Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Mshana jr hajaonekana siku nzima.
Au ligi ya uingereza imembana?
 
Guasa! Leta hiyo ramani ya Vita ya mzulu. Kama senema.
Ilikuwa khatari sana makumazahn mwenyewe anasema inachukua muda kuizungumzia ila tukio lenyewe hata dakika 3 hazikuisha kwani kilichotokea walitegemea kumkuta yule mlinzi wa mlango wa miiba akiwa kalala matokeo yake jamaa alikuwa macho wakaanza kufikiri nini cha kufanya hapo yule mzee mzulu alikuwa karibu yangu na kunionyesha ishara kisha akaanza kutambaa kuelekea kule mlangoni na kidogo kidogo yule nyoka mrefu mweusi akazidi kumkurubia yule mjivuni mara ghafla yule mlinzi akahisi kitu na kujongea karibu ya chungu cha majani kisha akaokota jiwe na kulirusha sehemu alohisi duh jiwe likampata yule mzee mzulu kichwani wote tukabaki na butwaa nini kitatokea lakini yule nyoka wala hakujitingisha mpaka yule mjivuni akayaangalia yale majani kivivuvivu kisha akaangalia mashariki dalili ya mapambazuko akaipekecha mikono yake labda ajipe joto.
Hapo kilitokea kitendo yule nyoka mweusi akamfikia adui yake tukaona miili miwili ikijinyonganyonga kisha tukasikia sauti kama ya kijiti kikavu miili yote ikaenda chini kisha yule mtu mkubwa akamkalia adui yake akiwa bado anatapatapa mpaka alipotulia.
Akatufanyia ishara ya kusonga mbele na kila mtu akashika nafasi yake ilikuwa ndo nataka nitoe amri ya kushambulia ila kuna mtu mmoja karibu yangu meno yake yakawa yanagongana aidha kwa baridi au uwoga nami nikapigwa na mghafala na kumpiga na kitako cha bunduki kweli kelele zake zikakoma ila wakati nimempiga kidole chake kikaangukia penye kifyatuo cha bunduki nayo ilipita inchi chache kichwani pangu basi hakukuwa na ishara nyingine ya vita.
Nikapiga risasi zangu kumi wakati nachochea zingine nikamkumbuka yule mtoto flossie nikamuona akipanda ukuta huku akisaidiwa na Yaya wake nikajua atakuwa salama mara nikasikia upande wa pili wa ukuta sauti ya bougwan ikiwa juu basi sasa tukawa na kazi ya kuwalenga wajivuni wale waliokuwa wanakimbilia mlango wa miiba na wale walio kuwa wanajaribu kupanda ukuta. Inachukua muda kuelezea lakini ni muda mchache sana ulitumika na sasa nikadhani vita imekwisha nikamuona mtu anakimbia juu ya chungu za maiti hakuwa peke yake umslopogaaz alikuwa nyuma yake kumbe ni yule mkubwa wa wajivuni japo alikimbia kwa kasi lakini adui yake alizidi kumkurubia akasimama aah ni wewe mjivuni nilie sema nawe usiku wa jana? ni wewe mjivunaji mkamata watoto wa kike aah ni wewe ulie taraji kukabiliana na umslopogaaz mkuu wa ukoo wa makwlilisini wa kabila la wazulu !aah ni vema maombo yako yametimizwa basi yule mjivuni akapeleka mkuki wake na yule mzee akasogea nyuma kidogo kisha akalipunga shoka lake hewani lolipotua lilikata mabega yanapoungana na shingo !kisha akaiangalia maiti ya adui yake na kusema lilikuwa pigo zuri !pigo takatifu! pigo lenye nguvu.
 
Abunuwasi na Abdul wale watu walikuwa kiboko wale full vituko but wanafundisha kuna kisa kimoja masikini kaenda kumshukuru tajiri jirani yake kuwa amekula chakula kwa harufu ya mboga toka kwa tajiri yaani alikuwa ana lumangia tajiri akaenda kushtaki alipwe harufu yake ya mchuzi masikini akawa ana haha kesi imemkalia vibaya mara Abunuwasi anapita kumuuliza akamuhadithia mpaka mwisho Abunuwasi akasema nitakusaidia kisha kaanza kutangaza kuwa pana sherehe nyumbani pake akanunua mahitaji yote wageni wamefika lakini cha ajabu mchele upo kule moto upo huku nyama kule wageni wakachachamaa wakiongozwa na tajiri hii haiwezekani hiki chakula kitaiva vipi bila kufanya hivi? Abunuwasi ndipo alipoamka na kusema bwana tajiri kisa hiki ni sawa na ulivyo mshtaki masikini kesi ya harufu ya mchuzi wako.
Ongeza nyingine!
 
Ongeza nyingine!
Jamaa alikuwa akili nyingi kuna kipindi alijenga ghorofa basi muda ukapita akaja mtu kutaka kuinunua ile nyumba abunuwasi akamwambia nitakuuzia ya juu hii ya chini nitakaamwenyewe basi hati ikaandikwa hivyo muda ukapita abunu akawa hana pesa na anadaiwa akaenda kwa yule aliemuuzia nyumba ya juu kumuomba amuazime pesa jamaa akakataa basi abunu akaona isiwe kesi mimi mji huu umenishinda nataka kuhamia mji mwingine ila nyumba yangu sitaiacha nitaondoka nayo sasa shikilia nyumba yako wakati naichukua yangu akaanza kubomoa huku anamwambia jiraniii shikilia vizuri nyundo zinapigwa pote pana tikisika vumbi mtindo mmoja jamaa ilibidi amwite na kumpatia pesa abunuwasi.
 
Nimepeleka mawazo mbali Sana, miaka nikiwa darasa LA sita 1970 nilisoma kitabu hiki .Kimejaa ufundi wa ajabu.Inkubu'
 
Swadakta swahiba wangu mada imewafikirisha wenye mada na pia wenye kupenda vitu vya kale hisia zinarudi nyuma na kukumbuka mbali
Nilikuwa offline nilikuwa visiwa vya mbali hakuna network kabisa! Nimekosa uhondo mwingi
 
Uhondo upi tena swahiba wako ulokupita? Haya khabari za huko visiwani?
Uhondo wa post naona umetupia vifungu kadha
1474819585241.jpg
mambo ya visiwani hayo
 
Back
Top Bottom