Nasema hivi, Kila mtu ana taste yake mkuu, mimi nimezungukwa na wengi ambao wameoa na wengine wakiona mwanamke mweupe wanababaika ila trust me kuna watu hawashtuliwi na rangi ya chai kwani sio utamu.
Sikiliza ka stori cha kizushi.
Kuna jamaa alikua na mwanamke wake mweusi kiasi na alikua akimpenda sana, baada ya muda walianza shindwana na kutoelewana kwa sababu mbalimbali. Ila mojawapo ni yule mwanamke baada ya mchizi kumhidumia vizuri basi akang'aa na kuanza kuonekana ana uweupe kwa mbali, basi ikawa kero... Leo bebi nataka queen elisabeth, mara nataka yale cocoa butter, mara labda nikijaribu himalaya nitakua nang'aa zaidi. Ameacha kuona rutuba za jamaa zinafanya kazi anaona juhudi zake.
Basi baada ya muda ile hali ilimchosha mwenzetu na akawa analalamika sana, alimpenda na rangi yake ya uweusi mzuri (ukizingatia ameachana na toto leupe la tanga) sasa akaona isiwe kesi akajumlisha akatoa, mambo yakaisha.
So weusi wazuri wapo. Na kumbuka uzuri wa mtu au kitu upo machoni kwa mtazamaji, kama akili yako umeiseti kuwa weupe wazuri, they will always be.
Maisha yanaendelea