Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Wapangaji NHC wapewa siku 90 kulipa bilioni 9/-
na Marietha Mkoka
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), linadai sh bilioni 9 kutoka kwa wapangaji wake na limetoa siku 90 kwa wadaiwa hao sugu wawe wameshalipa, vinginevyo watatimuliwa. Kati ya madeni hayo, wapangaji wa NHC mkoa wa Dar es salaam ambao baadhi yao ni watumishi wa umma na wafanyabiashara wazito, wanadaiwa sh bilioni saba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Mkurugezi wa Matawi na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema fedha hizo lazima zipatikane ili shirika liweze kujiendesha na kuimarisha mipango yake ya maendeleo iliyojiwekea kuanzia mwakani.
Tunawapa miezi mitatu kuhakikisha wanalipa madeni ya shirika, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo kuwaondoa ili shirika lipangishe wapangaji wengine, alisema Mndolwa.
Kwa mujibu wa Mndolwa, NHC linahitaji kufanya ujenzi wa nyumba zingine 15,000 ndani ya miaka mitano ijayo na madeni ya fedha wanazodaiwa wapangaji wa shirika hilo ni sehemu ya mapato ya kukamilisha mradi huo.
Alisema kuanzia Januari 2011, wapangaji wote wa NHC, wanatakiwa kulipa kodi za pango kupitia taasisi za kibenki zitakazopendekezwa na shirika hilo ili kupunguza usumbufu wa foleni wa ulipaji wa kodi kwa baadhi ya vituo vyao.