Wanyonya damu walikuwa wanaipeleka wapi damu?

Wanyonya damu walikuwa wanaipeleka wapi damu?

Avatar yako yaukweli
40281.jpg
 
Hakuna ukweli wowote ni uzushi tu,pia ikazushwa eti kuna wachuna ngozi!

Ikaja ukiwa na kipara unakatwa kichwa! Mara ukiwa na mwanya unakatwa kichwa!

Ikaja ukiwa na alama ya M kiganjani unakatwa mkono!

Hizi ni hadithi za kufikirika tu za utotoni.
Mmh mengine nahisi yana ukweli, miaka ya 93 kwenda 94, wilaya ya ukerewe na bunda kulikuwa na wakabaji ila hawa walikuwa wanakuminya koo kishirikina na hawakuachii mpaka wahakikishe umekojoa au kunya ndio wanakuachia ila wanachukua kinyesi nasikia mambo ya madini enzi hizo nyarugusu na nyamongo zilikuwa zinavuma sana, akina mama mimba zilitoka sana tu, na wananchi walipokuwa wanaripoti vituoni serikali inakana kuwa hakuna kitu kama hicho, wale watu walipotea baada ya wanakijiji kujichukulia hatua na kuwaua, kwani wanha wanajuana
 
Upo sahihi Kuna mzee amethibitisha yeye ni miongoni mwa waliokuwa wakifanya kazi hiyo anasema walikuwa mawakala wa kukusanya damu na waliweza kukopeshwa fedha za kuwa na miradi kama usafirishaji ama maduka na mashamba makubwa ambayo yalitumika kukusanya watu kutoka maeneo ya mbali (vibarua) ambao hao katika kuwaua hawakushtukiwa kwa haraka kwani ilikuwa vigumu kupata profile zao kutoka kwenye jamii, lakini mchezo huo ulikuwa mkubwa nchi nzima Iringa kuna mtu alikuwa maarufu Chalamila kuelekea Sadani alikuwa anafanza hayo,Mbozi kuna akina Bantu orodha ndefu tu walifanya kazi hiyo. Walipewa vifaa vya kuhifadhia damu na mahala pa kukabidhi walipewa, pia damu nyingi ilivuka mipaka kwenda nje, kwa mujibu wa mzee huyo, anasema kulikuwa na mzungu waliyekuwa wakiwasiliana naye kwa utaratibu wa chain kama wanavyofanya watoa taarifa ambapo watu say wapo 05 lakini A hamfahamu C, ingawa A anampa B na B anakabidhi kwa C hadi E kwa utaratibu huo.
Wanaopinga ni hiki kizazi cha dot com.
Bwana @uhurukenyata kwa maelezo yako ni kwamba haya matukio yalikuwa ni kweli. Hawa jamaa hiyo damu walikuwa wanaifadhi wapi? Je walikuwa wakinyonya wanaimaliza kwenye mwili wa mnyonywaji maana kama nilivyosema hapo kwenye post yangu #1 unatoaje uhai wa mtu ili kuokoa uhai wa mtu?
 
Miaka ya 1980 na 1990 kwenda 2000 kulikuwa na watu wanadaiwa kuwa ni wanyonya damu. Magari ya msalaba mwekundu tulikuwa kukikutana nayo lazima tutoke mbio kwa hofu ya kunyonywa damu.

Binafsi mimi kuna watu pale kijijijni kwetu mkoani kilimanjaro walikuwa wakihusishwa na unyonyaji damu. Mmoja nadiriki kumtaja alikuwa akiitwa Michael Ibrahim wa kijiji cha Longuo. Huyu bwana alikuwa akiogopwa na kila mtu.

Watoto wadogo wakimwona walikuwa lazima wakimbie. Pia baadhi ya wakina mama nao pia walikuwa wakimwogopa. Kuna taarifa za wakati huo kukutwa kwa miili ya watu wakiwa wamekufa na huku miili yao ikiwa imegongwa mihuri kuonyesha kuwa yule marehemu kanyonywa damu. Na wengi wa watu ambao walikuwa akisemwa kuwa ni wanyonya damu walikuwa ni watu wenye kipato. Hivyo kipato chao kuhusishwa na unyonyaji wa damu.

Kilichonifanya nilete huu uzi hapa ni kutaka kujua hii kadhia ni kweli ilikuwepo? Na kama ni kweli hiyo damu walikuwa wanapeleka wapi?

Sababu mimi nachojua ni kwamba damu ni kwa ajili ya tiba yaani kwa ajili ya kumwongezea mtu aliyepungukiwa na damu.

Sasa inakuwaje utoe uhai wa mtu kwa ajili ya kuokoa uhai wa mtu?
Nikweli hawa wanyonya damu Mumian walikuwepo. walikuwa wakara wa serikali kama walivyo wwngine. zamani ilikuwa ngumu kumuomba mtu ajitolee kutoa damu. hivyo walikuwa wanavizia watakayempata wanamdrain damu yote maana damu ya mtu mmoja ingeweza kuikoa maisha ya mtu zaidi ya mmoja.

Ila wale matajiri walikuwa wanaitwa wanyonya damu kwa kuwa husudu tu kama leo unavyosikia kila tajiri ni freemason ndivyo ilivyokua.
 
Hakuna ukweli wowote ni uzushi tu,pia ikazushwa eti kuna wachuna ngozi!

Ikaja ukiwa na kipara unakatwa kichwa! Mara ukiwa na mwanya unakatwa kichwa!

Ikaja ukiwa na alama ya M kiganjani unakatwa mkono!

Hizi ni hadithi za kufikirika tu za utotoni.
Wachuna ngozi sio story,ni kweli
 
Mkuu kipindi naishi pale maili sita tulikuwa tunaogopa kupita kule kwa babu sambeke tukiambiwa ananyonya damu nadhani akuna ukweli wowote ilikuwa ni hadithi tu
 
Mpaka sasa hatujapata ushahidi wa kutosheleza kuhusu hawa jamaa.
 
uchunaji ngozi ulikuwepo mkoa wa mbeya.niliwahi ona documentary yake live
Mie nlishaiona ngozi ilotupwa kwenye shamba LA shule mbozi huko, kipind haya mambo yanavuma. Sijui ilikuawaje ikaachwa pale kila ni ya binaadam
 
Nakumbuka wachuna ngozi wawili walikamatwa mbozi mbeya wakiwa na ngozi waliyoichuna,yaani yule binadamu aliyechunwa huwezi kukuangalia mara mbili,
Kuna watu wakatili sana kwenye dunia hii
Nilishuhudia tukio hili kwa macho yangu, sikusimuliwa! Ngozi ya binadamu ikiwa imechunwa, Vwawa Police Post, Mbozi nadhani it was 1998 kama sikosei! Ile memory huwa haipotei ndani ya kichwa changu.
 
Nilishuhudia tukio hili kwa macho yangu, sikusimuliwa! Ngozi ya binadamu ikiwa imechunwa, Vwawa Police Post, Mbozi nadhani it was 1998 kama sikosei! Ile memory huwa haipotei ndani ya kichwa changu.
Ninacho kwambia nakijua wala sijahadisiwa
Wale walikua wanachukua Damu kwa Nguvu
Huo Ndio ukweli
 
Nasikia walikuwa na kioo chao wakikumulika nacho basi unalegea kisha unaanza kuwafuata mwenyewe..

Binafsi nilikuwa napenda sana hizi scenario za wanyonya Damu, maana nilikuwaga napata sababu ya kutoroka shule kihalali.

Nakumbuka nimewahi kuzusha zaidi ya mara nne kwamba nimewaona wanyonya damu jirani na shule, ili tutimue mbio kurudi majumbani, na mara zote nilifanikiwa kurudisha watu nyumbani.
 
NASIKIA ILIKUA NI KWELI KWASABABU WANANCHI WENGI WALIKUA WABISHI KUTOA DAMU NA DAMU ZILIKUA ZINAHITAJIKA HIVYO ILIBIDI IFANYWE NGUVU.
BINAFSI MAMA MKUBWA WANG'S ALIULIWA KWA KIFO CHA AINA HIYO NA TULIVYOWAITA POLISI WALIKUJA WAKAMKAGUA WALIPOKUTA TU MUHURI KWAPANI BASI SHUGHULI ILIISHIA HAPOHAPO NA MWILI ULIKABIDHIWA TU NDUGU WAKAZIKE SABABU WAUAJI WAMESHAJITAMBULISHA KWA MUHURI. HILO TUKIO LILIFANYIKA TAREHE 9/12/1961 AMBAPO NDIO ILIKUA SIKU YA UHURU HIVYO HATUWEZI KUISAHAU
HIVYO SIO STORY TU HAYO MAMBO YALIKUWEPO KWELI.
NIMEMUELEWA SANA MTOA UZI SABABU NINAISHI MAENEO HAYO ALIYOYATAJA HAPO
 
Hakuna ukweli wowote ni uzushi tu,pia ikazushwa eti kuna wachuna ngozi!

Ikaja ukiwa na kipara unakatwa kichwa! Mara ukiwa na mwanya unakatwa kichwa!

Ikaja ukiwa na alama ya M kiganjani unakatwa mkono!

Hizi ni hadithi za kufikirika tu za utotoni.
Kipara, ngozi ni Kweli wewe
 
Miaka ya 1980 na 1990 kwenda 2000 kulikuwa na watu wanadaiwa kuwa ni wanyonya damu. Magari ya msalaba mwekundu tulikuwa kukikutana nayo lazima tutoke mbio kwa hofu ya kunyonywa damu.

Binafsi mimi kuna watu pale kijijijni kwetu mkoani kilimanjaro walikuwa wakihusishwa na unyonyaji damu. Mmoja nadiriki kumtaja alikuwa akiitwa Michael Ibrahim wa kijiji cha Longuo. Huyu bwana alikuwa akiogopwa na kila mtu.

Watoto wadogo wakimwona walikuwa lazima wakimbie. Pia baadhi ya wakina mama nao pia walikuwa wakimwogopa. Kuna taarifa za wakati huo kukutwa kwa miili ya watu wakiwa wamekufa na huku miili yao ikiwa imegongwa mihuri kuonyesha kuwa yule marehemu kanyonywa damu. Na wengi wa watu ambao walikuwa akisemwa kuwa ni wanyonya damu walikuwa ni watu wenye kipato. Hivyo kipato chao kuhusishwa na unyonyaji wa damu.

Kilichonifanya nilete huu uzi hapa ni kutaka kujua hii kadhia ni kweli ilikuwepo? Na kama ni kweli hiyo damu walikuwa wanapeleka wapi?

Sababu mimi nachojua ni kwamba damu ni kwa ajili ya tiba yaani kwa ajili ya kumwongezea mtu aliyepungukiwa na damu.

Sasa inakuwaje utoe uhai wa mtu kwa ajili ya kuokoa uhai wa mtu?

Wewe si ulikuwa kiongozi kwenye awamu zote tangu JKN hadi JMK ulishindwaje kuyajua hayo - Joke!!
 
Back
Top Bottom