Ashikiliwa kwa kukutwa na Koki 330 za bomba, mali ya Mamlaka ya maji Katavi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MUWASA) Mpanda wamefanikiwa kumnasa Gaudensia Assenge (45) kwa kukutwa na koki 330 za bomba ambazo zinadaiwa ni mali ya wizi.

Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Kaster Ngonyani amesema mtuhumiwa amekutwa na koki hizo nyumbani kwake ambapo jeshi hilo limemshikilia na hatua kali zitachukiliwa dhidi yake.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA - Mpanda amesema mamlaka imekuwa ikipata hasara kwa baadhi ya koki kuibiwa mara baada ya kufungwa kwenye bomba za watumiaji.
 
Back
Top Bottom