Wanawake wengi siku hizi hawajui kupika chakula. Wanajaza viungo vingi kwenye mboga inapoteza ladha yake halisi

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Kwa utafiti wangu wanawake wengi wa siku hizi hawajui kupika au mapishi kwa ujumla wake.

Wanawake wengi wa siku hizi wanaamini viungo vingi kwenye mboga ndio mapishi mazuri.

Mbona inawekewa viungo vingi hadi inapoteza ladha. Hakuna tofauti ya mapishi ya nyumbani ya mboga fresh kabisa na mapishi ya KFC ambapo unakuta kuku alichinjwa hata miezi 8 iliyopita. Kwa KFC kuwekea kuku viungo vingi sana angalau ipate ladha ni sahihi maana kuku au mboga zao nyingi sio fresh, kuku ana miezi 8 toka amechinjwa, ukimla bila viungo ni tasteless kabisa.

Ukija huku kwetu tuna mboga fresh kabisa, ng'ombe au kuku amechinjwa leo ama jana ila viungo anavyowekewa anapoteza ladha kabisa. Unakua ni sawa inapata ladha ya viungo na sio mboga au nyama yenyewe, ile teste ya kuku au nyama halisi huipati.

Kwa mapishi ya siku hizi ukitaka kupata real taste ya nyama labda uende bar ule nyama choma au kuku choma au uchome mwenyewe nyumbani. Ama unywe supu tu.

Nyama inawekewa vitunguu maji, vitunguu swaumu, pilipili hoho, karoti, nyanya, meat masala, royco mchuzi mix na viungo vingine. Hapo huwezi kupata real taste ya nyama.

Mama zetu zamani walikua wakipika nyama viungo vichache sana unakula unapata ladha halisi ya kuku au nyama.

Kina mama acheni kurundika viungo vingi kwenye mboga, inapoteza ladha.
 
Wanaopika ni wanawake tu wanaume hawapiki?
Sexist bullshit.
Kwenye jamii zote sehemu kubwa ya wanaopika ni kina mama.

Ni kweli wanaume wanapika ila ni kwa kiasi kidogo sana.

Sio kila jambo lazima uwe na mawazo ya kijinsia.

Feminists mko negative muda wote. Hamuoni kitu chochote kizuri kwenye maisha. Hii Dunia ni ngumu sana kwenu.
 
Siupike wewe ukitakacho,kiongozi huongoza kwa mfano nunua huyo kuku siku hyo pika muonyeshe mfano mbona atajifunza,upendo wa kweli nikuelekezana tu mpaka mnakuwa mstari mmoja
Utapika kila mahala hata kwenye nyumba za watu? Hapa sijazungumza kua mwanamke wangu anapika hivyo, nimesema wanawake.
 
Kuna ndoa ilitaka kuvunjika ndani ya miezi mitatu tu baada ya Honey moon.......ktk mahusiano walikuwa wanakutana huko wanakula na kunywa saafi......kumbe yule shemeji yetu hajui hata chai inaandaliwaje (mtoto wa mboga saba).......

Ktk kikao cha familia ile namm nikahudhuria,nikajaribu kumsihi bro ampeleke hata Veta akajifunze,ila
Yule bro akamrudisha kwao,baba mkwe akataka nayeye kumuacha mkewe kisa hakumpa mafunzo mazuri mwanaye na ameleta aibu nyumbani, shemeji alifundishwa kupika pale nyumbani na mama na beki 3 wao,ndani ya miezi sita saizi yupo vizuri kabisa.Na hataki kaka ale magengeni😂😂

Dadaz jifunzeni kupika
 
Kuna ndoa ilitaka kuvunjika ndani ya miezi mitatu tu baada ya Honey moon.......ktk mahusiano walikuwa wanakutana huko wanakula na kunywa saafi......kumbe yule shemeji yetu hajui hata chai inaandaliwaje (mtoto wa mboga saba).......

Ktk kikao cha familia ile namm nikahudhuria,nikajaribu kumsihi bro ampeleke hata Veta akajifunze,ila
Yule bro akamrudisha kwao,baba mkwe akataka nayeye kumuacha mkewe kisa hakumpa mafunzo mazuri mwanaye na ameleta aibu nyumbani, shemeji alifundishwa kupika pale nyumbani na mama na beki 3 wao,ndani ya miezi sita saizi yupo vizuri kabisa.Na hataki kaka ale magengeni

Dadaz jifunzeni kupika
Sasa walimuozesha vipi hata kuchemsha chai mtihani? Malezi ya hovyo kabisa

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Inna kwa kweli kwa hii idara sina mashaka.😀
nakuamini, nakuonaga kule kwenye uzi wa vyakula uko njema huwa napita kimya kimya.
 
Back
Top Bottom