Wapangaji NHC wapewa siku 90 kulipa bilioni 9/-..............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Wapangaji NHC wapewa siku 90 kulipa bilioni 9/-


na Marietha Mkoka


amka2.gif
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), linadai sh bilioni 9 kutoka kwa wapangaji wake na limetoa siku 90 kwa wadaiwa hao sugu wawe wameshalipa, vinginevyo watatimuliwa. Kati ya madeni hayo, wapangaji wa NHC mkoa wa Dar es salaam ambao baadhi yao ni watumishi wa umma na wafanyabiashara wazito, wanadaiwa sh bilioni saba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Mkurugezi wa Matawi na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema fedha hizo lazima zipatikane ili shirika liweze kujiendesha na kuimarisha mipango yake ya maendeleo iliyojiwekea kuanzia mwakani.
“Tunawapa miezi mitatu kuhakikisha wanalipa madeni ya shirika, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo kuwaondoa ili shirika lipangishe wapangaji wengine,” alisema Mndolwa.
Kwa mujibu wa Mndolwa, NHC linahitaji kufanya ujenzi wa nyumba zingine 15,000 ndani ya miaka mitano ijayo na madeni ya fedha wanazodaiwa wapangaji wa shirika hilo ni sehemu ya mapato ya kukamilisha mradi huo.
Alisema kuanzia Januari 2011, wapangaji wote wa NHC, wanatakiwa kulipa kodi za pango kupitia taasisi za kibenki zitakazopendekezwa na shirika hilo ili kupunguza usumbufu wa foleni wa ulipaji wa kodi kwa baadhi ya vituo vyao.



h.sep3.gif
 
uongozi wa NHC umeamua jambo zuri,kwani kwa kufanya hivyo shirika litaweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini!!hii ni hatua nzuri sana!!
 
Tehe jamaa wanalipa Kodi kiduchu sana hawa nashangaa wanadaiwa walipeeeeeeee tu
 
Wakimaliza hilo zoezi waanze kufuatilia nyumba zao ambazo hazimo kwenye database yao huku wadosi wakiwa wamezitaifisha....
 
Mndolwa naye mnafiki siku zote alikuwa wapi?? lakini na nyie wapangaji mnaishije bila kulipa pango uliona wapi lipeni bwana. Nyie zenu mlizopangisha mbona mnawatoa wapangaji wasipolipa? Kodi zetu zimejenga nyumba hizo nyie mwakaa bure wapi na wapi lipeni tu
 
NHC NI SHIRIKA KUBWA SANA HEBU NENDENI NA WAKATI.I AM SURE ILE FOLENI PALE KWENYE MALIPO NI SABABU MOJAWAPO...ITS TOO INCONVINIENT AND BORING!!! KWA MFANO MIMI MARA NYINGI HUWA NASEMA NITAENDA LIPA KESHO MPAKA MWEZI MWINGINE UNAISHA......KWA NINI MSIBORESHE SYSTEM YENU YA MALIPO ILI IWE RAHISI KULIPA ,SAY, THROUGH MOBILE SERVICES eg MPESA,TIGOPESA etc???
 
Tangazeni nyumba ambazo wameshindwa kuzilipia wenye nia ya kulipa tuingie.
 
NHC boresheni system yenu ya kulipia na ndani ya hizo siku 90 deni liwe limekamilika..mifumo ya malipo yenye kujali muda,convinience inapatikana kirahisii kwa sasa.
 
Mndolwa naye mnafiki siku zote alikuwa wapi?? lakini na nyie wapangaji mnaishije bila kulipa pango uliona wapi lipeni bwana. Nyie zenu mlizopangisha mbona mnawatoa wapangaji wasipolipa? Kodi zetu zimejenga nyumba hizo nyie mwakaa bure wapi na wapi lipeni tu

Newvision kwa ukosoaji! Huyu kaanza kazi juzi juzi tu kutoka DAWASCOOOOOO. Aliwahi kufukuzwa Barclays kwa deal za mikopo ya kishikaji. Ila ndiyo safu mpya ya Nehemiah baada ya kupangua Wakurugenzi karibu wote wa NHC
 
Wakimaliza hilo zoezi waanze kufuatilia nyumba zao ambazo hazimo kwenye database yao huku wadosi wakiwa wamezitaifisha....

Nyingi ni za hao wadosi unaowasema walitaifishwa kipindi cha utaifishaji na kuna baadhi zimerejeshwa kwa wenyewe kwahiyo hakuna jipya kama haimo kwenye data base ujue sio yao.
 
huu uongozi ni wapuuzi wote kwanza mlikuwa wapi siku zote kulimbikiza BILION???STUPID..YAANI SIKU WANATANGAZA WAZIRI MHUSIKA UNGEFUKUZA TOP WOTE WANAOHUSIKA NA KULIMBIKIZA HAYA MALIPO HATA KAMA MTOTO WA MJOMBA SHANGAZI NA KUWEKA WAPYA..
 
Mndolwa naye mnafiki siku zote alikuwa wapi?? lakini na nyie wapangaji mnaishije bila kulipa pango uliona wapi lipeni bwana. Nyie zenu mlizopangisha mbona mnawatoa wapangaji wasipolipa? Kodi zetu zimejenga nyumba hizo nyie mwakaa bure wapi na wapi lipeni tu

Mkuu nadhani hujui vizuri historia ya msajili wa majumba NHC ilianzishwa lini na ina miliki nyumba zipi. Kwa kifupi kuna nyumba nyingi nyingi sana hazijajengwa na kodi wala na hao NHC bali zilitaifishwa enzi zile za uhujumu uchumi nyumba hizo nyingi zipo mitaa ya upanga na posta na baadhi zipo mtaa wa nkurumah na uhuru. NHC hawajawa na vision ya kuongeza makazi ya bei nafuu kwa mtaji wa nyumba za dhulma wangeweza kurahisisha maisha ya watanzania wengi kwa kujenga nyumba nyingine matokeo yake sasa hivi wanaingia ubia na matajiri wanabomoa za zamani wanajenga mpya na kuzipangisha kwa bei ya kuruka! Hakuna jipya hapa ni madudu tu mengine!
 
Back
Top Bottom