Jua kutofautisha ..haya maneno ..mwanamke ,malaya .. Msichana na mdada
Hao wote kwa ujumla wao; malaya, wasichana na wadada ni wanawake tu.
Kwa muktadha wa mwandishi, hakuwa-group, yeye kapiga jumla jumla.
Linapokuja suala la kimapenzi, halina cha msichana, mdada wala malaya.
Nadhani tungejikita katika udadavuzi wa mambo tunayokutana nayo falaghani.
Mleta uzi aliyoyaongea yana ukweli.
Watu wengi wanapenda sana 'ngozi' kama ngozi, ina thamani ya kipekee.
Kwanza ngozi halisi kwa kuitazama hujenga taswira ya unachokiangalia, inavutia hata kupelekea kuanzisha mahusiano.
Pia ngozi kama chakula kwa kuliwa kama kitoweo, ina ladha tamu sana kushinda hata nyama, mf: ngozi ya samaki, kuku, nguruwe ama ng'ombe.
Ukija kwenye masuala ya mapenzi sasa, ngozi halisi(kavu) kwa kuwa ni 'nature' ina thamani na hisia zaidi kuliko hiyo ngozi bandia('ndom).
Mambo ya 'ulaku' wasibebeshwe lawama wanawake pekee, hilo ni janga la kihisia na ni la kidunia kila mtu linamhusu.
Utakuta watu wanaanza vizuri kwa kuvalishana hiyo mipira, lakini mwishoni kwenye umaliziaji hujiona kama wanajipunja, na kwa pamoja hukubaliana kuvua kwa hiyari, kwamba lolote na liwe ilimradi tendo limalizike kwa ufasaha.
Sasa hapo kuna mwanamke wa kulaumiwa!
Wengine kwa uelewa wa kuwa ngozi halisi ina raha zaidi, hujitoza gharama kubwa kwa hiyari yao kumrubuni mwanamke ili kufikia matamanio yao tofauti na gharama za kutumia hizo mnazozisema kinga.
Tena wanaume wengine wakiwa kwenye 'ninakutaka mode' husimangwa kabisa kuwa 'wewe baba, unaniaminije na wala hatujawahi kuonana hata siku moja'?
Utakuta njemba inapanda kijingajinga ikimpa marks za juu huyo mwanamke huku ikikoroma 'mimi nimepima juzi na ninajiamini, wewe nipe tu hivyohivyo...hag...hag...hag! Njemba ikielekea kwenye kilele cha kubembeleza!
Hili jambo limekaa kama vile chatu anavyowinda mbwa.
Chatu hutengeneza mazingira ambayo mbwa hujisogeza kuliwa kwa kuridhika mwenyewe, huku akielewa kabisa kuwa anaenda kumezwa, lakini huwa hana namna ya kujidhibiti na kuweza kutoroka mtego wa adui yake, hilo huwa ndiyo jinsi alivyojichagulia, kujisogeza ili aliwe, maana hakuna namna nyingine.
Na kwenye mapenzi iko hivyo, hakuna wa kulaumiwa kati ya mwanamke ama mwanaume maana ni janga la kihisia.