Wadeni Sugu wa NHC kutangazwa katika Vyombo vya Habari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
1692106131948.png

Kutokana na kusuasua kulipwa kwa madeni linalowadai wateja wake, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekuja na kampeni iliyobeba mambo nane katika kuhakikisha inakusanya madeni hayo ikiwemo kuwatangaza katika vyombo vya habari.

Mpaka sasa shirika hilo linawadai wapangaji wake Sh23 bilioni fedha ambazo imeelezwa kama wangezipata zingeweza kufanyia shughuli mbalimbali za shirika ikiwemo ujenzi wa nyumba.

Akizungumza leo Jumanne Agosti 15, 2023 kuhusu kampeni hiyo iliyobeba kaulimbiu ya ' Lipa madeni yako kwa maendeleo ya Shirika na Taifa Letu', Meneja Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya amesema hatua hii ni baada ya kuelekea kuisha kwa miezi mitatu aliyoitoa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha bunge Julai 2023 ambapo aliagiza wadaiwa wote wawe wamelipa madeni yao ndani ya miezi mitatu.

“Wadaiwa sugu watakaokaidi maelekezo ya shirika watakuwa wameruhusu shirika kuwatangaza katika vyombo vya habari ili mashirika na kampuni nyingine yasiingie kwenye makubaliano ya kibiashara na mtu au kampuni inayodaiwa,”amesema.

Ameongeza kuwa ili kuweza kukusanya madeni katika kampeni hiyo shirika limemua kufanya mambo nane ikiwemo kuundwa kwa menejimenti ambayo itaanza kazi rasmi wiki hii ya kufuatilia madeni hayo.

Saguya amesema pia, shirika limeingia mkataba na wapangaji ya kuwaruhusu kulipa madeni yao kwa awamu.

"Kila mpangaji atapaswa kulipa deni lake kulingana na mkataba tulivyokubaliana na kama ana sababu maalum ahakikishe anaweka utaratibu madhubuti wa kulipa madeni yake anayodaiwa,"amesema Saguya.

Aidha amesema kwa wapangaji waliopo kwenye nyumba ambao watashindwa kulipa kodi na malimbikizo ya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa, atakuwa ameonyesha kuwa haitaji nyumba anayopanga na shirika litavunja mikataba yao ya upangaji na kuwaondoa kwenye nyumba kwa mujibu wa sheria.

Wakati kwa wale wapangaji wapya hakuna atajayeweza kupangishwa bila kulipa amana ya pango ya miezi mitatu na kubainisha kuwa hii itasaidia shirika kuzitumia amana hizo pale wanapoacha madeni na kuondoja kwenye nyumba.

"Lakini kwa wapangaji waliopo kwenye nyumba na ambao hawajakamilisha kulipa amana hiyo,wanatakiwa wawe wamelipa hadi ifikapo Desemba 31,2023,vinginevyo shirika litalazimika kusitisha mikataba yao ya upangaji,"amesema Saguya.

Vilevile shirika hilo limeanzisha makubuliano na taasisi inayotunza kumbukumbu za wadaiwa sugu katika taasisi mbalimbali (Credit Info Bureau) ili kupeleka majina ya wadaiwa sugu hao wasiweze tena kupata mikopo kwenye taasisi zingine za kifedha.

Ili kuepusha madeni ya mara kwa mara Meneja huyo amesema kuanzia sasa shirika halitampa mkataba mpya mpangaji ambaye anakuwa na rekodi mbaya ya kutolipa kodi kwa wakati.

"Hatua hii ya kutowapa mikataba mipya wapngaji wetu, imezingatia pia maoni ya wadau ambao walitaka wasiolipa kodi kuwapisha wenye uwezo wa kulipa kwani ukweli ni kwamba Watanzania wengi wamekuwa wakiomba upangaji katika nyumba zetu,"amesema Saguya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa msimamizi wa Miliki NHC, Elias Msese, amesema kampeni ya ukusanyaji madeni haya utafanyika ndani ya mwezi mmoja kuanzi sasa na kwa wale watakaokaidi maelekezo ya shirika watakuwa wamewaruhusu kuwatangaza kwenye vyombo vya habari.

MWANANCHI
 
Wakuu,naomba msaada wenu pia
Hiv nawezaje kupata apartment kweny hiz nyumba za NHC??na bei zake zikoje roughly?
 
Back
Top Bottom