Zitto: Ngoja kwanza; kwanza sahihisho kidogo, hivi Mauritania sio ndiyo kwa kiingereza ni Mauritius au? Kama hivi ndivyo, basi sahihisho ni kwamba hii nchi ni ya pili kwa utajiri baada ya Seychelles. HDI ya Mauritius ni 0.800 na Seychelles ni 0.800. I hope ulimaanisha nchi tajiri kuliko Tanzania!
Nirudi kwenye mjadala: Nisaidie mambo matatu: Mosi, ukitaka kupima mishahara sio vizuri kulinganisha na nchi zingine. Kuna msemo kwenye economics kuwa an inappropriate example leads to wrong formulation of questions and answers. Sasa katika hili, ukitaka kujua kama wabunge wetu wanalipwa vizuri au vibaya, inabidi ulinganishe mishahara yao na wafanyakazi wengine nchini Tanzania. Lakini tutapima mishahara kulinganisha ni nchi zingine tutapata majibu yasiyo. Kwa hiyo tukitaka kuwa fair tuangalie tunavyogwana hiyo keki ndogo miongoni mwa wabunge na wanasiasa wengine, walimu, madaktari, wahadhiri, n.k. Tupatie hizi statistics ndio tujue mambo yakoje.
Pili, wakati wabunge wanazidi kujiongezea posho kando na mshahara, wabunge haohao wameidhinisha sera ya kufuta utaratibu wa marupurupu katika sekta zingine. kwa mfano walimu walikuwa wanalipwa posho ya mazingira magumu ya kazi, ikafutwa. Wahadhiri walikuwa wanalipwa posho ya mafuta na ufundishaji, zote hizi zilifutwa. Sasa kwa nini kunakuwa na double standard?
Pili, katika nchi zilizoendelea mishahara ya wanasiasa huwa ndio ipo chini ukilinganisha na wafanyakazi wengine wa kada ya kati. Kwetu, hali ikoje?