchi ukishakuwa na watu kwenye system na ukawa unajua namna ya ku-force baadhi ya mambo basi wewe umeshatoboa.

Huyo Balthazar ana watu huko huko NHC na sector zote na kwa sababu hao anaowatumia wanajua awamu hii hakuna mwenye meno ya kuwang'ata wanaacha mambo yawe yalivyo hao wapangaji watalalamika wee mwisho wataelewa.
Uonevu tu !!
 
Baadhi ya Wafanyabiashara na wakazi waliopanga kwenye majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation - NHC) mitaa ya Kariakoo wamelalamika kupewa ‘notisi’ ya miezi itatu wakitakiwa kuhama kwenye majengo hayo pasipokuwa na mazungumzo yoyote.
Wekeni Wakili mzuri aende Mahakamani akaisimamishe hiyo notice kwanza. !!
 
Back
Top Bottom