Wapangaji NHC wapewa siku 90 kulipa bilioni 9/-.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapangaji NHC wapewa siku 90 kulipa bilioni 9/-..............

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Dec 1, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Wapangaji NHC wapewa siku 90 kulipa bilioni 9/-


  na Marietha Mkoka


  [​IMG] SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), linadai sh bilioni 9 kutoka kwa wapangaji wake na limetoa siku 90 kwa wadaiwa hao sugu wawe wameshalipa, vinginevyo watatimuliwa. Kati ya madeni hayo, wapangaji wa NHC mkoa wa Dar es salaam ambao baadhi yao ni watumishi wa umma na wafanyabiashara wazito, wanadaiwa sh bilioni saba.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Mkurugezi wa Matawi na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema fedha hizo lazima zipatikane ili shirika liweze kujiendesha na kuimarisha mipango yake ya maendeleo iliyojiwekea kuanzia mwakani.
  “Tunawapa miezi mitatu kuhakikisha wanalipa madeni ya shirika, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo kuwaondoa ili shirika lipangishe wapangaji wengine,” alisema Mndolwa.
  Kwa mujibu wa Mndolwa, NHC linahitaji kufanya ujenzi wa nyumba zingine 15,000 ndani ya miaka mitano ijayo na madeni ya fedha wanazodaiwa wapangaji wa shirika hilo ni sehemu ya mapato ya kukamilisha mradi huo.
  Alisema kuanzia Januari 2011, wapangaji wote wa NHC, wanatakiwa kulipa kodi za pango kupitia taasisi za kibenki zitakazopendekezwa na shirika hilo ili kupunguza usumbufu wa foleni wa ulipaji wa kodi kwa baadhi ya vituo vyao.  [​IMG]
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  uongozi wa NHC umeamua jambo zuri,kwani kwa kufanya hivyo shirika litaweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini!!hii ni hatua nzuri sana!!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tehe jamaa wanalipa Kodi kiduchu sana hawa nashangaa wanadaiwa walipeeeeeeee tu
   
 4. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wakimaliza hilo zoezi waanze kufuatilia nyumba zao ambazo hazimo kwenye database yao huku wadosi wakiwa wamezitaifisha....
   
 5. N

  Newvision JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mndolwa naye mnafiki siku zote alikuwa wapi?? lakini na nyie wapangaji mnaishije bila kulipa pango uliona wapi lipeni bwana. Nyie zenu mlizopangisha mbona mnawatoa wapangaji wasipolipa? Kodi zetu zimejenga nyumba hizo nyie mwakaa bure wapi na wapi lipeni tu
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi TANESCO walishamaliza kukusanya madeni?
   
 7. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  NHC NI SHIRIKA KUBWA SANA HEBU NENDENI NA WAKATI.I AM SURE ILE FOLENI PALE KWENYE MALIPO NI SABABU MOJAWAPO...ITS TOO INCONVINIENT AND BORING!!! KWA MFANO MIMI MARA NYINGI HUWA NASEMA NITAENDA LIPA KESHO MPAKA MWEZI MWINGINE UNAISHA......KWA NINI MSIBORESHE SYSTEM YENU YA MALIPO ILI IWE RAHISI KULIPA ,SAY, THROUGH MOBILE SERVICES eg MPESA,TIGOPESA etc???
   
 8. m

  mams JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tangazeni nyumba ambazo wameshindwa kuzilipia wenye nia ya kulipa tuingie.
   
 9. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  NHC boresheni system yenu ya kulipia na ndani ya hizo siku 90 deni liwe limekamilika..mifumo ya malipo yenye kujali muda,convinience inapatikana kirahisii kwa sasa.
   
 10. M

  MJM JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Newvision kwa ukosoaji! Huyu kaanza kazi juzi juzi tu kutoka DAWASCOOOOOO. Aliwahi kufukuzwa Barclays kwa deal za mikopo ya kishikaji. Ila ndiyo safu mpya ya Nehemiah baada ya kupangua Wakurugenzi karibu wote wa NHC
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nyingi ni za hao wadosi unaowasema walitaifishwa kipindi cha utaifishaji na kuna baadhi zimerejeshwa kwa wenyewe kwahiyo hakuna jipya kama haimo kwenye data base ujue sio yao.
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  huu uongozi ni wapuuzi wote kwanza mlikuwa wapi siku zote kulimbikiza BILION???STUPID..YAANI SIKU WANATANGAZA WAZIRI MHUSIKA UNGEFUKUZA TOP WOTE WANAOHUSIKA NA KULIMBIKIZA HAYA MALIPO HATA KAMA MTOTO WA MJOMBA SHANGAZI NA KUWEKA WAPYA..
   
 13. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu nadhani hujui vizuri historia ya msajili wa majumba NHC ilianzishwa lini na ina miliki nyumba zipi. Kwa kifupi kuna nyumba nyingi nyingi sana hazijajengwa na kodi wala na hao NHC bali zilitaifishwa enzi zile za uhujumu uchumi nyumba hizo nyingi zipo mitaa ya upanga na posta na baadhi zipo mtaa wa nkurumah na uhuru. NHC hawajawa na vision ya kuongeza makazi ya bei nafuu kwa mtaji wa nyumba za dhulma wangeweza kurahisisha maisha ya watanzania wengi kwa kujenga nyumba nyingine matokeo yake sasa hivi wanaingia ubia na matajiri wanabomoa za zamani wanajenga mpya na kuzipangisha kwa bei ya kuruka! Hakuna jipya hapa ni madudu tu mengine!
   
Loading...