Wanawake wanavutiwa na nini zaidi kwa wanaume

tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
14,933
Likes
5,129
Points
280
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
14,933 5,129 280
Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.

USAFI BINAFSI

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

KUJIAMINI

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya!
Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA

Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa' ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye ‘fiti' ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.

KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!

KUMSIFIA

Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao.
MWANAUME: "Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana, huyu ni Peter nilisoma naye A – Level, Tosamaganga Sekondari."
MWANAMKE: "Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli nampenda sana mume wangu jamani, tuna mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness. (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha."

ANGALIA TOFAUTI

Bila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini mwenzake, lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.
Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng'ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.
Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.
Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.

KIPAUMBELE

Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni'.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

TENDO LA NDOA

Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: "Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi. Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?
Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia ni wewe tu!
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
82,189
Likes
49,467
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
82,189 49,467 280
Wa huku magomeni kwetu mkwanja tu na mkwara wako ndo sifa kuu
Bhaaaas! Na wala si Migomigo tu. Mkwanja kwa asilimia kubwa sana (90 na kitu) ndo kila kitu popote pale, kuanzia Uswazi, daraja-kati, hadi Ushuani.

Wapo wataojishaua na kujifanya mkwanja si kitu lakini hayo ni mashauzi tu. Mbele ya mkwanja ni wachache sana wenye kuleta za kuleta.

Ila ndo hivyo tena...ukiisha na wenyewe wanapukutika kama majani ya mti kwenye msimu wa kupukutika majani (autumn).
 
Me370

Me370

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
994
Likes
8
Points
0
Me370

Me370

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
994 8 0
Wanawake Wanapenda Security tu. Anataka awe na uhakika wa kula, kulala, kuvaa vizuri, sex from time to time na cash to spend on her own. Alafu yeye atoe K tu.
Kiufupi mtatua shida zake zote au niseme mtoa PESA.
 
Me370

Me370

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
994
Likes
8
Points
0
Me370

Me370

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
994 8 0
Ukiisha na wenyewe wanapukutika kama majani ya mti kwenye msimu wa kupukutika majani (autumn).
Hii sio kweli inategemeana, Huwa hawaondoki hadi wampate anayekupiku. Fikiria situation Ushamzalisha mitoto kama mi tatu hivi, Hapo ka put on a lot of weight na havutii tena kivile baada ya kuwa mama. Hata mkwanja ukiisha huwa they tend tu stick around. Sometimes huwa wanaaangalia security ya watoto pia ila ndo hawakawii kuwa na libaba jingine pembeni kisiri.
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
82,189
Likes
49,467
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
82,189 49,467 280
Hii sio kweli inategemeana, Huwa hawaondoki hadi wampate anayekupiku. Fikiria situation Ushamzalisha mitoto kama mi tatu hivi, Hapo ka put on a lot of weight na havutii tena kivile baada ya kuwa mama. Hata mkwanja ukiisha huwa they tend tu stick around. Sometimes huwa wanaaangalia security ya watoto pia ila ndo hawakawii kuwa na libaba jingine pembeni kisiri.
Anaweza aka-stick around na bado akawa anatombesha nje vilevile. So no guarantees either way.

Sasa ukiwa naive ndo unaweza ukadhani kwamba hawezi kufanya chochote kwa sababu hana mvuto and what have you.

Nilichokuwa nakiongelea zaidi ni ule mvuto wa pesa. Ukiwa nazo hata uwe 'mbaya' kiasi gani utaonekana 'mzuri' tu, utapewa heshima za uongo na kweli, na kadhalika, na kadhalika.

Njuruku zikiisha basi hata zile 'perks' zinazokuja na hiyo status na zenyewe kama siyo kuisha basi zinapungua.

That's just the way the cookie crumbles.
 
Honey Faith

Honey Faith

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2013
Messages
15,844
Likes
5,769
Points
280
Honey Faith

Honey Faith

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2013
15,844 5,769 280
pesa ndo kila kitu mengine majaaliwa
 
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
29,405
Likes
7,471
Points
280
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
29,405 7,471 280
Pesa ................... Uko vipi kitandani................. Mengine ni mbwembwe tu.
 
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
5,174
Likes
653
Points
280
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
5,174 653 280
Hixo zote Mbwembwe tu! Pesa ndio kila kitu!
 
A

Andrew Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
317
Likes
37
Points
45
A

Andrew Jr

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
317 37 45
Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.

USAFI BINAFSI

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

KUJIAMINI

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya!
Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA

Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.

KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!

KUMSIFIA

Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao.
MWANAUME: “Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana, huyu ni Peter nilisoma naye A – Level, Tosamaganga Sekondari.”
MWANAMKE: “Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli nampenda sana mume wangu jamani, tuna mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness. (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha.”

ANGALIA TOFAUTI

Bila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini mwenzake, lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.
Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.
Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.
Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.

KIPAUMBELE

Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

TENDO LA NDOA

Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi. Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?
Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia ni wewe tu!
Umenena, lakini hiyo ni nadharia tu. Wanawake wa sasa wanachokipenda toka kwa wanaume, anafahamu Mungu. Yawezekana ukafanya kila ulichoainisha hapo juu na bado wakazingua.
Sali sana umpate mwanamke atakaekujali, haya mengine yatarekebishika.
 
Jaber Job

Jaber Job

Senior Member
Joined
Oct 2, 2013
Messages
122
Likes
6
Points
0
Jaber Job

Jaber Job

Senior Member
Joined Oct 2, 2013
122 6 0
Hii sio kweli inategemeana, Huwa hawaondoki hadi wampate anayekupiku. Fikiria situation Ushamzalisha mitoto kama mi tatu hivi, Hapo ka put on a lot of weight na havutii tena kivile baada ya kuwa mama. Hata mkwanja ukiisha huwa they tend tu stick around. Sometimes huwa wanaaangalia security ya watoto pia ila ndo hawakawii kuwa na libaba jingine pembeni kisiri.
Umeshasema watoto....unafikiria angekuwa mwenyewe angebaki? Uchungu wa mwana aujuae mama...na kuhusu libaba jingine pembeni kisiri,anayeanza na wewe malizia.
 
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Messages
5,554
Likes
193
Points
145
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined May 8, 2013
5,554 193 145
^^
Naam umegusa sifa za wanawake wa toleo la kwanza..original version.
Hawa wa toleo jipya wanashindana kutokuwa wao!
^^
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,724
Likes
3,408
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,724 3,408 280
Hili jukwaa nalo naona laanza kugeuka kuwa kama jukwaa la siasa...

Ushabiki mwingi kuliko tafakari yakinifu...
 
McDonaldJr

McDonaldJr

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Messages
6,429
Likes
6,386
Points
280
McDonaldJr

McDonaldJr

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2013
6,429 6,386 280
Duh nimeupenda uchambuzi wako ila hawa wanawake wa bongo.com wanaodhaminiwa na TGNP masnuraaa tupu utafanya yote kumbe unamegewa na chalii ambae hamfanyii ht 1 kati ya haya rude boys hawa dawa yao sarafu na kusimamia show kwa kiwango cha lami bhaaaaaasi huu u-gentlemen waliufaidi mama zetu toka kwa baba zetu
 
badiebey

badiebey

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Messages
5,888
Likes
485
Points
180
badiebey

badiebey

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2013
5,888 485 180
Mtoa thread unapatikana wapi aisee...umegusa kwenyewee....
Af nyie mnaosema mwanamke pesa kw hyo hamuwezi pendwa hadi umnunue mwanamke,hv hamjajifunza kw mushi wa ufoo saro ,na yule jamaa wa ilala?women want money cz hawapat hvo vitu hapo juu mtu anaona she has nothing to lose km anakosa penzi basi apate pesa,mfanyie hvo ur girl utaniambia,bt of coz girl anaejielewa(sio wote),...
 
Christine1

Christine1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
12,601
Likes
1,463
Points
280
Christine1

Christine1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
12,601 1,463 280
Hili jukwaa nalo naona laanza kugeuka kuwa kama jukwaa la siasa...

Ushabiki mwingi kuliko tafakari yakinifu...
hata mi nimeliona hilo best angu
 
Christine1

Christine1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
12,601
Likes
1,463
Points
280
Christine1

Christine1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
12,601 1,463 280
wangapi wana hizo pesa still wanagongewa,
still ndoa hazina amani na furaha na upendo?

sawa mwanaume lzm awe mtafutaji/mpiganaji kwa ajili ya familia yake bt pesa sio jawabu la kila kitu/mambo yote nawaambia ukweli.
kuna watu wana pesa lkn maisha yao utalia.
bora muishi kwa amani , furaha na upendo wa kweli, mkifanya kazi kwa bidii huku mkimtanguliza Mungu
plus hayo aliyosema mtoa mada hapo y msifanikiwe?
 
Forum statistics

Threads 1,252,297
Members 482,076
Posts 29,802,983