Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,875
Japo dunia inapinga ubaguzi wa rangi kwa nguvu zote, Sudan moja kati ya nchi zilizoko Afrika imeonekana kuwa ubaguzi ni kitu cha kawaida.
Nchini humo katika hali ya kuutukuza ubaguzi, mtu mweusi huwa wanamuita mtumwa. Pia nafasi nyingi za kisiasa zinakaliwa na waarabu na wanubi ambao ni weupe huku watu weusi wakifanya kazi za kawaida.
Nchini humo hata ndoa kati ya mtu mweusi na mweupe huonekana kama kitu kibaya kiasi cha mtu kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.
Ubaguzi wa rangi nchini Sudan umekuwa kama jadi ya taifa hilo tangu walipopata uhuru wao.
=
Reem Khougli na Issam Abdulraheem walikabiliwa na matusi kwa kuoana
Katika msururu wa taarifa zetu kutoka kwa waandishi wa habari wa Afrika ,Zeinab Mohammed Salih anaelezea juu ya unyanyasaji wa kutisha wa ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi nchini Sudan.
Onyo: Taarifa hii ina maneno makali
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yalienea pande zote za dunia kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd ambaye aliuliwa wakati polisi aliposhindilia goti kwenye shingo lake nchini Marekani, lakini Sudan inaonekana kuwa iko katika dunia tofauti juu ya suala la ubaguzi wa watu weusi.
Kulikua na kampeni kuhusu hashtag #BlackLivesMatter. Badala yake Wasudani wengi wanaotumia mitandao ya kijamii walimshambulia mchezaji soka maarufu mweusi , Issam Abdulraheem, na mwarabu mweupe ambaye ni msanii wa masuala ya vipodozi , Reem Khougli, baada ya kuoana.
"Kusema ukweli we msichana hii ni haramu ... malkia anaolewa na mtumwa ," mwanaume mmoja aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya kuona picha ya wawili hao.
Facebook mubashara kutoka fungate
Kulikuwa na makumi ya ujumbe- ambao sio wa kushangaza katika nchi ambapo Wasudani wengi ambao hujitazama kama Waarabu, kuliko walivyo Waafrika, mara kwa mara hutumia nene'utumwa'', na maneno mengine yasiyo ya dharau, kuwaelezea watu weusi.
Sudan imekuwa ni nchi inayotawaliwa na watu wenye ngozi nyeupe, wasomi wa kiarabu, ,huku Waafrika weusi wanaoishi katika maeneo ya kusini na magharibi wakiendelea kukabiliwa na ubaguzi na kuachwa nyuma kimaendeleo,
Ni jambo la kawaida kwa magazeti nchini humo kuchapisha maneno ya ubaguzi kuwahusu watu weusi likiwemo neno "mtumwa".
Sudan lilikua ni eneo kuu la biashara ya utumwa katika karne ya 19
Wiki chache zilizopita, mwandishi wa taarifa za maoni katika gazeti Al-Intibah linalomuunga amkono rais wa zamani wa Sudan Omar-al-Bashir - ,ambaye hakubaliani na suala la mwanamke kucheza soka, alimuelezea kocha wa kike wa timu ya soka ya Gunners, ambaye anatambulika sana kwa kuifunza timu ya wasichana ya Gunners kama mtumwa.
Na karibu kila chombo cha habari huwaelezea wahalifu wadogo wadogo katika mji mkuu , Khartoum, kama "negros" kwasababu wanawaona kama ni watu maskini na wala si watu wa jamii ya Waarabu.
Wakati nilipomuuliza Abdulraheem kuhusu kile anachoweza kusema juu ya unyanyasaji na ubaguzi aliofanyiwa yeye na mke wake, alisema : Sikuweza kutuma picha zaidi kwenye kurasa za mitandao yangu ya kijamii kwa kuogopa kupokea matusi zaidi."
Badala yake Abdulraheem mwenye umri wa miaka 29- na mke wake mwenye umri wa miaka 24 walifanya Facebook mubashara wakati wa fungate yao, wakisema kuwa wanapendana na ubaguzi hauna maana kwao.
Kufuatia malalamiko ya watu juu ya ujumbe huo, Ihsan Fagiri alitangaza kujiuzulu, lakini No To Women Oppression kikakataa kukubali kujiuzulu kwake, likisema kuwa hakua na maana hiyo aliyoiandika.
Kumekuwa na maandamano madogo ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Sudan
Ubaguzi wa rangi ni kitu cha jadi nchini Sudan, kihistoria na tangu uhuru wa taifa hilo , ambapo vyeo vya juu zaidi vya kazi vimekua vikijazwa na watu kutoka kaskazini - ambao ni wa jamii za Waarabu na Wanubi.
Takriban maafisa wote wa ngazi ya juu katika jeshi wanatoka katika jamii hizi, jambo linalowaruhusu kutumia ushawishi wao kumiliki sekta ya biashara.
Leo kama ikiingia katika idara yoyote ya serikali au benki mjini Khartoum , ni nadra kumuona mtu mweusi akifanya kazi muhimu.
Hakuna takwimu za kuaminika juu ya idadi ya watu kulingana na jamii zao, ukiachana na utajiri wao, lakini kikundi cha waasi wanaopigania haki za watu weusi cha Darfur kinakadiria kuwa 60% ya wakazi wa Khartoum ni weusi.
Wafanyabiashara wa utumwa 'walitukuzwa'
Ubaguzi wa rangi una mizizi yake tangu kuasisiwa kwa mji wa Khartoum mwaka 1821 kama soko la watumwa.
Kufikia nusu karne, karibu theluthi mbili ya watu waliokuwa katika mji huo walikua watumwa.
Sudan ilikuwa ni mojawapo ya maeneo ya Afrika ya kupata watumwa, huku watumwa waliosafirishwa kutoka kusini hadi kaskazini, na Misri , Mashariki ya kati na maeneo ya Mediterranean wakichukuliwa kutoka Sudan.
Bado wafanyabiashara ya utumwa wanatukuzwa-mtaa katikati mwa mji mkuu umepewa jina la al-Zubair Pasha Rahma, ambaye jhimaya yake ya biashara ilipanuka hadi katika maeneo ya ile inayoitwa Jamuhuri ya Afrika ya katikwa sasa na Chad.
Wanahistoria wanasema aliwakamata zaidi watumwa wanawake kutoka maeneo ya Sudan ambayo kwa sasa yanafahamaika kama Blue Nile na milima ya Nuba Mountains, pamoja na Sudan Kusini na kutoka katika jimbo la Oromia nchini Ethiopia. Alikua anafahamaika kwa jeshi lake la watumwa, ambalo liliwajumuisha watumwa waliotekwa kutoka Sudan Kusini.
Mtaa mwingine umepewa jina la Osman Digna - mfanyabiashara wa watumwa na kamanda wa kijeshi, ambaye biashara yake wakati huo iliyonoga wakati huo ilivunjwa na kisheria utumwa.
Biashara hiyo ilizuiwa rasmi mnamo mwaka 1924, lakini uamuzi wa kuizuwia ulikabiliwa na upinzani mkali kutoka zaidi kwa Waarabu na viongozi wa Kiislamu, miongoni mwao wakiwa ni Abdelrahman al-Mahdi na Ali al-Mirghani, ambao wengi wanamini walikua na watumwa wanawafanyia kazi katika ardhi yao iliyokuwa kando ya mto Nile.
Waliuandikia utawala wa kikoloni wakiutaka wasizuwie utumwa, lakini ombi lao lilipuuzwa.
Wanaume hao wawili, pamoja na vyama vyao vya kisiasa - Unionist na Umma - waliendelea kuwa na ushawishi mkubwa baada ya uhuru wakiingiza fikra za ubora wa Waarabu katika taifa jipya kwa kutoa karibu ajira zote kwa Waarabu na kushindwa kuendeleza maeneo yanayokaliwa na watu weusi.
Mjukuu wa Mahdi, Sadiq al-Mahdi,alihudumu kama waziri mkuu kuanzia mwaka 1966 hadi 1967 na tena kuanzia mwaka 1986 hadi 1989, wakati mtoto wake Mirghani, Ahmed, alipokua rais katika serikali ya Muungano iliyoundwa na wanaume hao wawili.
Wasomi wawili wa Sudan, Sulimen Baldona Ushari Mahoumwalidai wazi kwamba waligundua ushahidi wa Waarabu wa makundi yaliyoko wanaowatumikisha watu weusi kutoka kusini kama watumwa. Walisema makundi haya yalipewa silaha na jeshi la Sadiq al-Mahdi - na walikua ndio mwanzo wa wanamgambo wa Janjaweed, ambao baadae walishutumiwa kwa kwa mauaji ya kimbari ya Darfur.
Madai ya uvamizi wa watumwa yalikanushwa na serikali ya Ahmed Mirghani na Sadiq Mahdi, ambao waliendelea kuwa na ushawishi katika siasa za Sudan na wako karibu na serikali ya sasa, ambayo ilichukua mamlaka baada ya kumpindua madarakani Bwana Bashir mwaka 2019.
Uvamizi wa watumwa kusini mwa nchi uliripotiwa sana kuwa uliendelea hadi mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005, jambo lililosababisha watu weushi hasa Waafrika wa Sudan Kusini kujitenga na Sudan miaka mitano baadae.
Wanawake na watoto waliotekwa na makundi ya Waarabu kufanya kazi kwa ajili ya "bwana" bila malipo mara nyingi hawakuziona familia zao tena, ingawa mara kadhaa uhuru wao waliupata kupitia makundi ya msaada kama Christian Solidarity International.
Na tangu mzoizo wa Darfur ulipoanza mwanzoni mwa miaka ya 2000s, kundi la wanamgambo Waarabu wanaounga mkono serikali la Janjaweed limekua likiripotiwa mara kwa mara kwa kuvamia vijiji vya watu weusi, kuwauwa wanaume na kuwabaka wanawake.
Serikali ya mpito iliundwa na jeshi na makundi ya kiraia yaliyoongoza mapinduzi mwaka 2019, lakini haijawa wazi ikiwa kweli imejitolewa kushughulikia suala la mfumo wa ubaguzi wa rangi ndani ya taifa la Wasudan.
Chama cha Congress (SCP), ambacho ni mjumbe muhimu wa raia katika serikali, kinasema kwamba sheria zimekwisha pendekezwa za kutambua kauli za chuki kama uhalifu. Chini ya pendekezo la sheria hiyo, adhabu ya kutumia maneno ya ubaguzi wa rangi itakua ni kifungo cha gerezani cha miaka mitano, aliniambia msemaji wa chama cha SCP Mohamed Hassan Arabi.
Lakini weusi wengi hawafurahii nafasi ya jeshi katika serikali, ikizingatiwa kuwa lilikuwa ni sehemu ya utawala wa Bwana Bashir.
Mmoja wa mawaziri wachache weusi, Steven Amin Arno, alijiuzuru katika kipindi cha miezi miwili baada ya kuchukua mamlaka, akisema katika barua yake ya kujiuzulu ambayo ilionekana kwenye mitandao ya kijamii kwamba hakuna mtu aliyekua ana msikiliza.
Serikali haikutoa kauli yoyote kuhusu kujiuzulu kwake, jambo linalomaanisha kuwa alichokisema kilikua kweli.
"Kilichotokea kwangu kinaonesha kutengwa na taasisi ya ubaguzi wa rangi nchini ," aliniambia.
Nchini humo katika hali ya kuutukuza ubaguzi, mtu mweusi huwa wanamuita mtumwa. Pia nafasi nyingi za kisiasa zinakaliwa na waarabu na wanubi ambao ni weupe huku watu weusi wakifanya kazi za kawaida.
Nchini humo hata ndoa kati ya mtu mweusi na mweupe huonekana kama kitu kibaya kiasi cha mtu kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.
Ubaguzi wa rangi nchini Sudan umekuwa kama jadi ya taifa hilo tangu walipopata uhuru wao.
=
Maoni kutoka Sudan - ambako watu weusi huitwa watumwa
27 Julai 2020Reem Khougli na Issam Abdulraheem walikabiliwa na matusi kwa kuoana
Katika msururu wa taarifa zetu kutoka kwa waandishi wa habari wa Afrika ,Zeinab Mohammed Salih anaelezea juu ya unyanyasaji wa kutisha wa ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi nchini Sudan.
Onyo: Taarifa hii ina maneno makali
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yalienea pande zote za dunia kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd ambaye aliuliwa wakati polisi aliposhindilia goti kwenye shingo lake nchini Marekani, lakini Sudan inaonekana kuwa iko katika dunia tofauti juu ya suala la ubaguzi wa watu weusi.
Kulikua na kampeni kuhusu hashtag #BlackLivesMatter. Badala yake Wasudani wengi wanaotumia mitandao ya kijamii walimshambulia mchezaji soka maarufu mweusi , Issam Abdulraheem, na mwarabu mweupe ambaye ni msanii wa masuala ya vipodozi , Reem Khougli, baada ya kuoana.
"Kusema ukweli we msichana hii ni haramu ... malkia anaolewa na mtumwa ," mwanaume mmoja aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya kuona picha ya wawili hao.
Facebook mubashara kutoka fungate
Kulikuwa na makumi ya ujumbe- ambao sio wa kushangaza katika nchi ambapo Wasudani wengi ambao hujitazama kama Waarabu, kuliko walivyo Waafrika, mara kwa mara hutumia nene'utumwa'', na maneno mengine yasiyo ya dharau, kuwaelezea watu weusi.
Sudan imekuwa ni nchi inayotawaliwa na watu wenye ngozi nyeupe, wasomi wa kiarabu, ,huku Waafrika weusi wanaoishi katika maeneo ya kusini na magharibi wakiendelea kukabiliwa na ubaguzi na kuachwa nyuma kimaendeleo,
Ni jambo la kawaida kwa magazeti nchini humo kuchapisha maneno ya ubaguzi kuwahusu watu weusi likiwemo neno "mtumwa".
Sudan lilikua ni eneo kuu la biashara ya utumwa katika karne ya 19
Wiki chache zilizopita, mwandishi wa taarifa za maoni katika gazeti Al-Intibah linalomuunga amkono rais wa zamani wa Sudan Omar-al-Bashir - ,ambaye hakubaliani na suala la mwanamke kucheza soka, alimuelezea kocha wa kike wa timu ya soka ya Gunners, ambaye anatambulika sana kwa kuifunza timu ya wasichana ya Gunners kama mtumwa.
Na karibu kila chombo cha habari huwaelezea wahalifu wadogo wadogo katika mji mkuu , Khartoum, kama "negros" kwasababu wanawaona kama ni watu maskini na wala si watu wa jamii ya Waarabu.
Wakati nilipomuuliza Abdulraheem kuhusu kile anachoweza kusema juu ya unyanyasaji na ubaguzi aliofanyiwa yeye na mke wake, alisema : Sikuweza kutuma picha zaidi kwenye kurasa za mitandao yangu ya kijamii kwa kuogopa kupokea matusi zaidi."
Badala yake Abdulraheem mwenye umri wa miaka 29- na mke wake mwenye umri wa miaka 24 walifanya Facebook mubashara wakati wa fungate yao, wakisema kuwa wanapendana na ubaguzi hauna maana kwao.
Sura chache za watu weusi
Katika tukio la hivi karibuni, mkuu wa kikundi cha haki za wanawake kinachoitwa , No To Women Oppression, alitoa maoni yake kwenye picha inayoonesha kijana mmoja mweusi akiwa na mke wake mzungu kutoka Ulaya kwa kusema kuwa mwanamke yule, katika kumchagua mume wake, huenda alikua anaangalia kiumbe ambacho kinakosekana katika mabadiliko kati ya binadamu na nyani.Kufuatia malalamiko ya watu juu ya ujumbe huo, Ihsan Fagiri alitangaza kujiuzulu, lakini No To Women Oppression kikakataa kukubali kujiuzulu kwake, likisema kuwa hakua na maana hiyo aliyoiandika.
Kumekuwa na maandamano madogo ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Sudan
Ubaguzi wa rangi ni kitu cha jadi nchini Sudan, kihistoria na tangu uhuru wa taifa hilo , ambapo vyeo vya juu zaidi vya kazi vimekua vikijazwa na watu kutoka kaskazini - ambao ni wa jamii za Waarabu na Wanubi.
Takriban maafisa wote wa ngazi ya juu katika jeshi wanatoka katika jamii hizi, jambo linalowaruhusu kutumia ushawishi wao kumiliki sekta ya biashara.
Leo kama ikiingia katika idara yoyote ya serikali au benki mjini Khartoum , ni nadra kumuona mtu mweusi akifanya kazi muhimu.
Hakuna takwimu za kuaminika juu ya idadi ya watu kulingana na jamii zao, ukiachana na utajiri wao, lakini kikundi cha waasi wanaopigania haki za watu weusi cha Darfur kinakadiria kuwa 60% ya wakazi wa Khartoum ni weusi.
Wafanyabiashara wa utumwa 'walitukuzwa'
Ubaguzi wa rangi una mizizi yake tangu kuasisiwa kwa mji wa Khartoum mwaka 1821 kama soko la watumwa.
Kufikia nusu karne, karibu theluthi mbili ya watu waliokuwa katika mji huo walikua watumwa.
Sudan ilikuwa ni mojawapo ya maeneo ya Afrika ya kupata watumwa, huku watumwa waliosafirishwa kutoka kusini hadi kaskazini, na Misri , Mashariki ya kati na maeneo ya Mediterranean wakichukuliwa kutoka Sudan.
Bado wafanyabiashara ya utumwa wanatukuzwa-mtaa katikati mwa mji mkuu umepewa jina la al-Zubair Pasha Rahma, ambaye jhimaya yake ya biashara ilipanuka hadi katika maeneo ya ile inayoitwa Jamuhuri ya Afrika ya katikwa sasa na Chad.
Wanahistoria wanasema aliwakamata zaidi watumwa wanawake kutoka maeneo ya Sudan ambayo kwa sasa yanafahamaika kama Blue Nile na milima ya Nuba Mountains, pamoja na Sudan Kusini na kutoka katika jimbo la Oromia nchini Ethiopia. Alikua anafahamaika kwa jeshi lake la watumwa, ambalo liliwajumuisha watumwa waliotekwa kutoka Sudan Kusini.
Mtaa mwingine umepewa jina la Osman Digna - mfanyabiashara wa watumwa na kamanda wa kijeshi, ambaye biashara yake wakati huo iliyonoga wakati huo ilivunjwa na kisheria utumwa.
Biashara hiyo ilizuiwa rasmi mnamo mwaka 1924, lakini uamuzi wa kuizuwia ulikabiliwa na upinzani mkali kutoka zaidi kwa Waarabu na viongozi wa Kiislamu, miongoni mwao wakiwa ni Abdelrahman al-Mahdi na Ali al-Mirghani, ambao wengi wanamini walikua na watumwa wanawafanyia kazi katika ardhi yao iliyokuwa kando ya mto Nile.
Waliuandikia utawala wa kikoloni wakiutaka wasizuwie utumwa, lakini ombi lao lilipuuzwa.
Wanaume hao wawili, pamoja na vyama vyao vya kisiasa - Unionist na Umma - waliendelea kuwa na ushawishi mkubwa baada ya uhuru wakiingiza fikra za ubora wa Waarabu katika taifa jipya kwa kutoa karibu ajira zote kwa Waarabu na kushindwa kuendeleza maeneo yanayokaliwa na watu weusi.
Mjukuu wa Mahdi, Sadiq al-Mahdi,alihudumu kama waziri mkuu kuanzia mwaka 1966 hadi 1967 na tena kuanzia mwaka 1986 hadi 1989, wakati mtoto wake Mirghani, Ahmed, alipokua rais katika serikali ya Muungano iliyoundwa na wanaume hao wawili.
Wasomi wawili wa Sudan, Sulimen Baldona Ushari Mahoumwalidai wazi kwamba waligundua ushahidi wa Waarabu wa makundi yaliyoko wanaowatumikisha watu weusi kutoka kusini kama watumwa. Walisema makundi haya yalipewa silaha na jeshi la Sadiq al-Mahdi - na walikua ndio mwanzo wa wanamgambo wa Janjaweed, ambao baadae walishutumiwa kwa kwa mauaji ya kimbari ya Darfur.
Madai ya uvamizi wa watumwa yalikanushwa na serikali ya Ahmed Mirghani na Sadiq Mahdi, ambao waliendelea kuwa na ushawishi katika siasa za Sudan na wako karibu na serikali ya sasa, ambayo ilichukua mamlaka baada ya kumpindua madarakani Bwana Bashir mwaka 2019.
Uvamizi wa biashara ya karne ya 21
Kujiona wao ndio wa maana zaidi kwa wengi miongoni mwa wasomi Waarabu, ndio sababu kuu ya baadhi ya mizozo mibaya zaidi iliyoikumba Sudan tangu ilipopata uhuru, huku watu weusi ama wanadai usawa au ardhi yao wenyewe.Uvamizi wa watumwa kusini mwa nchi uliripotiwa sana kuwa uliendelea hadi mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005, jambo lililosababisha watu weushi hasa Waafrika wa Sudan Kusini kujitenga na Sudan miaka mitano baadae.
Wanawake na watoto waliotekwa na makundi ya Waarabu kufanya kazi kwa ajili ya "bwana" bila malipo mara nyingi hawakuziona familia zao tena, ingawa mara kadhaa uhuru wao waliupata kupitia makundi ya msaada kama Christian Solidarity International.
Na tangu mzoizo wa Darfur ulipoanza mwanzoni mwa miaka ya 2000s, kundi la wanamgambo Waarabu wanaounga mkono serikali la Janjaweed limekua likiripotiwa mara kwa mara kwa kuvamia vijiji vya watu weusi, kuwauwa wanaume na kuwabaka wanawake.
Ni mchache yaliyobadilika huko mwaka jana, huku ripoti za ubakaji na uchomaji wa vijiji zikiendelea licha ya mazungumzo ya amani yaliyoandaliwa na serikali ya muungano, ambayo inaongoza kipindi cha mpito cha miaka mitatu.Serikali ya mpito iliundwa na jeshi na makundi ya kiraia yaliyoongoza mapinduzi mwaka 2019, lakini haijawa wazi ikiwa kweli imejitolewa kushughulikia suala la mfumo wa ubaguzi wa rangi ndani ya taifa la Wasudan.