Wanawake wengi siku hizi hawajui kupika chakula. Wanajaza viungo vingi kwenye mboga inapoteza ladha yake halisi

Umesema kweli kabisa, Mimi huwa naacha kula nikikutana na situation hii na ni muhanga.
 
Kwa utafiti wangu wanawake wengi wa siku hizi hawajui kupika au mapishi kwa ujumla wake.

Wanawake wengi wa siku hizi wanaamini viungo vingi kwenye mboga ndio mapishi mazuri.

Mbona inawekewa viungo vingi hadi inapoteza ladha. Hakuna tofauti ya mapishi ya nyumbani ya mboga fresh kabisa na mapishi ya KFC ambapo unakuta kuku alichinjwa hata miezi 8 iliyopita. Kwa KFC kuwekea kuku viungo vingi sana angalau ipate ladha ni sahihi maana kuku au mboga zao nyingi sio fresh, kuku ana miezi 8 toka amechinjwa, ukimla bila viungo ni tasteless kabisa.

Ukija huku kwetu tuna mboga fresh kabisa, ng'ombe au kuku amechinjwa leo ama jana ila viungo anavyowekewa anapoteza ladha kabisa. Unakua ni sawa inapata ladha ya viungo na sio mboga au nyama yenyewe, ile teste ya kuku au nyama halisi huipati.

Kwa mapishi ya siku hizi ukitaka kupata real taste ya nyama labda uende bar ule nyama choma au kuku choma au uchome mwenyewe nyumbani. Ama unywe supu tu.

Nyama inawekewa vitunguu maji, vitunguu swaumu, pilipili hoho, karoti, nyanya, meat masala, royco mchuzi mix na viungo vingine. Hapo huwezi kupata real taste ya nyama.

Mama zetu zamani walikua wakipika nyama viungo vichache sana unakula unapata ladha halisi ya kuku au nyama.

Kina mama acheni kurundika viungo vingi kwenye mboga, inapoteza ladha.
Wanafikiri kuweka mafuta mengi na viungo Vingi ndio mapishi mazuri.
 
Hivi Biriyani lina viungo? yani nilete nyama home ipikwe bila vikolombezwo? unataka kufananisha mapishi ya mwaka 1800 na 2020? Kama wewe unapenda kula vyakula visivyoelewaka sema hivyo ila sio kwamba eti hawajui kupika, mpelekee mkeo nyama aweke jikoni na maji mwambie akatie nyanya then kula maana mpaka vitunguu na hoho hutaki... Wadada mna huruma sana aisee,poleni. Nawapenda sana wanawake wanaonukisha nyumba yaani upo getini ila unaskia vitu ndani vinanukia tu ukishaingia hutamani kutoka ila kuna mtu anataka ale kama hana taste buds vile
Asante sana kwakutukumbuka, yeye ale tu vyakuloweka
 
Au unapika supu ya sangara bila viungo.

Ahata vijijini kuna limao ndimu wanaweka kukata shombo.

ASITUFOKEE KUHUSU VIUNGO
Huyo atakuwa bahili tu hivi hata kama ni supu usiweke viungo? Anamjua kambale halafu amloweke tu aone raha yake
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kwa utafiti wangu wanawake wengi wa siku hizi hawajui kupika au mapishi kwa ujumla wake.

Wanawake wengi wa siku hizi wanaamini viungo vingi kwenye mboga ndio mapishi mazuri.

Mbona inawekewa viungo vingi hadi inapoteza ladha. Hakuna tofauti ya mapishi ya nyumbani ya mboga fresh kabisa na mapishi ya KFC ambapo unakuta kuku alichinjwa hata miezi 8 iliyopita. Kwa KFC kuwekea kuku viungo vingi sana angalau ipate ladha ni sahihi maana kuku au mboga zao nyingi sio fresh, kuku ana miezi 8 toka amechinjwa, ukimla bila viungo ni tasteless kabisa.

Ukija huku kwetu tuna mboga fresh kabisa, ng'ombe au kuku amechinjwa leo ama jana ila viungo anavyowekewa anapoteza ladha kabisa. Unakua ni sawa inapata ladha ya viungo na sio mboga au nyama yenyewe, ile teste ya kuku au nyama halisi huipati.

Kwa mapishi ya siku hizi ukitaka kupata real taste ya nyama labda uende bar ule nyama choma au kuku choma au uchome mwenyewe nyumbani. Ama unywe supu tu.

Nyama inawekewa vitunguu maji, vitunguu swaumu, pilipili hoho, karoti, nyanya, meat masala, royco mchuzi mix na viungo vingine. Hapo huwezi kupata real taste ya nyama.

Mama zetu zamani walikua wakipika nyama viungo vichache sana unakula unapata ladha halisi ya kuku au nyama.

Kina mama acheni kurundika viungo vingi kwenye mboga, inapoteza ladha.
Mtu anaweka viungo mpaka hamu ya chakulq inakatika

Sipendi viungo vinhi kweny chakula, tena kama nyama, samaki, kuku napenda vikiwa na ladha/harufu yake halisi bila viungo
 
Binafsi napenda vyakula viwe na viungo mfano nyama ikiungwa na nyanya na kitunguu pekee siwezi kula harufu yake inanishinda.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom