Wanaume wanaomuheshimu Mungu, na wanajiheshimu wenyewe wapo wengi tu, so far hakunaga uhaba wa wanaume kabisa. So kumng'ang'ania mtu asiyeniheshimu; sina hicho kipaji kabisa, plus ukiona yanakushinda sana hakuna aliyekufa kabla ya wakati kwa sababu ya kuwa single. My pride, my ego, my dignity, my peace of mind + my health ni vya muhimu sana, sasa siwezi kumruhusu mtu aniharibie tu kirahisi rahisi. Hayo mambo ya utaacha wangapi, ndo yanafanya wanawake waendelee kunyanyasika kwenye ndoa zao wengine hadi kufa kisa eti "Wanaume wote wapo hivyo hivyo". Vidole tu vinapishana sembuse binadamu.
Huwezi kushindana na mpumbavu kwa kuwa mpumbavu pia, atakushinda. Siwezi kuharibu maisha yangu in the name of kumkomesha mtu, wachepukiane tu huko wenyewe na upumbavu wao. Huyo mchepuko ni kahaba shimo refu na mimi mke ni kitu chema, nijikute tu nalower my standard kujilinganisha naye let alone kupigana ngumi sijui maneno na mchepuko. Ikitokea nahitajika kufight, I will fight her spiritually, of coz I'm from God you know. Mungu na anisaidie.