NHC toa semina kwa wapangaji wako

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,502
19,312
kuna watu wameishi NHC miaka zaidi ya 50, wanalipa kodi ndogo na hela wanazopata wanakula, hawajengi. ukitaka kuwaondoa wanasema twende wapi? mnatuonea rais tusaidie, mara mimi nimeishi miaka yote hapa mnataka niende wapi? tunahitaji NHC itoe semina kwa wapangaji wote kama ifuatavyo:

1. wapangaji wajue NHC ni shirika la serikali, zile nyumba zote ni za serikali, maana yake ni nyumba za watanzania wote hata wale ambao hawajawahi kupanga.

2. NHC iwaambie shirika lipo pale kufanya biashara, sio kutoa msaada, na wana uhuru kuendeleza.

3. wapangaji wakipata nafasi, wajue kuna siku watatakiwa kuondoka, hivyo wajiandae hapo sio kwao

4. ni haki ya NHC kufanya maendelezo na kupangisha mtu wanayemtaka. watu wasumbufu kama hao sisi watanzania hatutaki kuendelea kuwapangisha, hizo sio nyumba za msaada ambazo watu hata wakifa wanarithiana, ni nyumba zetu sisi walipa kodi.

5. sio wao tu ndio wenye haki kukaa humo, watanzania wengi sana huwa wanapenda kuishi kwenye hizo nyumba kwasababu ni za bei ya chini, ila hawapati nafasi kwasababu hao wanaoishi humo wakitaka kuhama huwa wanawauzia watu nafasi kwa pesa ndefu sana. biashara ndani ya biashara.

6. watu wanaokaa humo wanapohama, wanapofariki n.k, NHC waache kuchukua rushwa ili kumpa mwingine, inakuwaje mtu amekaa miaka 60, manake amerithishwa na hana mawazo ya kuhama, hapo ni kwake, sio pa NHC.

NB: kuna siku naamini serikali itaamua kufanya jambo kwenye hizi nyumba. watu wasipange zaidi ya miaka 10, kwasababu zinalemaza sana. wakati sisi wengine tunajinyima kula tujenge, wengine wanakula bata wakitegemea kuishi kwenye nyumba zetu kwa bei nafuu bila kuhamishwa tukitaka kufanya maendelezo. NHC NI NYUMBA ZETU WATZ, NHC NI NYUMBA ZETU WATZ, NHC NI NYUMBA ZETU WATZ kwasababu hilo ni shirika la serikali na serikali ndio sisi, hao wanaozuia maendelezo sio tu wanalihudumu taifa, wanatuhujumu wananchi wengine ambao tuna umiliki wa kitaifa kwenye hizo nyumba.
 
shida ya NHC ni rushwa. kupata tu nyumba mle hata kama unajua mpangaji husika anahamia mkoa mwingine, hela lazima itembee.
 
kuna mwaka jamaa alikuwa anahama, nikaomba niende NHC nimbadili, alinitajia milioni mbili, na bado ya kumpa mtu wa nhc. niliamua kununua kiwanja na kujenga ya kwangu. ajabu yake kwenye ile clip kariakoo, kuna watu wanajigamba kwamba wamekaa mle miaka 60 na wakitolewa pale wataenda wapi? yaani akili zimebaki mgando hadi hawajui kuwa NHC ni landlord tu, wanaweza kuachana naye wakapanga nyumba kwa landlord mwingine. 60 years amenyima haki ya watanzania wengine kukaa mle na bado anaona anaonewa na ana haki.
 
Shirika Hilo liuze hisa... serikali ipunguze umiliki..liende DSE...
nakuhakikishia, likifanya hivyo linaweza kuwa na maendeleo makubwa sana. kwa sasa ni shamba la bibi, ila wananchi wengi wakiwa na hisa, umakini na ubiasharabiashara utaongezeka, litakuwa shirika kubwa sana. kwa lilivyo sasaivi ni kama shirika la msaada au shamba la bibi la kupigia pesa. ndio maana mpangaji hadi anasimama anasema nimekaa miaka 60, mkiniondoa hapa mnataka niende wapi? seriously
 
Hizo ziwe zinapangishwa baada ya mda fulani mtu inakuwa yake
ikiwa hivyo nayo sio mbaya, si anakuwa ameilipia ili ile hela nyingine ikajengee watu wengine nao wapange iwe ya kwao? unachotakiwa kujua ni kwamba, hizo nyumba au hilo shirika ni mali ya WAtanzania wote, hivyo hata kuiuza au kuipangisha watanzania wote wanatakiwa wapewe haki, haiwezekani kitu cha kwetu wote afu kuna mtu amekaa pale 60 years kama yule mama anayesema anaonekwa kuhamishwa. kwasasa NHC hawajaamua kuziuza, hivyo waanapangisha, na wakitaka kufanya maendelezo wanafanya kwa uhuru manake ni mali na wamewapa miezi 3. huyo mama anasema hawezi kuhama kwani ataenda wapi? au uwa anakaa bure?
 
Hizo ziwe zinapangishwa baada ya mda fulani mtu inakuwa yake
Kwamba Watanzania wanalipa Kodi, inajengwa nyumba..halafu unapangishwa wewe kwa bei dezo maana shirika tunaliruzuku...ila bado unataka ukikaa kwa muda (?) Upewe iwe yako.

Sio lift tu tukupe, ila na machungwa tununue ule, stori tukupigie, ukilala tukuimbie na honi upige wewe... Ungekuwa karibu ungeita mvua.. haiwezekani ukawaza hivyo
 
ikiwa hivyo nayo sio mbaya, si anakuwa ameilipia ili ile hela nyingine ikajengee watu wengine nao wapange iwe ya kwao? unachotakiwa kujua ni kwamba, hizo nyumba au hilo shirika ni mali ya WAtanzania wote, hivyo hata kuiuza au kuipangisha watanzania wote wanatakiwa wapewe haki, haiwezekani kitu cha kwetu wote afu kuna mtu amekaa pale 60 years kama yule mama anayesema anaonekwa kuhamishwa. kwasasa NHC hawajaamua kuziuza, hivyo waanapangisha, na wakitaka kufanya maendelezo wanafanya kwa uhuru manake ni mali na wamewapa miezi 3. huyo mama anasema hawezi kuhama kwani ataenda wapi? au uwa anakaa bure?
Kama sijasikia vibaya yule mama kasema ana 60yrs sio kaishi hapo kwa miaka 60
Pia kwa kuwa ni shirika la taifa mwananchi kulipia kwa 20 30 yrs na kufanya iwe yake itakuwa imemuwezesha kuliko kutoka mkataba ukiisha hana pesa akatafute sehemu nyingine
 
Kama sijasikia vibaya yule mama kasema ana 60yrs sio kaishi hapo kwa miaka 60
Pia kwa kuwa ni shirika la taifa mwananchi kulipia kwa 20 30 yrs na kufanya iwe yake itakuwa imemuwezesha kuliko kutoka mkataba ukiisha hana pesa akatafute sehemu nyingine
ili iwe hivyo, inatakiwa hiyo fursa wapewe watanzania wote, sio wapewe baadhi tu ambao wameshapata hata bahati ya kuishi humo. sisi wengine kila mkoa tunaoenda tunapanga (pamoja na kwamba tunakotoka tuna nyumba zetu), unapanga kwa laki tatu hadi laki nne kwa mwezi, wengine kwenye shirika la kwetu sote wanapanga kwa laki au laki na nusu, anakaa miaka zaidi ya kumi na unataka huyohuyo aliyefaidika zaidi apewe kipaumbele kwenye mali ya kwetu sote. NHC ijenge nyumba, itangaze kwenye kadamnasi, watu wafanye applications, wanunue basi, au hata hizo walizopangisha watu wakitaka kuziuza watangaze na sio lazima yule aliyewahi kupata bahati ya kuishi humo ndio ajione ni mtoto sana wa Tanzania kuinunua kuliko wengine ambao hawajawahi hata kupata access kwenye mali ya kwetu wote.
 
Back
Top Bottom