Wanyonya damu walikuwa wanaipeleka wapi damu?

Wanyonya damu walikuwa wanaipeleka wapi damu?

Miaka ya 1980 na 1990 kwenda 2000 kulikuwa na watu wanadaiwa kuwa ni wanyonya damu. Magari ya msalaba mwekundu tulikuwa kukikutana nayo lazima tutoke mbio kwa hofu ya kunyonywa damu.

Kule Rukwa kuna kiongozi wa kanisa alipewa lift na gari la red cross baada ya gari lake kupata hitilafu njiani, alipofikishwa kwenye kanisa alikokuwa anakwenda kutoa sakramenti waumini wote walitokea dirishani kutokana na yeye kuteremka toka gari waliloamini ni la nyonyadamu
 
Mkuu ROGATH MCHAU hii kitu inachanganya sana. Kuna taarifa maeneo ya Rau ndio palikuwa panatisha sana. Nakumbuka miaka hiyo ukikatisha pale kcmc kwenda international school ilikuwa lazima muwe wengi.
 
Wapo mkuu mpaka Leo ila sasa nao wapo kwa technology mpya na jina jipya ambalo WATU WASIOJULIKANA na usafiri ni NISSAN JEUPE
 
Aliyeanzisha fikra hizi hakika alikuwa mtu mbaya sana. Ilifika wakati tukawa tunaambiwa kuwa Ubongonwa watu ulitumika kutengeneza Panadol.
Lakini huwa napata hisia kuwa baadhi ilikuwa wanasumbuliwa na wivu hadi kuibua uzushi kuchafua wenzao,ingawa watuhumiwa wa hayo makitu piaa baadhi utajili wao ulikuwa ni ule unaoleta mashaka
 
Hadi hatuendi shule kisa gari jekundu jamani,,halaf saa ingine mmekaa darasani mnashangaa tu ka mtu kanawashtua gari jekundu lile mbio zake sio za nchi hiii
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]acha kabisaaa yan mkisikia gari jekundu limepita hiyo sku full kuogopa

Ukirud nyumban unaambiwa kama hutak kuoga wanyonya damu watakubeba au wachuna ngozi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]acha kabisaaa yan mkisikia gari jekundu limepita hiyo sku full kuogopa

Ukirud nyumban unaambiwa kama hutak kuoga wanyonya damu watakubeba au wachuna ngozi
Full kutishwa tu
 
Miaka ya 1980 na 1990 kwenda 2000 kulikuwa na watu wanadaiwa kuwa ni wanyonya damu. Magari ya msalaba mwekundu tulikuwa kukikutana nayo lazima tutoke mbio kwa hofu ya kunyonywa damu.

Binafsi mimi kuna watu pale kijijijni kwetu mkoani kilimanjaro walikuwa wakihusishwa na unyonyaji damu. Mmoja nadiriki kumtaja alikuwa akiitwa Michael Ibrahim wa kijiji cha Longuo. Huyu bwana alikuwa akiogopwa na kila mtu.

Watoto wadogo wakimwona walikuwa lazima wakimbie. Pia baadhi ya wakina mama nao pia walikuwa wakimwogopa. Kuna taarifa za wakati huo kukutwa kwa miili ya watu wakiwa wamekufa na huku miili yao ikiwa imegongwa mihuri kuonyesha kuwa yule marehemu kanyonywa damu. Na wengi wa watu ambao walikuwa akisemwa kuwa ni wanyonya damu walikuwa ni watu wenye kipato. Hivyo kipato chao kuhusishwa na unyonyaji wa damu.

Kilichonifanya nilete huu uzi hapa ni kutaka kujua hii kadhia ni kweli ilikuwepo? Na kama ni kweli hiyo damu walikuwa wanapeleka wapi?

Sababu mimi nachojua ni kwamba damu ni kwa ajili ya tiba yaani kwa ajili ya kumwongezea mtu aliyepungukiwa na damu.

Sasa inakuwaje utoe uhai wa mtu kwa ajili ya kuokoa uhai wa mtu?
Acha kumuita michael ibrahim babu yangu kipenzi myonya damu akili kisoda wewe ulishawahi kushuhudia akinyonya damu jitu zima linashindwa kufikiri mtu anyonye damu aipeleke wap.ninyi si majirani pale mlikua mna wivu tu na maendeleo yake ushirika wa neema nzima yeye ndio alikua mtafutaji kwa bidii ninyi kwenu mlikua mnashinda kwenye baa za mbege badala ya kwenda kulima mashamba ya kosata
 
Miaka ya 1980 na 1990 kwenda 2000 kulikuwa na watu wanadaiwa kuwa ni wanyonya damu. Magari ya msalaba mwekundu tulikuwa kukikutana nayo lazima tutoke mbio kwa hofu ya kunyonywa damu.

Binafsi mimi kuna watu pale kijijijni kwetu mkoani kilimanjaro walikuwa wakihusishwa na unyonyaji damu. Mmoja nadiriki kumtaja alikuwa akiitwa Michael Ibrahim wa kijiji cha Longuo. Huyu bwana alikuwa akiogopwa na kila mtu.

Watoto wadogo wakimwona walikuwa lazima wakimbie. Pia baadhi ya wakina mama nao pia walikuwa wakimwogopa. Kuna taarifa za wakati huo kukutwa kwa miili ya watu wakiwa wamekufa na huku miili yao ikiwa imegongwa mihuri kuonyesha kuwa yule marehemu kanyonywa damu. Na wengi wa watu ambao walikuwa akisemwa kuwa ni wanyonya damu walikuwa ni watu wenye kipato. Hivyo kipato chao kuhusishwa na unyonyaji wa damu.

Kilichonifanya nilete huu uzi hapa ni kutaka kujua hii kadhia ni kweli ilikuwepo? Na kama ni kweli hiyo damu walikuwa wanapeleka wapi?

Sababu mimi nachojua ni kwamba damu ni kwa ajili ya tiba yaani kwa ajili ya kumwongezea mtu aliyepungukiwa na damu.

Sasa inakuwaje utoe uhai wa mtu kwa ajili ya kuokoa uhai wa mtu?
Ni kweli wiki ilopita tu msibani niliuliza swali hili kwa wazee..
Nasikia walikua wakiitwa Mumiani,Na ujue miaka hiyo hakukua Na taratibu wa kukusanya damu,mfano wa ilivyo sasa damu salama,Na kawaida hospital ni muhimu kuwe Na akiba ya damu
 
Damu ilikua inapelekwa Amani Muheza Tanga. Na mpaka leo wanachukua. Unaweza ukajipeleka mwenyewe ukatoa damu kwa malipo wakiwa hawana kabisa huwatumia mumiani kuleta hiyo damu. Kazi ya mumiani ina lipa sana. Matajiri wengi sehemu za Tanga mitaji yao walipatia huku. Kama huamini jitie umelewa maeneo ya Mafleta Muheza hata leo usiku. Kesho kwenu watakula ubwabwa
 
WACHUNA NGOZI WALIKUWEPO, SIO UZUSHI KWANI KUNA MIILI ILIOKOTWA IKIWA IMECHUNWA NGOZI NA NINA KUMBUKA WATUHUMIWA WALIKAMATWA ISIPOKUWA SINA KUMBUKUMBU YA KESI ZAO ZILIISHAJE
Mwaka juzi tu mwezi wa 5 Startv walitangaza mtu kachunwa ngozi huko Mbeya na kamanda wa polisi alithibitisha sema watu hawana kumbukumbu, haya mambo yapo.
 
Nakumbka enzi hizo niko darasa la kwanza,tulitimua mbio shule nzima baada ya kuona gar likidaiwa la wanyonya damu kitambo sana sijui kama ilikua ukwel.
mimi pia ilikua 2000 nikiwa darasa la kwanza

sijui ni uzushi tu maana hata sikuona kitu nilivyoona watu wanakimbia nami nilikimbia
 
WACHUNA NGOZI WALIKUWEPO, SIO UZUSHI KWANI KUNA MIILI ILIOKOTWA IKIWA IMECHUNWA NGOZI NA NINA KUMBUKA WATUHUMIWA WALIKAMATWA ISIPOKUWA SINA KUMBUKUMBU YA KESI ZAO ZILIISHAJE
Walihukumiwa wote wale waliotiwa hatiani kwenye kuhusika na maswala haya.
 
Back
Top Bottom