Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Wafanyabiashara wa maduka kutoka soko la Kariakoo wamefika makao makuu na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupinga notice walizopewa na shirika hilo kwa kuwataka kuhama ndani ya siku 90 kupisha mwekezaji mpya katika eneo hilo.
Wafanyabiashara hao wamesema, wao hawapingi maendeleo lakini muda uliotolewa na NHC ni mfupi sana na wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata hilo ili waweze kupata haki yao kwani muda waliopewa ni mfupi sana kwa wao kuhama kutokana wao kuwa na madeni na mikopo.
====
NOTISI YA SIKU TISINI (90) YA KUSITISHA MKATABA WA UPANGAJI WA NYUMBA NA 005 KWENYE KIWANJA NA 23 KITALU NA 31 MTAA WA TANDAMTI NA SWAHILI
Tafadhali husika na somo hapo juu;
Unafahamishwa kuwa Shirika la Nyumba la Taifa limeanza rasmi utekelezaji wa Sera va Ubia na wawekezaji binafsi na taasisi mbalimbali ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi Novemba 2022.
Hivyo basi Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango wa kuanza ujenzi kwenye Kiwanja tajwa hapo juu ambapo wewe ni mpangaji, hivyo tunakutaarifu kwamba unapewa NOTISI ya siku tisini (90) kuanzia tarche 02/06/2023 mpaka tarehe 31/08/2023 kusitisha mkataba baina yako na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye nyumba tajwa hapo juu.
Shirika limerejea kipengele namba 4.1 (c). (d) na 7.2 cha Mkataba wa Upangaji kinachompa mamlaka mpangishaji kuvunja mkataba ndani ya siku tisini (90) pale anapohitaji jengo lake kwa ajili ya matumizi mengine.
Kwa maelezo hayo, unapewa NOTISI ya siku tisini (90) ya kutakiwa kuhama katika nyumba unavoishi ili kupisha uendelezaji unaokusudiwa kufanyika katika kiwanja hicho.
Unaruhusiwa kuomba upangaji upya baada ya jengo jipya kukamilika kulingana na masharti ya kipindi hicho.
Pia soma: Wapangaji nyumba za NHC Kariakoo walalamika notisi za kuhama bila mazungumzo, wadai NHC wamempa dili mwekezaji mpya kimyakimya