Zitto,
Nionavyo mimi hapa sio swala la kutumia tena taratibu za kitabuni. Maendeleo yameshindikana chini ya RC na kulkikuwepo na hatari kubwa ya haohao viongozi wa ngazi za mitaa kufa ktk mfumo huu zaidi ya Mbunge.
Binafsi namtazama Mbunge kama waziri tu, kuna watendaji kazi, waajiriwa wa serikali kama wizara..lakini inapofikia maswali hujibiwa na waziri. Kwa hiyo Kila wilaya inakuwa kama wizara vile na katibu mkuu wake wakishiurikiana na Halmashauri ya jiji/wilaya/ manispaa.
halmashauri za miji yetu na wilaya zimeshindwa kufanya kazi hadi sasa. tena basi ukienda mikoani huko utawakuta hawa makatibu wa chama CCM wamechukua majumba, mali na kusimamamisha miradimingi tu. Pia kuna madiwani wamesimamisha miradi iliyokuwa imetangulia diwani aloachia ngazi kwa sababu kila diwani anakuja na mawazo yake mwenyewe ktk ujenzi wa taifa zima.
Yaani Utendaji kazi nchini umekuwa wa kichama na mapendekezo ya mtu na sio ya wananchi.
Binafsi nadhani hili sio swala la mfumo zaidi ila linatokana na nafasi za watu ktk mshiko wa ngawila. Kwa hiyo tulitazame kwanza kulingana na nafasi za watu kuliko mfumo maanake Ubinafsi ndio adui yetu mkubwa!.. Ni mbinu ipi ambayo itamwajibisha kiongozi mweka hazina wa wilaya ikiwa DC, Halmashauri za wilaya/jiji/ manispaa zote zimekuwa zikikwama kumaliza mipango ya maendeleo yao.
Nilichojifunza mimi huko mikoani sio tatizo la uvujaji wa pakacha ila tatizo kubwa ni mbebaji tofauti na Kitaifa ambacho pakacha lavuja!. Kidogo kinachopatikana hupigwa ktk sinia moja la pilau sasa hapo mjomba kuna wageni wa heshima wao huwa ndio wa kwanza kukaa mkekani!.
Kaka,
Tanzania kuna three levels of governance only.
1. Kijiji
Hapa unakuta serikali ya kijiji chini ya mwenyekiti wa kiiji na mtendaji ni Afisa Mtendaji wa Kijiji-VEO. Serikali ya kijiji ni serikali tosha ina mamlaka ya kukusanya kodi na kutunga sheria ndogondogo katika kijiji.
2. Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji
Hili ndio twaita baraza la madiwani chini ya Meya na mtendaji ni Mkurugenzi MTENDAJI-DED etc. wana mamlaka ya kukusanya kodi na kutuga sheria.
3. Taifa
Hapa unakuta Bunge na baraza la mawaziri chini ya Rais.
Hivyo ngazi ya Kata na ngazi ya Jimbo la uchaguzi ni ngazi tu kuchagua. Tena afadhali ya Kata ambapo kuna kamati ya maendeleo ya Kata na afisa mtendaji-WEO, jimbo la ubunge ni kasha tupu ambalo kazi yake ni uchaguzi tu.
Kiutawala ni kosa kubwa kumpa mbunge pesa ya maendeleo maana hana ngazi ya utawala. Hana watendaji huyu, ni mtu.
Kama twataka kuwa serious na pesa hizi za umma, then tuwe na marekebisho ya sheria za serikali za mitaa ili kuweka ngazi ya utawala katika eneo la Jimbo la uchaguzi na hivyo kuwa na kitu kama kamati ya maendeleo ya Jimbo chini ya uenyekiti wa Mbunge.
Mkandara-RC na DC ni extension ya serikali kuu katikangazi za chini. Nafasi hizi zifutwe tu. Tunahitaji uimara na ubora katika halmashauri.
Kuwapa wabunge fedha za umma bila chombo cha uwajibikaji ni ubadhirifu wa fedha za umma.