Waombaji ni wengi .. TB Joshua kiboko!

Waombaji ni wengi .. TB Joshua kiboko!

Kwa mwendo huu naomba Hon Ummy ahamishie bageti ya madawa kwenye matumizi mengine maana yaelekea maombi yaweza kuwa mbadala.
Maombi ni kwa wale wanaoamini. Imani ni uhakika wa mambo yatarajiwayo, kama huna imani inakubidi uendelee na kile unachokiona kinakufaa.
Kumbuka maradhi yote hayatibiwi maospitalini. Yapo yale ambayo mtu unasababishiwa na roho chafu ambapo kila ukipima hospitali unaambiwa hakuna kinachoonekana.
 
Mkuu ni ushauri wangu tu ikiwa huduma hii mnahitaji watu wasike neno la Mungu kwanini mnang'ang'ania mjini ambapo idadi kubwa ya watu wameshasikia habari njema ya wokovu? Unaonaje ukiongea na TB Joshua ili huduma hiyo muielekeze Itilima ambapo watu wengi bado hawajaamini? Achaneni na flypark hotel pelekeni huduma Yenu Simiyu mtabarikiwa.
Nashukuru kwa ushauri wako, ila wale wanaopata taarifa hizi wanasafiri toka sehemu mbalimbali na kuja kupata huduma hiyo.
 
Hayo maji ni Yale ya TB Joshua au ya kwake tuuu? Na yanauzwa bei gani au ni free deliverance mkuu?
Kwa namna nijuavyo, maji ni maji tu, yakiombewa ndo yanakuwa na baraka. Kwetu sisi tunaoamini maji yakishaombewa na Mtumishi wa Mungu aliye hai, hayawi maji tena - yanakuwa DAMU YA YESU.
Yale alotoka nayo kwa TB Joshua yako yamefungwa (yako siled)
 
Back
Top Bottom