Waombaji ni wengi .. TB Joshua kiboko!

Waombaji ni wengi .. TB Joshua kiboko!

Kama wachawi wapo sijawahi kulogwa.

Unamwamini Bwana Yesu Kristo kwa sababu ulimwona? Siyo kwa njia ya Neno?

Umesema huwezi kusema kama wachawi wapo ama hawapo. Biblia inasemaje? Unaiamini ama la?

Shetani hajawahi kuokoka lakini ajajua na anakiri juu ya Uwepo wa Mungu na Nguvu ililyo katika Jina na Damu ya Yesu.
 
Acha kutumia jina LA Tbjoshua ili update watu ,tbjoshua hana huduma wala mwanafunzi aliyempa eneo LA kufanyia huduma ,,huduma yake inapatikana Lagos Nigeria ikotun igbe,acha ulagai ,,,mimi ni mmoja ya wainjilist wake na ,hakuna kitu kama hicho ,,acha ulagai ,hell and heaven is there cjui unataka uingie wapi wapi,,,,
 
Amina
 
Habari waungwana!
Leo asubuhi nimebahatika kumtembelea Muombaji ambaye ni mwanafunzi wa TB Joshua. Niliwapeleka mambinti 2 kwa ajili ya kuombewa. Maajabu niliyoyaona sijawahi kuona tangu nimezaliwa.
Binti wa kwanza aliongea maneno mengi lakini alipojitambua hakujua nini kilikuwa kinaendelea. Katika baadhi ya maneno alosema ni hivi "sitaki asome ndiyo maana nilimwibia madaftari yake usiku, wakati wa vipindi nitakuwa namficha chooni"

Huyo binti nilipomuuliza kama kweli madaftari yake yalipotea akasema kweli yaliibiwa ...

Nikamuuliza kuhusu bibi yake .. akasema ni kweli bibi yake ni mchawi hadi wana kijiji walishataka kumchomea nyumba akakimbilia mjini kwa watoto wake ...

Swali: Hivi wachawi ni kwa nini huwa wanapenda kurudisha maendeleo ya watu wao wa karibu nyuma?
Kwa faida ya wale watakaotaka kwenda kuombewa: Mwombaji huyo yuko Kiseke jijini Mwanza, ila anafanya maombi Fly Park Hotel kila Jumatano na Jumapili. Sikuwahi kuhudhuria Fly Park, natarajia kuanza kwenda wiki hii! Hakika nimeuona mkono wa Bwana kupitia kwa mwanafunzi wa TB Joshua kwa jina anaitwa Zelamula.
Ebu wakati mwingine muwe na aibu na utapeli huu. TB Joshua hana mwanafunzi na ulisitumie jina la TB Joshua kutapeli. Jina linaloponya ni la Yesu pekee. Huduma za hotelini ni za kitapeli tu.
 
Inawezekana uliwahi kulogwa lakini hukulogeka vizuri
Kwahiyo nyie wateja wenu ni watu waliologwa....Asipoonesha kuanguka au kupagawa, ili mteja asiwakimbie mnamuambia hajalogeka vizuri arudi ili alogwe vizuri ili mje mumkamue vizuri hela zake...
 
Rafiki yangu alinipeleka kwenye kanisa mchungaji ni Mnigeria unaweza kulipata online linaitwa VPA church. Yule pastor wakati ananishika mkono ilikuwa kama short ya umeme imenipata, baada ya hapo alinieleza kwa kifupi yanayojiri kwenye maisha yangu. Hakuwa na mengi zaidi funga na kusali yatakwisha. Yalipanza kufunguka wala sikuamini. Siwezi kusema uchawi upo/haupo lakini ninachoelewa ninamhitaji Yesu katika maisha yangu.
Mungu asimame na hatima ya maisha yako Yesu ni jibu la maisha yako
 
Ebu wakati mwingine muwe na aibu na utapeli huu. TB Joshua hana mwanafunzi na ulisitumie jina la TB Joshua kutapeli. Jina linaloponya ni la Yesu pekee. Huduma za hotelini ni za kitapeli tu.
Anakuambia eti roho kamuongoza afanyie maombi hotelini..
 
TB Joshua ametuma mwanafunzi wake Tanzania?
Ana udhibitisho gani ametoka kwa SCOAN?
Nafikiri SCOAN wanawatumaga wale wise men na huwa na official report Emmanuel TV.
Je huyo anayo any identification kutoka SCOAN?
 
Anakuambia eti roho kamuongoza afanyie maombi hotelini..
Hotel howa na kumbi za mikutano mule ndani mimi mwenyewe kanisa langu linafanyia ibada hotel ya golden rose miaka mingi japo saivi nipo mkoa mwingine ni jambo la kawaida mbona.
 
Ndio maana mnaishia kuwapachika mimba wake na mabinti za watu..

Kwahiyo hata guest House maombi yanafanyika...hahahaga...

Huyo siyo Mungu ni pepo belzebuli..

Jinga kabisa .
Nitafia dini yangu,nitafia katika imani niliyoikuta,nitakufa kwa kuiamini biblia tu,mengine yanipitie mbali,siwezi kwenda kufanyiwa maombi hotelin,sehemu yenye walevi,mbinu chafu hufanyika,maovu yote kama usagaji,ulawiti,ubakaji,uzinzi na ujambazi hufanyika.hiyo sio nyumba ya ibada ni nyumba ya starehe tu
 
Acha kutumia jina LA Tbjoshua ili update watu ,tbjoshua hana huduma wala mwanafunzi aliyempa eneo LA kufanyia huduma ,,huduma yake inapatikana Lagos Nigeria ikotun igbe,acha ulagai ,,,mimi ni mmoja ya wainjilist wake na ,hakuna kitu kama hicho ,,acha ulagai ,hell and heaven is there cjui unataka uingie wapi wapi,,,,
Walio kinyume na Mungu hawawezi kuponya kwa jina la Yesu, pia kuna wanafunzi wa siri wa yesu, hivyohivyo wapo wanafunzi wa siri wa Tb Joshua, kuwa mwanafunzi means kufuata mafundisho ya mtu na sio lazima mwalimu ajue kuwa wewe ni mwanafunzi wake. Tb joshua kuwa na TV maana yake nikuwa na wanafunzi wengi duniani ambao yeye hawajui, nakufuata mafundisho yake kama kutoa pepo na nk ni kuenzi ufundishaji wake ambao amepewa na MUNGU.

Sioni tabu kwanini unamkeamea, kwani akitapeli?. kamisa kuwa Nigeria haimaanifu Mungu anaishia Nigeria( of all nation ina maana gani kama kanisa haliwezi pata wanafunzi nchi nyingine?)

Acha kuwaza mambo ya oficial communication za kanisa ambazo ndizo ziko centralized, huduma ya kiroho haiko centrallized ipo kila mahali kwa anayejifunza na kufuata vyema mafundisho.
 
Rafiki yangu alinipeleka kwenye kanisa mchungaji ni Mnigeria unaweza kulipata online linaitwa VPA church. Yule pastor wakati ananishika mkono ilikuwa kama short ya umeme imenipata, baada ya hapo alinieleza kwa kifupi yanayojiri kwenye maisha yangu. Hakuwa na mengi zaidi funga na kusali yatakwisha. Yalipoanza kufunguka wala sikuamini. Siwezi kusema uchawi upo/haupo lakini ninachoelewa ninamhitaji Yesu katika maisha yangu.

katika maisha yangu ya hapa JF mchango huu ndio ulionigusa zaidi.
hongera.
 
Hotel howa na kumbi za mikutano mule ndani mimi mwenyewe kanisa langu linafanyia ibada hotel ya golden rose miaka mingi japo saivi nipo mkoa mwingine ni jambo la kawaida mbona.
Yani wewe kumbe ndo yule tapeli unafanyie mambo hapo Golden Rose ...?? Mbona hayo mombi yameshindwa kumaliza tatizo la ma.laya hapo Mrina nyuma ya Golden Rose..

Acheni utapeli nyie...
 
Yani wewe kumbe ndo yule tapeli unafanyie mambo hapo Golden Rose ...?? Mbona hayo mombi yameshindwa kumaluza tatizo la ma.laya hapo Mrina nyuma ya Golden Rose..

Acheni utapeli nyie...
Me wala sio mchungaji bali ni mfanyabiashara na hapo golden rose ni wakristo wa kawaida kama wa kwa farther babu na burka au st. Theresa mbona hilo tatizo pia usiwahusishe wa upande huo?
 
Me wala sio mchungaji bali ni mfanyabiashara na hapo golden rose ni wakristo wa kawaida kama wa kwa farther babu na burka au st. Theresa mbona hilo tatizo pia usiwahusishe wa upande huo?
Hapana! Siwezi wahusisha wa huko maana hapo Golden Rose huku maombi yanaendelea na biashara inaendelea...Yani ni kama hayo maombi yahamasisha biashara hiyo..
 
Back
Top Bottom